Salva Rweyemamu SIYO Mtanzania(?)

Salva Rweyemamu SIYO Mtanzania(?)

Ngabu,
hayo ma-vyeti ya kuzaliwa bongo si unaenda tu pale uzazi na vifo una nunua na kuweka mwaka unaotaka wewe kuwa umezaliwa.........jamaa ana point anataka ku-make, tumsubiri tuone ni nini hasa hiyo point. Kwani msee mwkjj anatembea kwenye very thin line inayotenganisha watu wawili wenye tatizo la uraia ktk almost same circumstances.........interesting!!!!!!!

wrong assumption.. hawa watu hawana matatizo ya uraia! at least not yet. Kati ya hawa wawili Richa la kwake ni la rangi siyo uraia. Walioohoji uraia wa Richa walifanya hivyo kwa misingi ya rangi, na ninakumbuka vizuri nilipouliza kama angekuwa mtu mweusi ambaye amezaliwa Tanzania lakini wazazi wake siyo raia wa Tanzania kama wangemfurahia ashinde taji hilo? Hakuna aliyenijibu.

Sikujua kuna suala la Salva. Sasa hadi hivi sasa bado sijui kama anatatizo la uraia, ila kile "kipimo walichompimia Salim, Jenerali, yule mwandishi wa Zanzibar n.k" kiko tayari kuanza kupimiwa kwao.. watakitumia?
 
Nyani the questions themselves are not necessary, the implications of the answers are.
 
Mwanakijiji nadhani nitapunguza speed. Ukweli it is really stupid kuanza kutafutana uraia. I would not care uraia wa Ulimwengu kwa sababu there is alot he had offerd to the nation, so is Salim, so is Kinana, lakini what about Salva? Unajua hizi siasa ni wao wenyewe wamezileta ili kuwasideline watu wanaofaa kwa maslahi yao binafsi, nadhani haitakuwa dhambi, kama kisu alichotumia kumkata mwenzie asiye na hatia, kimkate mwenyewe.
 
Nilipokuwa nahitimisha makala yangu kuhusu "Hoyce Temu na Wabaguzi Mamboleo" nilisema hivi:

Hadi pale watakapotambua kuwa raia wote wa Tanzania ni sawa na wanastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wao. Vinginevyo tutaanza kuwabagua wao kwa ubaguzi wao hadi tuwe na taifa la wabaguzi wenye kubaguana ambao kila kukicha wanatafuta wa kumbagua.

Pointi niliyoiweka hapo, ndiyo msingi wa kuangalia suala hili. Hatuwezi kuapply sheria selectively, kuwa mkosoaji wa serikali au mwenye nyota yenye kung'aa uraia wake uhojiwe lakini inapokuja kwa walio mashabiki wa serikali uraia wao usihojiwe. Hasa inapokuja nafasi nyeti. Hata hivyo mada hii wala si nzito sana, ila majibu yake ndiyo yanatisha.

Hivi kama ikioneshwa pasipo shaka kuwa Salva, Balozi X na Katibu Mkuu wa Wizara Y, ni raia wa nchi jirani je tusiwavue majukumu hayo hadi watakapopata uraia wa Tanzania? Au kwa vile "Afrika ni moja" basi haja ya kuisimamia sheria ya Uraia ambao wao wenyewe CCM waliipitisha 1995 isimamishwe kwa muda.
 
Hivi ni nchi gani ulimwenguni inayoweza kuwapa nafasi nyeti watu wasiokuwa raia wake? Hapa ndipo mambo ya background check come into play...

tukumbuke..."ubaguzi haukomi"...(sijui na hii ni M.M. original...)...lol

to tell the truth i've had it with this 'huyu siyo raia'..'huyu sio mzawa'..na 'huyu sio mweusi' bs. it is so outdated and it is not us. and now i wonder when did we become like this?
 
mie raia wa Marekani tuone mtanifanya nini? nakuja bongo kila wakati na kura ya nilipiga vilevile
 
kama unakuja tu bongo kwa sababu ya kupiga kura nadhani hapo ndugu utaumia mwenyewe, cuz a single vote dont count and dont mean nothing esp, in tz sio kama nchi zilizoendelea a single vote is a bit deal, hushangai katika kila uchaguzi utaambiwa kura laki kadhaa zimeharibika, pengine yako ilikuwa moja wapo kijana, hahahaa !
 
Baada ya kufikiri kwa makini sana. Ninadhani kama tunataka tupunguze tatizo la maziwa matatu, basi Rwanda na Burundi ziunganishwe na Tanzania. Watu wa Rwanda na Burundi wengi sana wanajisikia nyumbani wawapo Tanzania, tatizo lao huja tu washakirudi Burundi au Rwanda. Kwa vile mipaka ya mwaka 1884 iliziweka nchi hizi zote pamoja kama Germany East Africa, nadhani muungano wa 1964 ulikosea sana kuwaacha pembeni Rwanda na Burundi. Nina imani kuwa tukishaondoa ile mipaka na kuwaweka chini ya mamlaka moja inayotoka Dodoma, basi Bujumbura na Kigali hakutakuwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tena.

Hayo mawazo yangu tu, inawezekana yakawa pumba.
 
...subiri wadau watakavyokushambulia.
 
Wajameni,
Wakati tunaendelea kukata majamboz hapa lakini, vipi picha ya mwenzetu Shy je yeye ni mkoloni???????? kwi kwi kwi
Anyway tuendelee
 
mtu kama si mtanzania yeye si mtanzania tu!....hapaswi kushika madaraka......

kwa mujibu wa sheria mtanzania anajuulikana ni nani.......lazima tufuate sheria kwenye hili na mengine, sio kuchagua kupiga kelele sheria hazifuatwi kumbe kwa vile zile zinamanufaa na sisis tu!
 
Mwalimu.. hilo ni wazo ambalo bila ya shaka siku moja litahitajika na kuna wakati hasa baada ya 1994 genocide, niliona kuwa next time upuuzi wa "wahutu na watutsi" unaanza kunukia tena.. Tanzania itajitendea vyema kama itaingia kwenye nchi hizo na kuziannex ili kuzuia mauaji ya kimbari kama yale.

Lakini kwenye tatizo la uraia kuna jambo moja jepesi sana ambalo linaweza kufanywa hata kesho tukipenda. Kubadili sheria ambayo haiwatambui watu waliozaliwa Tanzania baada ya 1961 na 1964 ambao wazazi wao hawakuwa raia wa Tanzania au Zanzibar kabla ya muda huo. Tunachoweza kufanya ni kuhalalisha watu wote waliozaliwa katika ardhi ya Tanganyika Huru na Jamhuri ya Zanzibar na wale waliozaliwa baada ya Muungano hata kama wazazi wao hawakuwa raia wa nchi hizo. Hii ingeondoa kabisa mambo ya kina Ulimwengu au haya ya sasa ya Rweyemamu.
 
Sioni tatizo kubwa hapo, wengine wengi tu wapo marekani na wana uraia huko, tunawajua na wakija huku tunakuwa nao tu kama kawaida.

FD
 
You are moving too fast.. wale wanaouliza kwanini leo.. wangeuliza kwanini Salim baada ya kuitumikia nchi kwa muda wote huo na kuwa Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa OAU.. aje kuulizwa nasaba yake na utii wake kwa nchi? Kwanini Jenerali Ulimwengu baada ya kuitumikia nchi vizuri kama Mkuu wa Wilaya na Mjumbe wa NEC aje aulizwe uraia wake pale alipoanza kuikosoa serikali? Point yangu ni point ya wao walioiweka there is no cutting line.. kama waliweza kuhoji uhalali wa "mwarabu" kuwa mgombea wa nafasi ya juu ya uongozi katika nchi yetu, iweje leo washtuke watu wanapohoji uhalali wa mtu mdogo kama Salva kupewa nafasi nyeti kama hiyo Ikulu?

Swali, Salva Rweyemamu alizaliwa wapi? na wazazi wake walizaliwa wapi, je ni raia?

Wamezaliwa sehemu inaitwa Ahabirabo, Kimbugu, Izigo, Muleba, Kagera, Tanzania.
 
Mi naomba kujibiwa: Why now? kwa nini Suala la Salva lizuke sasa hivi baada ya kupata appointment ya muungwana????????? Kwani kabla ya hapo alikuwa anaishi sayari ya mars au pluto? I can see immense level of hatred and character assasin, maana huyu Salva, mpaka wengine wamesema ndo aliharibu ndoto ya SAS kuwa rais. Granted. Mbona hawakumreport Immigration????? Kama kweli hakuwa raia? au kwa vile alikuwa inconsequential? hakuwa na madaraka? (lakini mtu anayeweza kuinfluence kiongozi wa nchi awe nani, nadhani ni heavy weight)

Kwa nini humu JF thread za uraia wa watu zinazuka pale tuu wanapokuwa wamepata either appointment au fame fulani kwenye nchi yetu? mfano Richa Miss TZ (of all people), Salva, Ikulu, Bandora Ubalozi nk????? Hapana mi naona kuna unafiki na double standards humu kwa walio wengi. Mbona sijawahi kusikia mwenyekiti wakijiji au mtu yeyote asiye na madaraka akifuatiliwa uraia wake? atleast hata humu JF? Mi nina walakini na ndo maana naamini kwamba, TANZANIA IMEJAA WASANII KUANZIA KWA WANANCHI MPAKA VIONGOZI WETU. Ni wachache saaaana walio sincere katika wayafanyayo. TUNAPENDA SANA SHORTCUT katika maisha yetu.

Ni dhambi kubwa kumhukumu au kuhoji uraia wa mtu kisa anatokea, Mbinga, Rukwa, Tarime, Kasulu, Ngara au Karagwe kwa sababu hizi sehemu ziko mipakani. Siamini kwamba mtu ni mtz halisi kwa vile anatokea Singida, Pwani na Tabora. This is pure nonsense Na hapa ndo tutamalizana kwa sababu tunapenda siasa za victimization. Wonder what happened to the politics of hope za watu fulani humu JF! Sikatai kuhoji na kushughulikia illigal immigrants, ila zoezi liwe fair and balanced lisitarget watu solely kwa kuangalia wanakotoka au pua zao.

Hili la Salva lisingezuka kama jamaa angekuwa anatokea Singida au kwingeneko. We jiulize leo Mungai anaitwa Mkikuyu, ila kwa vile anatokea Iringa no body has ever questioned that, Iam sure ingekuwa tofauti kama huyu Mungai angekuwa anatokea Kagera, Kigoma au Mara. Huu ni upuuzi na hapa ndo wengi hatutakubaliana na hizi sisa za opportunism katika nchi yetu. Au jiuliuze kama Burundi na Rwanda zingekuwa prosperous countries, nani angeuliza uraia wa watz wa mipakani huko kaskazini? lakini kwa sababu wana shida, vita nk. wanaoishi karibu ya nchi hizi wanaonekana kuwa wale wale. Sasa baadhi yenu mkijidai kwamba mnaheshimu na kudumisha fikra za mwalimu naona ni UNAFIKI, Nyerere couldnt be privy to these kind of stupid assumptions and politics za kuvictimize watu kwa kuangalia pua au sura ya mtu. Na ndo maana tumeweza kuwa taifa huru na la amani. The old man knew what he was doing.

selfishness and love can never go together. Kama kweli tumeamua kufanya hili zoezi, basi tulifanye kwa maslahi ya nchi na siyo kwa maslahi ya kuumizana na wivu kwa baadhi ya wenzetu. Na wote tujue, unaweza kumchagua rafiki, ila hutamchagua jirani, wote duniania hakuna aliyechagua azaliwe wapi na kwa nani, it was geographical accident, sasa kwa nini Byamungu, Mugisha, Saitoti au Odinga au Mwanawasa waumizwe kisa wana majina yanayofanana na raia wa nchi jirani? Its all nonsense na kwa hili we are going no where.
 
Nakuunga mkono mpambanaji. Naona hapa kumeanza kutokea uozo na unalelewa pole pole. Naanza kuona hisia za ubaguzi wa kikabila hapa, huku watu wakijifanya wanatetea utaifa kwa hoja za kitoto. Lilipozuka hili la Salva nilishangaa kwani yeye haingii madarakani bali anapewa kazi kama wengine tu, tena wenye uraia wa kununua na wasio na uzalendo hata kidogo. Sijui kama wasimamizi wa JF wanaona huu ni mjadala wenye afya kwa Watz au nao wameamua kupanda mbegu na kuinyunyizia maji....watavuna matunda yake. Watu wenyewe wanaomjadili Salva hawamjui, na wala hawana hakika na uraia wao lakini wamaeamu kuleta hisia chafu na kuwashirikisha wenzao wenye fikra hizo hizo hapa hapa JF. We're doomed!

Ningewaelewa kama aliyeanzisha mada hii angesema anajua moja, mbili, tatu kuhusu utata wa uraia wa Salva, halafu akataka aelezwe inakuwaje mtu huyo huyo amekuwa karibu na viongozi wetu kwa muda mrefu...Sasa tuna Watanzania milioni 40. Tutakuwa tunamtilia shaka kila anayetueliwa na kuhoji kama ni raia? What is our driving force? Kuzaliwa mikoa ya mpakani?

Icadon hapo juu kaeleza jinsi anavyomfahamu Salva. Hakuna hata mmoja analeta data hapa, ni porojo porojo na porojo. Ni upumbavu na mawazo ya kichawichawi yaliyoimaliza Rwanda na yaliyoitesa Afrika Kusini kwa miongo mingi. Ujinga mtupu!
 
Mh! Tunakoelekea, Mungu ndiye anajua!

Hivi, ngoja niulize. Aliyeanzisha mada hii alisukumwa na nini? Na ameanza lini kupata msukumo huo? Alihisije utata wa uraia wa Salva kulingana na sheria ya uraia ya Tanzania? Na kwanini salva? Na kwanini sasa?

Mimi nilidhani watu wanamjadili Salva kama mwandishi wa habari, uwezo na udhaifu wake kitaaluma. Hiki ni kitu alichonacho Salva. Hili la uraia tumelichomoa wapi?

Maswali 6. Majibu?
 
Nchi nyingi duniani wana vitambulisho pengine baadhi ya WTZ hawaelewi ndio sababu wanaona huu ni ubaguzi. serikali ilipoamua kuwe na vitambulisho ni katika kuona keki ya taifa inagawanywa kwa haki kwa raia wake wote.

Hatuwezi kuwanyima WTZ haki yao ya kujiamulia mambo yao na kuwaendekeza wageni ati tusiwe wabaguzi. Kama Salva ni Mtanzania then well and good. Lakini kama sio Mtanzania ni lazima tujiulize kulikoni? Leo hii MTZ hawezi kupewa baadhi ya nafasi katika mataifa mengine kama yeye sio raia wa nchi hizo. Alipochaguliwa Dr. Migiro UN nchi za jirani walikuja juu na kuuliza kwa nini TZ inapata kazi nyingi kule kwenye umoja wa mataifa hawakujali kama ni mweusi au la walikuwa na shauku kama raia wao angechaguliwa. Leo hii hakuna hata anayeonyesha uzalendo wakati shillingi yetu inaposhuka value kila kukicha na kuna tetesi kuwa wengi kwenye maamuzi sio WTZ, Je huo uchungu wataupata wapi? Sio hawa ambao baada ya kufaidi wanakwenda kwao na kutucheka ujinga?

Mfano hai upo kwenye artical ya kwanza ya the East African Je, tuendelee kulifumbia macho hili?
 
Back
Top Bottom