Askari Muoga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 6,112
- 4,663
Kwa iyo ulitaka chadema wavamie kituo cha polisi wakamtoe
Kwa hyo polisi huwa wanawasubiri vionvozi wa juu ili watoe dhamana? Nauliza tuu
Mbona hata wewe kipindi fulani umewahi kuwa sehemu ya upotoshaji [yale ambayo ulikuwa unayaamini tofauti na sisi tulivyokuwa tunayaona[tafsiri yako upotoshaji ni mtizamo tofauti kuhusu jambo husika]Yanaheshimiwa mawazo yenye ukweli au yanayokaribiana na ukweli na sio upotoshwaji wa makusudi unaojenga chuki. Wanaopiga porojo humu wameenda Simiyu wakahakikisha kua CHADEMA hawamjali Mwalimu? Mbona tuliofika Simiyu tupo hapa tutavumilia vipi uongo wa mchana kweupe?
Tumaini Makene?Kumekuwepo na upotoshwaji wa makusudi unaofannywa humu kuhusu Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar Kamanda Salum Mwalimu, watu hawa kwa makusudi makubwa na unafki wanajifanya kumuonea huruma kamanda Mwalimu aliyewekwa ndani Kwa makosa ambayo hayaeleweki zaidi ya kuyaita kuwa ni uchochezi. Baadhi ya watu leo wanajifanya kumshauri Kamanda Mwalimu aachane na CHADEMA eti chama hakimjali. Tangu lini wapinzani wakubwa wa CHADEMA wakawatakia mema viongozi wao?
Kamanda Mwalimu ni miongoni mwa maofisa wa ngazi ya juu kabisa wa CHADEMA na ni moja ya vijana wasomi na makini wanaotegemewa na Chama pande zote mbili za bara na visiwani. Kwa msiokua na kumbumbu ni kwamba Kamanda mwalimu ndiye aliaminiwa na Chama sambamba na Makamanda wengine mpaka kufikia kukabidhiwa mikoba ya aliyekua katibu mkuu wa zamani wa CHADEMA Dr. Slaa kukaimu nafasi hiyo kwa muda mpaka kufikia kumpata Katibu Mkuu mpya wa Chama Dr. Mashinji. Chama kinafahamu na kinatambua umuhimu wa huyu mtu muda wote. Fisi wanaosubiria mkono wa binadamu uanguke waendelee kupiga kelele zao na kujipotezea muda.
Wanaofanya propaganda za kitoto na za kizamani humu watambue kwamba Wanasheria wa Chama, viongozi wa juu wa chama, viongozi wa kanda, mikoa wilaya na kata wanafanya jitihada za juu chini kushughulikia suala hilo kuhakikisha kamanda Mwalimu anatoka haraka ingawa kuna sababu za makusudi zisizolingana na kosa analodaiwa kufanya ili kuendelea kumrudisha rumande. Ni matumaini yetu kuwa haki inatendeka na ni muhimu kuziipuuza propaganda zinazofanywa na watu wachache mitandaoni wasiokua na kazi za kufanya.
Mwisho ni kuwaomba makamanda wetu wawe wavumilivu, wapuuze propaganda za wanafki wachache wanajifanya kuwaonea viongozi CHADEMA huku nyoyo zao zimejaa unafiki. Masuala ya wanachadema yanashughulikiwa na wana chadema wenyewe na sio kwa huruma za wanafki na wapinzani wa CHADEMA. Ifike mahali kila mtu atumie muda wake kulijenga taifa pamoja na Chama chake na sio kushindia kwenye pooltable na mitandaoni kuandika propaganda zisizokua na faida yeyote zaidi ya kuchochea chuki na ubaguzi.
Na huyu naye utakuta mishipa ya shingo imemtoka eti anapigania demokrasia!MAHANJU
Hili ni Jamvi la 'WHO DARS TO SPEAK' wewe umekuwa ukiandika mengi na sisi tumekuwa tukiyaheshimu mawazo yako na ni hivyo sioni sawa kwa wewe kuanza kuwakwaza wanajamvi wenzako ambao wanamawazo tofauti kwa kuwaita kuwa ni 'Genge' Waache watiririke kama vile wewe unavyotiririka
Mbona arusha yule jamaa alichangishiwa pesa ya kulipa faini? Hivi muweka Hazina wa chama mkoa ni muhimu kuliko naibu Katibu mkuu? Chama cha kibaguziUngeanza kuwalaumu waliomkamata,halafu jiulize alifanya kosa gani kubwa mpaka anyimwe dhamana?
Acha unafiki na ubaguzi wa kikabila.
Mbona arusha yule jamaa alichangishiwa pesa ya kulipa faini? Hivi muweka Hazina wa chama mkoa ni muhimu kuliko naibu Katibu mkuu? Chama cha kibaguzi
Kuishi kwingi kuona mengi!kheee mbona mazito..
Kwasababu mnasema nyinyi hii si kauli ya kichochezi,h aya maneno angeongelewa mwenyekiti wa kile chama kitukufu yangekuwa ya kichochezi na ungepanda kizimbani,msipende kupost ili mpate likes tuu,sasa mwalimu amenyimwa dhamana na chama kimefuatilia kimeambiwa hamna dhamana,mlitaka mbowe na wenzake wavamie mahabusu na kupokonya silaha na kuvunja milango ili atolewe?muwe mnaandika mambo yenye afya kwa taifa jameni,h ii siyo insta usifiwe kwa wingi wa likes[emoji33] [emoji15]Kwa kweli wacha aendeleee kunyea debe ili akitoka aafanye maamuzi mengine kwa kweli Mbowe ni noma sana yuko busy na NHC hathamin utu wa katibu wake looh inaumauma sana
Mwenyekiti CCM JF
Kwani huyo amepigwa faini?Mbona arusha yule jamaa alichangishiwa pesa ya kulipa faini? Hivi muweka Hazina wa chama mkoa ni muhimu kuliko naibu Katibu mkuu? Chama cha kibaguzi