Salma Kikwete: 'I am very dissappointed by you'

Salma Kikwete: 'I am very dissappointed by you'

Mamba haoi mjusi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Japo ametumia lugha ya kigeni kwa wanakijiji ambao hawakuelewa, pia si wajibu wao kushangilia maana kupewa msaada au dawa ni jukumu la serikali. Kuna watu akiwa kijijini kwao anajidai anajua kizungu. Hao vodacom wana sera za kurudisha faida kwa jamii. Mama Kikwete rekebisha kauli si wote CCM.
 
:A S angel::A S angel::A S angel::A S angel: KWANI KAWAKOSEA NINI MAMA WA WATU?? NDIO MAAANA HATUENDELEI TUMEZIDI MASUFURIA,, KUFANYA MFANYE NYIE TU AKIFANYA FULANI MNAUMIAJEEE HAHAAA, NA BADO MTAMSOMA TUU HADI 2'40 TUOMBE UZIMA TU..USHANIFAHAMU UZURI

Huyu mama kama 'kiongozi' anapaswa kuwa mfano mzuri hasa pale anapoongea na wananchi ili waweze kuupokea ujumbe anaoutuma. Kiongozi mzuri anatakiwa ajiweke katika hali ya wale anayewaongoza, awe mnyenyekevu bila kuwa dhaifu na kuonyesha heshima inayostahili. Kufanya kinyume cha hayo ni kuonyesha hali ya kuwadharau unaowaongoza, jambo ambalo litafanya uongozi wako usizae matunda yaliyotarajiwa.

Ni mara nyingi nimekuja humu jamvini nikilalamika kuhusu viongozi kuchanganya Kiswahili na Kiingereza hasa wanapoongea na wananchi wa kawaida. Kwangu mimi, kufanya hivyo ni kutojitambua kuwa unaongea na nani na inaonyesha kuwa huna nia ya kufikisha ujumbe unaouzungumzia.Ni vyema kutumia lugha inayofaa kwa kila namna ya kadamnasi.

Tabia nyingine ya viongozi wetu ni kujiweka juu kuliko wananchi. Rafiki yangu Adam Lusekelo, aliandika kuwa ni ajabu tu mara kiongozi anapochaguliwa, ghafla anapata busara ya kuwaambia watu wafanye nini. Jambo hili haliishii hapo tu, bali hata kwa wake za viongozi, mara nao wanakuwa wanasiasa! Ni muhimu kuelewa kuwa wananchi nao wana busara zao, wao ndio wanaoishi katika mazingira hayo siku nenda rudi. Ni muhimu basi, kwa kiongozi yeyote kufanya mazungumzo/mjadala na wananchi kuhusu maendeleo yao.
 
Dingiswayo... Tunakoelekea, imekuwa kawaida kwa viongozi kutupia maneno ya kiingereza wanapo address wananchi. Na naomba niunge mkono kwa ujumbe aliotoa Mama Salma Kikwete. Ila tu hayo maneno aliyo ongea kwa kiingereza angeongea kwa Kiswahili ingekuwa effective, sio kwa sababu ya ueleweka wa lugha bali kwa uzito wa ujumbe.

That is to say angesema "Akina mama mmeniangusha sana" ujumbe ungefika zaidi kuliko hiyo ya expression of dissapointment.

Bila shaka kitendo alichokifanya Mama Salma Kikwete cha kuwasilisha msaada kwa kina mama kinastahili kupongezwa.

Tatizo nililoliona hapa ni matumizi ya lugha ya kigeni kwa watu ambao sidhani kwamba walimuelewa. Katika kuongea lugha ya kigeni alijitenga au kujiweka pembeni na wale wananchi. Nakumbuka katika miaka ya 80 tulikuwa tuaona aibu kuongea Kiingereza katika daladala tusije tukaonekana kuwa tunajifanya wasomi. Siku hizi imekuwa ni sifa kufanya hivyo!

Lugha nzuri inayopendeza siku zote huvutia msikilizaji. Kumkaripia mtu mzima kunampa unyonge na hasira dhidi yako na mwishowe hukupuuza. Kama ulivyosema, kuna namna nyingi tu mtu unaweza kufikisha ujumbe bila kuchafua hali ya hewa.
 
first lady nadhani alitakiwa kuwa muimba ngonjera!!!
 
Upinzani at its best in Tanzania, yaani kwa nini firstlady katumia kimombo ni hoja ya upinzani..pheeeew
 
Nilicho kipenda kwa 1st Lady ni jinsi ilivyokuwa CONFIDENT na FORCEFUL alikuwa anaonekana anaamini kile anachoongea (which is good thing) na hii inaonyesha kuna transformation ya kuelekea uanasiasa kamili, sasa sijui ni kutokana na mazingira aliyokuwepo (uwanja wa nyumbani) au ni Kwamba anafikiri kuwa wananchi wanaona kuwa Voda imepelekwa na yeye kwa hiyo anapata goodwill for future ambition (just speculating) ... its my initial assessment lets wait and see.
 
Leo katika taarifa ya habari ya saa 2 usiku nimemuona Salma Kikwete akiwaambia kina mama wa kijiji kimoja mkoani Pwani (sikulishika jina la kijiji): "I am very dissappointed by you"! Aliposema hayo nilitaka kusikia kwa nini aliyasema maneno hayo kwa Kiingereza kwa wakina mama wa kijiji hicho. Alisema kuwa vodacom wamewaletea msaada, sasa baada ya kina mama kumshangilia, wao walijikunyata. Alimalizia kwa kuwaambia kuwa waache tofauti zao za ki itikadi na washangilie kwa sababu msaada huo umeletwa kwa faida yao.


Mkuu, hilo naona ni tatizo dogo sana. Mimi naumia sana maana bado sijapata jibu, hivi huyu mama anatumia hela toka fungu gani anapokuwa katika utalii kama huo? Ama kweli Watanzania tunaibiwa na hakuna wakuinuka na kusema neno juu ya wizi huu!
 
mtanzania gani anaejua engish?mnaleta pumba hapa mbona hamuwacheki wazungu wanaokosea kiswahili aau et ww n great thinker?au great tenker?
 
Mtanzania gani anaejua English yote ?mbana hamuwacheki wazungu wanaokosea Kiswahii kia siku?acheni kuwa matanki thinker
 
.

1. I’m disappointed by the government’s decision (i.e., I think the decision would affect me negatively, although it might be good for the nation).

2. I’m disappointed at the result (i.e., the result does not reflect well the effort).

3. I’m disappointed in you (i.e., I believed in you / your ability, but you betrayed my trust).

4. I’m disappointed with your performance (i.e., I still believe in you, but your performance was below my expectation).

5. I’m disappointed about something (i.e., I’m displeased with the process / event(s) that brought about the unexpected outcome).
.

Kiboko ya English...!!!!

Very encouraging to see such a good teacher......where is your working station, so that I can bring my unborn child to acquire skills and knowledge from you, the teacher????
 
Labda sikumsikia vizuri...lakini suala zima la kuzungumza Kiingereza mbele ya wanakijiji akina mama wa rika tofauti kama wanafunzi wake wa darasani kilinishangaza sana.

Usimwonee huyo mama bure, hana tofauti na sisi Watz wengine tuliobaki, wote tuko hivyo ukiangalia sana, kuanzia bungeni mpaka mitaani, ukienda mitaani kwenye mabaa ndio utashangaa mimi naona watu wengi tu akifika anaanza kumwongelesha dada muuza bar kiingereza dada asipomuelewa anachekwa na kusimangwa mpaka basi!
Leo hii ukisema uwaulize watu hapa JF kama Bunge liwe kwa kiingereza au Kiswahili utashangaa na majibu yake, watu wengi watataka liwe kwa Kiingereza ingawaje sehemu yetu kubwa hatuelewi kiingereza vizuri, hivyo kwa kifupi mama Kikwete amekuwa muhalisia wa sisi tulivyo!
 
hoja hapa ni kutumia lugha ngeni na kukaripia wananchi. Yeyote yule angeweza kukosea kwa sababu kiingereza sio lugha yetu ya kwanza.

na hili kosa wamekuwa wakifanya sana wale wanaojiita wasomi, kuongea kingereza ama vingereza na watu wasiojua lugha hiyo. Sasa sijui huu ndio usomi gani, maana msomi anajua nini anaongea wapi na kwa namna gani na akina nani ili ujumbe wake ufike.

Au ndio mashauzi na kujitia kujua? Ila kwa huyu mama ana matatizo mengine ya kisaikolojia yanamsumbua.
 
na hili kosa wamekuwa wakifanya sana wale wanaojiita wasomi, kuongea kingereza ama vingereza na watu wasiojua lugha hiyo. Sasa sijui huu ndio usomi gani, maana msomi anajua nini anaongea wapi na kwa namna gani na akina nani ili ujumbe wake ufike.

Nashauri mojawapo ya dira ya nchi yetu iwe kukuza na kuthamini lugha ya Kiswahili kwa kuwa ndiyo inayotuunganisha. Jambo hili limo ndani ya kazi kubwa ya kurudisha uzalendo, Watanzania kujivunia taifa lao na lugha yao. Nakumbuka enzi zile ambazo Tanzania ilikuwa taifa kubwa. Tulikuwa tunajivunia u Tanzania wetu na lugha yetu!
 
Mtanzania gani anaejua English yote ?mbana hamuwacheki wazungu wanaokosea Kiswahii kia siku?acheni kuwa matanki thinker
Swala hapa sio kukosea au kuchanganya Lugha, swala ni utumiaji wa Lugha kwa watu ambao hawailewi, Wazungu hata siku moja hawawezi kufanya hivyo, kama hawezi Kiswahili atasema kwamba hajui kiswahili na ataomba kutafsiriwa na kama anajua kiswahili basi ataongea chote na atakapokosa neno ataomba kutafsiriwa kwa maana anajua bila hivyo hataeleweka,
Mfano mzuri Bw.Kikwete alipokuwa anafungua daraja la mt Malagarasi linalojengwa na Benki ya Dunia kigoma, yule mkuu wa wa benki ya Dunia ambao ndio wafadhili aliwahutubia wananchi wa Kigoma kwa Kiswahili kitupu, na lengo lake lilikuwa ni kwamba kila mtu aelewe kwamba Wazungu ndio wanajenga lile Daraja na sio Ngedere, hivyo angeongea kiingereza ujumbe usingefika!
 
Leo katika taarifa ya habari ya saa 2 usiku nimemuona Salma Kikwete akiwaambia kina mama wa kijiji kimoja mkoani Pwani (sikulishika jina la kijiji): "I am very dissappointed by you"! Aliposema hayo nilitaka kusikia kwa nini aliyasema maneno hayo kwa Kiingereza kwa wakina mama wa kijiji hicho. Alisema kuwa vodacom wamewaletea msaada, sasa baada ya kina mama kumshangilia, wao walijikunyata. Alimalizia kwa kuwaambia kuwa waache tofauti zao za ki itikadi na washangilie kwa sababu msaada huo umeletwa kwa faida yao.

kama hajagundua kuwa wamechokwa na CHAMASUMU chao basi nae ni kilaza ka mwenza
 
Alipokuja mke wa Tonny Brair, mama Salma alitoa hotuba kwa Kiswahili(Yaani sehemu aliyotakiwa hasa kuzungumza kiingereza).
Ajabu mbele ya hao wanakijiji wanaozungumza Kiswahili na kizaramo tuu anajidai kuzungumza kiingereza.
Ahahaha!
 
Upinzani at its best in Tanzania, yaani kwa nini firstlady katumia kimombo ni hoja ya upinzani..pheeeew

Unajuaje kama mimi ni mpinzani? Kwa kuliona hili ndicho kimekufanya uone huo ni upinzani? Binafsi ninaamini kuwa haya niliyoandika hayahusiani na siasa za upinzani bali tabia ya viongozi wetu mbele ya wananchi. Hebu fungua macho uangalie mambo kwa upana zaidi, uzingatie yale yaliyoongeelwa kwenye mada. Ningeyaandika haya hata kama alieytamka hayo angetoka CUF, CHADEMA, TLP n.k. Tukiwa na muelekeo wa kuona kila kitu kama 'upinzani' itakuwa ni vigumu sana kupata maendeleo katika nyanja mbalimbali.
 
Back
Top Bottom