Sakata la Warere Beach hotel kwa mtalii mgeni, Serikali ichunguze, wahusika wachukuliwe hatua, wametia doa sekta ya utalii nchini

Mentojo

Member
Jul 10, 2021
36
67
Katika pitapita zangu za leo nimekutana na tweet hii ya binti kutoka Nigeria,aliyekuja Tanzania kwenye matembezi na kusherekea sikukuu yake ya kuzaliwa .



Ameeleza namna ambavyo alikuwa amelala Warere beach hotel na usiku wa manane akashangaa kuna mwanaume kitandani anampapasa papasa na kutaka kumbaka.
Kwa namna alivyoandika habari hii naona kuna shida kubwa sana katika hiyo hotel..kuna shida namna polisi aliporipoti walivyolichukulia na kushughulikia jambo lake.

Lakini pia to me namuona kama binti ambaye ni very strong,kama asingekuwa na hizo evidence huenda angeambiwa kapika hili jambo.Pamoja na kwamba kalitoa wakati huu ambao tuna issue ya uzinduzi wa royal tour ni vyema serikali yetu ilifuatilia kwa karibu na kutoa majibu ya sakata hili.

Nimeangalia hiyo tweeter namna inakuwa retweeted na baadhi ya comments za watu kucancel Plans zao za kuja Tanzania baada ya hiyo habari...ni aibu kwa kweli..wahusika wawajibishwe na binti huyo arudishiwe fedha zake. Kama kuna hotel zingine wenye tabia kama hii zikomeshwe pia mara moja ili kuendelea kulinda na kukuza sekta yetu ya utalii.Raisi wetu anajitahidi sana lakini unakuta tuna watu wenye akili mgando kama hao wa hiyo hotel.Kama room ilifungwa,namna ya mtu mwingine kuingia ni ipi?

UPDATES
Tayari serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia commision ya utalii imetoa statement na kwamba uchunguzi umeanza mara moja

UPDATES
Jeshi la polisi Zanzibar,limeeleza kuhusu ukweli wa tukio hili,lakini Bi.Zainab inasemekana alidai fidia ya dola 10,000 ambapo fidia za namna hiyo hutolewa mahakamani,hivyo alishauriwa kupeleka kesi hiyo mahakamani,ata hivyo hakuwa na uthibitisho wa kutosha kwani alieleza anamtambua mtuhumiwa kwa harufu tu.





20220417_075439.jpg
 
Back
Top Bottom