Simu yoyote ya android inaweza ingia hawa malware ila tatizo la mediatek ni kwamba ni rahisi kuiroot, inakuwa na bugs ambazo application inaweza kujipa root.
Application ikishajipa root inajibadili kutoka application ya kawaida hadi system app. Nikisema system app namaanisha application zinazokuja na simu kama vile sms, gallery, calender etc. Hivyo hata ukieka ant virus inakuwa haisaidii sababu ant virus haiwezi kugusa hizo system apps inascan tu app unazodownload, kifupi malware anakuwa na nguvu kushinda hata hio ant virus.
Sababu pia ni system app hata ukifanya hard reset haisaidii sababu system apps hazifutiki ukifanya hard reset.
Ndio maana mtaani simu za mediatek kama huawei za bei rahisi, Tecno, Itel etc zina matatizo sana unaskia mtu analalamika simu yangu inaonyesha video za ngono, mwengine anakwambia nikiwasha data yanakuja matangazo etc.
Kibaya zaidi ni kwamba simu nyingi za mediatek hazipati updates, hasa hasa monthly updates za security toka google, hivyo hata kama kuna patch ya kusolve hivi vitu hizo simu hazipati