Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,231
Akitoa salamu za Mwaka mpya wa 2021 kwa wananchi wa Tanzania, Mh Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema , ametoa mwongozo wa kudai Tume huru ya uchaguzi kuanzia sasa, amesema kwa hali ilivyo nchini Tanzania ni vigumu kushiriki uchaguzi wowote bila Tume huru ya uchaguzi
Amewaomba wadau wote kuhakikisha wanadai Tume huru ya uchaguzi bila kuchoka, ndani ya nchi na kwenye majukwaa yote ya kimataifa , huku akitoa mifano ya nchi za Ghana, Kenya na Malawi kama kielelezo cha mafanikio ya upatikanaji wa Tume huru kutokana na juhudi za wananchi wa nchi hizo.
Mimi binafsi naunga mkono madai ya Tume huru ya Uchaguzi nchini Tanzania, natoa wito kwa Watanzania kupigania Tume huru ya uchaguzi kwa udi na uvumba ili kuwezesha mchakato huru na wa haki wa kupata viongozi na hatimaye kuondoa manung'uniko, laana na mikosi kwenye nchi, kupigania Tume huru halijawahi kuwa kosa mahali popote kwenye dunia hii wala Ahera, Haki huinua Taifa.