Ipo hivi, kwanza kabisa Hii fact ni maalum tuu kwa flagship(high end) Maana ukiliweka hili katika ujumla wake, hamna anayemkuta Samsung kwa technology ya ku compress battery kubwa mpaka sasa kwa hizi kampuni kubwa zote unazozisikia, hapa nazungumzia Iphone, Oppo, infinix, nokia, tecno, Xiaomi, n.k
Samsung M51 na F62, wote hawa wana 7000mAh(# doesn't lie endurance rating za gsmarena zinaongea, hivyo hawadanganyi), ni mara mbili ya hio uliyotaja, kwenye hizi kampuni kubwa hakuna aliyefikia hapo, wengi wamegota kwenye 6000mAh.
Kwahio unakuja kugundua sio kwamba hawawezi, ila kuna sababu.
1. Sifa ya flagship ili ipendwe inaanzia kwenye muonekano, na huwezi zungumzia muonekano huu bila ku consider unene wa simu, battery kubwa inahitaji space kubwa, na kwa sababu ukubwa wa simu kwa juu(urefu×upana) ni limited kwa size ya kioo unachotaka kutumia, basi sehemu itakayo kua affected ni Unene, matokeo yake ni simu kubwa ambayo ni ngumu ku i manage mkononi.
NOTE : Moja ya sifa ya flagship ni display kubwa, sasa imagine simu kama Note 20 ultra yenye kioo cha inch 7 kasoro nukta halafu iwe nene, utaishikaje?
2. Uzito, ieleweke battery ni hardware, hivyo size inavyokua kubwa uzito unaongezeka, Sasahivi kampuni nyingi za simu zinashindana katika kuhakikisha wanatengeneza simu nyepesi isimkere mtumiaji hata akiweka mfukoni, na tukumbeke ushindani huo ni wa kwenye hizi high end sababu ndio zinaipa kampuni sifa na kutambulisha technologia yao mpya, au ushaona Samsung A02s inashindanishwa kwenye battle la simu na kampuni nyingne? Hapana.
Flagship zinatengenezwa na material/hardware bora/imara mfano tempered glass, Aluminium flame n.k, hivi vyote vinaongeza uzito kwenye simu, while low end wanatumia ma plasti kote,
Hivyo basi kuachana tuu na battery simu inakua nzito tayari, sasa ukibugi kwenye battery unashangaa unatengeneza simu ya nusu kilo na ushee, sitanii (ulefone power Armor 13, ina nusu kilo), sasa hii uite flagship? Angalia Samsung S21 ultra mwenye 5000mAh pamoja na battery ndogo kulinganisha na M51 lakini material yake mazito yameifanya imzidi Uzito M51 yenye 7000mAh iliyotengenezwa kwa plastic, lakini ukija upande wa pili M51 amemzidi note 20 ultra unene tena kwa mbali tuu(ana 9.5mm, amenakiza 0.5mm agonge 1cm), sababu ni nini? Utagundua ni battery, kitu ambacho Samsung hawezi kubali kwenye flagship zake.
3.Space, Ieleweke ukisikia simu ina kitu hiki na hiki cha ziada, jamani hivi vitu vinaanzia kwenye hardware, hivyo vinahitaji space kuvi accommodate, flagship hua inaongezewa features mfano heart rate sensor, wireless charging, camera bora, speaker bora, au hio note 10 uliyoitaja, inahitaji space zaidi kwa ajili ya ku accommodate ile S-pen, ambayo kimahesabu hio pen tuu imechukua sehemu ya 900mAh, umeona sasa? n.k n.k, hivi vitu vyote vinahitaji space, hivyo kufanya eneo la battery kua finyu..
4. Businesses strategies, battery ni hitaji kubwa sana kwenye simuu, kuna watu hilo tuu ndilo kipaumbele chake kikubwa kwenye simu, hivyo atatafuta lets Say M31s sababu ya battery then ametosheka, Mwingne anahitaji vyote, atanunua flagship kupata features bora, halafu atachukua yenye battery kubwa itakayomsaidia kwenye bussy days, hiki ni kitu cha kawaida, sema tuu wengine pengine kutokana na hali za kiuchumi hio option inaangukia kwenye viswaswadu.
Mfano binafsi nina Samsung kubwa, halafu nina kijisamsung Duos cha Batani kwa ajili ya backup, tayari mpaka hapo ni deal kwa kampuni.
5. Upgrade, Kila Mwaka Kampuni zinatoa flagship mpya yenye features mpya za kuvutia, binadamu hata kama alichonacho kinamtosha, ila ana shauku ya kupata kikubwa zaidi kadiri ya mda. Hivyo hata kama wana uwezo wa kuweka 7000mAh leo hii, hataweka ila ataanzia kwenye 3500mAh ili mwakani akiweka 4000mAh bado uone kuna improvements, mfano note 10 plus ana 4100mAh na note 20 ultra ana 4500mAh, tayari kuna watu wanashawishika kununua note 20 ultra kwa sababu hio,
Sasa mtu alinunua S21 ultra kwa sababu ya battery ya 5000mAh, leo hii ukamletea s22 ultra ina 5000mAh tena atanunua ya nini?..
Mtazamo wangu,
Nunua Simu ambayo utaitumia bila kua na mawazo ya kuangalua battery percentage, Simu ambayo Bila kuzima Data basi inakufikisha mda wako wa kulala huku ikiwa imebaki na charge incase ya dharura ya umeme, binafsi sikumbuki ni lini nilizima data kwenye simu yangu, naperuzi kokote na kwa kujiyosheleza ila jioni nachezea 50%-40%, Sikumbuki ni lini niliwasha simu yangu, mana sijawa na sababu ya kuizima na haijawahi zima sababu ya charge.
Moja ya stress ambazo ni kero kwenye simu basi ni charge, simu ni yako lakini unaitumia kwa kuichungulia,
Sitaki kuzungumizia wale rafiki zangu wa,
please wait.....
Unfortunately Jamiiforums has stoped...
Camera is not responding.......
Twitter has crashed......
Naweza nisababishe watu wagombane na keyboard huko.