Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,893
3,200
Amani iwe nanyi nyote.

Kwa wale wazee wenzangu mtakubaliana na mimi kwamba Tanzania ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo ingeendelea na mfumo wa Ujamaa chini ya chama kimoja kuliko ilivyo sasa.

Uchumi wetu ulianza kuyumba mara tu awamu ya pili chini ya Mzee Ruksa, Alhaji Ali Hassani Mwinyi ilipoingia madarakani na kuusaliti Ujamaa wa Hayati Mwl. JKN.

Hadi kufikia mwaka 1987, uchumi wa Tanzania ulikuwa unaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Hii ina maana uchumi wetu ulikuwa mkubwa kuliko hata wa Kenya ambayo ndiyo kinara kwa kuwa na uchumi mkubwa katika ukanda huu kwa sasa!

Miaka ya 1990 tulipokubaliana na mambo ya kipuuzi kama nchi, tukapoteana kabisa na hali yetu haijatengamaa mpaka kesho. Fedha yetu inazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka huku kukiwa na pengo kubwa sana kati ya wenye nacho na wasionacho.

Hivyo ushauri wangu ni serikali kufanya kila linalowezekana kuturudisha katika mfumo wetu wa Ujamaa; Sera inayotutofautisha sisi na majirani zetu. Hii itasaidia kuleta ustawi kwa wote na kutuondolea kero ya kuwa na viongozi wezi na vibaka waliojificha kwa mavazi ya uongozi.
Asalaam Aleykum.
 
Amani iwe nanyi nyote.
Kwa wale wazee wenzangu mtakubaliana na mimi kwamba Tanzania ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo inganya kila linalowezekana kuturudisha katika mfumo wetu wa Ujamaa; Sera inayotutofautisha sisi na majirani zetu. Hii itasaidia kuleta ustawi kwa wote na kutuondolea kero ya kuwa na viongozi wezi na vibaka waliojificha kwa mavazi ya uongozi.
Asalaam Aleykum.
Uchumi uliyumba kipindi Cha Nyerere akaamua kumuangushia jumba bovu mwinyi
 
Huna akili!

Nadhani hata kuzaliwa utakuwa umezaliwa mwaka 1995.

Kama ulikuwa na akili miaka ya 1982- 1985 na ulishuhudia namna watu kwalivyokuwa wanavaa viraka na kuogea majani ya mipapai kama sabuni sidhani kama unaweza kuja kuandika huu upuuzi wako hapa.

Ujamaa ni laana.
Masikini wanapenda ujamaa sio kwa kuwa unawanufaisha ila ni kwakuwa unawafanya wote muwe masikini
 
Laiti kama siku moja nikawa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi nchi hii, nitahakikisha nafanya kila linalowezekana kuirudisha hii nchi kwenye msitari. Tanzania ni nchi kubwa na tajiri sana na inapaswa kuwa hivyo hata kwa hali ya maisha ya wananchi wote pia na siyo kwa wachache tu.
 
Itatimia mkuu...ikimbilie hiyo siku kwa nia utaifikia
 
Wewe uliishi kipindi cha ujamaa au umesoma tuu history ? Kwa data zipi za mwaka 1987 kuwa Tanzania ilikuwa imara kiuchumi kuliko Kenya??

Kimsingi by that time kutokana na vita vya Uganda na Sera zetu za ujamaa zilisababisha nchi kuwa na madeni makubwa saana

Vile vile wizi na ufisadi pamoja na uhujumu uchumi ulisababisha mashirika mengi ya umma kutokuwa na perfomance nzuri.

Wananchi kutokuielewa vzr Sera ya ujamaa na kujitegemea hili pia lilikuwa tatzo.

Ili kuinusuru nchi kulikuwa hakuna namna lazima tuingie kwenye mfumo WA uchumi huria.....

Shida yetu SASA baaada ya kuingia huko ufisadi na wizi bado ni tatzo pesa nyingi za kuleta maendeleo Kwa umma zinanufaisha watu wachache saana (wanasiasa).

Uwepo wa tofauti kubwa ya kipato Kati ya walio nacho na wasio nacho ni matokeo ya kimfumo hususani huu WA kibepari Ila serekali SASA ndio Baba WA wasio na nacho inatakiwa ipambane kutoa huduma Bora za msingi kwa wasio nacho mfano elimu Afya miundombinu n.k...

But Kwa bahati mbaya viongozi hawatuthamini watu wa Hali ya Chini haha tunaishi Kama yatima tuu kwenye nchi hii.

Lastly ni vema tujikite kwenye kuchapa Kazi kujikwamua kwenye kundi la wasionacho..
 
Hata hivyo hakuna chenye unafuu duniani...ukimwacha huyu uende kwa yule utasema bora huyu tena.Tupo duniani ya mapambano,twende nayo ivoivo
Kweli kabisa lakimi Ujamaa na Ujima...
Ulishindwa kutokana pingamizi kubwa kutoka kwa Mataifa ya Ulaya na marekani na kufikia hatua ya Kushuka kwa Thamani ya Pesa yetu...

Nafikiri Unafuu ni Kuunda hiyo BRICK currencies tu ambayo itakuwa Against na mataifa ya ulaya na Marekani..
NA fair enough itajumuisha Mataifa mengi so it will be hard kupambana nayo..
 
Tanzania ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo ingeendelea na mfumo wa Ujamaa chini ya chama kimoja kuliko ilivyo sasa.
Aaah!...ujamaa ulifeli pakubwa tu.

Uchumi wetu ulianza kuyumba mara tu awamu ya pili chini ya Mzee Ruksa, Alhaji Ali Hassani Mwinyi ilipoingia madarakani na kuusaliti Ujamaa wa Hayati Mwl. JKN.
Una takwimu kuthibitisha hili ?.... anyway Mwinyi aliwakuta Wadanganyika wapo hoi kiuchumi na alijitahidi mno kubadili hali.

Hadi kufikia mwaka 1987, uchumi wa Tanzania ulikuwa unaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Hii ina maana uchumi wetu ulikuwa mkubwa kuliko hata wa Kenya ambayo ndiyo kinara kwa kuwa na uchumi mkubwa katika ukanda huu kwa sasa!

Miaka ya 1990 tulipokubaliana na mambo ya kipuuzi kama nchi, tukapoteana kabisa na hali yetu haijatengamaa mpaka kesho.
Uongo mtupu, weka takwimu kuthibitisha hili.

Hivyo ushauri wangu ni serikali kufanya kila linalowezekana kuturudisha katika mfumo wetu wa Ujamaa; Sera inayotutofautisha sisi na majirani zetu. Hii itasaidia kuleta ustawi kwa wote na kutuondolea kero ya kuwa na viongozi wezi na vibaka waliojificha kwa mavazi ya uongozi.
Huwezi kutumia kanuni ile ile iliyokufelisha utegemee kupata matokeo mazuri.
 
Aaah!...ujamaa ulifeli pakubwa tu.

Una takwimu kuthibitisha hili ?.... anyway Mwinyi aliwakuta Wadanganyika wapo hoi kiuchumi na alijitahidi mno kubadili hali.

Uongo mtupu, weka takwimu kuthibitisha hili.

Huwezi kutumia kanuni ile ile iliyokufelisha utegemee kupata matokeo mazuri.
Screenshot_20231210-065624_Chrome.jpg
Screenshot_20231210-065600_Chrome.jpg
 
Aaah!...ujamaa ulifeli pakubwa tu.

Una takwimu kuthibitisha hili ?.... anyway Mwinyi aliwakuta Wadanganyika wapo hoi kiuchumi na alijitahidi mno kubadili hali.

Uongo mtupu, weka takwimu kuthibitisha hili.

Huwezi kutumia kanuni ile ile iliyokufelisha utegemee kupata matokeo mazuri.
Mkuu nimekuwekea hapo rejea ya gazeti la The Citizen la tarehe 17/04/2017 ambalo lilinukuu toka IMF. Ofcourse awamu ya 5 kama tungeenda nayo kwa miaka 10 tu nina uhakika Tanzania ingekuwa kubwa tena kama ilivyokuwa zamani. Lakini kwa mwendo huu wa kutambaa tunaoenda nao kwa sasa, tutasubiri sana kwa kweli.
 
Kwanini awamu ya 5 na sio zingine ?
 
Oooh!..hivyo kuanzia 1982-1984 Tz ilikuwa na GDP kubwa ila ndio kipindi hiki nchi ilikuwa inapitia tanuru gumu sababu ya athari za Vita ya Kagera.

Watanzania waliimbishwa ujamaa ila kiuhalisia hawakuuelewa vyema.
Ni kweli unachosema Mkuu, kuna baadhi ya mambo yaliyopelekea hiyo hali ngumu;
1. Athari ya njaa iliyotokana na ukame miaka ya mwanzoni mwa 70 (1973/1974)
2. Vita ya Kagera dhidi ya Nduli Idi Amin
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom