- Nilipochukua kadi ya uanachama wa CCM, nilikuwa mtumzima mwenye akili timamu, na nilijiunga na CCM kwa hiari yangu na sio kulazimishwa na mtu ay kwa sababu ya kukosa mlo mahali, wala kufukuzwa na anybody, na nilijiunga na CCM baada ya kuyaona mengi sana nje ya Tanzania, ingawa CCM ya sasa sio ile niliyojiunga nayo then lakini bado nininaamini kuna nafasi ya mabadiliko ambayo yataletwa na wanachama hai wa CCM kama mimi.
Mkuu FM ES, sikuzungumzia ulilazimishwa, ama kufukuzwa kokote. Ni haki ya raia wa Tanzania kujiunga na chama chochote bila kuvunja sheria za jamhuri.
- Maneno yako either ni misguided, au ni kwa ajili ya kutafuta cheap popularity hapa JF lakini ninayosema ndio ukweli halisi, ndio maana huko Visiwani hakutakuwa na muafaka hata siku moja, Seif hawakalilishi interest ya wa-Visiwani wote, ndio maana Pemba inaipigia kura CUF siku zote, sasa uamuzi ni wako kuyafukia matatizo na kujifanya hayapo au kuyavaa na kutafutia ufumbuzi, lakini ninaamini kuwa Seif anawakilisha interest ya waarabu.
JF Where We Dare to Talk Openly!, inaletwa hoja na data,tunajadiliana, kueleweshana na pia kuweka misimamo. Sasa unaposema natafuta Cheap popularity nakushangaa!!!. Ina maana hata kama unaandika vitu vya uongo, uzushi na viletavyo matabaka nikae kimya kwa sababu nikisema nitakuwa natafuta umaarufu kupitia kwako. Sidhani kujadili hoja hapa kuna mtu anatafuta umaarufu, na nitafute umaarufu wa nini?. Ingekuwa tuko kwenye jukwaa la siasa pale Mwembe Yanga, Dar ama Mkuyuni, Mwanza tukajibizana labda ungesema natafuta umaarufu. Sema labda unataka kila usemalo watu wawe NDIO MZEE. Mimi hilo sina, akiboronga yoyote hapa ama kwingineko namwambia, na akifanya jambo zuri namsifia.
Mimi sina chama, mkweli katika hivi vyama kwangu ndio namfagilia. Unaposema Seif hawakilishi matwakwa ya wa visiwani, ndio maana Pemba inaipigia CUF. Nadhani huanalii na kinyume chake, kama Seif hawakilishi matakwa yaw wa-visiwani, basin a wagombea wa CCM vilevile manake hupata kura zaidi Unguja. Lakini kama utawafananisha wote bora ya CUF, manake wana angalau Mwakilishi toka Unguja. Tukiacha hilo, Karume alipata 53.2% kura na Seif 46.1%. Kweli hapa kwa uchambuzi wako utasema kuwa kuna anayeonesha kuwakilisha zaidi ya mwenzake matakwa ya Zanzibar. Lakini hata hivyo, Zanzibar inajulikana kuwa CUF hushinda na uchaguzi kuchezewa. Kumbuka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Baada ya CCM kujua wameshindwa Mh. Ali Ameir Mohammed, aliitisha kikao cha waandishi wa habari na kusema hawaakubali matokeo. Na hii ilioneshwa hata kwa TV, Salmin akakimbilia Dar kuja kueleza kashindwa, Nyerere akafanya safari ya ghafla ya Zanzibar, akaongea na Mwenyekiti atangaze kuwa CCM wameshinda. Yule Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanziba kwa haraka haraka alikosea mpaka kuchanganua asilimia ya kura za washindi na zilizoharibika. Na alipotangaza tu matokeo alionekana akikimbua maswali ya waandishi. Ali Ameir alipoulizwa vipi mlisema hamtakubali matokeo, nadhani unakumbukaalijibu nini. Hivyo kusema CUF haikubaliki Zanzibar hilo labda kwa asiye na macho, masikio na ufahamu. Seif kuwakilisha interest za Waarabu hiyo itakuwa ni kampeni chafu ya CCM, kama vile wasemavyo CHADEMA ni chama cha wachaga.
- Na also, nimewahi kukaa miji ya Port Said Egypt, Aquaba Jordan/Israel, Mukhala South Yemeni, Hodeida North Yemen, Jedda Saudia, na Dubai, nimejionea kwa macho yangu Muarabu mweusi anavyonyanyaswa kama mbwa na waarabu weupe, kama bado huelewi tafuta ile documentary moja ya Mzee wa education Mazruhi aliyoifanyia Zanzibar ndio utanielewa ninachosema, kwenye hili sina ubaguzi mkuu ila ninasema straight from my soul, na nina ushahidi mwingi ambao siwezi kuuweka hapa kuhusu juhudi za Seif na anaowafanyia kazi.
Kama una maanisha Professor Mazrui (Ali Alamin Mazrui), naona umeandika Mazruhi kweli ni msomi. Si kila andiko la msomi laweza kuwa rejeo, hata nami naweza andika kuhusu CCM inavyoviua vyama vya upinzani kwa mlango wa nyuma, lakini si wote watakubaliana na nilichoandika. Hiyo "Documentary" ina jina gani ili niiafute nione?. Hivyo kuhusu kama kweli kuna kuonewa waarabu weusi sehemu nyingine, haibadili ukweli wa Zanzibar. Duniani watu wengi wanakandamizwa, Australia (Aborigins) hata New Zealanda nk. Sasa hatuwezi kugeneralize kuwa kwa kuwa wazungu wa Australia walitokea UK, basi wa UK wote ni wabaya kwa kuwakandamiza wenye asili ya Australia (Aborigins).
MKUU NARUDIA TENA, ULICHEMSHA NA UNACHEMSHA UNAPOTETEA WATU KWA KUANGALIA RANGI ZAO. Hakuna mtu aliingia mkataba na Mungu azaliwe na rangi fulani.