Tokea Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ujitokeze kujibu kejeli zilizotolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wake, Seif Sharrif Hamad dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, waandishi mbalimbali wa makala magazetini wamekuwa akionyeshana ujuzi na wendawazimu wa kufikiri.
Wengine wanadai UVCCM ilikurupuka, imepoteza mwelekeo, inaelekea kubaya, imekosa hoja na baadhi yao wanafikia mpaka hatua ya kupotosha kuwa tamko lililotolewa na jumuiya hiyo ya CCM kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wake, Francis Isaack Mtinga lilisheheni matusi dhidi ya Lipumba na Seif.
Wapo wanaofikia hatua ya kumsifu Seif kuwa ni msomi aliyeweka rekodi ya kufaulu vizuri wakati akisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka ya 1970, hivyo kwao ni kutukanwa anapokosolewa kuhusu msimamo wake wa kutotaka kura za maoni zitumike kuamua suala la kuwa na Serikali ya Mseto Zanzibar na kungangania vinginevyo.
Hata Lipumba, profesa wa uchumi naye eti anatukanwa kuambiwa kuwa anaburuzwa na Seif katika uongozi wa CUF huku wakijua ni kweli.
Wanasema Lipumba wala Seif hawawezi kuwa na akili za kuku, lakini hawasemi kwa nini wasiwe hivyo kama wanasahau kwa urahisi misimamo yao ya kila mara ya kutamba kwamba CUF inaweza kufanya lolote kwa vile ina nguvu za umma.
Ni akili za kuku pekee ndizo zinaweza kumfanya mtu atambe hivi leo, lakini kesho akiambiwa tekeleza suala hili kwa kutumia tambo zako anageuka ghafla na kusema haiwezekani, ndivyo ilivyo kwa Lipumba na Seif.
Wanasahau mithili ya kuku kwamba siku zote walikuwa wakitangaza dunia nzima kuwa chama chao kina nguvu nyingi Visiwani kuliko CCM, lakini leo wanaoogopa kuingia kwenye kura za maoni ili umma unaowaunga mkono kwa kiasi kikubwa utumike kubariki Serikali ya Mseto, ileile ambayo wamekuwa wakiingangania siku nyingi na tayari Seif alishatangaza kuwa ikiundwa yeye ndiye atakuwa Waziri Kiongozi.
Kuweka rekodi ya kufaulu Chuo Kikuu zaidi ya miaka 30 iliyopita siyo kigezo cha akili wala ubora kisiasa wala katika uongozi wa umma kwa vile hayo ni mambo mawili yanayotofautiana kwa kiasi kikubwa.
Inawezekana alifaulu na kuweka rekodi hiyo kwa sababu alikuwa bingwa wa kukariri kwa ajili ya mitihani badala ya kujifunza ili kujua, ama aliweka rekodi hiyo kwa vile alishirikiana na aliyekuwa mhadhiri wake kuonyeshwa mitihani na kuifanya kabla ya siku kufika tofauti na wenzake.
Inawezekana aliweka rekodi hiyo kwa vile siku hizo alikuwa na akili timamu, lakini sasa akili zake zimeathiriwa na kuukosa urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alioanza kuufukuzia kwa miaka 23 iliyopita.
Wanaodhani kwamba kuweka rekodi ya kufaulu vizuri mitihani ya chuo kikuu ni kipimo cha ubora katika uongozi wa kisiasa au kijamii wanakosea sana.
Unaweza kufaulu vizuri mitihani shuleni au chuoni, lakini ukawa bomu katika uongozi wa umma kutokana na sababu mbalimbali, moja kati yake ikiwa ni ubinafsi kama alionao Seif anayedhani ni haramu kwake kutokuwa Rais wa Zanzibar angalau kwa siku moja tu.
Kama ana akili sana nawaomba wanaomtetea katika hilo waongee naye, wamwelimishe kwamba kwa vile CUF ina nguvu sana Visiwani Zanzibar kama anavyosema mara nyingi na kibaraka wake Lipumba basi wasiogope kura za maoni.
Wawaambie Wazanzibari kuwa msimamo wa CUF ni kutaka iundwe Serikali ya Mseto, hivyo kwa vile wanaiunga mkono kwa wingi wapige kura kubariki matakwa hayo na hakika watakubali kwa vile ndiyo msimamo wa chama wakipendacho kama madai hayo yana ukweli.
Wamwambie atumie akili alizokuwa nazo darasani wakati akisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa uamuzi mzito kama wa kuwa na Serikali ya Mseto kati ya vyama tofauti wakati Katiba inasema chama kinachoshinda uchaguzi mkuu ndicho kinaunda serikali, hivyo wakaichagua CCM na mgombea wake wa urais ni suala linalopaswa kuamuliwa na Wazanzibari wote na si kikundi kidogo cha kina Seif, Ismail Jussa Ladhu, Machano Khamis Bakari au Juma Duni Haji.
Wamwambie asiwe na hofu, aende kila kijiji Unguja na Pemba akanadi msimamo wa chama chake na kwa sababu anasema kina nguvu hakika katika kura za maoni za kutaka iundwe Serikali ya Mseto wapiga kura wataipa ushindi mkubwa CUF dhidi ya CCM.
Kungangania tu eti rasimu ya mazungumzo ya muafaka baina ya CCM na CUF ilipendekeza kuwe na Serikali ya Mseto wakati ukijua tafsiri halisi ya neon rasimu kuwa siyo mkataba wa kisheria wala makubaliano ya mwisho ni upofu wa fikra, uduni wa kufikiri na ndiyo maana wote wanaozungumza vinginevyo dhidi ya tamko la UVCCM ni vizuri waelewe kuwa chombo hicho cha vijana wa CCM hakitabomolewa kwa makala za magazeti.
UVCCM itabaki ileile ikiwa na nguvu na ushawishi uleule katika jamii.