john achila mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 137
- 273
Waliokufa kabla ya Yesu kuja duniani wataokolewaje?
Waliokufa kabla ya Yesu kuja, yaani watu wa Agano la Kale, wataokolewaje?
Swali hili linaulizwa na baadhi ya watu kwa sababu tunajua kuwa kuokolewa ni kupitia damu ya Yesu tu, ndiyo tunapata ukombozi wa hakika wa dhambi. Sasa waliokuwa wanaishi katika Agano la Kale wataokolewaje, ilhali Kristo alikuwa hajafa bado, na damu iondoayo dhambi ilikuwa haijamwagika?
Ni kweli ukombozi unapatikana kupita damu ya Yesu tu. Lakini ni vizuri kufahamu kuwa Agano jipya halikuja kulifanya agano la kale liwe uongo, badala yake limekuja kulikamilisha agano la kale, kama Bwana wetu Yesu alivyosema mwenyewe katika Mathayo 5:17: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza”.
Ili kuelewa vizuri connection kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, hebu tutafakari mfano ufuatao.
Taasisi moja imedahili wanafunzi wake walioingia kupitia mfumo wa makaratasi, kwamba mwanafunzi ili akubalike kujiunga na chuo, hana budi kuwasilisha fomu zake (hard copy) katika ofisi ya taasisi hiyo.
Lakini mwaka mmoja baadaye, taasisi ikabadili mfumo na kuanza kudahili wanafunzi wapya kupitia mfumo wa kieletroniki, kwamba ili mwanafunzi akubalike kujiunga na taasisi hiyo, hana budi kutumia mfumo wa kielekroniki (soft copy), hata akiwa nyumbani, kupitia internet. Na kwamba hakuna mwanafunzi yeyote atakayeweza kupokelewa bila kutumia mfumo huo, kwani ni rahisi na mwepesi katika kutunza kumbukumbu.
Swali: je, mfumo huo mpya ulioanza, utawafanya wale wanafunzi wa zamani ambao walitumia mfumo wa zamani kuwa si wanafunzi halali tena wa taasisi hiyo? au itawafanya wale waliokwisha kuhitimu zamani, waliotumia mfumo wa zamani, vyeti vyao kuwa batili?
Jibu: Ukweli ni kwamba wataendelea kuwa wanafunzi, isipokuwa, watakaojiunga upya hawana budi kutumia mfumo mpya, kwa sababu mfumo wa zamani utakuwa umeshabatilika, hautumiki tena.
Kadhalika, na Agano la Kale ni hivyo hivyo. Agano la Kale ulikuwa na mfumo wa zamani wa kuwasogeza watu karibu na Mungu. Matendo matakatifu ya watu ya IMANI kwa Mungu ndiyo yaliwasogeza karibu na Mungu.
Lakini muda ulipofika, ulikuja mfumo bora zaidi na mwepesi na wa haraka, ambao utamwingiza mtu katika ufalme wa Mungu kirahisi na kwa uhakika zaidi.
Huo ndio mfumo wa Agano Jipya kupitia agano la damu ya Yesu Kristo, na si tena damu ya mafahali na kondoo, kama maandiko yanavyosema katika Waebrania 10:1-11: “Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi"… “Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi, ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi”.
Hiyo ilifanya Agano la kwanza liwe chakavu na agano la pili liwe jipya, sawa sawa na Waebrania 8:13: “Kwa kule kusema, Agano Jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka”.
Kwa hiyo lilipokuja Agano Jipya, basi agano la kwanza likafanyika kuwa la kale, lisilotumika tena, hivyo kwa sasa halifanyi kazi tena KATIKA KUOKOLEA.
Abrahamu alimwamini Mungu kuwa katika ahadi zake na ufunuo mpya ambao Mungu alimpa katika Mwanzo 12 na 15. Kabla ya Musa, hakuna Bibilia iliandikwa, lakini mwanadamu aliwajibika kwa yale Mungu alikuwa amefunua. Katika Agano la Kale lote, WAUMINI WALIOKOKA. NI KWA SABABU WALIMWAMINI MUNGU kuwa siku moja atawaondolea shida ya dhambi.
Vitabu vya Mwanzo 15:6 na Warumi 4:3-8, vinatuambia kwamba, Abrahamu ALIMWAMINI Mungu. Hiyo ilitosha Mungu akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Kwa hiyo, waliokuwepo ndani ya Agano la kwanza kabla ya Bwana Yesu, hao watahesabika kuwa watakatifu, sawa sawa tu na waliopo sasa katika Agano Jipya leo. Ndiyo maana akina Musa, Eliya, Henoko, Ibrahimu, Daudi, Danieli, na wengineo, wanatajwa kuwa miongoni mwa watakatifu, tena MASHUJAA WA IMANI, japokuwa hawakubatizwa, wala kumwona Masihi.
Baada ya Yesu kuja na damu yake kumwagika, basi wote watakaozaliwa baada ya hapo, hawana budi kulitumia Agano Jipya, na kuachana na lile la kale, kuhusu kuokoka. Ye yote atakayejitumainisha kwa Agano la Kale, basi hataweza kuokoka kabisa.
Hiyo ndiyo sababu ni kwa nini tunapaswa tulijue sana Agano Jipya na misingi yake. Tukianza kuwatazama watu wa Agano la Kale, pasipo kujua misingi ya Agano Jipya, tutajikuta tunachukua vitu visivyofaa kwa wakati wa sasa. Kwa mfano, tukimtazama Daudi na maisha yake na kanuni alizokuwa anatembelea, si zote zitatufaa sisi watu wa Agano Jipya. Tazama, japokuwa Daudi aliupendeza Moyo wa Mungu sana, lakini alikuwa na wake wengi na alikuwa na visasi na maadui zake.
Tutachukua na kujifunza imani ya Daudi, unyenyekevu wa Daudi na mengine mazuri, lakini hilo la kuoa wake wengi, Agano Jipya linalikataza; hilo la kulipiza kisasi Agano Jipya limetuzuia (Mathayo 5:38-39). Yesu anasema, kila amwachaye mkewe na kuoa mwingine azini, na ndoa ni mke mmoja, mume mmoja, si zaidi ya hapo (Mathayo 19:5-6).
Hatuna budi kumsikiliza aliye mkuu zaidi ya Daudi, na Sulemani, na Musa, na Eliya, ambaye ni Yesu, anayetajwa kama Mjumbe wa Agano Jipya (Waebrania 9:15; Waebrania 12:24).
HIVYO, WALIOKUFA KABLA YA YESU KUJA DUNIANI, WALIOKOLEWA KWA IMANI KWA MUNGU. IMANI KWA MUNGU ILITOSHA MUNGU KUWAHESABIA HAKI.
BAADA YA YESU KUJA NA DAMU YAKE KUMWAGIKA, WOTE WATAKAOZALIWA BAADA YA HAPO, WAMEOKOLEWA KWA DAMU YA YESU, KULINGANA NA AGANO JIPYA.
KINACHOHITAJIKA KATIKA WOKOVU KATIKA VIZAZI VYOTE, IMEKUWA NI IMANI.
Mungu amekuwa sehemu ya wokovu wa mtu kila wakati.
Mfalme Daudi katika Zaburi 2:12, aliandika: “Heri wote wanaomkimbilia”.