Salaam kutoka Zanzibar - Hotuba kamili - Msikie SEIF SHARIF HAMAD-Si mchezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salaam kutoka Zanzibar - Hotuba kamili - Msikie SEIF SHARIF HAMAD-Si mchezo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 7, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Maalim Seif: “Kikwete akome kutufitinisha Wazanzibari!”7/02/2009
  Kauli ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, katika Mkutano wa Nane wa Maombolezi ya Januari 2001, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar, tarehe 31 Januari, 2009

  Hotuba kamili Seif Sharif Hamadi - Mzanzibari,CUF Katibu Mkuu

  Waheshimiwa wananchi wenzangu, sote tunakumbuka kwamba tarehe 27 Januari 2001 nchi yetu ilikumbwa na maafa makubwa. Watanzania wenzetu, hususan Wazanzibari, waliuawa, wengine wakafanywa walemavu wa maisha, wengine walibakwa, wengine wakafungwa, wengine mali zao zikaharibiwa na kuporwa, na wengine wakakimbilia Mombasa kama wakimbizi, kwa mara ya mwanzo. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa la Tanzania.

  Na hawa (wahanga wa maafa hayo) kosa lao lilikuwa nini? Kosa lao ni kushiriki maandamano ya amani kudai haki zetu. Kimsingi walidai kwamba uchaguzi wa 2000 ulikuwa ni uchafuzi, wakataka urejewe. Wakadai tuwe na katiba mpya Bara na Zanzibar. Wakadai tume huru za uchaguzi Bara na Zanzibar. Lakini kwa watawala, hiyo ilikuwa ni dhambi; kwa hivyo,serikali chini ya usimamizi wa CCM wakaamrisha majeshi: majeshi wanaolipwa kwa fedha za kodi za Watanzania, watumie risasi na silaha zilizonunuliwa kwa fedha za kodi za Watanzania, wawauwe Watanzania wenzao. Na kama alivyosema, Mheshimiwa Duni, baada ya hayo yote kutokezea, Bwana Mkapa anawatunza wale wauaji – anawapa vyeo zaidi – na Amani Karume anawapongeza majeshi kwa kufanya kazi nzuri.

  Waheshimiwa wananchi, mimi napenda tujuwe kuwa msiba huu ni wa wana-CUF peke yao. Msiba huu ni wa Wazanzibari sote. Kuna wengine wenye mtazamo finyu wataona CUF wameshikishwa adabu, lakini wakumbuke ‘Tumbili akisha miti, huja mwilini.’ Mghani Utenzi amesema wazi wazi kwamba kuna viongozi wa chama cha Afro Shirazi wakubwa tu, nao walipoteza maisha yao. Kwa hivyo, tusiangalie mambo hayo kwa ufinyu kwamba ni CUF.

  Huu ni msiba kwa taifa. Wajibu wetu Wazanzibari ni kuwakumbuka wenzetu, tusiwasahau, tuwaenzi. Na kuwaenzi wenzetu ni kuendelea na mapambano yale ambayo yalisababisha damu zao zitoke. Hakuna kurudi nyuma. Yeyote yule ambaye atarudi nyuma kwa namna yoyote ile, huyo ni msaliti na muuaji kama wauaji wenyewe, kabisa. Ni lazima, ni lazima, sote kabisa tuungane kuhakikisha kuwa dhulma katika nchi yetu inaondoka moja kwa moja. Lazima dhulma iondoke. Hakuna mizinga, hakuna bunduki, hakuna rupleni ambayo itaturudisha nyuma katika kudai haki zetu. Tutadai haki zetu mpaka zote zimalizike, lakini tutazipata haki zetu. Lazima tuzipate haki zetu, tusiwasaliti wenzetu.

  Waheshimiwa, nasema bado yale yaliyowafanya wenzetu wapoteze maisha, bado madai yetu yapo pale pale. Bado tunataka katiba mpya; hili ni dai ambalo mpaka leo ni halali. Tunataka tume huru ya uchaguzi. La kusikitisha, mimi nilidhani yaliyotokea 2001 watawala watajifunza, lakini bahati mbaya watawala wetu wana vichwa vigumu. Kwao kubwa ni kuhakikisha namna gani wataendelea kubakia kwenye madaraka kwa gharama yoyote ile. Maisha ya binaadamu kwao si kitu, kitu ni wao waendelee kubaki na madaraka, basi.

  Wamesahau kuwa waliowaua wenzetu 2001, wengi wao na wao weshakufa. Mwenyezi Mungu hana haraka, lakini anahukumu hapa hapa duniani, akhera ni malipo tu. Nao watahukumiwa, huko akhera kutakwenda hisabu tu basi. Sawa sawa!?

  Waheshimiwa, nasema tena nasikitika kuwa watawala hawajifunzi. Na ushahidi kuwa watawala hawajifunzi ni kauli alizozitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, katika ziara aliyoifanya Zanzibar katika visiwa vya Unguja na Pemba.

  Kikwete alisema mengi, lakini mawili makubwa niliyoyashika mimi ni haya: alipokuwa Pemba anawaambia Wazanzibari, kwamba haki ya Wazanzibari ni kuchagua mbunge, mwakilishi na diwani, basi. Lakini ukija kwa uchaguzi wa kumpata kiongozi mkuu wa Zanzibar, Wazanzibari hawana haki hiyo. Hiyo ndiyo kauli ya Kikwete. Na kwa kweli chaguzi za 1995, za 2000 na za 2005 zimeonesha kuwa huo ndio mtindo. Kwa hivyo Kikwete anatwambia kabisa kuwa na 2010, yeye ndiye ataamua nani awe rais wa Zanzibar. Huo ndio ujumbe wa Kikwete.

  Waheshimiwa, na hapa nawaomba ndugu zetu wa CCM waifahamu: ingawa Kikwete kasema wapinzani, lakini kakusudia Wazanzibari. Ndugu zetu wa CCM, nyinyi wenyewe ni mashahidi, mwaka 2000 mlikuwa na mtu mlomtaka, mlomchagua nyinyi wenyewe, wana-CCM wa Zanzibar, lakini watawala wa Bara walikuwa hawamtaki. Wakamuweka mtu wanayemtaka wao.

  Kwa hivyo, msidhani kauli ile tunaambiwa CUF peke yetu. Hapana, tunaambiwa Wazanzibari kwa ujumla wetu. Inawezekana kabisa na 2010, CCM mkawa na mgombea wenu, lakini madam hamtaki Bwana Kikwete, basi huyo mgombea wenu asahau. Huo ndio ujumbe wenyewe alioutoa Kikwete, kwamba mwenye haki ya kutupatia rais wa Zanzibar ni Kikwete mwenyewe na CCM yake ya Bara. Huo kwa ufupi ndio ujumbe wa Jakaya wa Mrisho wa Kikwete.

  Ujumbe wa pili, ambao kautolea hapa hapa Kibandamaiti, ni kwamba ati wako tayari kupambana na wapinga Mapinduzi na akasema watayalinda Mapinduzi yao kwa gharama zozote. Jamani nataka mnisikie vizuri: kauli ya Kikwete na namnukuu: “Tutayalinda “Mapinduzi Yetu”, kwa gharama zozote!”

  Mimi ninavyojuwa – na tunavyoambiwa – ni kwamba Mapinduzi yale yalikuwa ni ya Wazanzibari, kwamba kiongozi wa Mapinduzi alikuwa Mzee Abeid Amani Karume na wenzake kina Said Washoto. Tunaambiwa ni Wazanzibari ndio waliofanya Mapinduzi, au sio? Haya Kikwete ni Mzanzibari? Mimi ninavyojuwa – na Profesa (Lipumba, ambaye ni Mnyamwezi na kimila ni mtani wa Kikwete) – kwamba Kikwete ni Mkwere. Zanzibar haimuhusu shikio wala ndewe. Leo vyereje Kikwete asema: “Tutayalinda Mapinduzi yetu!” Vyereje!?

  Hapo pana mambo makubwa Wazanzibari, lakini leo si wakati wake kuyazungumza. Inshallah siku za mbele tutayafunua moja baada ya moja, kwa nini Kikwete katoa kauli ile. Na kwa kweli anaposema kuwa atapambana na wapinga Mapinduzi, anakusudia wale ambao watampinga mgombea atakayeteuliwa na yeye, Kikwete. Usijali kama wewe ni CCM au CUF, madhali unapingana na mtu aliyemleta yeye, wewe ni mpinga Mapinduzi yao. Ndio maana nasema Wazanzibari tuone kuwa hili suala si dogo. Haambiwi CUF, twaambiwa Wazanzibari kwa ujumla wetu.

  Wananchi, jambo la kushangaza, wenzetu watawala – hawa watawala wa Bara – jambo wanaloliogopa kwa Wazanzibari ni umoja wa Wazanzibari; kwa sababu ndiyo sera yenyewe. Nguvu zao (watawala wa Bara ni) ‘wagawe uwatawale.’ Mtakumbuka alipokuwa mtawala Mkapa lile linamkera, pale pale hakuweza kujizuia…. Pale pale kwenye jukwaa alipopewa nafasi ya kusalimia, akaanza kusema: “Tunatoa salamu kwa mababu za hao wapinga Mapinduzi, vijukuu vyao, vitukuu vyao hawatawali hapa.” (salamu za Mkapa katika sherehe za mwaka 2002 za Mapinduzi ya Zanzibar. Baada ya Muafaka wa pili wa 2001, CUF ilishiriki katika sherehe hizo kama chama na Mkapa aliogopeshwa sana na namna umma wa Kizanzibari wenye sare za CUF na CCM ulivyokusanyika pamoja kwa mara ya mwanzo kwenye sherehe kama hizo).

  Ebo! Wewe badala ya kufurahi kwamba Wazanzibari kwa umoja wao wanasherehekea Mapinduzi kwa mara ya mwanzo, unakasirika. Lakini si ujinga, analijua analolifanya, kwamba lile aliliona inawasogeza Wazanzibari wawe karibu pamoja na hilo watawala wa Tanganyika hawataki kuliona. Na hili, Jakaya Kikwete, kwa hili kashtushwa sana na mshikamano wa Wazanzibari. Kashtushwa sana na umoja wa Wazanzibari. Wazanzibari sasa hivi wamekuja juu kusema kuwa tutalinda nchi yetu, Zanzibar ni nchi na itabaki kuwa nchi mpaka Kiama. Wazanzibari wameshikamana kulinda rasilimali zao, hasa za mafuta. Sasa Kikwete hili linamuuma sana.

  Linamuuma sana tu, kwa sababu wao wamo katika kutekeleza mkakati tangu aliouwacha Julius Nyerere kwamba Zanzibar itoweke katika ramani ya dunia. Sasa mshikamano wenu Wazanzibari unawafanya wao wasifanikiwe. Kwa hivyo, alilokuja kufanya Kikwete ni kujaribu kuwagawa tena Wazanzibari kwa kutumia wimbo wa Mapinduzi. Tena, mimi nashukuru Mungu, kasema ‘Mapinduzi yetu,’ katumia wimbo wa Mapinduzi yao. ‘Mapinduzi yao’ si Mapinduzi ya Wazanzibari, jamani. Mujuwe hilo!

  Kwa hivyo, anataka kutumia wimbo huo atugawe, lakini kachelewa. Kachelewa. Hatugawiki tena ng’o! Tena namwambia Jakaya wa Mrisho wa Kikwete akome, akome, akome! Akome kutuletea fitna katika nchi yetu. Akome, akome kuja kutugawa Wazanzibari. Fanya chokochoko zako huko huko Bara. Namna gani, bwana!?

  Tena anajisifu mwenyewe: “Miye Zanzibar naijuwa!” Waijuwa Zanzibar weye? Wee waijuwa Zanzibar? Ati mwenyewe anaijua Zanzibar kaja ’77 akiwa afisa dawati pale Kisiwandui (ofisi ndogo ya CCM, Zanzibar). Wakati huo Maalim Seif tayari ni mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. Wakati huo Maalim Seif ni Waziri wa Elimu wa Zanzibar. Wakati huo Maalim Seif ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Wakati huu Maalim Seif ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Yeye (Kikwete) mtoto mdogo tu, nani Kikwete? Nani huyu, kabisa!? Namwambia Jakaya wa Mrisho wa Kikwete kwamba enzi za kuja na shanga mununue nchi yetu umepitwa na wakati.

  Eti CCM imeleta maendeleo. Maendeleo gani? Tumejenga barabara! Barabara ipi mulojenga? Mimi nasema tena, hao vibaraka uliowaweka hawajaleta maendeleo yoyote Zanzibar na sisi Wazanzibari ndio tunaojuwa. Ati umekuja hapa kumtetea Amani Karume kuwa kaleta maendeleo; na mwenyewe bila haya anasema ati Kikwete na Karume ni mama mmoja, baba mmoja, watoto mapacha. Hujasema jipya Kikwete. Na tunajua kwa sababu hiyo, kwa wewe na yeye baba yenu na mama yenu ni CCM – ati leo CCM huyo huyo ni baba, huyo huyo ni mama, ni khuntha.

  Khuntha CCM imemzaa Kikwete na Karume, ati wanasema ni mapacha. Hatushangai, ndio maana ufisadi unaotokea Zanzibar, watu wanachukuliwa ardhi zao, Kikwete mhm! Kimya, hasemi kitu. Fedha za serikali, kodi zinazokusanywa kutoka bandarini, kutoka airport, kutoka kila mahali zinakwenda nyumba kubwa. Kimwete mhh! Kimya. Lakini hatushangai, CCM inazaa mafisadi, Bara na Zanzibar.

  Kwa hivyo ninalosema, Mheshimiwa Kikwete, ujumbe wako Wazanzibari wameupokea, kwamba 2010 kushamuonea choyo Mkapa, nawe wataka kuua. Keshamuonea choyo Mkapa kwamba mikono yake ina damu, na yeye Kikwete anataka mikono yake iwe na damu vile vile. Basi Wazanzibari tunakusubiri njoo! Njoo! Njoo! Wazanzibari tunakusubiri njoo!

  Sisi tulikuamini uliposema 2005 kwamba mpasuko wa Zanzibar unakuuma kweli kweli na kwamba utafanya kila njia ili uumalize. Tukakupa mashirikiano yote Kikwete. Wakati napita kwenye matawi kuelezea suala hili, sehemu nyingi nikiulizwa: “Hivyo Maalim, unamuamini Kikwete?” Nami jibu langu lilikuwa: “Simuamini lakini tumpururie, atajinyonga mwenyewe huyu!” Mwenyezi Mungu hamfichi mnafiki. Lile ambalo lilikuwemo kwenye moyo wa Kikwete, juzi kalitapika. Sawa sawa? Bila ya siye kushiriki, mwenyewe kalitapika. Wazungu wanasema: “the true colors of Kikwete have now come out!” Rangi sahihi za Kikwete sasa hivi zinakuja juu. Sawa sawa?

  Sasa anajiandaa kutuua tena Wazanzibari. Tunamwambia aje. Lakini tunakwambia, tunakwambia, tunakwambia: Inshallah mara hii, mara hii, mara hii, utakavyoipiga, tutaicheza hivyo hivyo.


  Hotuba kamili: Machano Khamis Ali - Mzanzibari ,Makamu Mwenyekiti - CUF

  7/02/2009

  “Ikiwa kuwalinda albino kumemshinda, Kikwete atawezaje kuyalinda Mapinduzi?”

  Kauli ya Makamo Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali, katika Mkutano wa Nane wa Maombolezi ya Januari 2001, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar, tarehe 31 Januari, 2009

  Waheshimiwa wananchi, tumeshamsikia Maalim Seif. Sasa mimi sina makubwa. Ninachosema ni kimoja tu: Basi jiandaeni. Maana yake sio (Maalim Seif) aseme, halafu tufanyiwe, halafu tuje tulaumiane. Ikiwa tunakuja kuuliwa, na siye tunasema tutacheza itakavyopigwa, maana yake ni kuwa akija (Kikwete) atukute tumejitayarisha. Ama sio?

  Waheshimiwa, mimi nasema Mheshimiwa Kikwete anaendeleza zile lugha za kisanii tu, kwa sababu hana uwezo yeye wa kuyalinda Mapinduzi. Mapinduzi ya Zanzibar yanalindwa na Wazanzibar wenyewe. Na leo Wazanzibari tukiamua Mapinduzi basi, leo leo yatakuwa hayapo, lakini ni siye siye Wazanzibari ndio tunaoyalinda.

  Nasema kama Kikwete anao uwezo wa kuyalinda Mapinduzi, kwanza angewalinda Albino wanaouliwa kama wadudu. Hawa ni binaadamu, wanakufa katika nchi yake, anashindwa kuzuwia. Ataweza kuzuia watu wakitaka kuyapindua Mapinduzi? Kwa hivyo ni usanii tu. Au atwambie, kwa sababu magazeti yanaandika kuwa albino wanakufa kwa sababu ya ushirikina wa watu kutafuta mali na vyeo, ni miongoni mwa hao wanaotafuta vyeo na hivyo anaruhusu wale wauliwe? Kama harusu, hana uwezo wa kuyalinda Mapinduzi. Kwanza atuoneshe mfano, awalinde albino wasiuliwe. Akituonesha mfano kwamba albino hawafi – na kawazuia yeye – basi tutaamini anao uwezo wa kuyalinda Mapinduzi. Nawalinde wale.

  Kinachosikitisha, ni mtu asiye huruma. Mimi nikifikiri huyu Pinda ndiye aliyekuwa hana huruma, kumbe yeye (Kikwete) ndiyo hana huruma. Pinda kalia Bungeni. Kikwete ashazunguka nchi nzima hii, hajawahi hata kutoa kauli kuwaonea huruma albino. Ana huruma huyu? Albino wanakufa ndani ya nchi yake, tena kule Bara, yeye hana habari nao. Pinda mwenzake kalia, kafika kutoa kauli kinyume na katiba ya nchi na sheria ya nchi, anasema hao wanoua nanyi waueni. Uchungu aliouona wale watu wanavyopoteza maisha. Yeye (Kikwete) hajasema lolote, badala yake kaja Zanzibar anataka kutugawa.

  Lakini nataka niwambieni waheshimiwa mufahamu kwamba, sasa hivi Wazanzibari hawagawiki. Juzi nimefatwa ofisini na mtu wa CCM, ananambia Kikwete kachelewa. Nikamuuliza kwa nini, ananambia: “Sisi dai letu ni Zanzibari bwana, sio kutuganya tena. Tushachoka. Sisi tunataka nchi. Tutambulie kama nchi. Asitwambie kwamba Zanzibar nini sijui nini. Hapana, atwambie anakubaliana na sisi kuwa hii nayo ni nchi. Akikubali hilo, sawa atakuwa rafiki yetu. Hakukubali hilo, sisi Wazanzibari –
  hakuna CUF hakuna CCM – tushaamua, hatutaki tena! Sisi hapo (kwenye msimamo huo) hatuondoki tena

  Halafu (Kikwete) anatwambia: “Ooh, CUF wasitegemee kupata serikali. Mtachagua wabunge na wawakilishi.” Mie namkumbusha maneno hayo aliyasema baba yake wa taifa, Nyerere. Nyerere alisema atamuona rais wa sita wa Tanzania, alimuona? Hana hakika, basi Kikwete. Haya anayeyajua ni Mungu, sio Kikwete. Kikwete unabahatisha tu, huna hakika. Suala la kuwa 2010 CCM inaondoka au inabakia, hilo anajua Mungu tu, halijui Kikwete. Na kama yeye anapanga hilo, na Mungu anapanga lake. Tungojee.

  Tusisitushwe na hilo. Labda nia yake turudi nyuma, tusijitokeze kwa kufikiria yale yale kuwa hawa hawatupi serikali. Tusifike huko. Hapa ndipo tunapoanzia sisi Wazanzibari kulinda haki ya nchi yetu.

  Sasa hilo ni moja na dogo. Kubwa nataka muelewe kuwa sisi Zanzibar na Tanzania hatuna tume za uchaguzi. Hawa watu (tume zilizopo) wamewekwa na CCM kuisaidia CCM itawale maisha. Mumesikia Mbeye huko (kwenye uchaguzi mdogo wa Mbeye Vijijini). Na hapa Zanzibar nataka mutambue muwa huyu mwenyekiti wa sasa tume hii alikuwa ndiye sekreterieti wa tume iliyopita. Uchaguzi uliopita masheha waliwazuia watu wasiandikishwe, Tume ikasema inathubutu masheha kuzungumza nao, masheha hawakwenda kuitikia wito wa Tume; na Tume ikabakia kunyamaza kimya. Hiyo ndiyo tume iliyopita na ndiyo tuliyonayo sasa hivi.

  Kwa hivyo hili ndilo suala la kulifanyia kazi. Usije ukategemea kupata haki yako kupitia tume ya uchaguzi, hupati. Jipange, jitayarishe, ona kwamba haki yako unaipata kutokana na uwezo aliokupa Mwenyezi Mungu. Sawa?

  Daftari linakuja, vitimbi mtaanza kuviona. Kama kutishwa ndio tushaambiwa hivyo, kama kuuliwa ndio pashaagizwa hivyo. Kwa hivyo, musije mukafikiri haya yanayosemwa yanasemwa kwa 2010, inaweza ikawa yanasemwa kwa wakati huu huu wa Daftari. Wasije wakatufumba, tukaona wao wataanza 2010 kumbe wao wataanza sasa hivi. CCM haaminiki. Akikwambia tukutane Mwembeladu, wewe kamngoje Micheweni.

  Tushukuru kwamba CCM wenzake wa Zanzibar hawakubaliani naye. Kwa hivyo, tuungane na wananchi wenzetu – wa CCM – ambao wanakubaliana na sisi katika kuitetea nchi. Yeye kaja kupandikiza chuki, nyinyi musiwachukie CCM. Wananchi Zanzibar musiwachukie CCM.
  Tushirikiane nao tujiandikishe kwenye Daftari, twende kwenye uchaguzi tuone ikiwa CCM hii iliyosema Zanzibar si nchi itabakia madarakani.


  Hotuba kamili: Juma Duni Haji -Mzanzibari,Katibu Naibu Mkuu - CUF
  “Wanaoua albino wauawe, walioua Wazanzibari je?”
  7/02/2009

  Kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Mhe. Juma Duni Haji, katika Mkutano wa Nane wa Maombolezi ya Januari 2001, uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti, mjini Zanzibar, tarehe 31 Januari, 2009

  Sina hakika, lakini juzi nilipokuwa natizama Bunge (vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano), alipoulizwa Mheshimiwa Pinda (Waziri Mkuu) kuhusu mauaji ya maalbino, nadhani ilikuwa tarehe 27 Januari, siku ambayo watu sisi pia waliuliwa, basi namna vile alivyokuwa na huzuni, vile alivyokuwa akilia masikini na mie nikawa ninalia. Lakini kilio cha Pinda na changu kidogo vilikuwa tafauti, maana Pinda alichoambiwa na Kiongozi wetu wa Upinzani Bungeni (Hamad Rashid Mohammed) haoni kuwa si vizuri yule anayedhaniwa kupiga au kuua albino, apelekewe mahkamani, maana (kabla ya hapo) kwa namna alivyoona uchungu, Pinda alikuwa amesema anayeuwa albino naye auliwe.

  Nikasema lo, Mashallah! Anayeua albino anaye auliwe, aliyewaua Watanzania na Wazanzibari tarehe 27, afanywe nini? Maana kama ni mwanaadamu na ni uchungu wa roho, roho ya albino na roho ya Mzanzibari ni sawa sawa. Tafauti iliyopo ni kwamba yule aliyemuua albino hajapatikana, bado anasakwa, lakini walowaua Watanzania na Wazanzibari tarehe 27 wanajuilikanwa. Tena wengine, baada ya kuua, Mheshimiwa Mkapa kawatunza vyeo, ati wamefanya kazi nzuri kutuua.

  Sasa, kufa ni kufa, roho ni roho. Kamisheni ya Mheshimiwa Hashim Mbita ilishathibitisha yaliyotokea wakati huo wa tarehe 27, basi tungelitegemea angalau wao wakafikishwa mahkamani; maana wanajuilikanwa. Lakini Mheshimiwa Pinda analia kwa uchungu, anasahau kuwa sisi pia tunalia kwa uchungu. Lakini sisi tulipouliwa watu walipewa vyeo. Wanapewa vyeo kwa kutuua? Ee, Mungu we! Hilo ndilo lililonisikitisha.

  Sasa kama hilo halitoshi, nikasikitika zaidi kwa Mheshimiwa Kikwete unakuja Zanzibar, badala ya kutusahaulisha yaliyotokea, unatukumbusha? Mashallah, hivo wewe ndo rais kweli weye!?

  --------------------------
  Hizo ndizo siasa ziliyopo Zanzibar ,hakuna kushughulikia ufisadi wakati waliopo madarakani ndio mafisadi dawa yao ni kampeni ya kung'olewa ,Viongozi wa Upinzani T/Bara mnayaweza hayo -CHADEMA.TLP,SAU,NCCR na vyenginevyo mpira kuelekea uchaguzi MKUU @ 2010 ndio umeanza ,naona mpo na mafisadi
  mmoja akioza wameoza wote msemo wa kiswahili huo lazima muufanyie kazi kikwelikweli ,hakuna kulala ,tunatahitaji kuona CCM inang'olewa natumai mumefahamu.
   
  Last edited: Feb 7, 2009
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hizi siasa za CUF na Seif!

  Hivi bado kuna Mtz anaamini vifo vya 2001 Mkapa alifanya mauaji? Tena ya makusudi? Ili apate faida gani wakati tayari alikuwa raisi wa JMT?

  Kazi kweli kweli!
   
 3. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Siasa za Unguja & Pemba zina matatizo yake,lakini na hawa Waungwana nao inatakiwa wajue kuchuja maneno na kuelewa wanazungumza na nani.....Tukienda mwendo huu tutakuwa hatumalizi matatizo bali itakuwa uchochezi na kuonyeshana nani zaidi!!!Serikali inashindwa kujadili masuala ya Zanzibar kwa uwazi...Tunaweza kushiriki vizuri kwenye migogoro ya ndani ya Congo (DRC),Comoro,Kenya,Madagascar,Somali na hata Zimbabwe iweje tunashindwa kwetu.....Nina imani Serikali ikielekeza nguvu zake kwenye kutafuta suluhisho la Mgogoro wa zanzibar tutaweza....Tusiende Zanzibar kwa kofia zetu za Itikadi za vyama...Tukazungumze huko kama watendaji wa serikali.
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Maneno mazito sana haya Mwawado, ila I do not care what kama kiongozi wa taifa huko Zanzibar anaweza kuongea hizo lugha to the public, basi ni vyema Bara tukawalinda ndugu zetu weusi wa huko, tena by anymeans necessary na infact ndiyo the only interest we have na huko anyways!
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Unamaanisha wasio weusi sii ndugu zetu FMES?

  Mbona unaanza kuwa mbaguzi ndugu yangu?
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Feb 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hawawezi kujenga hoja bila vitisho?
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu vipi hivi unajua sababu iliyomfanya Karume kuomba Muungano na Mwalimu? Sometimes siasa ziwe zinafika mwisho, our interest kule ni ndugu zetu na sio anything else, maana tunajua kua kuna Sultani mmoja kule London, anaisubiri sana Zanzibar,

  - Ndio maana siasa za Seif ni za Visiwani, na sio Bara infact he does not care kuhusu Bara sasa kwa nini sisi tumjali? Rais gani mtarajiwa anyeongea lugha za hovyo kwa wananchi kama huyu Seif, I mean na hawa CUF nao tumewaambia sana kwamba as long wana huyu kiongozi wataishia kuchezewa na kulia lia tu sijui mpaka lini!
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kufanya biashara IKULU ni mauaji au hujui ,amekabidhiwa sehemu nyeti anaenda kugeuza genge la biashara ,eti kuna Mtz ?kaitafute ripoti ya akina Mbita ndio utajua ,kuna watu wameshiriki wakati wa Hitler na wamefikishwa mahakamni au hujui ? Mzalendo halisi hatakiwi kuzubaa ni lazima awe macho na nchi yake ,na hakuna zaidi ya hapo ,ndipo utajiita Mzalendo ,lakini nchi inaporwa wewe umekaa hivi Mkapa alifanya biashara Ikulu ? We vipi salama lkn? Kama unajiita mzalendo basi ni lazima uwe na uchungu wa Nchi yako watu wanaliibia Taifa wewe unahoji nani aseme ? Seif na wengine ni viumbe ambavyo ikifika siku yao wataaga dunia tu,hilo halina mjadala lakini mnapopata kiongozi akasimama kidete na kutetea haki ya wanyonge basi ni lazima apewe heshima yake na anapotokea mwengine akaikanyaga haki ya wanyonge basi ni lazima asemwe ,haitokuwa busara ikiwa wewe ni mzalendo wa kweli unaona nchi inavurugwa,nchi inaibiwa,walioko serikali ambao wamepewa dhamana wanatumia serikali na vyombo vyake kuwepo madarakani kwa ajili ya maslahi binafsi wewe mzalendo ukakaa kimya ,hivi uzalendo wako utakuwepo wapi ?

  Isitoshe Wazanzibari wanaposemea Zanzibar ujue ndio wanaisemea Tanganyika vilevile muamko na muamsho unaopatikana huko vilevile utawaamsha wanaodhalilishwa kimaisha ambapo muiba kuku anasekwa rumande na anaeiba mabilioni anatembea mitaani huku serikali ikijua kuwa ni mwizi wa mali ya Taifa ,mwizi ambae alitakiwa hata dhamana asipewe na ndio wezi wa wahujumu uchumi ,na kwa vile ni viongozi hawa walikuwa wasipate hata wakili wa kuwapapatua kwani mawakili ni watu ambao wana uwezo wa kuibadili kweli na kuonekana uongo au sio kweli ?
  Usiwe mwoga tetea taifa lako.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nani hao hawawezi kujenga hoja ? Unajua inawezekana sijakuelewa hasa kwa kuandika maneno yako matano ambayo yanakulinda usimalise yale uliyonayo kwa kukupa uendelezaji wa baadae ,ni moja ya technics za kuzungumza katika kujadiliana.

  Ila kitu kimoja ni lazima mufahamu siasa hazitaki hoja hasa unapokuwa kwenye majukwaa ,pale hakuna bunge au kikao cha bajeti ,umezunguukwa na wananchi wanaotaka kusikia kile kilichondani kabisa na kinachosisimua ,anaezungumza kwa hoja katika mikutano ni mmoja tu ambae ni Lipumba(Prof) na mara nyingi akishazungumza mikutani miwili mitatu utaelewa mikutano yake mingine akiwa ziarani.

  Waliotimua vumbi la kumueleza Kikwete ni wanamapinduzi wenyewe kuanzia Seif Sharif(Aliekuwa CCM na vyeo vingi kapitia ndani ya CCM nae ameikataa CCM na hatorudi tena ) mpaka Machano (Aliekuwa mkubwa wa Polisi Zanzibar na CCM ameikataa CCM na hatorudi tena) mtu wa msimamo,Juma Duni haji halikadhalika alikuwa CCM ameikataa na hatorudi tena . Hao ni wazalendo halisi wa Zanzibar na wameshafungwa kwa kesi za kihaini za kubuniwa.Hawakuambiwa wanataka kumrudisha sultani ,maana ushahidi huo haupo mnao nyinyi mnaodumazwa na kasumba za wagawe uwatawale.

  Na wewe unaesema kuwa Karume aliomba Muungano kwa Baba yenu Nyerere kama huyajui bora unyamaze tu.
  Msimamo wa WaZanzibari ni kuingoa CCM madarakani basi hakuna jingine hayo ya kurudisha sultani wamewaachia WaTanganyika wadanganywe ili wazidi kuruhusu mafisadiwa CCM ili walinde maslahi yao binafsi ,na moja ya njia za kuiondoa CCM wameshaigundua ni kuungana kwao ambako kumeleta matunda Pemba na Unguja kilichobaki ni kuiondoa madarakani kwa nguvu na palipobakia ni padogo sana na hapo ndio pako njiani kumalizwa ,CCM si chama cha kuwekwa madarakani kwani kama kilikuwa na nia njema kwa mataifa haya mawili leo hii watru wangekuwepo mbali sana ,amani wanayoiona ipo ikitoweka sababu ni wao.
   
  Last edited: Feb 7, 2009
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hii ndio lugha iliyowaangusha CCM kule Pemba ,lugha hii ndio inayowafaa CCM ,lugha hii ndio inayovutia wananchi ,lugha hii ndio ya kufahamika kwa raia wanyonge waliochoka na CCM na lugha hii ndio inayozungumzwa katika majukwaa zaidi inapotokea kujibu mapigo ,hutakiwi kwenda mahakamani unajiamini panda jukwaani mwaga pigo ,mwananchi akiondoka hapo kaburudika na amefurahi alichokiendea amekipata na mojakwa moja anaunga mkono chama ,sasa utakwenda majukwaani uanze kufafanua na kuwataja mafisadi wakati hakuna hatua yeyote inayowakumba mafisadi ,unafikiri mwananchi mara ya pili atakusikiliza ,ataona ni watu wamekuja kutuhadithia lakini kwenye mkutano hiyo ya CUF haendi kuhadithiwa mwananchi kumeibiwa nini anaenda kuambiwa Kikwete Serikali yako ni wezi,unawadanganya wananchi, hakuna maendeleo yeyote yale uliyoyaleta, CUF hawakwenda kumwambia mwananchi tutafikisha habari bungeni anaambiwa mtu direct ,huu si wakati wa kutoa nyaraka zinazohusiana na wezi wa serikali huu ni wakati wa kuwambia mlioko serikalini mnakwiba mnawadanganya watu unaenda kuleta habari za kwenda kumlinda mtu mweusi ,ndio hayo hayo waliokwenda kusema kina Kikwete watayalinda mapinduzi wakati wananchi walioahidiwa faida ya mapinduzi wanapiga miayo ,hivi hao wanaolalamika na wanaohutubiwa ni waarabu kama kuna maendeleo wangeona CUF ni waongo na haina hata haja ya kwenda kuwasikiliza ,lakini watu walifika na aliyoyasema Kikwete yote yamekuwa ni uongo ulio wazi ,hakuna kuheshimiana na mtu muongo.Unaposema barabara ni nzuri kama mgongo wa ngisi ,fahamu kuwa wanaozitumia barabara ndio wale wanaokusikiliza sasa hawaoni hizo barabara zao ? kama si dharau na kuwafanya vipofu ni kitu gani ? Mwananchi anaenda kusikiliza nini jawabu ya viongozi wa upinzani kwa Mheshimiwa RAISI upo tunataka kuona akina Slaa na Zito na wengine wakirapu kinamna hiyo dhidi ya CCM sio kutafuta nani mwizi ,wezi wapo na hawawezi kukamatwa chini ya Utawala wa serikali yao ya CCM ni kujidanganya wandugu hawa wang'olewe kwanza ndipo washitakiwe kikwelikweli.Unafikiri angepata dhamana mtu ?
   
  Last edited: Feb 7, 2009
 11. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Field marshall ulikuwa na maana gani uliposema kuna Sultani mmoja kule London, anaisubiri sana Zanzibar? pili sijuwi kama ulikuwa unazifatilia hutuba za mwalimu katika uhai wake ?mara kwa mara alikuwa alisema wakoloni ni watu wabaya wabaya sana sana sana na wanachi karibu sote tulikuwa tunaelewa alikuwa anamainisha ni watu gani ukiangalia leo yale ambayo yote mwalimu alikwisha yaona na kuyapigania yasiwepo kwetu ndio yapo wale wakoloni aliokuwa anawahofia mwalimu leo ndio wanasauti na mamlaka katika uchumi wetu sasa hii nikusema WAKOLONI wanareshwa ku reclaim walivyo viwacha wakati ule mwalimu analipigania taifa hili ?
   
 12. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu FM ES, maneno yako mazito, nikujuavyo uCCM hivyo lazima utumie kila njia kuitetea CCM. Lakini lugha za ubaguzi kwa sasa hazifai. Hizo historia unazotoa kuwa tunatakiwa linda watu weusi hazifai. Mandela alifungwa na wazungu, lakini alipopata uRais hakuwafanyizia wale wazungu. Bali aliwaacha hata katika Serikali, kumbuka Waziri wa Fedha alikuwa mzungu. Hata alipolihutubia Bunge la Uingreza, aliwashangaza wazungu pale alipozungumzia madhila ya makaburu, lakini mwishoni akasema yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

  Ukianza kufunua historia, kuwa wale weusi ndio ndugu, na hawa weupe (ama wekundu, njano) sio ndugu, ukiwamaliza weupe utaelekea wapi?. Kwa Zanzibar hakuna ubishi kuwa CUF wako juu, sasa tusitumie njia za kubaguana, hatujengi bali tunabomoa, na siku zote uongo hujitenga na ukweli. Kama ingekuwa CUF wana tatizo Zanzibar wasingekuwa wanashinda chaguzi lakini wanaibiwa kura. Hivyo tusianze ingiza rangi katika kupingana, tutumie sera.
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Amesahau ile nyimbo ya mayai hayarudi ? Sasa haya sijui ni mayai ya ZANZILLA
  Hawa CCM wamewafanya WaTz wote kuwa wapo chini ya ukoloni wao,hakuna sehemu katika Tz hii ambayo inawapa tabu kama Zanzibar ,wanajua fika kuwa maslaha yao yatatoweka Tanzania nzima siku tu Zanzibar ikirejea Nchi kamili na pia kuwepo kwa Taifa la Tanganyika ,asikudanganye mtu CCM haitodumu hata mwaka mmoja ,maana hawana ile imani ya kuongoza nchi imani yao ni kwa maslaha yao tu ni genge moja kubwa ambalo ni hatari sana hapa Tanzania ,mwananchi hafadiki kwa hali yeyote ile ,hakuna faida hata moja ,anachopata Mtanzania ni jasho lake mwenyewe,faida inaingia kwa CCM wachache ambao wamo katika sehemu mbalimbali serikalini na kila mmoja anmega kivyakevyake.Ila Zanzibar wamejikusanya na kusema CCM basi imetosha na inatosha kuwepo madarakani kwa muda wote huo ,cha kushangaza bado waTanganyika tu kuikataa CCM isiendelee kutuburuza kwa maneno ya kujiulu.
   
 14. J

  Japhet Member

  #14
  Feb 7, 2009
  Joined: Jan 26, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Loh!!! Siamini nilichokisoma, ebu wana JF nisaidie: Hivi zile ni hotuba kwa wananchi au ni Taarabu a.k.a rusha roho a.k.a mipasho??????? ....ama kweli waliosema mdebwedo (ze comedy) hawakukuosea....
   
 15. M

  Mkuu Senior Member

  #15
  Feb 8, 2009
  Joined: Jan 1, 2007
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mzee FM ES
  Ninakuona mzee nawewe uzalendo kama unakushinda unajaribu kuonyesha rangi yako halisi hojazako nilikuwa ninapenda sana kuwa ni hoja ambazo zimekwenda shule
  Lakini kwa hili mzee naona kama umeteleza au ndio hasira tu hizo za PM?MIMI SIKUJUA KAMA unawatetea weusi tu serayako mzee jaribu kuirekebisha sio nzuri unaheshimika sana mzee fmes
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,573
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Mkisoma kwa makini ni kwamba maalim Seif na wafuasi wake wanaamini kuwa Tanganyika imeivamia Zanzibara na inaikalia kimabavu,kwa maana ningine Tanganyika ina i occupy Zanzibar...Kwa kifupi Maalim anaamini kuwa si mungano bali ni uvamizi,sasa kama wazanzibari ndiyo wanachoamini sijui nini kitafanyika maana inaonyesha kunaweza kutokea vurugu nyingine tena.
  Kwa mfano quote hii hapo chini inaonyesha kuwa muungao haukubaliki huko Zenji na wanaamini Tanganyika ni kama makaburu wanaowanyonya na ndio maana hawapati maendeleo.

   
 17. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Naamini sii msimamo wa Wazanzibari wote ..ni wakina Seif na baadhi ya wanachama wa CUF...na mawazo kama haya basi Seif hawezi kuaminika kuiongoza Zenj!

  Mbona Bara Wazanzibari wapo wengi tu wanapeta na biashara zao? Kariakoo na juzi nilikutana nao Mbarali-Mbeya wakifanya biashara ya mchele kule?
   
 18. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ukimwona mtu anaishambulia CCM na kushabikia CHADEMA upande wa Bara huku akiipiga vita CUF hasa hasa Zanzibar basi mujue analake jambo!! tena anaposhabikia ubaguzi wa rangi na kuonyesha hisia zake za chuki waziwazi kwa kuwabagua Wa Zenji wenye asili za kiarabu mtu kama huyu ni wakuogopwa kama UKIMWI!! mtu huyu ni mgonjwa na anahitaji kulazwa ICU ili atibiwe!!

  Tuache unafiki linapokuja suala la Zanizibar na mauwaji ya halaiki huko Pemba 2001!
  Damu za wenzetu zilimwagwa na leo tunajaribu kuhalalisha mauwaji hayo kupitia mlango wa nyuma! oo Usultani, tuwalinde wenzetu weusi, bla, bla, bla, upuuzi mtupu!!!
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Irrelevant, kama Seif ana haya mawazo siku nyingi sana kwa nini hakuyasema kule Mbeya kwenye uchaguzi mdogo wa bunge majuzi kwa nini ameenda kuyasemea Visiwani? Wewe unajua kua angesema haya maneno Mbeya CUF wasingepata kura hata moja, yaani kweli unategemea Tanzania bara tutakwua na patner in leadership huko visiwani ambaye ni capable wa kutema hizi sumu to the public? Are you kidding me or what?

  - CCM imeangushwa Pemba big deal kwani haikuangushwa Karatu? au Kigoma kwa Zitto, na vipi kwa Ndesamburo CCM haikuangushwa? Mkuu unaelewa maana ya siasa za vyama vingi? Sasa kama kushindwa Pemba ni big deal then hivi vilio vyenu vinatoka wapi? Okay maneno yenu haya yanawaamusha wananchi then kilio cha nini?

  Mkuu mpaka mtakapoachana na huyu Seif ndio mnaweza kuona matunda ya uhuru, jamaa kumbe ni mtupu kabisa kisiasa now I see kumbe wananchi wa huko Visiwani sio wajinga, no wonder mnalilia kwenye sidelines for the last 15 years, mara mgome kuapishwa, halafu tena mnakuja mbio kulilia ruzuku, mara mgome kumtambua rais wenu huko, lakini mkinyimwa hela tu za ruzuku mnamtambua haraka haraka, Mkuu wangu mawazo yako sio ya wananchi wengi huko Visiwani, labda wewe tu na Seif, poleni sana!
   
 20. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
   
Loading...