Sakata la Panda Hill: Mkuu wa Mkoa na RPC Mbeya mnapaswa kuachia nafasi zenu haraka

Glenn

JF-Expert Member
May 23, 2015
65,821
156,964
Nchi ya maelekezo kila mahali, kuna siku mtaleta maafa makubwa sana nchi hii.

Ndugu Watanzania, tukiwa katikati ya sakata la DPW, lilibuka sakata la mwanafunzi wa Panda hill school kupotea, kwa jina Ester.

Sakata hili lilivuta hisia za wengi kiasi cha waziri mkuu kutoa tamko kuwa anawaagiza polisi wantafute kwa haraka ili apatikane.

Jambo hili lilizua gumzo kubwa na hisia kali katika jamii.

Katika kupotea kwake Ester, inasemekana aliacha ujumbe usemao " mjihadhari na mwl Jimmy"

Jamii ilijiuliza kwanini Jimmy?

Baada ya agizo la Waziri mkuu, mtoto alipatikana kwa haraka sana, ikadaiwa alikuwa kwa muuza mkaa kwa jina baba Jose akishirikiana na mama muuza genge, mara fundi cherehani...mkanganyiko.

Wote tulishuhudia Ester akihojiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa na alirudia kumtaja Jimmy kuwa ashughukiwe bila ya kufunguka zaidi.

Leo tena kwenye vyombo vya habari, nimeshtushwa mnoo kumsikiliza Ester akihojiwa na ameelezaza kuwa;

1. Mwl Jimmy aliingia bwenini akisaka wanafunzi waliochewa kutoka bwenini.
2. Alimkuta Ester ametoka kuoga na akiwa na kanga moja
3. Akampiga kuwa kwanini amechelewa kuwahi darasani
4. Akamsukumiza kitandani, akamziba mdomo na shuka na KUMWINGILIA KIMWILI

WAZAZI/WALEZI WA ESTER
1. Wamelalamika kuwa mtoto alipopatikana mazingira yalitia shaka
2. Pamoja na mashaka viongozi waliwazuia kuongea tofauti na MAELEKEZO waliopewa
3. Sasa wanaomba haki itendeke kwani ukweli ulifichwa.

MASWALI YANGU KWA MKUU WA MKOA NA RPC
1. Kwanini mlificha ukweli wa jambo hili?
2. Kwanini mkuu wa mkoa alikuwa soft sana alipoiongelea shule ya Panda hill na zaidi akiwamwagia sifa?

3. Hii shule ya Panda hill ni ya kigogo gani serikalini?

HITIMISHO
Mazingira ya kupotea na kupatikana kwa Ester yalizua maswali mengi sana ( HUENDA HATA JINA BABA JOSE NI MAELEKEZO TU).

1. Alitorokaje shuleni wakati kuna geti na ukuta mrefu?

2. Kwanini alimtaja Jimmy?

3. Polisi na mkuu wa mkoa walishindwa nini kumwita Jimmy ahojiwe mbele ya mtoto majibu sahihi yapatikane?
4. Ni lini mtuhumiwa kama huyo hakuchukuliwa hatua za haraka bali waliamua kumfuata kwa muda wao?

4. Kwanini mkuu wa mkoa hakujitokeza tena kuliambia taifa undani wa sakata hilo badala yake Pandahill schooll ndio walipewa nafasi ya kutoa taarifa?

SAKATA HILI LINA VIASHIRIA VYA RUSHWA.

ANGALIZO:
Ninasikitika sana endapo Ester angekuwa ni binti yangu.
1. Jimmy angekuwa mlemavu au mfu kabisa.
2. Hayo maelekezo mliyowapa wazazi...ingekuwa mimi mngenifunga au kunizika, pasingetosha.

Katika maisha yangu kamwe huwezi kumdhalilisha mtoti na mwanamke mbele yangu nikavumilia...sasa awe binti yangu dunia yote ingeiona gharabu yangu.

Kwa mazingira haya Mkuu wa Mkoa na RPC mbeya:
1. Mmewakosea sana watoto wa kike kwa kutokumpa Ester haki yake.

2. Mmewakosea wazazi wote.

3. Mmelikosea na kulikosesha taifa la Tanzania.

ACHIENI NGAZI HARAKA
Screenshot_20230701-130311_Instagram.jpg
 
kwani yanayotendeka shule za bweni mangapi.
yule mtoto aliyeuliwa kule arusha lilizimwa kimya.
kujaza watoto kwenye magari mpaka wakapata ajali.
ni mengi ila hayo polisi hayana pesa sababu sio kesi ya simu
Hili litaleta maafa, si kila mzazi anaweza kuzibwa mdomo kwa pesa wala vitisho.

Mimi najijua kuwa kwenye utu huwa sina bei.

Nitakupoteza fasta bila woga
 
Binti wa kidato Cha 5, mwenye akili timamu, anasoma masomo ya sayansi. Baada ya kubakwa na mwalimu Jimmy anaondoka kwenda kukaa kwa muuza mkaa Baba Jose badala ya kwenda kuripoti polisi au kurudi na kuripoti nyumbani.

Pelekeni mahakamani ili tijue mbivu na mbchi. Uongo na ukweli haupikiki chungu kimoja. Ma classmates wataitwa na tabia halisi ya Esther itawekwa hadharani
 
Ni saw huenda binti ana tabia mbaya, hii haimpi mwalimu uhalali wa kumdhalilisha.
Kazi ya mwalimu ni kubadili tabia.

Pili, maringira ya kulizima hili sakata liko wazi, mwenye shule analinda sifa ya shulw.

Kuhusu mahakama, huu ndio wito wa wazazi sasa wanataka ukwwli na haki vipatikane
 
Binti wa kidato Cha 5, mwenye akili timamu, anasoma masomo ya sayansi. Baada ya kubakwa na mwalimu Jimmy anaondoka kwenda kukaa kwa muuza mkaa Baba Jose badala ya kwenda kuripoti polisi au kurudi na kuripoti nyumbani.

Pelekeni mahakamani ili tijue mbivu na mbchi. Uongo na ukweli haupikiki chungu kimoja. Ma classmates wataitwa na tabia halisi ya Esther itawekwa hadharani
Huyu dogo nae anatafuta kiki au huruma ya jamii,
Why asingeenda kwa kwa wazazi wake? Why usiende mripot police soon, sasa saizi hata evidence hazipo, anatafuta tu wa kufa nae, ila hakuna kitu atasema kitaaminika tena,
 
Mkuu umewahi kupatwa na jambo ukawachukia hadi wazazi wako?

Kama kuna ukweli kuwa alibakwa anaweza kujikuta anawachukia watu wote hadi wazazi waliompeleka shule.

Pili hatuoni kuwa Jimmy alitajwa tangu mwanzo alipoacha barua kabla hajatoroka?

Angemtaja Jimmy baada ya kupatikana hata mimi ningetilia shaka
 
Hapo ticha ajiandae kisaikoliojia kushughulikiwa na wanaharakati uchwara
Haya mambo yapo mkuu.

Kuna shule ya kulipia karibu na ninapoishi, kuna mwl Jina James alikuwa akitembea na wanafunzi wa darasa la 7, ilipojulikana, shule walimhamishia shule yao nyingine kimya kimya kulinda hadhi ya shule...tusikatae wala kukubali kirahisi, ukweli utafutwe kwanza
 
Back
Top Bottom