Salum Mwalimu ukitoka mahabusu achana na CHADEMA

Salum Mwalimu ukitoka mahabusu achana na CHADEMA

Na leo pia nichukue fursa kumwomba Mh. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba na Naibu wake Hamad Masauni hawa makomredi wetu waungwana kuwaomba waingilie kati dhamana ya kijana mwenzetu Salum Mwalimu Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ametelekezwa na viongozi wa chama hicho huko Bariadi Mkoani Simiyu.

Akisota mahabusu bila kupata dhamana, kama mfurukutwa wa chama makini Chama Cha Mapinduzi iliyona viongozi vijana makini kama akina Antony Mtaka RC Simiyu nadhani watanzania wameshaona viongozi wa CDM walivyowabaguzi kwa kumtelekeza kijana huyu huku bariadi.

Nasema wamemtelekeza kwasababu sasa ni wiki ya pili Salum Mwalimu anasota rumande bila ht kiongozi yoyote wa ngazi ya kitaifa au hat wabunge wa CDM kwenda kumtia moyo. Tumeowaona juzi Lowassa na Mbowe walivyoitwa Central Polisi wabunge wa CDM na wafuasi wao walivyohamasishana kuelekea polisi kati huku wakijipiga selfie na kurusha mtandaoni.

Mtakumbuka Tundu Lissu alipokamatwa Singida na kuletwa Dar tuliona viongozi wakuu wa chama hicho wakiongozwa na Mbowe walivyohamasishana kuwahi polisi hadi mahakamani lakini kwa Salum Mwalimu watu wamekaa kimya wako busy na vikao vya kugawana ruzuku huku kiongozi mwenzeo hakisota rumande, juzijuzi Godbless Lema alipokamatwa Arusha tuliyoona hamshahamsha ya kwenda kumtoa na wakili akatumiwa hivi hawa mawakili wa CDM wanafanya kazi kwa upendeleo?

Mbona simsikii Kibatala, Mh James Millya wala Malya hata Lissu wakienda Bariadi au kwakuwa Bariadi hakuna TV? Nadhani atakuwa amejifunza kuanzisha mchezo na walaghai niwaombe tena viongozi wangu makini Mwigulu, Mtaka Antony na Masauni muingilie kati kumsaidia kijana mwenzenu akae nje akiendelea na kesi yake.
 
Angekamatwa Mbowe mawakili wote wa chama wangehamia huko......huu usaliti na ubaguzi ndani ya CDM sijui utaisha lini.
 
hahahahaha akitoka hapo atakuwa amejifunza kitu, sasa hivi hao mawakili uliowataja watakuwa busy kuhakikisha mwenyekiti wao anafungua kesi mahakamani ya kudaiwa kodi na NHC, watakwenda kumtetea Mbowe asitolewe kwenye jengo na ikiwezekana hilo deni NHC walifute "wasimsumbue" mteja wao hahahahaha
 
Ukweli mtupu,kwanza ni katibu mkuu wa chadema Zanzibar yeye kutwa kujenga chama bara na kuacha kushawishi wazanzibari....wanamtumia kwenda sehemu ngumu ili aumizwe arusha na moshi wapo wateule.Hakika umefika wakati ajitathimini.

Huyo Salum Mwalimu ni Naibu katibu mkuu wa CHADEMA wa nchi huru ya Zanzbar ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya 2010 ni nchi kamili yenye raisi wake na mamlaka kamili.Kilichompeleka huko Simiyu nchi isiyo yake ni kitu gani? Kama sio kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.Tanzania bara ina Naibu katibu wake mkuu ambaye ni John Mnyika .Sasa huyo Naibu katibu mkuu wa Zanzibar kimemleta nini wakati Naibu katibu mkuu CHADEMA bara Mheshimiwa Mnyika hajawahi kwenda nchi ya Zanzibar kuendesha siasa za ndani za ile nchi.

Analeta uchochezi kwenye nchi isiyo yake
 
Ukweli mtupu,kwanza ni katibu mkuu wa chadema Zanzibar yeye kutwa kujenga chama bara na kuacha kushawishi wazanzibari....wanamtumia kwenda sehemu ngumu ili aumizwe arusha na moshi wapo wateule.Hakika umefika wakati ajitathimini.
Namshangaa sana nilitarajia atakwenda Zanzibar kushinikiza maandamano ya UKUTA yeye ameng'ang'ana na Tanganyika.
 
Huyo Salum Mwalimu ni Naibu katibu mkuu wa CHADEMA wa nchi huru ya Zanzbar ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya 2010 ni nchi kamili yenye raisi wake na mamlaka kamili.Kilichompeleka huko Bariadi nchi isiyo yake ni kitu gani? Kama sio kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.Tanzania bara ina Naibu katibu wake mkuu ambaye ni John Mnyika .Sasa huyo Naibu katibu mkuu wa Zanzibar kimemleta nini wakati Naibu katibu mkuu CHADEMA bara Mheshimiwa Mnyika hajawahi kwenda nchi ya Zanzibar kuendesha siasa za ndani za ile nchi.

Analeta uchochezi kwenye nchi isiyo yake
Hapo ndio Lumumba huwa siwaelewi,vinyonga sana halafu hamna kumbukumbu!Mlipopeleka vifaru na jeshi kutoka bara hamkuwa mnaingilia nchi yenye mamlaka yake kamili wakati ule wa uchaguzi wa marudio?
 
Basi aende ccm kwa waliomweka ndani!Kuna zaidi ya viongozi 38 wa CDM wako ndani mpaka sasa!Hii yote ni kutokana na ujinga na ulimbukeni wa wenye dola!Unamuwekaje mtu rumande muda wote huo bila kumfikisha mahakamani?Hii ni aibu kwa jeshi la mwendokasi!
Waache wakae kwani ni mapapai yale?
 
Huyo Salum Mwalimu ni Naibu katibu mkuu wa CHADEMA wa nchi huru ya Zanzbar ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya 2010 ni nchi kamili yenye raisi wake na mamlaka kamili.Kilichompeleka huko Bariadi nchi isiyo yake ni kitu gani? Kama sio kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.Tanzania bara ina Naibu katibu wake mkuu ambaye ni John Mnyika .Sasa huyo Naibu katibu mkuu wa Zanzibar kimemleta nini wakati Naibu katibu mkuu CHADEMA bara Mheshimiwa Mnyika hajawahi kwenda nchi ya Zanzibar kuendesha siasa za ndani za ile nchi.

Analeta uchochezi kwenye nchi isiyo yake
Halafu msiongee kama wapiga ramli,wekeni sheria ambayo inamzuia mzanzibari kufanya siasa bara!Katiba ya jamhuri ya muungano imetoa uhuru kwa "mtanzania" kukusanyika ndani ya ardhi yake bila kujali mipaka!
 
Kwani ameteuliwa kushika wadhifa wapi? Unaposema Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar una maana gani?
 
Mlipopeleka vifaru na jeshi kutoka bara hamkuwa mnaingilia nchi yenye mamlaka yake kamili wakati ule wa uchaguzi wa marudio?

Majeshi na vifaru viko zanzibar siku zote hata saa hii.Nenda utawakuta wako vikosini mwao hapo zanzibar hakuna kipindi wanakuwa hawapo zanzibar, acha uongo.
 
Mtoa post auche uongo, salum mwalimu yupo simiyu sio geita.
 
Kwani ameteuliwa kushika wadhifa wapi? Unaposema Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar una maana gani?
Kwahiyo wazanzibar wengine kufanya mkutano bara ruksa ila yeye kwakuwa ni naibu katibu mkuu zanzibar basi marufuku!lumumba mnaua bongo za vijana kufikiri
 
Majeshi na vifaru viko zanzibar siku zote hata saa hii.Nenda utawakuta wako vikosini mwao hapo zanzibar hakuna kipindi wanakuwa hawapo zanzibar, acha uongo.
Unadhani hatukuona vifaa vikishushwa kutoka kwenye meli vikitokea bara?
 
Back
Top Bottom