Salaam kutoka Zanzibar - Hotuba kamili - Msikie SEIF SHARIF HAMAD-Si mchezo

Field marshall ulikuwa na maana gani uliposema kuna Sultani mmoja kule London, anaisubiri sana Zanzibar?

- Mkuu wangu kumbe ulikuwa hujui hilo? Kwamba anayetengenezewa njia ya utawala na Seif ni huyo kjana Sultan aliyeko London? Ukienda kwenye archives za JF utakuta tumewahi kuyajadili sana hapa infact kuna topic moja hata picha yake huyo Sultan iliwekwa hapa, Ndio maana tunaomjua vizuri Seif huwa hatumtiliii maanani sana maana tunajua nia yake, hayo maneno hawezi kuyasema akiwa Mbeya, ndio maana anakimbilia kuyasenma Visiwani siku zote, akiwa Bara anakuwa kimyaaa.
 
Naamini sii msimamo wa Wazanzibari wote ..ni wakina Seif na baadhi ya wanachama wa CUF...na mawazo kama haya basi Seif hawezi kuaminika kuiongoza Zenj!

Mbona Bara Wazanzibari wapo wengi tu wanapeta na biashara zao? Kariakoo na juzi nilikutana nao Mbarali-Mbeya wakifanya biashara ya mchele kule?

Hata mimi siamini kama ni msimamo wa wazanzibari wote lakini cuf si ndio chama chenye nguvu huko visiwani?
Maalim Seif kama mwanasiasa naona maneno ya JK kuwa wataulinda muungano kwa nguvu zao zote yamewatisha ukizingati uchaguzi mkuu ni mwaka kesho. Bado tutasikia mengi sana inavyoonyesha ila sijui JK atafikia hatua kama ya Mkapa ama vipi, kwasababu muungano nadhani unapewa sapoti na watanzania wengi na JK anataka afunge bao lakisiasa.
Tusubiri tuone.
 
Mkuu FM ES, maneno yako mazito, nikujuavyo uCCM hivyo lazima utumie kila njia kuitetea CCM.

- Nilipochukua kadi ya uanachama wa CCM, nilikuwa mtumzima mwenye akili timamu, na nilijiunga na CCM kwa hiari yangu na sio kulazimishwa na mtu ay kwa sababu ya kukosa mlo mahali, wala kufukuzwa na anybody, na nilijiunga na CCM baada ya kuyaona mengi sana nje ya Tanzania, ingawa CCM ya sasa sio ile niliyojiunga nayo then lakini bado nininaamini kuna nafasi ya mabadiliko ambayo yataletwa na wanachama hai wa CCM kama mimi.

Lakini lugha za ubaguzi kwa sasa hazifai. Hizo historia unazotoa kuwa tunatakiwa linda watu weusi hazifai.

- Maneno yako either ni misguided, au ni kwa ajili ya kutafuta cheap popularity hapa JF lakini ninayosema ndio ukweli halisi, ndio maana huko Visiwani hakutakuwa na muafaka hata siku moja, Seif hawakalilishi interest ya wa-Visiwani wote, ndio maana Pemba inaipigia kura CUF siku zote, sasa uamuzi ni wako kuyafukia matatizo na kujifanya hayapo au kuyavaa na kutafutia ufumbuzi, lakini ninaamini kuwa Seif anawakilisha interest ya waarabu.

- Na also, nimewahi kukaa miji ya Port Said Egypt, Aquaba Jordan/Israel, Mukhala South Yemeni, Hodeida North Yemen, Jedda Saudia, na Dubai, nimejionea kwa macho yangu Muarabu mweusi anavyonyanyaswa kama mbwa na waarabu weupe, kama bado huelewi tafuta ile documentary moja ya Mzee wa education Mazruhi aliyoifanyia Zanzibar ndio utanielewa ninachosema, kwenye hili sina ubaguzi mkuu ila ninasema straight from my soul, na nina ushahidi mwingi ambao siwezi kuuweka hapa kuhusu juhudi za Seif na anaowafanyia kazi.
 
- Nilipochukua kadi ya uanachama wa CCM, nilikuwa mtumzima mwenye akili timamu, na nilijiunga na CCM kwa hiari yangu na sio kulazimishwa na mtu ay kwa sababu ya kukosa mlo mahali, wala kufukuzwa na anybody, na nilijiunga na CCM baada ya kuyaona mengi sana nje ya Tanzania, ingawa CCM ya sasa sio ile niliyojiunga nayo then lakini bado nininaamini kuna nafasi ya mabadiliko ambayo yataletwa na wanachama hai wa CCM kama mimi.

Mkuu FM ES, sikuzungumzia ulilazimishwa, ama kufukuzwa kokote. Ni haki ya raia wa Tanzania kujiunga na chama chochote bila kuvunja sheria za jamhuri.

- Maneno yako either ni misguided, au ni kwa ajili ya kutafuta cheap popularity hapa JF lakini ninayosema ndio ukweli halisi, ndio maana huko Visiwani hakutakuwa na muafaka hata siku moja, Seif hawakalilishi interest ya wa-Visiwani wote, ndio maana Pemba inaipigia kura CUF siku zote, sasa uamuzi ni wako kuyafukia matatizo na kujifanya hayapo au kuyavaa na kutafutia ufumbuzi, lakini ninaamini kuwa Seif anawakilisha interest ya waarabu.

JF “Where We Dare to Talk Openly!”, inaletwa hoja na data,tunajadiliana, kueleweshana na pia kuweka misimamo. Sasa unaposema natafuta “Cheap popularity” nakushangaa!!!. Ina maana hata kama unaandika vitu vya uongo, uzushi na viletavyo matabaka nikae kimya kwa sababu nikisema nitakuwa natafuta umaarufu kupitia kwako. Sidhani kujadili hoja hapa kuna mtu anatafuta umaarufu, na nitafute umaarufu wa nini?. Ingekuwa tuko kwenye jukwaa la siasa pale Mwembe Yanga, Dar ama Mkuyuni, Mwanza tukajibizana labda ungesema natafuta umaarufu. Sema labda unataka kila usemalo watu wawe NDIO MZEE. Mimi hilo sina, akiboronga yoyote hapa ama kwingineko namwambia, na akifanya jambo zuri namsifia.

Mimi sina chama, mkweli katika hivi vyama kwangu ndio namfagilia. Unaposema Seif hawakilishi matwakwa ya wa visiwani, ndio maana Pemba inaipigia CUF. Nadhani huanalii na kinyume chake, kama Seif hawakilishi matakwa yaw wa-visiwani, basin a wagombea wa CCM vilevile manake hupata kura zaidi Unguja. Lakini kama utawafananisha wote bora ya CUF, manake wana angalau Mwakilishi toka Unguja. Tukiacha hilo, Karume alipata 53.2% kura na Seif 46.1%. Kweli hapa kwa uchambuzi wako utasema kuwa kuna anayeonesha kuwakilisha zaidi ya mwenzake matakwa ya Zanzibar. Lakini hata hivyo, Zanzibar inajulikana kuwa CUF hushinda na uchaguzi kuchezewa. Kumbuka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Baada ya CCM kujua wameshindwa Mh. Ali Ameir Mohammed, aliitisha kikao cha waandishi wa habari na kusema hawaakubali matokeo. Na hii ilioneshwa hata kwa TV, Salmin akakimbilia Dar kuja kueleza kashindwa, Nyerere akafanya safari ya ghafla ya Zanzibar, akaongea na Mwenyekiti atangaze kuwa CCM wameshinda. Yule Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanziba kwa haraka haraka alikosea mpaka kuchanganua asilimia ya kura za washindi na zilizoharibika. Na alipotangaza tu matokeo alionekana akikimbua maswali ya waandishi. Ali Ameir alipoulizwa vipi mlisema hamtakubali matokeo, nadhani unakumbukaalijibu nini. Hivyo kusema CUF haikubaliki Zanzibar hilo labda kwa asiye na macho, masikio na ufahamu. Seif kuwakilisha interest za Waarabu hiyo itakuwa ni kampeni chafu ya CCM, kama vile wasemavyo CHADEMA ni chama cha wachaga.

- Na also, nimewahi kukaa miji ya Port Said Egypt, Aquaba Jordan/Israel, Mukhala South Yemeni, Hodeida North Yemen, Jedda Saudia, na Dubai, nimejionea kwa macho yangu Muarabu mweusi anavyonyanyaswa kama mbwa na waarabu weupe, kama bado huelewi tafuta ile documentary moja ya Mzee wa education Mazruhi aliyoifanyia Zanzibar ndio utanielewa ninachosema, kwenye hili sina ubaguzi mkuu ila ninasema straight from my soul, na nina ushahidi mwingi ambao siwezi kuuweka hapa kuhusu juhudi za Seif na anaowafanyia kazi.

Kama una maanisha Professor Mazrui (Ali Alamin Mazrui), naona umeandika Mazruhi kweli ni msomi. Si kila andiko la msomi laweza kuwa rejeo, hata nami naweza andika kuhusu “CCM inavyoviua vyama vya upinzani kwa mlango wa nyuma”, lakini si wote watakubaliana na nilichoandika. Hiyo "Documentary" ina jina gani ili niiafute nione?. Hivyo kuhusu kama kweli kuna kuonewa waarabu weusi sehemu nyingine, haibadili ukweli wa Zanzibar. Duniani watu wengi wanakandamizwa, Australia (Aborigins) hata New Zealanda nk. Sasa hatuwezi kugeneralize kuwa kwa kuwa wazungu wa Australia walitokea UK, basi wa UK wote ni wabaya kwa kuwakandamiza wenye asili ya Australia (Aborigins).

MKUU NARUDIA TENA, ULICHEMSHA NA UNACHEMSHA UNAPOTETEA WATU KWA KUANGALIA RANGI ZAO. Hakuna mtu aliingia mkataba na Mungu azaliwe na rangi fulani.
 
Mandela alifungwa na wazungu, lakini alipopata uRais hakuwafanyizia wale wazungu. Bali aliwaacha hata katika Serikali, kumbuka Waziri wa Fedha alikuwa mzungu. Hata alipolihutubia Bunge la Uingreza, aliwashangaza wazungu pale alipozungumzia madhila ya makaburu, lakini mwishoni akasema yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

- Wakati Mandela anawafurahisha wazungu wako mkuu, ilikuwa ni kwa expense ya wananchi wanyonge wa Soweto ambao mpaka leo hawajui kama walishpata uhuru au bado maana maisha yao ni yale yale tu kama kabla ya uhuru.

Ukianza kufunua historia, kuwa wale weusi ndio ndugu, na hawa weupe (ama wekundu, njano) sio ndugu, ukiwamaliza weupe utaelekea wapi?. Kwa Zanzibar hakuna ubishi kuwa CUF wako juu, sasa tusitumie njia za kubaguana, hatujengi bali tunabomoa, na siku zote uongo hujitenga na ukweli. Kama ingekuwa CUF wana tatizo Zanzibar wasingekuwa wanashinda chaguzi lakini wanaibiwa kura. Hivyo tusianze ingiza rangi katika kupingana, tutumie sera.

- Ndugu yangu niliwahi kuihsi miji ya Sanah, Aden, Mukhala na Hodeida North/South Yemen, Aquaba kwenye border ya Jordan/Israel, Jedda Saudia, Port Saed Egypt, na Khartoum Sudan, nimejionea kwa macho yangu jinsi mwarabu mweusi anavyonyanyaswa, infact hata saa ya kuswali jioni waarabu weupe husali kwenye side yao na waarabu weusi husali kwenye kona yao, kwa mara ya wkanza rangi ilitamnkwa rasmi kwenye uchaguzi wa rais Dodoma, unakumbuka? Sasa zile tabia za kuficha ficha mambo tuziache mambo ni kukwekwa hadharani ili yatatuliwe, Seif tunajua njama zake maana zipo tepu zake nyingi sana akizungumza in private ndio maana wanaojua vizuri humcheka sana Lipumba na kumita mtumwa wa Seif.

Hatuwezi kumpa nafsi Seif ya kutugawa kwa ajili ya waarabu wa Oman.

Thanxs!
 
- - Na also, nimewahi kukaa miji ya Port Said Egypt, Aquaba Jordan/Israel, Mukhala South Yemeni, Hodeida North Yemen, Jedda Saudia, na Dubai, nimejionea kwa macho yangu Muarabu mweusi anavyonyanyaswa kama mbwa na waarabu weupe,........ na nina ushahidi mwingi ambao siwezi kuuweka hapa kuhusu juhudi za Seif na anaowafanyia kazi.

Mkuu naona kama vile ndani ya kitengo cha propaganda.

Tueleze pia jinsi Wabara tunvyonyanyasika tukianzia kwa makaburu,... na bado Wachina mizizi haijakomaa sawasawa, sijui itakuwaje.
 
JF “Where We Dare to Talk Openly!”, inaletwa hoja na data,tunajadiliana, kueleweshana na pia kuweka misimamo. Sasa unaposema natafuta “Cheap popularity” nakushangaa!!!. Ina maana hata kama unaandika vitu vya uongo, uzushi na viletavyo matabaka nikae kimya kwa sababu nikisema nitakuwa natafuta umaarufu kupitia kwako. Sidhani kujadili hoja hapa kuna mtu anatafuta umaarufu, na nitafute umaarufu wa nini?. Ingekuwa tuko kwenye jukwaa la siasa pale Mwembe Yanga, Dar ama Mkuyuni, Mwanza tukajibizana labda ungesema natafuta umaarufu. Sema labda unataka kila usemalo watu wawe NDIO MZEE. Mimi hilo sina, akiboronga yoyote hapa ama kwingineko namwambia, na akifanya jambo zuri namsifia.

- Mkuu usingekua mbaguzi kama unavyodai basi Mkapa alipomkataa Salim kwa sababu ya urabu wake, tungekusikia au tungewasikia wajumbe wetu kule Dodoma wasiopenda ubaguzi kama wewe, au ni wewe tu bongo nzima usiyependa ubaguzi mkuu?

Mimi sina chama, mkweli katika hivi vyama kwangu ndio namfagilia. Unaposema Seif hawakilishi matwakwa ya wa visiwani, ndio maana Pemba inaipigia CUF. Nadhani huanalii na kinyume chake, kama Seif hawakilishi matakwa yaw wa-visiwani, basin a wagombea wa CCM vilevile manake hupata kura zaidi Unguja.

- Wote ni wasanii, lakini tuko nao kwenye muungano kwa hiyo ni lazima kuwavumilia, lakini point yako ninaikubali kwamba CUF hibiwa kura za Pemba na sio Unguja, kwa sababu nimeshawahi kuliona daftari la wapiga kura kule wala sio siri kuwa CUF hibiwa kura za Pemba, lakini sio Unguja hata siku moja! Na pia katika ku-deal na wasanii wawili CCM tumechagua ku-deal na shetani tunaowajua.
 
- MKUU NARUDIA TENA, ULICHEMSHA NA UNACHEMSHA UNAPOTETEA WATU KWA KUANGALIA RANGI ZAO. Hakuna mtu aliingia mkataba na Mungu azaliwe na rangi fulani.

Mfumwa,

Hata mimi nadhani kama ni FMES naemfahamu hapa JF kama ameteleza ulimi kama Pinda na Alibino!

FMES over swala hili la Ubaguzi wa rangi Tz ni vema ukubali umekosea na kuwaomba Watz msamaha!

Wawe weusi, wekundu, waarabu..ili mradi ni Watz inatosha ni ndugu zetu!

Nawakilisha!
 
- Maneno yako either ni misguided, au ni kwa ajili ya kutafuta cheap popularity hapa JF lakini ninayosema ndio ukweli halisi, ndio maana huko Visiwani hakutakuwa na muafaka hata siku moja,
[/QUOTE]

Kwani wewe nani hadi unalosema liwe ndio kweli? Yaani pumba zako unazotunga na kuhadithiwa ndio unalazimisha uaminiwe!!! Sasa nani anatafuta cheap popularity hapa kama sio wewe?
 
Last edited by a moderator:
matakwa ya Zanzibar. Lakini hata hivyo, Zanzibar inajulikana kuwa CUF hushinda na uchaguzi kuchezewa. Kumbuka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Baada ya CCM kujua wameshindwa Mh. Ali Ameir Mohammed, aliitisha kikao cha waandishi wa habari na kusema hawaakubali matokeo. Na hii ilioneshwa hata kwa TV, Salmin akakimbilia Dar kuja kueleza kashindwa, Nyerere akafanya safari ya ghafla ya Zanzibar, akaongea na Mwenyekiti atangaze kuwa CCM wameshinda. Yule Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanziba kwa haraka haraka alikosea mpaka kuchanganua asilimia ya kura za washindi na zilizoharibika. Na alipotangaza tu matokeo alionekana akikimbua maswali ya waandishi. Ali Ameir alipoulizwa vipi mlisema hamtakubali matokeo, nadhani unakumbukaalijibu nini.

- Ukienda kwenye archives yote haya utayakuta yapo nilishayasema siku nyingi sana, ila ahsante kwa kunikumbusha tena.

Hivyo kusema CUF haikubaliki Zanzibar hilo labda kwa asiye na macho, masikio na ufahamu. Seif kuwakilisha interest za Waarabu hiyo itakuwa ni kampeni chafu ya CCM, kama vile wasemavyo CHADEMA ni chama cha wachaga.

- Wanaosema anything sio tatizo ila kama wanaweza kujenga hoja na kzuitetea maana hizo ishu zote mbili zimeshawahi kujengewa haja hapa JF, na kinachobaki ni macho na uelewo wa msomaji.
 
Mfumwa,

Hata mimi nadhani kama ni FMES naemfahamu hapa JF kama ameteleza ulimi kama Pinda na Alibino!

FMES over swala hili la Ubaguzi wa rangi Tz ni vema ukubali umekosea na kuwaomba Watz msamaha!

Wawe weusi, wekundu, waarabu..ili mradi ni Watz inatosha ni ndugu zetu!

Nawakilisha!

- Baaada ya uchaguzi wa Dodoma ninamjua kiongozi mmoja tu alijitokeza kusema ukweli, naye ni Sumaye aliandika artcle moja unaikumbuka aliposema CCM tumekula nyama ya mtu, alikemea sana udini na ubaguzi wa rangi kwenye uchguzi wa urais wa CCM 2005, wengine wote walitoka kimyaa as nothing happened kwa hiyo mkuu aliyekose ahpa ni wewe unayetaka kuficha ficha mambo halafu uchguaiz wa rais ufike tena waanze kubaguana, huku wewe ukiiimba kuwa hakuna ubaguzi.

Thnaxs!
 
- Wakati Mandela anawafurahisha wazungu wako mkuu, ilikuwa ni kwa expense ya wananchi wanyonge wa Soweto ambao mpaka leo hawajui kama walishpata uhuru au bado maana maisha yao ni yale yale tu kama kabla ya uhuru.

Mkuu FM ES, Mandela ana akili sana, kama angefanya utani mwanzoni ile nchi isingetawalika, wangemfanya kama wamfanyiavyo Mugabe. Kuanzia jeshi mpaka polisi walijaa hao makaburu pamoja na baadhi ya wazulu. Hivyo hakutaka visasi, unapozungumzia visasi unajua kuwa Wazulu walio wengi walikuwa upande mmoja na makaburu. Kama Mandela angetaka kisasi, kisingeishia kwa Makaburu tu, kingefika mpaka kwa Wazulu waliokuwa wanatumiwa. Lakini hata Wazulu hakuwatupa kumbuka Chifu Buthelezi. Mitaa ya Soweto ni kama mitaa ya mabanda ya Korogosho, Dandora, Kangemi kule Kenya. Na pia nchi nyingi maisha ni kama yaleyale tokea tupate uhuru, huwezi kusema maisha yaliyo Soweto ni kwa sababu Mandela aliwafurahisha wazungu kwa kusamehe yaliyopita.

- Ndugu yangu niliwahi kuihsi miji ya Sanah, Aden, Mukhala na Hodeida North/South Yemen, Aquaba kwenye border ya Jordan/Israel, Jedda Saudia, Port Saed Egypt, na Khartoum Sudan, nimejionea kwa macho yangu jinsi mwarabu mweusi anavyonyanyaswa, infact hata saa ya kuswali jioni waarabu weupe husali kwenye side yao na waarabu weusi husali kwenye kona yao, kwa mara ya wkanza rangi ilitamnkwa rasmi kwenye uchaguzi wa rais Dodoma, unakumbuka? Sasa zile tabia za kuficha ficha mambo tuziache mambo ni kukwekwa hadharani ili yatatuliwe, Seif tunajua njama zake maana zipo tepu zake nyingi sana akizungumza in private ndio maana wanaojua vizuri humcheka sana Lipumba na kumita mtumwa wa Seif.

Ndugu yangu baadhi ya hizo nchi nami nimefika, sikuwahi kuona kuwa waarabu waliswali kwao, nami mweusi na weusi wenzangu tukaswali tofauti. Huo ni uongo mkubwa unazusha. Kama unasema tabia za kufichaficha mambo tuziache, tuweke vitu hadharani. Tunaomba utuwekee hizo tepu za Seif ambazo umetaja ni nyingi ili nasi tuzisikie. Kama mtu ni hatari unaficha nini?.
 
Kwani wewe nani hadi unalosema liwe ndio kweli? Yaani pumba zako unazotunga na kuhadithiwa ndio unalazimisha uaminiwe!!! Sasa nani anatafuta cheap popularity hapa kama sio wewe?

- Irrelevant and pure nonesense, hapa ndio mwanzo na mwisho wa uwezo wako kufikiri, pole sana mkuuu!
 
- Mkuu usingekua mbaguzi kama unavyodai basi Mkapa alipomkataa Salim kwa sababu ya urabu wake, tungekusikia au tungewasikia wajumbe wetu kule Dodoma wasiopenda ubaguzi kama wewe, au ni wewe tu bongo nzima usiyependa ubaguzi mkuu?
- Wote ni wasanii, lakini tuko nao kwenye muungano kwa hiyo ni lazima kuwavumilia, lakini point yako ninaikubali kwamba CUF hibiwa kura za Pemba na sio Unguja, kwa sababu nimeshawahi kuliona daftari la wapiga kura kule wala sio siri kuwa CUF hibiwa kura za Pemba, lakini sio Unguja hata siku moja! Na pia katika ku-deal na wasanii wawili CCM tumechagua ku-deal na shetani tunaowajua.

Mkuu FM ES, unaposema mbona hukunisikia nikipiga kelele kuhusu ubaguzi aliofanyiwa Salim wakati wa mchakato wa CCM. Mhh!!, nashindwa hata kukuelewa, manake hunijui mimi ni nani?. Hivyo huwezi uliza mbona sikupinga la Salim. Na kama wajumbe wa CCM hawakupinga, sio sababu na mimi sikupinga, japo mimi sina chama.

Nawe jee ulipinga kuhusu Salim?, jibu ni rahisi haukupinga, manake hata leo unadiriki kuwabagua wazanzibar kwa rangi zao.

Sasa naanza kukuelewa vizuri ubaguzi wako, kwenye post yangu mojawapo ktk hii thread nilikuuliza ukishawamaliza kuwatenga weupe (pia manjano, wekundu nk) utafuata wapi?. Naona umejibu katika hili, unaposema kuwa wote Karume na Seif ni wasanii na umefikia kuwaita SHETANI!!!!, hivyo kwa wazanzibar ni shetani, manake mmeamua ku-deal na shetani mnaowajua. UBAGUZI MWINGINE MKUBWA SANA!!!!!. Pia usinilishe maneno kuwa nimesema CCM huiba kura Pemba tu, CCM huiba Pemba na Unguja, tena zaidi huiba Unguja.

- Baaada ya uchaguzi wa Dodoma ninamjua kiongozi mmoja tu alijitokeza kusema ukweli, naye ni Sumaye aliandika artcle moja unaikumbuka aliposema CCM tumekula nyama ya mtu, alikemea sana udini na ubaguzi wa rangi kwenye uchguzi wa urais wa CCM 2005

Waliopiga kelele kuhusu ubaguzi aliofanyiwa Salim si Sumaye peke yake. Wako wengi tu wenye majina makubwa wakiwemo pia na raia.

Mkuu FM ES, UBAGUZI WA RANGI NDUGU YANGU HAUKUFIKISHI POPOTE, HUENDA UKAJA HATA KUKUKUMBA, KUWAKUMBA WANAO AMA WAJUKUU ZAKO. Kweli unaweza zidi kulitetea hilo, Muungwana akikosea huomba radhi, na waungwana humsamehe.
 
Mkuu FM ES, unaposema mbona hukunisikia nikipiga kelele kuhusu ubaguzi aliofanyiwa Salim wakati wa mchakato wa CCM. Mhh!!, nashindwa hata kukuelewa, manake hunijui mimi ni nani?. Hivyo huwezi uliza mbona sikupinga la Salim. Na kama wajumbe wa CCM hawakupinga, sio sababu na mimi sikupinga, japo mimi sina chama.

- Hapana kama ungekwua mchukia ubaguzi ningekusikia maana nilimsikia Sumaye peke yake akilalamika lakini sio wengine kwa sababu ya kuamini kuficha ficha, no inatakiwa yatolewe nje kama ninavyofanya ili yashughulikiwe.

Nawe jee ulipinga kuhusu Salim?, jibu ni rahisi haukupinga, manake hata leo unadiriki kuwabagua wazanzibar kwa rangi zao.

- Kwa sababu ndio siasa za Seif, hayo maneno ya juu hayawezi kukubalika na sisi wananchi, maana ni matusi sana na hivyo ni vyema akaeleshwa mapema kwamba akileta siasa zake za kibaguzi tunajua sababu na hatuwezi kumpa nafasi.

Sasa naanza kukuelewa vizuri ubaguzi wako, kwenye post yangu mojawapo ktk hii thread nilikuuliza ukishawamaliza kuwatenga weupe (pia manjano, wekundu nk) utafuata wapi?. Naona umejibu katika hili, unaposema kuwa wote Karume na Seif ni wasanii na umefikia kuwaita SHETANI!!!!, hivyo kwa wazanzibar ni shetani, manake mmeamua ku-deal na shetani mnaowajua.

- siwezi kujibu hoiaj za hicni namna hii mkuu maana kama wewe hatumii maneno kama shetani sisi tunatumia wka nia njema, Seif aache siasa za Pemba na kutuletea taifa, abaki nazo huko huko Pemba lakini hawezi kumtukana rais wa Jamhuri kwa visingizizio vya sias zake za kibaguzi, majibvu ni kwamba we know him na siasa zake na hatuwezi kumruhusu, Karume alipokuwa akilazimisha wananchi waarabu na wesui kuaona hakuwa mbaguzi ila alikuwa anajaribu ku-deal na ukweli kama mimi sasa,

UBAGUZI MWINGINE MKUBWA SANA!!!!!. Pia usinilishe maneno kuwa nimesema CCM huiba kura Pemba tu, CCM huiba Pemba na Unguja, tena zaidi huiba Unguja.Mkuu FM ES, UBAGUZI WA RANGI NDUGU YANGU HAUKUFIKISHI POPOTE, HUENDA UKAJA HATA KUKUKUMBA, KUWAKUMBA WANAO AMA WAJUKUU ZAKO. Kweli unaweza zidi kulitetea hilo, Muungwana akikosea huomba radhi, na waungwana humsamehe.

- Hawawezi kuiba kura Unguja kwa sababu hakuna wa kumpigia kura Seif kule Unguja, huwa wanaiba kura za Pemba tu, ubaguzi upo na ni lazima uemwe wazi, hapa ndicho kinachomsumbua Seif, na hatutampa nafasi kuleta siasa zake za ki-Pemba kwenye Muungano.

Unajitahidi, lakini bado kidogo ingawa pia kuna hoja nzito unazitoa, lakini la ubaguzi wa Seif na hali halisi ya huko linakupa taabu sana ingawa ninajua kua una background nzuri sana ya CUF, mkuu wangu nilipokuwa US Seif alikuwa akija sana kule na alikuwa akiletwa na yule bwana mdogo Baharia wa Houston ambaye enzi zile alikua akiishi Boston, siku hizi huyu bwana mdogo baada ya kumuelewa Seif ameamua kuacha mambo ya CUF na kula kuku ndio maana humsikiii Seif akienda tena US kama zamani, bwana mdogo alikua msela mwenzangu ndio maana Seif hana ujanja wowote ndugu yangu, ninamjua vizuri sana ni mbaguzi anayetaka kujitenga na Pemba hawezi pata hiyo nafasi maana hatuwezi kumpa CCM.

Thanxs!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu FM ES, Mandela ana akili sana, kama angefanya utani mwanzoni ile nchi isingetawalika, wangemfanya kama wamfanyiavyo Mugabe. Kuanzia jeshi mpaka polisi walijaa hao makaburu pamoja na baadhi ya wazulu. Hivyo hakutaka visasi, unapozungumzia visasi unajua kuwa Wazulu walio wengi walikuwa upande mmoja na makaburu. Kama Mandela angetaka kisasi, kisingeishia kwa Makaburu tu, kingefika mpaka kwa Wazulu waliokuwa wanatumiwa. Lakini hata Wazulu hakuwatupa kumbuka Chifu Buthelezi. Mitaa ya Soweto ni kama mitaa ya mabanda ya Korogosho, Dandora, Kangemi kule Kenya. Na pia nchi nyingi maisha ni kama yaleyale tokea tupate uhuru, huwezi kusema maisha yaliyo Soweto ni kwa sababu Mandela aliwafurahisha wazungu kwa kusamehe yaliyopita.

- Mandela alifurahisha wazungu huku ndugu zake wakifa njaa kule Soweto, ndio maana leo Mugabe ni hero kule SA.
 
...Wazanzibari (Unguja na Pemba) walio wengi wakiwemo wafuasi wengi wa CCM hawapendezwi na muungano. Kwanini 'Tanganyika' aka Tanzania Bara inang'ang'ania?

...sababu za kiusalama (wa majini) pekee hazitoshi kutufanya kuendelea kuungana bila ridhaa ya wananchi wa huko...Maneno ya maalim Seif taratiiibu yanageuza mwelekeo, walengwa sasa ni Wazanzibari wote, sio wafuasi wa CUF pekee,...

hapo pakijachanganywa na zile vuta nikuvute Zanzibari ni nchi ama sio nchi, mara tuchimbe mafuta yetu, nanyi mchimbe madini yenu, ipo siku patakuwa hapatoshi...

zinatafutwa 'combustible material' tu moto uwake!
 
Na Mwandishi Wetu
Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele​

WAKATI Rais Jakaya Kikwete anajua kwamba Zanzibar kuna mgogoro, hata kama anaupaka rangi na kuuita "mpasuko;" na mgogoro umeleta maafa kisiasa, kiuchumi na kijamii, kauli zake akiwa ziarani Pemba zimepanua ufa.

Rais ameshangaza na hasa amesikitisha kila mpenda amani ya kweli kwa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliyosema yanachochea hata mwananchi wa kawaida kulazimika kufikiri kuwa, kiongozi mkuu wa nchi, kiongozi wa chama kikubwa na kizee, aliyetoa ahadi ya kupatia ufumbuzi mgogoro Zanzibar, amefeli.

Amefeli kwa sababu, siyo tu kwamba ameonyesha kushindwa kuleta ufumbuzi alioahidi Wazanzibari, Watanzania na ulimwengu mzima, bali pia ameshindwa kuwa mkweli.

Si mara moja tumesema katika safu hii, kwamba Rais Kikwete ana wajibu wa kuchukua dhamana aliyopewa na wananchi na Katiba, ya kuhakikisha watu wote ndani ya Jamhuri wanaishi kwa amani na utulivu.

Wala hatuzungumzii amani na utulivu kama inavyotajwa na CCM. Tunakusudia utengamano wa kwelikweli kwa jamii yote. Kwa kuwa rais mwenyewe amekiri kuna tatizo Zanzibar, maana yake anakiri hakuna utengamano huo.

Hatuna nia wala sababu yoyote ya kumvua rais koti aliloamua kuvaa pale alipomwagia upupu wananchi wa Visiwani akiwaambia kwamba chama wanachounga mkono huenda kisipate kuongoza nchi asilani.

Rais si lazima awe shahidi wa upande mmoja. Anaweza kuwa kiongozi wa chama chake, lakini ni shuhuda wa matukio matatu mfululizo. Haya ni yale yanayohusu hujuma na wizi wa kura za Wazanzibari pale walipoonyesha utashi wao tangu mwaka 1995.

Haki na uhuru wa wananchi wa Zanzibar, ya kuchagua viongozi wanaowataka, haiwezi kuchukuliwa kuwa maasi kufikia hatua ya kuwazomea, kuwasimanga na kuwanyima maendeleo.

Kwa kauli za rais, hata waliokuwa wamebakiwa na chembe ya mashaka kuwa huenda wapinzani Zanzibar walikuwa wanashindwa kweli katika uchaguzi, sasa wamethibitisha hila na mabavu yanayotumika kupora haki ya wananchi.

Rais anawaambia wananchi kuwa wanaweza kupata wabunge, madiwani na viongozi wengine, ila itawachukua muda mrefu kuongoza serikali au wasipate kamwe fursa hiyo. Hii ina maana pana.

Maana pekee inayopatikana haraka ni kwamba wapinzani ni viumbe waliolaaniwa. Hawawezi kuingia ikulu; hata kwa ubia na vyama vingine pale matokeo ya ushindi yanapolazimu iwe hivyo.

Inahitaji ujasiri usio wa kawaida kiongozi kulaani wananchi na uhuru wao, na utashi wao na bado akaendelea kuwa rais wao. Huko ni kupandikiza woga, fitna, chuki na hata uadui kisiasa.

Wananchi wa Zanzibar wanajua kuwa katika mazingira huru na haki, wana uwezo wa kutwaa serikali. Lakini kama watawala wameamua kuvuruga mfumo uliojengwa kikatiba – wa siasa za ushindani – basi wajue wanakotuelekeza siko.
 
Hotuba kamili Seif Sharif Hamadi - Mzanzibari,CUF Katibu Mkuu

Waheshimiwa wananchi wenzangu, sote tunakumbuka kwamba tarehe 27 Januari 2001 nchi yetu ilikumbwa na maafa makubwa. Watanzania wenzetu, hususan Wazanzibari, waliuawa, wengine wakafanywa walemavu wa maisha, wengine walibakwa, wengine wakafungwa, wengine mali zao zikaharibiwa na kuporwa, na wengine wakakimbilia Mombasa kama wakimbizi, kwa mara ya mwanzo. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa la Tanzania.

- Ameanza vizuri, lakini hap[o kwenye kubaka anasema uongo na hana sababu kwani wote tunajua kwua wananchi waliuliwa siku hiyo, lakini ya kubaka ni kuongeza chumvi for what?

Na hawa (wahanga wa maafa hayo) kosa lao lilikuwa nini? Kosa lao ni kushiriki maandamano ya amani kudai haki zetu. Kimsingi walidai kwamba uchaguzi wa 2000 ulikuwa ni uchafuzi, wakataka urejewe. Wakadai tuwe na katiba mpya Bara na Zanzibar. Wakadai tume huru za uchaguzi Bara na Zanzibar. Lakini kwa watawala, hiyo ilikuwa ni dhambi; kwa hivyo,serikali chini ya usimamizi wa CCM wakaamrisha majeshi: majeshi wanaolipwa kwa fedha za kodi za Watanzania, watumie risasi na silaha zilizonunuliwa kwa fedha za kodi za Watanzania, wawauwe Watanzania wenzao. Na kama alivyosema, Mheshimiwa Duni, baada ya hayo yote kutokezea, Bwana Mkapa anawatunza wale wauaji – anawapa vyeo zaidi – na Amani Karume anawapongeza majeshi kwa kufanya kazi nzuri.

- Huyo sasa anazidi kuharibu, maandamano hayakupewa kibali na serikali kwa hiyo yalikuwa ni maandamano haramu, swali ni je serikali ilikuwa right kwenye kuwawua wananchi hao? hapana ilikuwa ni excessive na un-necessary force na linaweza kujadiliwa legally kuhusu makosa ya Mkapa kuruhusu mauaji, lakini Seif hana sababu ya kubadili ukweli kwa sababu ya ku-score cheap na short term popularity ambazo in the long run haziwezi kuwasiadia wananchi wa huko Visiwani, kwa sababu yeye aksiema uongo kama anavyofanya so far kwenye hii hotuba, then anawapa nafasi ya kujibiwa uongo na watawala!
 
- Hapana kama ungekwua mchukia uabguzi ningekusikia maana nilimsikia Sumaye peke yake akilalamika lakini sio wengine kwa sababu ya kuamini kuficha ficha, no inatakiwa yatolewe nje kama ninavyofanya ili yashughulikiwe.

Mkuu FM ES, HUNIJUI, ndio maana huwezi jua wakati Salim anabaguliwa nilipinga ama la. Lakini kwa kusema ukweli nilipinga vibaya mno. Na hili la kubaguliwa Salim halikuanza leo. Wakati yuko AU (OAU) kama Katibu Mkuu alirudi kwa Mwalimu kumuuliza achukue fomu. Hapo ndio hili lilianza, na mwanzilishi ni Mama fulani mtu mzito aliyeko CCM (namuhifadhi jina, bali mme wake kawahi kuwa bosi Nyaraka za Taifa), alifikia kumwambia Nyerere kuwa unataka tutawaliwe na Mwarabu?. Mwalimu kuona mambo yamekuwa makubwa akamwambia Salim usichukue fomu. Hivyo halikuanza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa 2005, bali zamani kidogo.

- Kwa sababu ndio siasa za Seif, hayo maneno ya juu hayawezi kukubalika na sisi wananchi, maana ni matusi sana na hivyo ni vyema akaeleshwa mapema kwamba akielta siasa zake za kibaguzi tunajua sababu na hatuwezi kumpa nafasi.

Maneno ya Seif (kwa uelewa wako kuona kakosea) hayawezi kufanya wazanzibar wote wasio weusi uwabague. Dhambi ya mtu mmoja haifanyi wengine wote waibebe.

- siwezi kujibu hoiaj za hicni namna hii mkuu maana kama wewe hatumii maneno kama shetani sisi tunatumia wka nia njema, Seif aache siasa za Pemba na kutuletea taifa, abaki nazo huko huko Pemba lakini hawezi kumtukana rais wa Jamhuri kwa visingizizio vya sias zake za kibaguzi, majibvu ni kwamba we know him na siasa zake na hatuwezi kumruhusu, Karume alipokuwa akilazimisha wananchi waarabu na wesui kuaona hakuwa mbaguzi ila alikuwa anajaribu ku-deal na ukweli kama mimi sasa,

Nashukuru, ndio uelewa wangu ndio maana natoa hoja za chini, wewe mwenye hoja nzito Mola akuzidishie.
Hivi unataka kusema CCM hawatoi kauli za ajabu. Kikwete alipokuwa Pemba juzi juzi aliwaambia nini kuhusu wapinzani kupata nchi. Na hata Pinda Alhamisi hii iliyopita naye kazungumza hilohilo kuwa wapinzani hawawezi kushika madaraka akiwa Bungeni. Unataka wapinzani wajibu nini?, kama viongozi wanaweza toa kauli ambazo zinaashiria kuwa hawawezi toa nchi hata pale wanaposhindwa. Karume alifanya kosa kubwa sana kulazimisha watu waoane, hiyo ni kuvunja haki za binadamu. Kuoana ni kupendana na si kulazimishana. SASA NIMEKUONA TENA JINSI UNAVYOUNGA MKONO UVUNJAJI WA SHERIA HASA HAKI ZA BINADAMU.

- Hawawezi kuiba kura Unguja kwa sababu hakuna wa kumpigia kura Seif kule Unguja, huwa wanaiaba kura za Pemba tu, ubaguzi upo na ni lazima uemwe wazi, hapa ndicho kinachomsumbua Seif, na hatutampa nafasi kuleta siasa zake za ki-Pemba kwenye Muungano.

Hivi kama unakubaliana nami CUF ilishinda uchaguzi wa 1995, hao watu walitoka wapi?. Na kama unasema CUF hawapati kura Unguja, ulizia kwa nini waliyagawa tena majimbo baada ya uchaguzi wa 1995. Unajua CUF walichukua mpaka jimbo iliyopo Ikulu (Ngome ya CCM), unalijua hilo?. Na mpaka sasa CUF wana mwakilishi Unguja. Kuhusu uizi Pemba huwa wanatumia vikosi vya usalama. Wakati karibia na uchaguzi wanajeshi, askari, zimamoto, KMKM, uwt kibao huhamishiwa zenji, hapo ndio huiba kura toka kambini. Lakini vituo vya raia kwa Pemba wanaiba kiasi kidogo manake jamaa wako ngangari kama walivyokuwa ngangari CHADEMA kwenye jimbo la Mheshimiwa Ndesamburo (Ndesapesa), unajua yaliyojiri kwa hili jimbo?.

Unajitahidi, lakini bado kidogo ingawa pia kuna hoja nzito unazitoa, lakini la ubaguzi wa Seif na hali halisi ya huko linakupa taabu sana ingawa ninajua kwua una background nzuri sana ya CUF

Sijatoa hoja yoyote nzito nje, siwezi kukubali kuwa Seif mbaguzi kwa kushinda Pemba, na CCM wanaoshinda Unguja tu nao sio wabaguzi. Tena CUF huwa wana wawakilishi na Unguja, nani wabaguzi hapo. Hili suala CCM mnatumia “Divide and Rule” kama wakoloni ni baya sana. Fanyeni maendeleo ya haki kote Unguja na Pemba mtaliondoa jinamizi linalowasumbua, sio kuiba kura.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom