Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amepinga vikali madai kuwa CHADEMA, wanachama na viongozi wake waliafikiana kususia uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, akisema hakuna kikao rasmi kilichopitisha uamuzi huo, na kuitaka CHADEMA kuweka wazi nyaraka za maamuzi hayo endapo zipo
Akihutubia wananchi wa kata ya Kwediboma wilayani Kilindi mkoani Tanga siku ya Jumapili, Salum Mwalimu amesema kuwa Watanzania wamechoka na utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na hatua ya kuwaambia wananchi wasishiriki uchaguzi ni sawa na kukabidhi ushindi kwa CCM kwa hiari
Soma Pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Salum Mwalimu, ambaye zamani alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar), alikosoa vikali msimamo wa CHADEMA wa kupinga ushiriki kwenye uchaguzi, akisema hatua hiyo ni kutokuwa na imani na wananchi wanaotaka mabadiliko kupitia sanduku la kura
Amesema CHAUMMA itaendelea kushiriki uchaguzi kwa nguvu zote kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kidemokrasia ya kuleta mabadiliko