Salute kwa waliosoma PCB/PCM

Salute kwa waliosoma PCB/PCM

Aisee...kipind nipo o-level nilikuwa na mapenzi na PCM lkn nilibadili gear hewani nikaenda zangu PCB huku basic mathematics naijua ipasavyo.....
Na mimi nilikuwa na ndoto kama zako.
Siku wakati tunajaza fomu za kuchagua shule za A-level, nilijishauri sana kivipi nitaweza kuchaguliwa shule maalum kama Mzumbe, Kibaha, Ilboru na Tabora boys kwa urahisi.

Nikaangalia historia ya nyuma kidogo kwa waliotutangulia nikabaini ili uweze kuchagulia hizo shule kwa ufaulu wa kawaida ni vyema uchague PCB, ndio nikaichagua PCB ya kwanza, lengo likiwa nikichaguliwa hizo shule nitaenda kubadili niende PCM.

Lakini baada ya selection kutoka nikawa sijafanikiwa kuchagulia miongoni mwa hizo shule.

Pia nikashauriwa kutobadili comb, nikakubali kusoma PCB kwa shule niliyochaguliwa maana niliambiwa utakuwa Daktari na mimi nikaridhia.

Nilikomaa kufa na kupona, nikafaulu na kufurahi sana, nikafanya Application za MD nikagonga mwamba japo nioibahatika kuchaguliwa kozi nyingine ya Afya
Kuifaham basic mathematics kulinisaidia kuweza kusolve maswal ya Physics hakika kwangu physics nilikuwa chai kwangu....pia mapenz yangu ya mathematics kuliniboost kuiweza BAM...
Pia mimi Phyz niliipenda sana na nilitumia muda mwingi na gharama kubwa kuisoma kuliko masomo mengine, huku wenzangu wa PCB walikomaa na Bios na Chemia.

O-level nilisoma Addition Maths kwa sababu nilikuwa na ndoto za kusoma PCM, hilo lilinisaidia sana kusoma BAM na nilikuwa naifaulu sana kwa kupata A huku nikowa naisoma kwa siku chache kabla ya mtihani
Huyu chemistry tulikuwa tunaita kamastarehe....biology skupata SHIDA kuikariri maana hapo ni mwendo Wa kukariri tu BS....
Chemia nilikuwa naisogeza bila shida ila Bios kukariri ilisaidia japo nilikuwa natumia muda mwingi kuikariri
Kwangu mim niliamin kuwa PCB wengi hawawezi Physics hivyo muda mwingi nilisoma hilo somo.....hakika nilifurahia kusoma physics....
Na mimi pia hivyo hivyo nilikomaa na Phyz na ndio iliyoniokoa kwa ufaulu wa kuridhisha maana Bios sikufaulu vizuri kama wengine wabobezi wa PCB kwa kukomaa na Bios na Chemia
 
View attachment 848895lol

hao waliosoma hizo kombi walikua wanasoma sana jamani,

Leo nataka kujua was it worth?LOL

naomba mliosoma hizi kombi msaidie watoto wafanye right choice..

ningependa kujua;ulisoma nini kati ya hizo?matarajio yako yalikua nini? umeachieve?nini changamoto ulizokumbana nazo mpaka umefikia hapo?

currently huku mtaani,PCB ni madaktari na PCM ni ma engineer

nauliza hivi kwa nini mnatoka kusoma kozi ngumu advance then mnachagua masomo magumu Zaidi huko chuo???😀😀😀😀😀😀😀😀

je wanafanya hivi kwa kuwa hamna choices nyingi?
Nlikuwa sipendi kuwa H_kunani nikachagua PCM physics ikanitia kidole, iyo satuti hata hainihusu, iyo mnayooita historia ya sayanyi wanasoma lakini hawagundui kitu poa tu, maana fundi mkuu Max plank aliambiwa na mwalimu wake enzi izo anasoma university of Munich aachane na Physics eti vitu vyote vimeshagunduliwa, Akasema yeye hasomi eti agundue chochote bali anafurahia kusoma vitu vilivogunduliwa tayari. Lakini akagundua mambo kibao na akawa father of Quantum mechanics. Suala la kugundua ni la mmojammoja
 
Kipindi namaliza O level pale Azaboi. Kichwani kwangu hakukuwa na combination niliyokuwa naiwaza zaidi ya PCM.

Nakumbuka kwenye machaguo nilijaza PCM mara tatu. Headmaster akawa anatugombeza tuliojaza kama mimi, akisema inaweza kutuletea tabu endapo matokeo yakija tofauti na matarajio.

My answer was "there's nothing else that can replace PCM"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aisee mim nilisomaga PCM ndanda boys. matarajio yangu yalikua kua engineer ila huwez amin sasa hivi mimi ni auditor (CPA).usiniulize ilikuaje maan hata mm mwenyewe sijielew ilikuaje had nikawa huku.. DESTINY YAKO ANAIJUA MUNGU WEW PAMBANA TU UTAJUA MBELE YA SAFARI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa O'level nilipenda sana niwe Civil Engineer ndo chanzo cha kusoma PCM na nzuri zaidi hesabu ilikua inapanda vizuri, so nikasonga nayo mwisho nilikuja kusoma Mining Engineering [Lengo nilipenda jina lianze kuandikwa Eng. GREGO].

Kiukweli msuli wa PCM hasa advance sio wa kitoto huku mnyama Mechanics, Inorganic chemisty, Organic chemistry

Ila hakuna somo rahisi kama Hesabu sio kama maHistory mwl anaweza akaamua akunyime marks maksudi maana jibu sio moja kama hesabu njia nyingi jibu ni moja. History nilisoma kwa fimbo chini ya Academic Master [Nilikua nakula Miswaki ya kutosha nikifaulu sana ni D]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom