Sakata la uenyekiti ACT: LIMBU amvaa Zitto

Alfred Daud Pigangoma

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2009
Posts
1,833
Reaction score
972
MWENYEKITI wa Chama cha Mabadiliko na Uwazi (ACT-Tanzania), Kadawi Limbu, amemtaka mwanachama mpya wa chama hicho Zitto Kabwe, kuachana na mawazo ya kugombea nafasi ya uongozi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu hadi atakapotimiza miezi sita ya uwanachama wake.

Limbu ambaye anapinga kuondolewa kwenye nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

¡°Mimi bado ndio mwanyekiti wa ACT- Tanzania kwa vile barua inayodaiwakuniondoa katika nafasi ya uenyekiti haikuwa halali na ili nifanya kupeleka suala hilo mahakamani kwa ajili ya kupata muongozo,¡±alisema Limbu.

Limbu, alisema hivyo kwa vile katiba ya chama hicho inaelekeza wazi kwamba mwanachama yeyote anayetaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi ni lazima uwanachama wake uwe umetimiza zaidi ya miezi sita tangu ajiunge na chama hicho.

¡°Mkiangalia mtaona Zitto ambaye amejiunga na chama hicho hivi karibuni katika mazingira tata, katiba haimruhusu kugombea nafasi yeyote katika chama chetu ni muombe kwamba andelee kuwa mwanachama wakawaida tu,¡±alisema Limbu.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo, alimtaka Katibu Mkuu wa Chama hicho Samson Mwigamba kuacha kuwapotosha wanachama kuhusu uchaguzi huo kwani uchaguzi huo siyo halali kutokana na mwenyekiti huyo kwena mahakamai kupinga kuondolewa katika nafasi hiyo
.
Akizungumzia chanzo cha mgogoro huo, Limbu alisema yote hayo yamechangiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutokana naofisi hiyo kufanya kazi kwa utashi huku ikitoa taarifa zinazochanganya katika vyama.

Aliwataka wanachama wa chama hicho kutambua kuwa msajili huyo siyo anayepanga uongozi ndani ya vyama vya siasa.
Limbu alidai kuwa ameamua kumpeleka Msajili katika Ofisi za Taasi ya Kuuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai kuwa amekula njama katika kumpa barua ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Limbu alitoa angalizo kwamba atapigana hadi kufa kuliko kuona chama hicho walichokianzisha kwa gharama kubwa kukiona kikiangukia mikononi mwa mafisadi.

Alisema kuna watu wanajiita wazalendo lakini ukiwafuatilia utabaini kuwa wamejivika kofia hiyo kwa ajili ya kunyang¡¯anya haki za haki za watu, watu hao ni sawa na majambazi.

Msemaji wa ACT-Tanzania, Abdallah Khamis, alisema katiba ya chama hicho, iliyoko kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, inaonesha kwamba mwanachama yeyote anaweza kugombea nafasi yeyote ya uongozi endapo ametimiza siku saba tangu ajiunge na chama hicho.

Pia alisema kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa kwa vile chama hicho hakina mgogoro wa kiuongozi mahakamani bali wanachojua shauri lililoko mahakamani ni la mtu binafsi.

¡°Huyu sio mwenyekiti tena wa chama chetu naomba muelewe hivyo amejiita mwenyekiti atakuwa amefanya makosa na kuna hatari ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria kuweni makini naye,¡±alisema Khamis.

Khamis, alimuonya aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa chama hicho kuacha kupitapita mitaani na kuwapotosha wanachama badala yake kama anataka kuwa kiongozi ajipange kugombea na yeyote katika uchaguzi huo Mach 28 mwaka huu.
Po
 
Matumizi mabaya ya Ruzuku ya Chadema ndo yanayomuwewesesha huyu kibaraka wa ufipa. Aliyemwambia Zito anagombea nani? Mbona watu wanaweweseka na vionjo,je likianza movie si ndo watatembea uchi?
 
MWENYEKITI wa Chama cha Mabadiliko na Uwazi (ACT-Tanzania), Kadawi Limbu, amemtaka mwanachama mpya wa chama hicho Zitto Kabwe, kuachana na mawazo ya kugombea nafasi ya uongozi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu hadi atakapotimiza miezi sita ya uwanachama wake.
Limbu ambaye anapinga kuondolewa kwenye nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
¡°Mimi bado ndio mwanyekiti wa ACT- Tanzania kwa vile barua inayodaiwakuniondoa katika nafasi ya uenyekiti haikuwa halali na ili nifanya kupeleka suala hilo mahakamani kwa ajili ya kupata muongozo,¡±alisema Limbu.
Limbu, alisema hivyo kwa vile katiba ya chama hicho inaelekeza wazi kwamba mwanachama yeyote anayetaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi ni lazima uwanachama wake uwe umetimiza zaidi ya miezi sita tangu ajiunge na chama hicho.
¡°Mkiangalia mtaona Zitto ambaye amejiunga na chama hicho hivi karibuni katika mazingira tata, katiba haimruhusu kugombea nafasi yeyote katika chama chetu ni muombe kwamba andelee kuwa mwanachama wakawaida tu,¡±alisema Limbu.
Hata hivyo, mwenyekiti huyo, alimtaka Katibu Mkuu wa Chama hicho Samson Mwigamba kuacha kuwapotosha wanachamakuhusu uchaguzi huo kwani uchaguzi huo siyo halali kutokana na mwenyekiti huyo kwena mahakamai kupinga kuondolewa katika nafasi hiyo.
Akizungumzia chanzo cha mgogoro huo, Limbu alisema yote hayo yamechangiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutokana naofisi hiyo kufanya kazi kwa utashi huku ikitoa taarifa zinazochanganya katika vyama.
Aliwataka wanachama wa chama hicho kutambua kuwa msajili huyo siyo anayepanga uongozi ndani ya vyama vya siasa.
Limbu alidai kuwa ameamua kumpeleka Msajili katika Ofisi za Taasi ya Kuuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai kuwa amekula njama katika kumpa barua ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Limbu alitoa angalizo kwamba atapigana hadi kufa kuliko kuona chama hicho walichokianzisha kwa gharama kubwa kukiona kikiangukia mikononi mwa mafisadi.
Alisema kuna watu wanajiita wazalendo lakini ukiwafuatilia utabaini kuwa wamejivika kofia hiyo kwa ajili ya kunyang¡¯anya haki za haki za watu, watu hao ni sawa na majambazi.
Msemaji wa ACT-Tanzania, Abdallah Khamis, alisema katiba ya chama hicho, iliyoko kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, inaonesha kwamba mwanachama yeyote anaweza kugombea nafasi yeyote ya uongozi endapo ametimiza siku saba tangu ajiunge na chama hicho.
Pia alisema kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa kwa vile chama hicho hakina mgogoro wa kiuongozi mahakamani bali wanachojua shauri lililoko mahakamani ni la mtu binafsi.
¡°Huyu sio mwenyekiti tena wa chama chetu naomba muelewe hivyo amejiita mwenyekiti atakuwa amefanya makosa na kuna hatari ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria kuweni makini naye,¡±alisema Khamis.
Khamis, alimuonya aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa chama hicho kuacha kupitapita mitaani na kuwapotosha wanachama badala yake kama anataka kuwa kiongozi ajipange kugombea na yeyote katika uchaguzi huo Mach 28 mwaka huu.
Po

Mods hii ni Breaking News?????
 
ACT kumekuchaaaaa.....ACT Tanzania Vs Tanzania Wazalendo....ngoma bado mbichi
 
Wameanza mgogoro hata week hawana dah kweli chama cha majambazi kweli kweli
Na bado ndio kwanza movie imeanza zitto utajuta.
Mods acheni uzi huu watu wasemezane!
 
A baby is being born same time a man is murderd.!!
 
Zito awe makini kwa sabababu ameshawatuhumu majaji kuwa wanamkandamiza.Je,hiyo kesi dhidi ya ACT,na yeye Zito anataka kuwa mwenyekiti wake,haitahukumiwa kumkandamiza yeye?
 
Simba ukawa
coastalunion ukawa
act ukawaa
 
Ningewashauri ACT msitafute umaarufu kwa mgongo wa CHADEMA kwani hii inaweza kuwajengea shida mbeleni. Eleweni kuwa mnapingana na nani haswa. Kama mkielekeza kasi zenu CDM ni dhahiri mtakuwa upande mmoja na CCM. Kadhalika kwa CDM. Hivyo kwa kuwa Zitto ashajiunga ACT, aachwe ajenge chama chake, na wanachadema nao wandelee na ujenzi wa chama chao. Muda ni ukuta!
 
hiki chama kipo kwa msimu wa uchaguzi tu,lengo ni kuchukua makapi yatakayoachwa na ukawa na ccm!Pia wafuata upepo nao watapokelewa lakini kabla ya2016 watakuwa wamesambaratika kwa chuki na lawama!
 
OeYbgs3k2z afev4HFDI7coWPZeIAAAAASUVORK5CYII=

na hawa wanaitaji jina lao
 
Huyu Limbu anatumwa na Mbowe,huyu Limbu ni msaliti huyu,nyie ACT mlikosa mtu wa kumweka Mwenyekiti hadi mkamuweka huyu karaghabaho Limbu?
 
Mh Zitto ameisoma hiyo katiba kweli?
Kama ameisoma hiyo katiba na akaielewa basi huyu ni mtu hatari sana kwenye taifa hili! na wala hafai kuwa kiongozi ndani ya nchi hii
Kwanza atakuwa amerudia kosa lile ambalo alifukuzwa nalo chadema,kosa la kuvunja katiba sheria na kanuni za chama
mm nafikiri pengine zito hajaisoma hiyo katika ya chama chake cha act
 
Back
Top Bottom