Ni sawa lakini kwa matumizi yapi haswa?? speed ya internet? kuandika message au kupiga na kupokea simu? hembu niambie kwa basic uses kama hizo ni nini hasa tofauti ya speed. ukizingatia hapa kwetu mtandao ni sawa sawa
mkuu mambo ni mengi sana nitajaribu kulist vichache.
1. hayo mambo madogo madogo ukiyafanya mengi kwa pamoja kitaalamu wanaita multitasking yanahitaji simu iwe na nguvu. mfano mtu ana insta, facebook, snapchat, twitter, wechat, telegram na app nyengine za kijamii kibao na zote anazifungua kwa wakati mmoja, simu ndogo itachemka ila simu kubwa yenye ram kubwa na cpu ya maana itaweza kuzifungua vizuri tu.
2. speed ya internet haihusiani na perfomace, ila simu kubwa huwa na modem nzuri zaidi kuanzia mobile data vitu kama 3G na 4G hadi kwenye wifi.
-simu isio na 4G haiwezi kuwa na speed nzuri
-simu yenye 4G ya kizamani haiwezi kupata Speed ya 4G ya kisasa kama vile LTE Advance ya TTCL.
3. zipo apps kubwa na nzito ambazo huwezi kuzirun kwenye simu yako ndogo, mfano dolphin emulator, video editors kama cyberlink, video converters mbalimbali, games kubwa kubwa etc. unaweza jaribu ku convert hata video ya dakika 10 kwenye simu yako ndogo uone itachukua muda gani.
4. simu kubwa huwa za kwanza kupata technology za kisasa, dunia hii kila siku kuna technology kubwa, mfano hii technology ya sasa ya virtual reality huwezi ipata kwenye kisimu cha laki mbili tatu, utaikuta kwenye simu kubwa zenye perfomance kubwa, zipo technology nyingi nyingi nyengine kama vile x265 (HEVC), vp9 na codecs nyengine za video, sote tunaenda youtube na kuangalia video moja na quality moja ila wewe unatumia mb 600 mimi natumia mb 400 sababu kifaa changu kinakubali codec mpya za video na chako hakikubali.
5.pia simu kubwa hufanya mambo kwa upesi zaidi, storage perfomance yake ni kubwa, unakuta wote tunafungua app moja yako inatumia sekunde 1 yangu robo sekunde, unaweza ukaona utofauti mdogo ila in long run mimi nitakamilisha mambo mengi na naweza kusave mda mwingi zaidi.
6. hata kwenye kupiga na kupokea simu mwenye simu nzuri ni likely akawa anaskia anaempigia na kupigiwa vizuri japo sio mara zote, zipo pia simu ndogo zinaskia vizuri.