Salome: Diamond Platnumz ft Rayvanny - General Views

Na hii dabate itaendelee kwa muda mrefu lakini mwisho sote tutajua kuwa Saida ndiye alikuwa na kipaji na ndio maana huyu Muta hajamtoa msanii mwingine baada ya hapo ...kama kweli ni 'professional promoter'!?
Vivyo hivyo huyu anayesema kurudia nyimbo (remake) ni kitu cha kawaida ajiulize kipindi wimbo huu unatoka ulihit kiasi gani kulinganisha na nyingine za wakati huo alafu uangalie miaka 16 baadae ni nyimbo ngapi zimetolewa mpaka urudiwe huo!? Hata mimi naweza kukaa studio usiku kucha lakini kipaji changu kikategemea wengine kunitoa.
cc: chige
Kutomtoa mwingine si sababu cuz' Felician Mutta yeye biashara yake ilikuwa ni muziki kupitia FM Studio na wala hakuwa na time ya kumuibua mtu!! Na hili ni kawaida kama zilivyo studio kadhaa duniani!! Nyingi ya hizi studio kama sio zote zinachofanya ni kukupa exposure na kukuingiza sokoni kama ulikuwa ni wa mtaani tu.

Hili suala la kurudia sijui kwanini unaona ni big issue wakati ni jambo la kawaida sana! Kwanza kwa level aliyofanya Diamond huwezi kuita remake bali ni sampling. Kwahiyo unataka kusema ikiwa over the past 16 years wimbo uliorudiwa ni Maria Salome peke yake basi ndo kwamba over the past 16 years hakuna wimbo bora kama Maria Salome?! Serious?! Kama hoja ni kufanya sampling au remake au hata cover mbona kuna ngoma kibao tu?! Young Tusso alifanya sampling ngoma ya Mwana FA (Bado Nipo Nipo Kwanza). Ingawaje hakufanya kibiashara lakini Christian Bella alifanya cover ya Ukimuona ya Diamond... sasa unataka kuniambia Diamond ni bora kuliko Christian Bella?! Barnaba alifanya cover ya Upendo ya Ambwene, juzi juzi tu hapa Jide ametoa Ndi ndi ndi ambayo ni cover song ya Naava Grey wa Uganda!

Hapa sijataja zile zinazofanywa pasi na makubaliano kv Mbagala vs Kafara ya Tanzanite.

Kwamba hata wewe unaweza kushinda studio... hoja ya kushinda studio haikuhusiana na masuala ya kipaji! Unachodai ni kwamba tunapima watu kwa kuangalia wanamiliki nini... ndipo nikakukumbusha watu wanavyokesha studio kufanya kazi na hivyo kushangaa kauli ya kwamba tunawapima kutokana na kile wanachomiliki as if huwaoni wanavyo-struggle kufanya kazi!

Lakini kama unataka kulinganisha ni nani borakati ya Diamond na Saida sidhani kama utakuwa unataka kufanya ulinganifu sahihi! Au ndo yale yale ya Kili Music Awards unawaweka Mwana FA kundi moja na Khadija Kopa!!!
 
Ni kweli una lugha kali lakini uzuri ni kwamba, ukielewa mitusi iliyomo mle basi fahamu ushakuwa mtu mzima vinginevyo utaishia kudhani anazungumziwa ngongoti mwanadamu kumbe ngongoti mlingoti ukiwa unasoma network 101%!! Tena Raymond ndo kazidi kumwaga mitusi sema the kid is so smart... huwezi kujua kwamba sehemu kubwa ya mashairi yake ya verse ya kwanza ni mitusi tupu!!
Watoto wa siku hizi ni welevu tofauti na sisi miaka 20 iliyopita. Nadhani mziki pendwa wa aina hii hauna tija kwa jamii. Lazima turudi nyuma na kujitathmin.
 
Watoto wa siku hizi ni welevu tofauti na sisi miaka 20 iliyopita. Nadhani mziki pendwa wa aina hii hauna tija kwa jamii. Lazima turudi nyuma na kujitathmin.
Nyuma imeshapita ndugu yangu na haitakuja kutokea ikarudi tena! Hao wenyewe walioshi huko nyuma hawataki kurudi nyuma ndo waje kurudi akina Diamond ambao hata nyuma yenyewe hawaijui inafananaje!
 
Diamond anavunja record yake mwenyewe ya kufikisha viewers millioni moja kwa siku nne aliyofikisha wakati wa wimbo wa Kidogo.... Ila safari hii anaivunja kwa kufikisha viewers millioni moja ndani ya siku tatu tatu.... Mpaka dakika hii wimbo huu wa Salome umefikisha viewers 812,000.... Congratulation Diamond Platnumz
 
Wana jamvi wenzangu kwakweli ni furaha sana kusikia diamond anasikiliza ushauri na kurudia baadhi ya nyimbo,
Ungepata muda zisikilize na hizi pia, kusema kweli SAIDA ni mtunzi na anajua alichokuwa anafanya,

Baada ya hapo diamond kama unapitiaga uku hebu mshirikishe saida mfanye track yeyote ile maana we unafit popote ,pangezi ratiba mtoe Ngoma moja , hebu tuputie hiz
0.
1

2.

3.

4.

5.

6.

Kwakweli huyu Dada apewe heshima, wasanii wwngine nanyie copy,
 
Within 30 Hours!!!

1M.png
 
Nianze kwa dhati kabisa kukupongeza ndg Nasib kwa kazi nzuri ya muziki inayokupa mkate wa kila siku lkn pia ukiitangaza nchi yetu kimataifa.Mimi sio shabiki mkubwa sana wa miziki yako lkn huwa nafuatilia na ipo mingi naipenda sana mfano wimbo wako ule wa Nitampata wapi na Ule wa Je utanipenda? Kwetu mbagala, na ule ulioshirilikiana na Davido hiyo ni baadhi ya nyimbo,lkn lengo sio hilo lengo nikutaka kukuomba kwa dhati kabisa umsainishe Saida Karoli katika lebo yako ya WCB,wengi tumeona majina ya Akina Raymond,harmonize na Mavoko yalivyoweza kupaa juu kimuziki bila shaka ni wakati sasa wakutumia Atalanta yako na uwezo wako kumrudisha Saida Karoli ktk ulimwengu wa Mziki maana tangu utoe ule wimbo wa Salome naona watu wanamzungumzia sana,okoa vipaji vya wakongwe sio mbaya hata Mr Nice akiongezwa ktk project hiyo
Nikutakie kazi njema za kimuziki ukiwezesha wengi inajiwekea hazina mbinguni
 
Huu wimbo nimeupenda sana. Nadhani huu utakua in wimbo Wa pili kutoka kwa Diamond kunikaa kichwani.
Ila kilichonivutia kwenye huu wimbo ni verse ya kwanza na chorus yake basi.
Kingine kuhusu wimbo huu ni masikitiko yangu kwamba utachuja haraka sana (hilo Nina uhakika nalo).
Pia ni wimbo wenye beat na rythms nzuri lakini mashairi yake hayampi muimbaji Uhuru Wa kuuimba mbele ya hadhira kwa aina ya picha inayojengwa na wimbo huo au aina ya ujumbe unaopatikana baana ya kuifunua tafsida iliyotumika.
Ni wimbo ambao ukipigwa ndani ya familia lazima ubadirishe channel au ukisikia mtoto anauimba lazima utamkataza tu.
Kingine watu wanachopaswa kukitambua ndani ya wimbo huu, ukiondoa Chorus, Diamond hajaimba bali anachombeza-chombeza tu.
Ni ngumu kusimama na Huyu Dogo Raynav kwa namna anavyo yafinyanga mashauri yake na utiririkaji wake...Dogo yupo vizuri ila anahitaji mwongozo mzuri. Hataweza kufanikiwa kwa kujificha nyuma ya tafsida, ni vizuri awe na mashairi clean na tafsida ziwe chache pale inapohitajika lakini si wimbo wote kuuchafua halafu unatafuta tafsida ili 'kuuficha' ujumbe ulioukusudia.
 
I love the song
hasa ile verse ya 3 anayoimba Raynav.... mie mwenzako nyang'anyang'a naweza isikiliza mara mia nisichoke
 
Kwa kweli video ya wimbo wa Diamond (Salome) ni nzuri Sana, ila kilicho niboa ni kuwa,hivi kulikua na ulazima gani wa kuvaa kinaijeria wakati ungeweza hata kuvaa kimasai kama ulitaka kuonesha utamaduni wetu,kwa nini uwatukuze wao. Hivi wao wanaweza kutoa video huku wamevaa kimasai kwa mfano.? Tanganza utamaduni wa nchi yako kwa ndo unako toka. Tuache ujinga.
 
Back
Top Bottom