Salute kwa waliosoma PCB/PCM

Salute kwa waliosoma PCB/PCM

ni vizuri kusikia kutoka kwa wazoefu waliosoma hayo madude lol..kudos mkuu…mie nawalaumu hao waliopewa dhamana ya elimu, walitakiwa wa UPDATE syllabus kila baada ya muda,ili iendane na mabadiliko ya mazingira. Pia hawa hawa waliopewa dhamana ya elimu walitakiwa waichagize serikali iinvest kwenye fani za uhandisi,ila wizara ya elimu kama wizara nyingine ziko passive tu..wangepropose serikalini vitu vinavyotakiwa vifanyike nadhani wangepata baraka za Magu……………...
Creativity ni level za chini sana bongo,hakuna kufikiri nje ya box,mtu akishapata kitengo ni kitambi tu anakifanyia kazi
 
Kuna ukweli mmoja nilikutana nao katika soma soma yangu,hasa kwa vijana waliopita CoET. Hapa kwenye kipengele cha malengo,vijana wengi walikuwa hawasomi kwa malengo kwa maana kusoma fani ambazo walikuwa wanazipenda,wengi walikuwa wanasoma fani kulingana na matokeo yao,hapa hasa wadau waliosoma Telecom,au CIT kwa pale UDSM.

Huu utaratibu wa kusoma kwa kufuata matokeo umewaathiri vijana wengi sana na bila shaka wengi wanajuta.

Hii ilikuwa kila alie pata one kali anakimbilia Telecom au CIT,naimani zama Telecom na CIT zimekwisha siku hizi,zimerudi zile zama ukweli na umama wa fani za uhandisi. Hapa najua watanielewa wachache sana.

Ila Secular kizungumkuti sana....

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni kuwa elimu yetu iko theoretical sana kuanzia level za chini,na inamuandaa mwanafunzi kufaulu mtihani,si kupambana na changamoto za maisha,sasa mtu mpaka ajielewe anataka nini unakuta ni too late
 
mie naona hamna choices nyingi,watoto wachague course wenye interests nazo . lazima kuwe varieties,kuna course kibao zinazoweza kuwa added kwenye mitala ya secondary na chuo..sio lazima kuingia kwenye u engineer makozi magumu,lol kuna environmental science,Psychology,Accounting,Business ,Photography etc Masomo yanayoweza kusomwa kwenye shule za secondary na baadae chuo

Hizo kozi "rahisi" ulizozitaja zinataka nchi iliyoshiba, nchi iliyokwisha jitosheleza kwenye kekta muhimu kama uhandisi na utabibu. kuna badhi ya mambo ili nchi ifanikiwe inabidi iwe na wataalamu wake wenyewe. Mfano huwezi kukodisha maaskari (madaktari) wakati wa vita, nchi inabidi itumie wasomi wake kutibu wanajeshi walioumia.
 
o-level nilisoma sayansi matokeo yametoka masomo ya arts yote nina alama D na masomo ya sayansi nikapata F yote!!! nilidata hadi bi mkubwa akawa hana amani kama yeye ndo kafeli
ushauri ukaja nikasome madiploma ya arts kwa D zangu uku wengine wakisema sayansi uwezi hata kidogo, umetuletea miswaki minne... lakini nafsi aikukukubali kabisa. nilikuwa bado najiona mimi ni doctor na moyoni nashudiwa kabisa sayansi naiweza
nilikaachini na almashauri yangu ya kichwa, nikatoa tamko nalisiti masomo manne yote ya sanyansi yani bios, chemia, phys na maths,
nyumbani wakasema wewe huna akili ya kusoma masomo ya sayansi kasome cozi yoyote kwa D zako za arts lakini sio kulisiti, humna uwezo na sayansi na niliambiwa kama utaki kusoma cozi za arts kaa nyumbani saidia kazi na swala la kusoma lifute kwenye maisha yako
niligoma kuchuku ushauri wa cozi za arts hadi bi mkubwa akasema weww utakuwa na maisha ya shida sana, kwa jinsi alivokuwa anaongea nilihisi hii itakuwa ni laana lakini mwisho nikomaa na malengo yangu kulisit
nikaanza halakati za kulisiti msuli mnene nyumbani masomo manne yote ya sayansi nilikuwa nasoma usiku nilisoma kwa interest sana haya masomo na nilikuwa naelewa sana, nasoma mpaka mama alikuwa akanza kuelewa kuwa nipo serious
cha ajabu siku namuomba mama ela ya kulipia masomo ya kulisiti necta akagoma kunipa kabisa yani lakin mimi nilikua naendelea na kusoma tena usiku mnene, zikabaki siku tatu usajili naecta kufungwa na mama ajanipa hela nakumbuka niilingia chumbani kwa mama mw
mweyewe nikachukua kama laki na nusu kwenye mkoba wake nikaenda kulipia kituo cha kufanyia mtihani kimya kimya lisiti nikatulia nazo
mama alikuwa anashangaa tu! hela ajatoa mtu anakomaa kusoma usiku, hadi siku ya mtihani inafika asubuhi sisemi naenda wapi mpaka namaliza mitihani yote mama akujua kitu
wakaiti nasubiri matokeo ya kulisit siku mama akawa analalama kuna mtu kaiba hela yake na mimi nikajitokeza kuw ndo mimi nilichukua nikamuonesha na lisiti za kulipia pepa akagomba lakini mwisho akatulia
matokeo yanatoka nikapiga B B chemia, bios, phys maths nikapiga C
A- level nikachukua PCB, msuli wa PCB si kitoto lakini Mungu hakuniacha nikapiga one ya tisa, sasa nivyoandika hapa mimi ni doctor na mama ananikubali sana jembe lake kwa misimamo yangu
masomo ya sayansi sio magumu kama ukiwa unayasoma kwa kuyakubali kutoka moyoni. wanasema kama unataka kujua kitu kipende kwanza alafu kifanye kwa mapendo yote, lazima ukiweze tu

NOTE: kama unaamini unaweza kufanya jambo lolote ata kama linaonekana ni la kichizi kwa kiasi gani wewe endelea kuamini na onesha juhudi kwenye jambo lako hakika utafanikiwa tu
Hahahaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom