GE2025 Samia: Vijana tukalinde Amani, tusikubali kushawishiwa kuharibu Amani yetu

GE2025 Samia: Vijana tukalinde Amani, tusikubali kushawishiwa kuharibu Amani yetu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni leo Oktoba 12, 2025, Runzewe, Mkoa wa Geita amesema;

"Nchi inayoitwa JMT iko moja peke yake, na toka nchi hii imeundwa tumepigana vita moja tu na Idi Amin na kwasababu alituchokoza, lakini miaka nchi hii iko salama"



Soma
 
Ila Maza umewasahau sana vijana , ndio maana Wana hasira
 
Wanahubiri amani huku wameshika mapanga, mtu anikumbushe huo wimbo.
 
Amani ya ili ninyi mle mema ya nchi kwa utulivu amani bila haki huo ni utulivu ni amani kibudu tu, aman ya watawala kutoheshimu raia, haki za raia, kuonea raia, kuua na kupoteza wakosoaji, amani ya majitu kugawana pesa za umma, amani ya kusfiasfia ccm na maviongoz majizi jizi, amani ya viongoz kurithisha madaraka kwa watoto wenu, amani ya ccm mtawale kwa nguvu haiwezekani..mamamaeee wallah MUNGU ANAWAONA.
 
Pole yake. Kwa mtazamo wangu namuona kama Kiongozi ambaye atapata changamoto nyingi sana kwa sababu tu ya kupotoshwa na kushauriwa vibaya na wahuni wachache walio mzunguka.

Yeye alitakiwa ndani ya miaka minne ya utawala wake alio upata kwa bahati nasibu, kuandaa tu mazingira ya uchaguzi huru, halafu angewaachia watu wapambane. Sasa amelewa madaraka, hata anako kwenda sidhani kama anakufahamu!

Kuruhusu makundi haram ya utekaji, mauaji, wizi, ubadhirifu, nk. Vimemshushia kwa sehemu kubwa heshima aliyokuwa nayo hapo kabla.
 
Kosa kubwa la Samia ni kunyamazia utekaji na uuaji unaoendelea, imethibitisha ni mhusika mkuu.

Hakuna mtanzania atakayekubali hili, umwage damu za watu, wakubali kuongozwa nawe. Haiwezekani
 
Ni kama mama Samia kaacha kuhuburi ilani ya CCM nayeye kaingia kuhubiri maandamano
katishika na maandamano mpaka anaacha kuhubiri ilani ya chama chake, huu mtindo umewashika hata wale wagombea shikizi nao wanahubiri amani kana kwamba nchi haina amani? Wametishika na maandamano hewa! Je wakikutana na maandamano halisi hali itakuaje?
 
Nakuhakikishia, kwa uoga uliokuwepo sasa kwa hao waliojuu, wakiona tu kikundi kimeanza kuandamana au tairi limechomwa moto barabarani watakimbia kama kuku.
 
Back
Top Bottom