McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,737
Mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu ameahidi endapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi wa Oktoba 29, atafanya uboreshaji mkubwa wa Uyole, mkoani Mbeya, kwa kujenga kituo cha kimataifa kitakachokuwa lango la biashara kwa nchi za Kanda ya Kusini mwa Afrika.
Akizungumza leo Jumamosi Septemba 27, 2025, Mwalimu amesema Uyole lina nafasi ya kipekee kijiografia kwani linaunganisha Tanzania na mataifa yasiyo na bandari kama DRC Congo, Zambia na Malawi. Amesema si sahihi wafanyabiashara kusafiri Dar es Salaam kwa bidhaa wakati Uyole linaweza kuwa kitovu cha biashara, akilifananisha na “Congo ndogo.”
Mwalimu pia ameahidi kujenga barabara ya njia sita kutoka Uyole hadi Tunduma, akibainisha kuwa barabara hiyo ya kimkakati ilipaswa kujengwa miaka 25 iliyopita.