Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Mrithi wa Nchimbi mwenyekiti UVCCM (umoja wa vijana Taifa) Taifa, RIdhwan kikwete katangaza leo kupitia gazeti la Tanzania daima kuwa ana mtu wake anayemtaka...

Conflict of interest - In Tanzania anything goes, well its their time but when the day comes they shouldn't cry.
 
Hivi nyie hamna akili??? nani amewaloga??

Hamuoni jinsi wanavyotoa masharti magumu kwa elimu ya makabwela huku wakisomesha watoto wao huko majuu kwa kodi zetu?? mlidhani wanawasomesha watoto wao kwa manufaa ya nchi yetu???

Wamewasomesha kwa manufaa ya viongozi ambao ndio wazazi wao. Kwa kusoma kwao watakuwa na uchungu na nchi hii kuliko sisi wenye nchi, wanaijua nchi hii kuliko sisi wanakijiji, na kwa taarifa yenu mtapiga kelele ambazo wataziita changamoto na mtakoma.....

Tanzania ina wenyewe ati
 
Ndio Chukua Chako Mapema hiyo mkuu wewe mkulima katafute shamba bado mapori yamejaa hayana watu..

Naona jibu lako ninaweza kuwaumiza watu. Kuna ubaya gani kama akichukua jembe lake na kuingia CHADEMA?
 
kweli wewe una machungu post. Tuchangie ipi? Umesha ulizia nafasi yako kwenye vyama vingine kama CHADEMA?
 
SAM
Nimekupata ila nilikuwa bado nachapisha bahati mbaya umeme ukaleta tatizo lakini mada ya kuchangia ni hii ya sasa..!!
 
ogwalumapesa
umeshaipost hii thread naona umeirejeza tena
 
Mrithi wa Nchimbi mwenyekiti UVCCM (umoja wa vijana Taifa) Taifa, RIdhwan kikwete katangaza leo kupitia gazeti la Tanzania daima kuwa ana mtu wake anayemtaka awe mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa, Zainabu Kawawa (mtoto wa kawawa Rashid) anagombea uenyekiti taifa, Violet Mzindakaya (mtoto wa Mzindakaya Mbunge wa Sumbawanga, na mtuhumiwa wa ufisadi wa sh bilioni 10 kutoka B.O.T) anagombea ijapokuwa kuna minongono kuwa mwishoni atamuunga mkono kipenzi cha Ridhwan ,Mwamvita Makamba(mtoto wa makamba katibu mkuu wa CCM) nae ana mtu wake.

Wana JF nauliza sisi wototo wa wakulima nafasi yetu ipo wapi? katika jumuia kama watoto wa Nyerere, Makongoro, Madaraka, Ana na watoto wa mzee Ruksa Mwinyi Husein, na Abas wangetaka kuwaweka marafiki zao waliosoma nao (kwa maana na wao wanesoma)jumuia ya vijana(UVCCM) igekuwa wap?

Ndio wakati wa kufunua macho ili muone kwamba CCM ni chama cha mafisadi na inabidi kuiogopa CCM kama ukoma. Sasa hivi ili kuwa na sauti ndani ya CCM au kushika nafasi ya uongozi ni lazima uwe na jina zito pia maarufu la Baba au mama, vinginevyo WE URIE TU. Pia uwe tayari kutoa takrima kwa hao wanaokupigia debe ili upate nafasi hiyo, kama unatoka katika familia ya kimaskini na huna uwezo wa kutoa takrima 'rushwa' kwa kiwango ambacho kitawaridhisha wapiga debe wako basi WE URIE TU.

CCM sasa hivi ni chama cha kifisadi, kwa hiyo ni wakati mzuri wa kuvitathmini vyama vya upinzani na hatimaye uchague kila kinachoendana na maadili yako mbali mbali kuhusu Tanzania yetu. Na ukienda huko waambie UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.

Watanzania tunataka waungane na kuunda chama kimoja chenye nguvu ili wakiondoe chama cha mafisadi madarakani. Ndio, Tanzania bila mafisadi inawezekana kabisa.
 
Mkuu sam,
Binafsi siamini watu wanaohama chama kwa sababu ya kutafuta ULAJI.. ndio maana nikatanguliza CCM -Chukua Chako Mapema.
Nje ya hapo wanakaribishwa lakini wasiwe na mategemeo kwani opeo wao upo ktk chaguzi za viongozi.
 
Mkuu sam,
Binafsi siamini watu wanaohama chama kwa sababu ya kutafuta ULAJI.. ndio maana nikatanguliza CCM -Chukua Chako Mapema.
Nje ya hapo wanakaribishwa lakini wasiwe na mategemeo kwani opeo wao upo ktk chaguzi za viongozi.
wanakaribishwa wapi? CHADEMA?
 
Aaaaah mkuu yamekuwa hayo tena?.. haya Upinzani!
Inabidi uonyeshe upinzani kwa vitendo.. ukienda bongo washkaji wako wote ni CCM damu. Wakianza kukupa good time na hela za CCM inabidi useme "NO". Lini bongo mzee, mwaka huu huendi?
 
Duh, washikaji wangu wengi CUF si unajua tena Uislaam! wengine ndio hao wabangaizaji hawana dini.. kwi kwi kwii!..
Bongo mkuu najiandaa nipo safarini utanisikia tu... kazi inaanza Columbus kwenye ngoma za kizeee! - tukalishwe sumu.
 
Hiyo nchi mafisadi na watoto wao (Kikwete na Makamba) watatawala milele mpaka watanzania wanywe maji ya chooni (sio nyasi tena kama alivyosema Mramba).

Anayetegemea maendeleo Tanzania chini ya ccm anaota ndoto za mchana. CCM wataongoza, wataiba, watashinda uchaguzi, na wakistaafu wataweka watoto wao na hakuna yoyote atakayewafanya chochote. Watanzania wengi maneno matupu na wengine tamaa tu imewajaa. Masikini wapinzani watapiga kelele na kulipua mabomu yote lakini ccm wataendelea kula nchi mpaka watu wafe kwa njaa kama ile ya sudan na ethiopia miaka ya 90.
 
Lakini jamani navyosikia huyo Ridhwan ni mwana JF imekuwaje leo kaingia CCM kwa kasi kiasi kwamba itamletea matatizo mengi hali anamwacha baba yake akizidi kuharibu... JF ipo kumpa picha na kukosoa pale baba yake anapoenda mrama sasa vipi au naye ndio hivyo tena kaamua kuvua kanzu!
 
Lakini jamani navyosikia huyo Ridhwan ni mwana JF imekuwaje leo kaingia CCM kwa kasi kiasi kwamba itamletea matatizo mengi hali anamwacha baba yake akizidi kuharibu... JF ipo kumpa picha na kukosoa pale baba yake anapoenda mrama sasa vipi au naye ndio hivyo tena kaamua kuvua kanzu!


Si mpaka akubali kuwa babake anaharibu. Yeye anajua mambo yanakwenda shwari kabisa!
 
Angalau sasa nimepata uhakika kwamba kweli Ridhiwan ana mtu anayemuunga mkono kwa nguvu zake zote.Nikiwa kama kada mwandamizi wa UVCCM na CCM.

Sina tatizo na hilo na wala sio dhambi kufanya hivyo.Zaidi sana,naamini anatumia haki yake ya msingi na uhuru wa kujiamulia mambo pasipo kuvunja sheria. Ni bahati mbaya kwamba watu wanaanza kuonesha hisia za woga kutokana na kijana huyu kuwa mtoto wa mkuu wa nchi.

Narudia,huu ni woga tu. Na hili halipo kwenye siasa tu. Suala la woga wa majina makubwa kuleta hofu kwa watu lipo hata kat ika fani ya michezo.Timu inaweza kufungwa mapema kisaikolojia kutokana na hofu tu ya majina makubwa yanayounda timu pinzani.Lakini kwa wanaojua michezo,mwamuzi wa mwisho ni dk 90 (kwa mchezo wa soka).

Na katika siasa ni vivyo hivyo, mwamuzi wa mwisho ni wapiga kura, sio majina ya wagombea na wala sio majina ya wanaowaunga mkono. Na kama ikatokea kambi ya Ridhwan itashinda, basi naamini watakuwa wameshinda kutokana na maandalizi ya kutosha ya kujinadi kwa wapiga kura, pamoja na mikakati makini katika kujenga hoja. Suala la mjina ya wazazi wao halina uzito.

Ila kuna jambo ningependa kufahamu. Ni kambi ipi pinzani aliyoizungumzia bwana Ridhiwani kwamba inatoa upinzani mkali kwao? Maana yametajwa majina mengi kuonesha nia ya kugombea nafasi hiyo. Hata hivyo, kutokana na maelezo ya Ridhiwan ni kambi moja tu ambayo amekiri kuonesha upinzani mkali kiasi cha kutengeneza tuhuma dhidi yake.

Nisaidieni jamani!
 
Kuna umakini na kujenga hoja ndani ya CCM? Tangu lini? Ingekuwa ndiyo hivyo basi CCM isingekuwa imetekwa nyara na mafisadi. Maana wao wakishaonyesha mapesa yao yaliyopatikana kifisadi basi hoja na umakini hutupwa pembeni maana CCM hapendwi mtu ila pochi lake.

Kitathmini vizuri chama chako kuhusu haya yanayosemwa utagundua yana ukweli na labda unaweza kubadilisha mwelekeo wa chama chenu.
 
Kuna umakini na kujenga hoja ndani ya CCM? Tangu lini? size]


ushawahi hudhuria mikutano ya ccm ? uliweza kuanalyse maongezi yao, maamuzi yao ? kama hujawahi kwenda then you are talking something you dont know ! umakini wa kujenga ni pale hoja makini zinapojengwa na chama makini ccm !
 
Back
Top Bottom