Ni kwamba Musa hakuandika matukio yote katika vile vile vitabu vitano vya mwanzo (mwanz,kutoka,hesabu,torat,walawi) ila aliwaagiza waisrael wawasimulie matukio yote watoto wao, sasa walipowasimulia watoto wao hawakuwasimulia kama wataalam wa histori pia waliwasimulia watoto wao kama mambo kamawalivyoyaona kwa macho si kama wataalam wa elimu ya viumbe, mazingira,sayansi nk.
Mfano. Waliona maji ya mto naili yamekua mekundu tena yana nuka rangi hiyo ikawa nyekundu kama damu tukio hilo walisimulia kua Maji yaligeuka kua damu.
Hivyo inawezekana kutokana jinsi walivyowasimulia bila kua na elimu ya mambo waliwasimulia vibaya waandishi wa mambo ya kale kwamba mvua ilinyesha dunia nzima.
Baadhi ya vitu vilivyosimuliwa vibaya kutokana na ukosefu wa elimu na kusimulia jambo kama walivyo liona ni haya..
NB. Mungu hufanya miujiza kwa aina kuu mbili ambazo ni
1. Mungu anatenda jambo fulani la pekee kabisa lisiloweza kutokea kwa namna yoyote ile hapa duniani bila uweza wake mfano Kufufua mtu.
2. Mungu anatenda jambo fulani linaltokea mara kwa mara kumsaidia mtu fulani katika mzingira ya pekee nalo hilo ni muujiza sababu limetokea kwa maongozi ya Mungu wakati uleule anapolihitaji mtu yule
Kuvuka Bahari ya shamu
Kutokana na vitabu vya historia (Kutoka) inasemekana kua sehemu walipovuka waisrael katika bahari ya shamu hapakua na maji mengi sana, maji yalikua yamekupwahivyo walipita vizuri. Lakini wakati wamisri wanavuka maji yakajaa. Hivyo walipomua wanasimulia watoto wao walisema kua maji yaligawanyik/yalikauka wakapita
Maelezo haya niliyaandika katika moja ya thread zangu humu..
Ukituliza akili na kuchambua haya niliyoandika waweza papaya kitu