Sanaa ya kifo

Sanaa ya kifo

Hii itanifaa nikiifanya Avatar
Chukua na hii
Graveyard_2012-06-15_17-24-34-36.jpg
 
42e6a14c8b4a9b299b842cd9a83af7c3.jpg
Hii ni habari ngeni kabisa kwa wale watakaobahatika kusoma hii mada na pia wale wenye kupenda kujifunza vitu vipya ni sanaa ya kifo katika uhalisia wetu bila kuchanganya na doctrines za kiimani na kiasili.

Kwenye mada nyingi tumeona uhayawani wa mwanadamu tumeona kwa sehemu kubwa jinsi kiumbe hiki kiitwacho binadamu kilivyo kipumbavu na kisicho na chembe ya uelewa kuhusu yale yatokeayo na ayafanyayo kila siku.

Binadamu anaongozwa na hisia zaidi ya vile avipendavyo kuliko uhalisia na uelewa wa yale yanayotokea kila sekunde kila dakika na kila saa ya pumzi yetu
si mara haba tumeona tumeona picha zinazowakilisha matukio mbalimbali ya kutisha na kusikitisha matukio ya ajali nk. Wengi tumeyaandikia maelezo ya mbwembwe kulingana na hisia zetu na umahiri wetu katika kuonyesha uchungu lawama hasira nk.

Matukio hayo ni wenzetu ambao tayari hatunao tena ni marehemu wameshamaliza safari yao hapa duniani na sasa wako mahali pengine wakipumzika au wakiendelea na safari yao lakini katika hatua nyingine.
Hawa tunawaita wafu, kila mmoja akiwa kafikia umauti wake kwa style yake.

Wengine kwa mateso makubwa wametuachia majonzi na huzuni ambazo zina chukua muda kufutika katika hisia na kumbukumbu zetu, lakini pamoja na hayo yote natuangalie kwa mtazamo mwingine hiki kitu kinachoitwa KIFO ili tuweze kuwa na ufahamu mwingine tofauti na ule tuliozoea kuwa nao huko nyuma kwa njia hii ile huzuni simanzi na majonzi kwa wapendwa wetu vinaweza kupungua na kutufanya tuishi kwa utulivu zaidi.
------------------------------
Si watu haba ambao hawatakubaliana nami kwa kile nitakachoandika hapa wengi watanihukumu kwa namna ya ajabu kabisa siwalaumu kwakuwa ni mazoea ya wengi kuwa wanafiki na waoga kupindukia, na kuwa na ile dhana ya kuwa kinachosemwa na wengi ndio sahihi ndio ukweli ndio uhalisia
Hatutaki kubadilika Hatutaki kujifunza mambo mapya hatutaki kusoma na kuzitafsiri hisia zetu za ndani kabisa kwa muktadha mwingine.

Tunakumbuka kusahau kuwa ni katika hizo hisia zetu za ndani kabisa ndimo kweli yetu inapotoka na kweli hiyo tunapobahatika kuifahamu hatuna budi kuitafsiri kwa wengine bila woga wala kuficha ficha hata kama tutaitwa majina yote mabaya na kuonekana tunakwenda kinyume na kanuni za kutunga za mwanadamu.
****************************

Sehemu ya pili

Kifo kwa tafsiri ya rahisi na iliyozoeleka kwa mwanadamu si neno zuri si neno la kuvutia wala kutajwatajwa hovyo ni neno lililonakshiwa kwa vikolombwezo vyote kwa kutisha na kuogofya sana lakini Kifo ni jambo bora na la bahati nadra kutokea, kifo ni daraja la kuvukia kwenda kwenye hatua nyingine ya maisha ya juu zaidi mepesi zaidi mazuri zaidi! Kifo ni mwendelezo wa uumbaji ni kama tunaposema elimu haina mwisho uumbaji nao hauna mwisho.
Unajua kaka kuna vitu vingine au kitu kingine hakiwezi kusimama bila kitu kitu kingine ndio kama ilivyo kwa kifo huwezi kukielezea kifo bila imani kaka.

Na ukijaribu kutenganisha lazima utakosea kama ulivyokosea katika baadhi ya nukta.

Kwanza lazima ujue kabisa ya kuwa KIFO ni kiumbe kama kilivyo kiumbe UHAI.
 
Kifo sio kiumbe ....na wala kifo sio mchakato....bali kifo ni mwanzo wa safari ndefu isiyo na mwisho
Ili kiambishi cha kifo kilete maana inabidi kuwepo na muunganiko wa vitu viwili
1. Mwili jumba uharibikao
2.pumzi roho yenye uhai isiyo na mwisho
Ili kifo kitokee ambacho ni kitendo cha roho kutengana na mwili inabidi kwanza kuwe na muunganiko wa hivyo viwili
Kilichopo hapa ni ziraili ama malaika wa kifo ama mtoa roho anayefanikisha mchakato mzima kuelekea mwanzo wa kifo usio na mwisho...kwahiyo kifo kama kifo sio kiumbe na sio jambo lenye tamati kiroho ama kimwili
 
Hapa sasa ndio somo linapo anzia. Kifo ni kiumbe na kilianza kifo kuumbwa kisha ukaumbwa Uhai.

Kuliltea swali kuhusu KIUMBE ROHO" nilikuwa na maanisha na huo ndio ulikuwa ni wakati wake.

Nilichokiona hapo ni ufahamu wako mdogo juu ya tamko KIUMBE.
 
Ok sawa asante kwa mtazamo hasi
 
Tumia akili yako vizuri.
Ktk maelezo hayo yote ni ujumbe upi unataka kutuaminisha?
Hizo ntantalila... Zote zinatokana tafit zip za post life?

Information zilizopo kwenye vitabu vya imani at least zimefafanua two destinations i.e peponi na jehanamu japo detail zinatofautiana za yatakayofanyika peponi.
Japo wanakubaliana jehanamu is all about mateso.

Ungetumia akili yako kuwasahidia binadamu namna ya kuipata destiny njema ningeona unaitumia akili yako vixuri.
Kuliko kuwafundisha paradoxical destination of another life without clues of wht kind of life.

Unajitia kumkataa Mungu huku hekima yako haitoi mbadala .

Nikusihi tu. Tumia akiri yako vizuri
Nani sasa unaye msema
 
Hivi kuna uhusiano gani kati ya kupata 'haja' wakati wa kuzaliwa pia na wakati wa kukata roho?

**Naruhusu kurekebishwa.
 
Kifo ni adhabu,
Ila inabidi tukitarajie tu hakuna namna ya kukikwepa.
Watu wanaogopa kifo kwani hawajui wapi watakwenda baada ya kufa.
 
tatizo sio kufa watu tunaogopa moto(motoni) ndo maana tunaogopa kifo kwasababu huwezi fika huku na mwili wa nyama inabidi ufe kwanza?
 
tatizo sio kufa watu tunaogopa moto(motoni) ndo maana tunaogopa kifo kwasababu huwezi fika huku na mwili wa nyama inabidi ufe kwanza?
Roho haifi... Dhana ya moto ni pana sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom