unafiki wa sitta ni huu.
richmond ilipofutwa, sitta aliamua kuanzisha kampuni yao yeye, karamagi na msabaha lakini wakachelewa kwenda brela wakazidiwa ujanja na dowans, kuona wamezidiwa ujanja na dowans sitta akamshawishi waziri wa nishati afute mkataba na dowans. Pamoja na kwamba dk. Rashid alielezea athari zake na ambazo ni hizi za sasa kuilipa dowans mabilioni ya shilingi hawakusikia. Kisha akamteua dk. Mwakyembe kuongoza tume kwa kushirikiana na wabunge wa chadema wakati anajua mwakyembe, (waziri mkuu wa sitaa ikiwa atapata urais), ana interests zake za umeme wa upepo singida! Huo ndiyo unafiki mkubwa wa samuel sitta. Mgombea urais kwa tiketi ya chadema 2015! Sasa watanzania ukweli wameujua, icc imeeleza ukweli wote, lowasa hajaonekana mahali ametajwa, walioshirikishwa kwenye unafiki wa sitta na wenzake wakiwemo chadema kumdhalilisha mpiganaji lowassa sasa wanahaha wengine wameanza kujikomba kwa lowassa! Jamani watanzania tutafuteni ukweli kwanza kabla ya kujigongagonga. Huu ndiyo ukweli na wananchi wameanza kuujua na ndiyo maana pale udsm juzi alipoingia akiwa na rais, wasomi wa kweli walimshangilia.