Salome: Diamond Platnumz ft Rayvanny - General Views

Salome: Diamond Platnumz ft Rayvanny - General Views

Habari wanajf!!
Mimi ni jirani wa ali kiba (msanii anayeishi kwa mama na kula ugali wa shikamoo).
Nadhani inafahamika kuwa mdogo wetu ali kiba ni kula kulala,asubuhi hii nimeskia ali kiba anaplay ngoma ya salome ilyo kuwa released na msanii wa karne simba vampire hivyo nimeshawishika kuamini kuwa ali kiba ni fan wa simba....
Ebu acha upeku peku Jiran Looh
 
Mkuu....
Naomba nikuje huko mjini Daslam, nikuite aunt....
Mjini kuna shida wanaume wazee wanapenda mabinti, ma-aunty wanapenda young boys, ni fujo tu. Usishangae aunty anatukanwa na binti wa form four wamechukuliana bwana😀😀
 
Habari wanajf!!
Mimi ni jirani wa ali kiba (msanii anayeishi kwa mama na kula ugali wa shikamoo).
Nadhani inafahamika kuwa mdogo wetu ali kiba ni kula kulala,asubuhi hii nimeskia ali kiba anaplay ngoma ya salome ilyo kuwa released na msanii wa karne simba vampire hivyo nimeshawishika kuamini kuwa ali kiba ni fan wa simba....

Ndiooooo
 
Ila wimbo wame cover wa Saida Karoli, kama hawakuelewana kuna kesi hapa.

Hii hata si sampling, hii ni cover version.

Huu wimbo wa Saida Karoli kila mtu anayefuatilia muziki anajua, mpaka kuna movie moja ya Kimarekani ya Tyler Perry inaitwa "Peeples" umepigwa kama soundtrack.

paper work zilifanyika mkuu.Muta Felicien aliekua meneja wa Saida kitambo alihusika since Saida alikua akiuza haki zote za umiliki(sijui kwa kujua au kutojua) kwake.sidhan kama Saisa atafaidika na lolote hapa.

btw:nimependa ubunifu wa video na kiwango cha Raymond..kazi nzuri
 
Siwezi kumponda Diamond kwa kufanya cover ya Saida Karoli la hasha!!!! bali namsifu sana kwa mambo yafuatayo:

1.cover imekuwa taamu kuliko maelezo...boonge la nyimbo

2.Jamaa anajua kusoma nyakati saaaana....wabongo tu ndio mnaoponda kwakuwa mnaufahamu wa Saida...but Domo now anapotoa nyimbo dizain ni kama halengi bongo tuuu,analenga africa nzima....and yeeees hii nyimbo itasumbua mnoooo africa kutokana na mahadhi yake

3.Good strategy,bonge moja la lifting gear kwa msanii wake Rayvanny....tunasubili nyingine atakayofanya na Mavoko

All in All ..tuache utimu uchwara, WCB ni balaaaaaaaah!!!!!! Big up kwaooooo.....
 
Mwanamuziki wa kimataifa anayeshika namba mbili africa nzima kuwa na followers 2.7million nyuma ya David Adeleke Adedeji AKA Davido, Diamond Platnumz au ukipenda muite Simba vampire leo ametoa ahadi ya kutoa ngoma yake mpya endapo ngoma yake aliyofanya na p square iitwayo kidogo itafikisha viewers million 5 katika you tube

Mpaka sasa video hiyo imetazamwa mara 4,763,745

Diamond Platnumz ameachia wimbo mpya 'Salome' aliomshirikisha Raymond



Mashairi


[Verse 1: RayVanny]

Kioo hakidanganyi mama
Umejipodoa umepodoka
Mwendo na shape vyote mwanana
Mi suruali yanidondoka
Tukimbizane nini Salome wangu?
Hiyo michezo ya jogoo
Mbona watizama chini Salome wangu?
Ukimuona jongoo
Inama kidogo
Shika magoti
Mi nimesimama kama ngongoti
Mtoto jojo sio roboti
Chumbani bingiribingiri 'samasoti'

[Chorus: Diamond Platnumz]

Unantenkenyaga ukinyonga Salome
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Unantenkenyaga ukinyonga kweli
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Aaah orera bakuru vani
Orera ngambee
Orera na Zari ma
Orera ngambe

[Verse 2: Diamond Platnumz]

Utamu kolea a porokoto
Ting'ali ting'ali ndani kwa moto
Ntamnyongea msokoto
Nteme sumu kali kama koboko
Eeh mapenzi yananipa shida
(Shida mama)
Ni donda lisilokuwa na tiba
(Tiba bwana)
Usije baby ukanicharanga
Ukanichambua moyo kama karanga
Mie baby kwenye msambwanda
Huwa siendagi nge nge ni nga nga nga

[Chorus: Diamond Platnumz]

Unantenkenyaga ukinyonga Salome
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Unantenkenyaga ukinyonga kweli
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Aah orera bakuru vani
Orera ngambee
Orera na Zari ma
Orera ngambe

[Verse 3: RayVanny]

Miee mwenzako nyang'anyang'a
Miee binzari we ndio nyanya
Baby kwang'waru
Nisimamie kama kangaroo
Ibane kangwaru
Babu Juma mpige kwakwaru
(Kwakwarukwa)

[Bridge]
Asa chambua kama karanga sasa
(Chambua kama karanga)
Ichambue kama karanga Salome
(Chambua kama karanga)
Asa washa, washa, moto washa, washa
Songa, songa, ugali songa, songa
Mpaka chini ka chi
Mpaka chini ka chi

Wenye wivu wajinyonge leo
(Wenye wivu wajinyonge)
Aaah wenye wivu wajinyonge sana
(Wenye wivu wajinyonge)
Wenye wivu wajinyonge kweli
(Wenye wivu wajinyonge)
Oooh wenye wivu wajinyonge sana
(Wenye wivu wajinyonge)

[Outro]

Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Macho kodo!)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Wale kodo!)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Ukinyonga)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(We ukisonga)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa

-----------
View attachment 402995

WCB walimalizana na Uongozi wa Saida kabla ya kutoa kibao

“Tunakushukuru sana uongozi wa Saida Karoli na mzee Felician Mutakyawa kutupa haki na baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome,” aliandika Sallam instagram.

“Tunatambua kwamba nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania,”

Atafutwe Saida Karoli alipwe stahiki yake jamani huyu dada!
 
Atafutwe Saida Karoli alipwe stahiki yake jamani huyu dada!
IMG-20160919-WA0051.jpg
IMG-20160919-WA0051.jpg
 
Haya saida amesha endorse mnapenda simba afeli enheee?
 
Back
Top Bottom