Sakata la uenyekiti ACT: LIMBU amvaa Zitto

Sakata la uenyekiti ACT: LIMBU amvaa Zitto

Matumizi mabaya ya Ruzuku ya Chadema ndo yanayomuwewesesha huyu kibaraka wa ufipa. Aliyemwambia Zito anagombea nani? Mbona watu wanaweweseka na vionjo,je likianza movie si ndo watatembea uchi?

Huyu Limbu nasikia ni ndugu wa damu wa Lissu ambaye ndiye hamtaki kabisa Zitto awe na maisha yake duniani. Nadhani anapokea maelekezo.
 
Poleni Madalali wa siasa, ACT Tanzania ipo, na itaendelea kuwepo. Karibuni kwenye uzinduzi wa chama tarehe 29/03/2015
 
BAADA ya kutimuliwa Chadema na kukimbilia Chama cha ACT-Tanzania, Zitto ameanza kuwekewa vigingi akitakiwa kutogombea nafasi yoyote ya uongozi wa kitaifa utakaofanyika 28 Machi mwaka huu.
Kigingi hicho, kimewekwa na Mwenyekiti wa ACT aliyesimamishwa uongozi, Kadawi Limbu, akisema Zitto aliyejiunga na chama hicho siku nne zilizopita anapaswa kusubiri mpaka atakapotimiza miezi sita ya uwanachama wake.


​
Limbu ambaye bado anajitambua kama mwenyekiti halali wa ACT-Tanzania, ametoa tamko hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

"Mimi bado ndiye mwanyekiti wa ACT- Tanzania kwa vile barua inayodaiwa kuniondoa katika nafasi ya uenyekiti haikuwa halali na ilinifanya nipeleke suala hilo mahakamani kwa ajili ya kupata muongozo,"amesema.

Kwa mujibu wa Limbu, katiba ya chama hicho inaelekeza wazi kwamba mwanachama yeyote anayetaka kugombea nafasi ya uongozi ni lazima uwanachama wake uwe umetimiza zaidi ya miezi sita tangu ajiunge na chama hicho.

"Mkiangalia mtaona Zitto ambaye amejiunga na chama hicho hivi karibuni katika mazingira tata, katiba haimruhusu kugombea nafasi yeyote katika chama chetu, nimuombe kwamba andelee kuwa mwanachama wa kawaida tu,"amesema Limbu.

Pia, amemtaka Katibu Mkuu wa ACT-Tanzania, Samson Mwigamba kuacha kuwapotosha wanachama kuhusu uchaguzi huo kwani sio wa halali kutokana na Limbu kufungua kesi ya kikatiba mahakamani kupinga kuondolewa katika nafasi ya uenyekiti.

Akizungumzia chanzo cha mgogoro huo, Limbu amesema yote hayo yamechangiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutokana ofisi hiyo kufanya kazi kwa utashi huku ikitoa taarifa zinazokanganya.

Limbu amefafanua kuwa ameamua kumpeleka Msajili katika Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa madai kuwa amekula njama katika kumpa barua ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Ametoa angalizo kwamba atapigana hadi kufa kuliko kuona chama hicho walichokianzisha kwa gharama kubwa, kikiangukia mikononi mwa mafisadi.

"Kuna watu wanajiita wazalendo lakini ukiwafuatilia utabaini kuwa wamejivika kofia hiyo kwa ajili ya kunyang'anya haki za wenzao. Watu hao ni sawa na majambazi,"amesema.

Hata hivyo, uongozi wa ACT-Tanzania, umesema katiba yao, iliyoko kwa Msajili wa vyama vya siasa, inaonesha kwamba mwanachama yeyote anaweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi endapo ametimiza siku saba tangu ajiunge na chama hicho.
 
Hala hala mti na macho, mbeleko ya Hon. Zito haimwenei tena. Njoo kwetu sisiem tukupe jimbo
 
zzk hakosi ugonjwa wa shinikizo la damu adi mda huu!!!
 
Hatakwenye kanga yappo
anawatessa naa atawatesa kwelii
 
We ulidhani nakutania nilivyokwambia nahamia siasani? Nimewachoka wewe na chige nimewaachia jukwaa lenu, niko busy na zito kabwe na uchaguzi mkuu

Huku utalimwa ban kila siku
 
Last edited by a moderator:
Bora nipewe ban ntashukuru kuliko vituko vyenu mnavyonifanyia, toka juzi sipumui na huyo ndomo wenu, niacheni

😈😈😈😈😈😈😈😈
 
Anakipindi kigumu sana huyu Kijana,inshallah mwenyezi mungu atamfanyia wepesi...
 
Nasikia pingamizi la Limbu limetupiliwa mbali na mahakama kuu leo hii!
 
Kwani zzk anataka kugombea uwenyekiti ACT? Kam atagombea basi act waangalie taratibu za kugombea,mwanachama hana hata mwezi agombee uongozi?
 
Back
Top Bottom