Salva Rweyemamu SIYO Mtanzania(?)

Salva Rweyemamu SIYO Mtanzania(?)

Salva Rweyemamu position is untenable until utata wa uraia wake uwekwe wazi hatuwezi kuendelea na ubabaishaji na viini macho vya kila siku lazima ahojiwe na ukweli ujulikane.

....who are you? ...na uache kuota mchana wewe
 
Baada ya kupitia thread hii yote nimegundua yafuatayo:

Mosi, watanzania hatuelewi umuhimu wa uraia, kama jinsi ambavyo nchi nyingine zina thamini uraia. Dunia nzima hakuna mahali mtu ambaye si raia anaweza kupewa kazi serikalini na hasa kama kazi yenyewe ni sensitive. Ikulu ni sehemu nyeti sana, na mtu aliye kwenye post kama ambayo amepewa Salva ana uwezo wa ku-access info nyingi sana ili aweze kujua namna ya kujenga na kutetea hoja zake pindi anapokutana na wana media ambao wako makini. Kama Ikulu ikishindwa kumpa info za kutosha maana yake ni kwamba atashindwa kuwasiliana na wana habari na hilo litaifanya serikaali iwe na wakati mgumu zaidi. Kwa hiyo hoja ya uraia mpaka hapo naona bado iko valid. Una imani gani na mtu ambaye huna uhakika na uraia wake, je akitumia hizo info kwa nia mbaya utamlaumu nani? Kazi aliyopewa Salva huwezi kulingaanisha na kazi za kubeba box za UK au US ambako illegal immigrant yeyote anaweza kuifanya na wala kusiwe na shida yoyote.

Mbili, hoja ya uraia imekuwa ikiibuka pindi linapokuja swala la maslahi. Kumbukumbu yangu inasema kwamba Jenerali Twaha Ulimwengu alikuwa kwenye timu ya kampeni ya BWM, lakini pindi alipoanza kuikosoa serikali, rungu la uraia lilimshukia. Kwa maneno mengine serikali ilijua wazi kwamba the guy was not a citizen lakini wakaja kuibua hoja hiyo ili kummaliza. Marehemu Nabwa aliwahi kuwa mwandishi wa Makamu wa Rais, alipokuja kuwa mwiba mkali kwa serikali ya Mapinduzi ya Zenji akashukiwa na rungu la uraia. Salim ili kukatwa makali ya ushindani kwenye kinyang'anyiro cha urais, alishukiwa na rungu la uarabu ambao una uhusiano mkubwa sana na swala la uraia. The list goes on ... swali, kama Salva aliweza kumdunda Salim na rungu la uraia ili akose urais kwanini na yeye asidundwe? Dhambi ya kula nyama ya binadam ukishaitenda itakuandama kila utakapoenda, Salva alianzisha mwenyewe na sasa ni zamu yake kushughuliwa, sioni kama ni dhambi kujadili uraia wake na hasa ikizingatiwa kwamba ni yeye ndie aliyeanzisha haya mambo na sioni sababu ya watu kumtetea. (Mtazamo wangu kwenye hili ni kwamba linatumiwa kimakosa, objective si ulinzi na usalama bali ni kukomoana na kumalizana, lakini kwa kuwa nae alicheza mchezo mchafu ngoja aonje machungu ya mchezo huo)!

Tatu, kuna watu wamekuja na swali la why now? Ni sawa na illegal immigrant akiamua kujilipua na kufanya kazi za kubeba box, hakuna mtu atakayemfuatilia. Lakini siku huyo illegal immigrant akionekana anapewa kazi sensitive ya akina Tony Snow, hakuna Mmarekani hata mmoja ambaye atakubaliana na hilo. Kama mtu ana doubt na uraia wa Salva ni bora aseme mapema ili achunguzwe na ijulikane wazi kwamba jamaa siyo raia. Kuuliza kwamba kwanini watu hawakuhoji hapo awali, jibu lake ni rahisi sana. Tulikuwa tunamuona kama mbeba box tu wa Bongo na kuwepo kwake Tanzania hakuwezi kuhatarisha usalama wa nchi. Kwa hiyo watu wameuliza uraia baada ya kuona amekwaa post nyeti ambayo ikishikwa na foreigner ni hatari maana huwezi kujua kama ana uchungu na Tanzania. Dr. Laurian Rutayisire alifundisha Mlimani miaka mingi mpaka akawa Associate Prof lakini alipoitwa kurudi Rwanda alienda mbio bila hata kuaga. Ukichunguza sana utakuta kwamba alisomeshwa na hela ya Tanzania, yet akashindwa kulipa fadhila kwa watanzania waliotoa kodi ya yeye kusoma. Je, mtu huyo ana uchungu gani na Tanzania? Suppose huyo mtu angekuwa alishafanya kazi Ikulu ya Tanzania, ungekuwa na uhakika gani kwamba siku ikitokea Kigali na Dar wametofautiana hawezi kutoa nyeti za Ikulu ya Dar? Tusiwe na mtazamo finyu wa ku-analyze mambo halafu siku yakija kulipuka ndipo tunaanza kulia lia kwamba ilikuwaje na huku watu walikuwa wamekaa kimya.

Makala ya gazeti la The East African iko wazi, Kamanzi amesema ana ndugu wengi wako Bongo, je tunajua wako ofisi zipi? Siku Kamanzi akihitaji info kutoka Ikulu yetu na kama kuna ndugu yake Ikulu unadhani atashindwa kuzipata? Let us be serious kwenye haya mambo na siyo kutanguliza mawazo kwamba mtu akija na hoja ya uraia basi inalenga kwenye wivu au kumharibia mtu kitumbua chake!
 
Inji yetu imetekwa na maharamia wa ndani na nje chini ya mwavuli wa SISIEMU.

Kazi yetu kubwa ni kujenga nguvu ya kuiengua SISIEMU madarakani.

Huko SISIEMU hakuna hata mtu mmoja anaye tufaa.

Wote wameoza,wamejipakaza ufisadi, wananuka damu za watoto na kina mama waliokufa kwa gharama ya ufahari Vilanja wetu.

SISIEMU must GO
 
...tatizo hakuna mtu hapa anabisha Tanzania kujali uraia na kuulinda,tatizo ni watu wanatumia system amabayo haipo kuleta majungu na kusingiziana na ukweli watakaokuwa victim ni wale ambao wakisingiziwa sio raia na system ndio wataadhibiwa hata kama ni uwongo na ukiwa upande wa mtandao hata kama sio raia utapeta tuu,hapa inabidi tujadili umuhimu wa kuweka system ya nchi kujua raia zake sio finger pointing tuu kwa wale tusiowapenda kwa wivu au sababu zetu wenyewe
 
Koba,
Nakubaliana na wazo lako la kuanzisha system ya nchi kujua raia wake. Tatizo langu liko sehemu moja, je tuna uwezo huo? Mwaka juzi wabunge wa CUF walikiri kuwasaidia wasomali kupata diplomatic passport na wale akina mama waliingia Ujerumani bila mgogoro na kuukana uraia wa Tanzania ili wapewe status ya ukimbizi. Leo hii ukienda kwa msajiri wa vizazi na vifo unapata cheti cha kuzaliwa ambacho ni kibali cha kupata ganda la kusafiria bila maswali kutoka pale Uhamiaji. Nchi yenyewe ile haina mwenyewe, ni kama nchi ya wahamiaji. Kumbuka kasheshe za Rwanda na Burundi miaka ya 1970 mwanzoni ilipelekea wahutu na watutsi kuingia Tanzania kwa wingi. Pia wako wahamiaji kutoka Uganda. Ukienda Mbeya wilaya ya Kyela kuna watu wa Malawi kibao. Ukienda Arusha akina Kinana wako kibao. Sasa unaanzia wapi kuwachambua watu ambao si raia?

Tulishachelewa kufanya hiyo kazi na ndiyo maana siku hizi swala la uraia limeishakuwa ni rungu la kumalizana kisiasa na kulipizana kisasi. Serikali nina uhakika inawafahamu wote ambao si raia hata wale walio na nyadhifa kubwa lakini ndiyo kama ulivyosema kwamba ukikubaliana na matakwa yao hakuna atakayekugusa lakini siku ukiwageuka ndiyo utaambiwa wewe si raia. Serikali ndiyo iliyoanzisha huo mchezo wa kunyoosheana kidole cha uraia na walifanya hivyo na wakafanikiwa.
 
Ninasikitika kweli inapotokea kwamba tunawashambulia watu ambao
wamezaliwa Tanzania au kukaa Tanzania maisha yao yote, na kuitumikia nchi yetu si ajabu vizuri kuliko sisi wengine, wakipata madaraka tunaanza kusema sio raia.

Watu ambao hata hawajui historia ya dunia wanakuja na statements ambazo hazina ukweli kabisa kuhalalisha madai yao.

Angalia Jews kokote walikoenda baada ya vita kuu ya pili na jinsi
walivyofanikiwa kupata madaraka sehemu walikokwenda mpaka wengine kuwa marais. Lakini sisi tunaanza kuwabagua Watanzania wenzetu, Waafrika wenzetu, kwa visingizio eti wametoka Rwanda, Burundi, Msumbiji, SA nk. Eti hakuna nchi duniani ambayo mtu asiye raia anaweza kupata sensitive position, what do you mean by asiye raia? Kama una maana mtu kama Rweyemamu, basi uko wrong. Hata rais wa ufaransa sasa ni mtu wa kuja, aliyekuwa kiongozi wa Tories UK ni mtu wa kuja nk.

Tunaacha kuhangaika na issue ambayo ndio tatizo la TZ, je mtu aliyepewa kazi ana uwezo? I don't care Rweyemamu wazazi wake walitoka wapi, kama amekaa Tanzania muda wote huo, yeye ni Mtanzania na niko tayari kumpa kura yangu hata kama anataka urais, bora awe na sifa na uwezo.

Ndio watu hao hao waliokuwa wanasema Salim sio Mtanzania. Jamani kueni and start thinking BIG. Hizi petty politics hazitufikishi kokote.
 
Hili suala ni nyeti lakini na kama tutaamua kuwa makini na kuangalia msingi wa jambo lenyewe ufumbuzi wake ni rahisi sana.

Bado nipo na mtazamo wa Mwanakijiji, assuming Salva alizaliwa Tanzania, swali linakuja je wazazi wake walikuwa watanzania kwa ama kwa kuzaliwa au kwa kuandikishwa kabla ya Uhuru wa Tanganyika 1961.

Tukishapata ufumbuzi wa uraia wa wazazi then tumepata jibu la uraia wa Salva.

Kwangu mimi haya mengine naona kama ni beating around the bush tu.
 
Hili suala ni nyeti lakini na kama tutaamua kuwa makini na kuangalia msingi wa jambo lenyewe ufumbuzi wake ni rahisi sana.

Bado nipo na mtazamo wa Mwanakijiji, assuming Salva alizaliwa Tanzania, swali linakuja je wazazi wake walikuwa watanzania kwa ama kwa kuzaliwa au kwa kuandikishwa kabla ya Uhuru wa Tanganyika 1961.

Tukishapata ufumbuzi wa uraia wa wazazi then tumepata jibu la uraia wa Salva.

Kwangu mimi haya mengine naona kama ni beating around the bush tu.


Masatu,

Sheria ya uraia inasema:
1. Kama mtu alizaliwa TZ kabla ya mwaka 1964
basi ni raia wa Tanzania. Naamini Rweyemamu alizaliwa Tanzania kabla ya siku Tanzania ilipozaliwa.

2. Kama mtu alizaliwa nje ya TZ na alikuwa TZ wakati wa muungano kama raia wa kujiandikisha, ataendelea kuwa raia wa Tanzania. Hapa ndio kwenye matatizo. Watanzania gani wa vijijini kwenye miaka hiyo ambao walikuwa wanajua kuna kujiandikisha ili uwe raia? Mtu alikuwa akihamia, anakaribishwa, anapewa shamba na kufanywa ni miongoni mwetu. Wajanja ndio wanatumia kipengere hiki ili kuwachafulia na kuwaharibia watu wengine. Wanaoathirika na ujinga huu ni watu wa mipakani na watu wa kawaida. Wajanja wanajua sheria zote na wanapata uraia hata kama ni kwa forgery.

Hili kundi ndilo pia watoto wao waliozaliwa baada ya muungano wanakuwa affected na sheria hii.
 
Mtanzania,

Ninakubaliana na wewe kwa asilimia nyingi sana kwenye hoja yako. Lakini kuna sehemu ndogo tu ambayo tunatofautiana. Mifano yako wa Jews ambao wamehamia kwenye nchi nyingine na kwenda kushika nyadhafa kubwa kubwa ninaikubali kabisa. Nadhani kitu unachokikosa kwenye hoja yako ni kimoja, hao wahamiaji walifuata taratibu zote za nchi na kuhakikisha wamepata uraia wao kwa njia halali. Mwanakijiji amesema swala hapa ni dogo sana, kama jamaa wazazi wake hawakuwa raia je alipofikisha miaka 18 alienda kuukana uraia wa wazazi wake? Maana kwa sheria ya Tanzania ukiwa na wazazi ambao siyo raia unakuwa na uraia wa nchi mbili ambao kwa Tanzania haukubaliki na wanakutaka ukifikisha 18 yrs uende kuukana uraia wa nchi moja na ubaki wa nchi utakayochagua. Nadhani kama mtu akifuata huo utaratibu hakuna ambaye atakuja na hoja nyingine. Tuna raia wangapi ambao walikana uraia wa wazazi wao na leo hii wanapeta Bongo kwa nyadhifa kubwa kubwa.

Swala la kwamba you don't care uraia wa mgombea urais hiyo ni opinion ya kwako. Almost nchi zote dunia nzima katiba za nchi zao zinataka Rais awe raia wa nchi husika. Kwa hiyo kigezo cha uraia bado kitamfunga huyo mgombea wako kama akiwa si raia wa hiyo nchi. Katiba ya CCM inataka mwanachama wa CCM awe raia wa Tanzania, kugombea ujumbe wa nyumba 10 lazima uwe raia, kugombea udiwani na ubunge lazima uwe raia wa Tanzania. Ina maana hao walioweka hiyo condition ni wajinga au hawana akili???

Mwisho kabisa umetoa hoja nzito sana, kwamba tunatakiwa kujadili issues za muhimu mfano uwezo wa mteuliwa kama anaiweza hiyo kazi. Kwa kweli hapo naona ndiyo tunamtoa knock out huyo jamaa (Salva), kama aliweza kutunga vya kutunga na kumzushia Salim kwamba si raia leo hii amepewa Ukurugenzi wa Habari Ikulu tutakuwaje na uhakika kwamba hataendelea kuwazushia wale wote ambao wanaonekana kuwa tofauti na serikali iliyomteua kuwa Ikulu? Kama kwenye kampeni alidiriki kumwaga sumu mbaya ya mgombea kwamba si raia akiwa ni mwandishi wa habari wa habari tu huko mtaani, je leo akiwa Ikulu hatawadanganya watanzania mambo ya uongo kuhusu baadhi ya watu? Au CREDIBILITY yake iko kwenye ku-spin na kuhandishi habari? Kigezo cha kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari Ikulu ni nini? Au ni zawadi ya kazi "nzuri" aliyofanya ya ku-spin news wakati wa mchakato wa kuteua mgombea wa urais kupitia CCM na hatimaye kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005?
 
...tatizo hakuna mtu hapa anabisha Tanzania kujali uraia na kuulinda,tatizo ni watu wanatumia system amabayo haipo kuleta majungu na kusingiziana na ukweli watakaokuwa victim ni wale ambao wakisingiziwa sio raia na system ndio wataadhibiwa hata kama ni uwongo na ukiwa upande wa mtandao hata kama sio raia utapeta tuu,hapa inabidi tujadili umuhimu wa kuweka system ya nchi kujua raia zake sio finger pointing tuu kwa wale tusiowapenda kwa wivu au sababu zetu wenyewe

Kwa maneno mengine unasema kuwa tusifanya background checks kisa itaonekana ni majungu?
 
Umefika wakati sasa sisi ktk JF hapa tuanze kuongoza haya mapambano, kila ambae mwenye uraia "tata" atungikwe hapa na ajadiliwe.

Sipingi kwa appointment ya Salva bali ningependa kuwe nma mjadala mpna na wa wazi kuhusu masuala haya ya uraia na kuweke precedence nzuri huko mbeleni.

Hivi hawa wabunge wetu ( walau hawa wa upinzani ) hawawezi kuwasha huu moto na sisi hapa tukawa ni ni catalyst ya kutia chachandu na kuwapa taarifa muhimu na nyeti ili hili jambo likaamsha mjadal wa kitaifa na hatimae serikali ikapeleka muswada na kuweka kuziba mapengo ya kinachonekana kama ni udhaifi ktk sheria yetu ya uraia?
 
Kimsingi issue ni kuwa kilichomuingiza huko Rweyemamu ni fitna. Fitna aliyoifanya ni kumchafua Salim, kwa hiyo ameingia kutokana na kumchafua Salim, kwa hiyo mjadala wote huu unatokana na fitna aliyofanya kwa Salim.
 
Kimsingi issue ni kuwa kilichomuingiza huko Rweyemamu ni fitna. Fitna aliyoifanya ni kumchafua Salim, kwa hiyo ameingia kutokana na kumchafua Salim, kwa hiyo mjadala wote huu unatokana na fitna aliyofanya kwa Salim.

Kwahiyo sasa fitna ina haunt mwenyewe... mwiba unapoingia ndio palepale unapotokea...
 
Kwahiyo sasa fitna ina haunt mwenyewe... mwiba unapoingia ndio palepale unapotokea...

Kweli kabisa, unajua siasa za namna hii si nzuri. Unaweza kufikiria Salva atakuwa kwenye hali gani kama inatokea by any chance Salima anakuwa rais, unajua jamaa huenda anadhani JK atakuwa rais wa maisha na atamwekea mwamvuli kwa kipindi chake chote. Amefanya mchezo wa hatari sana, unaweza ukajaona impact yake baadaye sana
 
Angola 15626 (USD 0.50)
Botswana 15626 (P3.00)
Ghana 15626 (50GhP)
Kenya 15626 (Saf: Kes 30, Celtel: Kes 35)
Malawi 15626 (MK 56.00)
Namibia 15626 (N$ 3.00)
Nigeria 34626 (N75)
South Africa 34626 (R2.00)
Tanzania 15726 (Tsh 600)
Uganda UTL: 5626
Celtel: 0903015626
MTN: 15626 (U700)
Zambia 15626 (ZK2100)
Zimbabwe 15626 (Z$1,160)

Non Participating Countries can use these codes:


Gambia 15626 (15 Dal)
Sierra Leone 15626 (1550 SL L)
Liberia 15626 (50 US cents)
Togo 15626 (CFA240)
Swaziland 15626 (50 US cents)

Kwa nini baada ya kukosa Senior citizen Makini kama Mwal.JKNyerere(RIP) Thamani ya sarafu yetu imechoka mbaya sana tu? Je Mwalimu wakati anawasomesha hawa warundi na wanyarwanda +Waganda alijua wataitumikia nchi yetu, je walimuogopa sana Mwal.Je yaweza kuwa wamechangia sana kudidimiza uchumi wetu?Manake Rwanda uchumi wake sasa nafikiri UNAPAA...
 
ni kazi sana kumtetea salva.........nilipenda kujua the fact kwamba kuna raia halali wa TZ ambao si weusi na kuna raia haramu ambao ni weusi. Salva kilicho mfika ni "auto-destruction"..............kama akishindwa ku-prove uraia wake basi iwe kama ilivyokuwa kwa wengine aidha cheerleading kwenye sidelines au booted out kabisaa ya uwanja!!!!.
Tatizo langu kubwa ni kuwa haya mambo ya "monday morning quarterbacking" si mazuri, tusiwe tuna subiri after the facts ndio tuanze kupiga kelele.
 
Jambo jingine CCM wenyewe wangeweza kulirahisisha sana. Watunge sheria inayowatambua watoto wote waliozaliwa katika Tanganyika Huru na Jamhuri ya Zanzibar na wale ambao walizaliwa katika Tanzania iliyoungana kuwa ni raia hata kama wazazi wao siyo raia. Ukiondoa wawakilishi wa Kibalozi mtu yeyote ambaye watoto wake wanazaliwa katika ardhi ya Tanzania, basi watoto hao ni Watanzania...
 
Back
Top Bottom