Salum Mwalimu ukitoka mahabusu achana na CHADEMA

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,416
Wadau, amani iwe kwenu.

Ni zaidi ya Siku tano sasa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu anasota Mahabusu huko Geita. Kwa cheo alichonacho ndani ya CHADEMA sikutegemea kama angeweza kusota rumande muda wote huu.

Wanachofanya CHADEMA si fair kabisa. Wanabagua watu wengine na kuwapendelea wengine. Alipokamatwa Tundu Lissu, CHADEMA wote walishtuka na viongozi wakuu wote walihakikisha kuwa anatolewa mahabusu mapema iwezekanavyo. Hali hiyo ilisababisha utetezi wa Tundu Lissu kusomwa nyakati za Usiku na kesi ya kuomba dhamana imevunja rekodi kwa kusikilizwa muda mrefu zaidi ambapo ilichukua masaa 5. Hatimaye Tundu Lissu kaachiwa kwa dhamana.

Godbless Lema, naye amesota rumande kwa siku tatu tu. viongozi wote wa CHADEMA akiwemo Mbowe walishtuka kukamatwa kwa Lema na walifanya kila jitihada kuhakikisha anapata dhamana na kweli wakafanikiwa.

Leo Salum Mwalimu maskini anasota rumande kwa makosa ya Freeman Mbowe. Ni Mbowe ndiye aliyempa kazi Kanda ya Ziwa ya kunadi UKUTA.

Nafahamu kuwa kinachomuweka Salum Mwalimu CHADEMA ni uwezo wake wa kujielewa awapo jukwaani. Ila hatakiwi kwa vile si MWENZAO! Hafanani na wao na ndio maana akikamatwa wao wanaona sawa tu.

Nimshauri sana Mdogo wangu Salum Mwalimu. Ni Bora akarejea Channel Ten kuendelea na kazi yake ya habari kuliko kuhangaika na CHADEMA. Kama itabidi afanye siasa basi ni bora akajiunga na ama CUF au hata ADC. Kuendelea kuwa kiongozi wa CHADEMA ni kupoteza muda.
 
Ukweli mtupu,kwanza ni katibu mkuu wa chadema Zanzibar yeye kutwa kujenga chama bara na kuacha kushawishi wazanzibari....wanamtumia kwenda sehemu ngumu ili aumizwe arusha na moshi wapo wateule.Hakika umefika wakati ajitathimini.
 
Sahihi kabisa Mkuu. Mbowe anatafuta sababu ya kumuumiza Salum Mwalimu
 
Basi aende ccm kwa waliomweka ndani!Kuna zaidi ya viongozi 38 wa CDM wako ndani mpaka sasa!Hii yote ni kutokana na ujinga na ulimbukeni wa wenye dola!Unamuwekaje mtu rumande muda wote huo bila kumfikisha mahakamani?Hii ni aibu kwa jeshi la mwendokasi!
 
Nani amtake huyo Salum Mwalimu
 
Kwa hiyo ccm mzima Magufuli tu ndio anachukia ufisadi au maana mpaka aanze lini wakati MTU mmemtuhumu mwizi kwa nini kama chama chenu mnachukia ufisadi msimpeleke polisi achunguzwe au takukuru
Hii ni Serikali ya Magufuli na CCM mwenyekiti wake ni Magufuli
 
duuuuh we jamaa ni mchonganishi aseee na inaonekana unaroho ya ubaguzi imekutawala
 
Lizaboni hii post ni ya kichochezi unawachonganisha chadema kwa nini lakini hakuna mengine ya kupost humu jf?

Sawa kutoa ushauri lakini ushauri mwingine.

nanukuu toka kwa viongozi wa ccm huu ulioufanya ni Uchochezi mwisho wa kunukuu.
 
Wewe hujawahi kuteswa /kukasilishwa na wazazi wako, ndugu wa karibu for that matter au hata CCM yako, uliwakana? Jibu ulilonalo rohoni ndilo jibu la hoja yako!
 
Back
Top Bottom