William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Quote: Seif
3. Jakaya Kikwete, kwa hili kashtushwa sana na mshikamano wa Wazanzibari. Kashtushwa sana na umoja wa Wazanzibari. Wazanzibari sasa hivi wamekuja juu kusema kuwa tutalinda nchi yetu, Zanzibar ni nchi na itabaki kuwa nchi mpaka Kiama. Wazanzibari wameshikamana kulinda rasilimali zao, hasa za mafuta. Sasa Kikwete hili linamuuma sana.
4. Linamuuma sana tu, kwa sababu wao wamo katika kutekeleza mkakati tangu aliouwacha Julius Nyerere kwamba Zanzibar itoweke katika ramani ya dunia.
Quote: Ngekewa
Inasikitisha karne hii mtu kuwa na mawazo haya. Inawezekana mtu mwenye elimu yake akazidiwa na utashi tu na labda mzee umepatwa na hilo. Kuamini kuwa Wazanzibari kutaka kuiondoa CCM lengo ni kurejesha usultani ni mambo ya karne iliyopita na huku Bara tunakotaka kuiondosha CCM tunataka kumrejesha Malkia? Tu watu wazima na wenye fikra tuache kuburuzwa na hisia zetu kwani tunapata elimu ili tuvitawale vitu kama hivi.
- Tizama sasa mkuu wangu, unasema ya kumrudisha Sultani ni ya karne iliyopita, meaning kwamba unakubali kuwa yaliwahi kuwepo kwa sababu kwani karne ina miaka mingapi? Sasa eti kwa kuamini kuwa ya kurudi kwa Sultan yaliwahi kuwepo karne iliyopita unakua ni mtu mwenye elimu lakini umezidiwa na utashi na unasikitisha eti bado ina make the same sense kwako mkuu?
- Sasa unasema kwamba utuuzima na fikra zetu zinakua ni za kuburuzwa, tunaposema kwamba malengo ya CUF Visiwani sio sawa na malengo yake Bara? Ni kweli tumepata elimu ili tuweze kuitumia na in this case tuweze kuelewa kwamba hotuba za Seif anapokuwa Bara hazifanani na anapokuwa Visiwani sasa ana agenda gani mkuu kama sio u-Pemba?
U-Pemba hauna nafasi kwenye Muungano wetu, ndio maana rais anasema ataulinda Muungano kwa nguvu zote, sasa Seif analilia nini kama anaupenda Muungano?