Fareed: Hivi neno mnafiki maana yake nini hasa? Kwa bahati mbaya sana, maadui wa Samuel Sitta, ambao ni mafisadi wa Richmonduli, rada, Kagoda, TICTS na wengineo, ndio . wamekuwa wakitumia neno hili ndani ya CCM na nje kujaribu kumpiga vita na kumchafua kiongozi huyu.
Kwa nyie msiojua, Samuel Sitta ni kiongozi shupavu, msema kweli, anayethubutu, mchapa kazi na kiboko wa mafisadi. Tanzania ingempata mtu kama huyu kuwa Rais nchi hii ingeondokana na umasikini katika kipindi chake cha kwanza tu cha miaka mitano! Msiwe wavivu wa kufikiri na kuburuzwa na mafisadi kumuita eti Sitta ni mnafiki, kwa lipi wakati yeye kila siku ameonesha uongozi na ushupavu wa kusema ukweli? -- eg kupinga hadharani malipo ya Dowans, kusema serikali iombe radhi kwa mgao wa umeme, na mengine mengi.
Kwa msiojua, hata CHADEMA wanamfahamu sana Sitta kuwa ni kiongozi makini ndio maana mwaka 2010 walimuomba agombee Urais kupitia chama hicho. Sitta alipokataa ndio ilibidi CHADEMA wambembeleze Dr. WILLIBROD SLAA agombee Urais wakati alikuwa anataka kutetea kiti chake cha ubunge wa Karatu.
Na kama CCM ikimsimamisha Sitta kuwa mgombea Urais wa 2015, basi CHADEMA watapata taabu sana kupambana naye jukwaani. Huu ndio ukweli, acheni uvivu nyie kwa kulishwa maneno na propaganda za mafisadi.
Nyie mnaomtetea Sitta wenu mnafuata mkumbo. Vita yake na EL ndio kilichompelekea akajiita Mpinga mafisadi ili kulipa kisasi kwa wana mtandao kwa kutopewa u-PM alioahidiwa 2005 wakiwa kwenye harakati za kuelekea uchaguzi mkuu. Bungeni ilikuwa ni platform yake pekee ya kumrudi EL. Kwanza Sitta atuambie alipokuwa TIC ndio kipindi Richmond ilisajiliwa, kama alijua ni kampuni feki mbona hakusema? Msishabikie vita - maslahi. Sitta huwezi kumtenga na mafisadi wengine.
Muulizeni huyo Sitta wenu ofisi yake aliyojenga Urambo iliyotumia zaidi ya sh. 470m halafu anamdanganya hadi Rais kuwa imetumia only 170m. Kama si ufisadi ni nini? Sitta alipoona CCM wanataka kumtema yeye na akina Mwakyembe, Mwambalaswa, Nape, Mpendazoe and others wakaanzisha CCJ iliyokuja hujumiwa baadaye na kukosa usajili wa kudumu, vinginevyo wengi wenu ndio mngejua true colours za Sitta!
Kuna kundi lao wakati huo walipokuwa mjengoni wakijiita wabunge wapinga mafisadi wakiwemo hao niliowataja hapo juu na akina Anne Kilango, Stella Manyanya, Lembeli, Selelii na wengineo waliweza kuwadanganya Watz kuwa wao ni tofauti na magamba wengine, kitu ambacho si cha kweli. Wanatumia umbumbumbu wa Wananchi wasiojua kupembua mbivu na mbichi kujijengea umaarufu. Wote ni wanafiki, yote hayo ni mbio za kuelekea ikulu 2015. Msituzingue!
alipokua TIC hakuwa na authority kwa kila uwekezaji kua na data kwanza kijana kabla ya kurukia jambo, tanzania tunapata 3% toka tanzanite one, hawa hawakupita TIC walienda kwa ofisi ya rais Mkapa moja kwa moja,. hapa inaonyesha kuna uwezekano wa Richmond kupita kwenye ofisis nyingine na siyo TIC na hata kama ilipita pale Sitta siyo mjinga wa kupitisha kitu cha ajabu akiwa mkurugenzi aje akipinge baadae kwa kuita feki ni ujinga hata kwa mtu asiokua na uzoefu au hata fisadi mroho yeyote. Richmond ikama ilipita TIC ilipita kwa Ole Naiko mtu wa karibu wa EL kwa sababu alikua anakaimu nafasi wakati wa kuelekea kwa kampeni za uchaguzi 2005.
Kama hili hujafanya umakini kulijua basi hata hilo la ofisi ya ubunge/uspika tuna mashaka nalo kwani kredibiliti na uchambuzi wako usiokua na upande unatia mashaka tayari kwa hoja yako ya hapo juu