Nazani Msumbiji kuna wilaya inaitwa GAZA,kama ile KAZA ya palestina!!Mkuu mbuzi mzee inamaana Samora Machel alitokea wilaya ya Gaza?, Great sons of Africa.
Kuna tetesi kuwa Marehemu Samara Machel alikula njama ya kumuua mwasisi wa chama cha FRELIMO marehemu Richard Mondrane,ambaye alikuwa anatarajiwa kuwa rais wa kwanza wa msumbiji.Marehemu aliuwawa kwa bomu la kutegwa,lililokuwa limetegwa kwenye barua aliyotumia jijini Dar es salaam,na alizikwa kwenye makaburi ya kinondoni!kwa wale waliofika jiji la maputo kuna monuments mbili moja ya Samora machel na Richard Mondrane kama kumbukumbu ya mashujaa wa Msumbiji!!
Huyu katikati ni nani? Nimemsahau kabisa jina:
Huyo wa katikati ni Raisi wa zamani wa Namibia, ndugu Sam Nujoma wa chama cha SWAPO. Naye kaishi Morogoro na Mbeya wakati wa kupigania Uhuru wa nchi zao. Wakati anastaafu urais miaka michache iliyopita alikuja kuaga na kushukuru Tanzania kwa msaada aliopata.
Sijui kama hawa atawakumbuka
Idimi, ukisoma ukurasa wa pili, utakuta ujumbe niliandika kuwa ni Sam Nujoma. Nilikuwa nimemsahau kabisa jina.
Safari, huyu wa kushoto sura naifahamu kabisa ila jina pia sikumbuki. Huyo wa kulia nakiri kuwa simfahamu. Ila kwa kuangalia picha, nahisi ndiyo Richard Mondrane.
Huyu Mondrane na yeye ni kuwa nilikuwa namsikia tu ila nilikuwa sijawahi kumuona. Ndiyo matatizo ya kuwa kijijini miaka hiyo maana nilikuwa nasikiliza tu Radio Tanzania bila kuwaona hao watu. Nakumbuka hadi leo kumsikiliza Samora Machel akiimba zile nyimbo mbili maarufu zilizokuwa zikiimbwa hadi jeshini (JKT) kama "Ife ana Frelimo zowona?!?!" Siku hiyo nililala almost asubuhi maana sikuweza kabisa kukatiza hayo matangazo. Asubuhi nilipomuambia Baba habari nzima, hakuamini kuwa na udogo wangu wote huo nimekaa hadi asubuhi.
Sawa Mkuu, nakupa MJI na nitajie hao jamaa ni NANI?
Hivi Mugabe huwa anakula nini??...manake naona yuko vile vile miaka nenda rudi
Machel's Tupolev 134A Samora Machel was dead along with 33 of the 44 ...
[
Hongereni CDM kwa mavazi yenye taswira ya ukombozi!