Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Hii nadhani ni fundisho kwa vijana wengine na wapenda nchi yao. Tusisubili wakati wa kuomba kura ndiyo tupambane na fisadi, hapo unakuwa si mpambanaji bali unafiki kiasi fulani au unatafuta njia ya kukutangaza si vita endelevu.
Nchimbi umezidi hii adhabu ni kali sana kwa huyu kijana
 
CCm sio fisadi ila bahati mbaya wananchi walichagua viongozi wa juu kabisa wachache ambao ni mafisadi.

Chama si majengo na magari. Chama ni wanachama na viongozi wake. Kama wanachama wanaona chama chao kinaongozwa na mafisadi na hawasemi chochote ili kuonyesha kutoridhika kwao basi wanakubaliana na chama chao kuwa ni cha kifisadi, vinginevyo wangepambana na hali hiyo na kuhakikisha viongozi wote mafisadi wanaondolewa madarakani na hata kunyang'anywa uanachama, mbona imekuwa rahisi mno kumnyang'anya uanachama Nape.
 
Just in Halmashauri Kuu ya UVCCM inayokutana Dodoma imemvua Uanachama wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Nape NNauye kwa sababu nyingine ikiwamo utovu wa nidhamu...wengine wenye habari zaidi watufahamishe zaidi.

Hiki kitu ni uhakika?

Maana naona tunaenda mbaaaali bila kupata undani wa tukio. Wamemvua kwa utovu gani wa nidhamu? Na agenda iligeuka lini kutoka uchaguzi kwenda kwenye uanachama wa mgombea?

Yebo Yebo ukipata habari zaidi tuwekee Mkuu.
 
Simply ni kwamba, wametoa mapendekezo ambayo ni lazima yakatihibitishwe na CC, kabla ya kwenda kwenye NEC, ujumbe wa NEC wa Nape unaanzia kwenye UV-CCM,

Kilichowafanya wakutane leo, ni kushinikizwa na CC, ili warudishe mapendekezo kwa CC kabla ya kuisha kwa kikao chake by September 9, maana rais anatakiwa kuwa safarini kwenda NY, US.

 
JK, Lowassa na Malecela.

teh teh teh teh teh teh

sasa kama ndio hao basi sisi ndio wapuuzi sana.
Ilikua je tunayejidai kumhenzi aliwakataa hawa jamaa harafu sisi tukajifanya kuwapa ushindi wa kishindo.

Tatizo wengi wetu tunajifanya kuzunguka sana sijui RA,sijui Makamba wakati straight foward ktk CCM tatizo ni JK na LOWASA.
 
Simply ni kwamba, wametoa mapendekezo ambayo ni lazima yakatihibitishwe na CC, kabla ya kwenda kwenye NEC, ujumbe wa NEC wa Nape unaanzia kwenye UV-CCM,

Kilichowafanya wakutane leo, ni kushinikizwa na CC, ili warudishe mapendekezo kwa CC kabla ya kuisha kwa kikao chake by September 9, maana rais anatakiwa kuwa safarini kwenda NY, US.


Bravo Mkuu, kurekebisha hapo tu kwa faida ya wengi hapa forum ni kuwa NEC ya UVCCM imeshamvua uanachama wa UVCCM na kwamba mpaka dakika hii haruhusiwi kuhudhuria kikao chochote cha UVCCM.

Wakati huo huo mapendekezo waliyopeleka CC ni kwa sababu ya Ujumbe wake wa NEC Taifa. Ni CC pekee yenye madaraka ya kumvua Ujumbe wa NEC. Huko kwenye CC Lowassa, Kawawa, Nchimbi, na Makamba wote ni miongoni mwa wajumbe.
 
Hiki kitu ni uhakika?

Maana naona tunaenda mbaaaali bila kupata undani wa tukio. Wamemvua kwa utovu gani wa nidhamu? Na agenda iligeuka lini kutoka uchaguzi kwenda kwenye uanachama wa mgombea?

Yebo Yebo ukipata habari zaidi tuwekee Mkuu.

Mkuu mbona habari hii ni confirmed soma Mwananchi la kesho ambayo tayari inapatikana hapa JF.
 
Mvutano mkali watarajiwa mkutano wa Vijana CCM Dodoma

Kizitto Noya na Saa Mohamed
Mwananchi
Date::9/6/2008


MVUTANO mkubwa unatarajiriwa kutawala kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kinachoketi Jumapili kuchambua majina ya wagombea wa nafasi ya mwenyekiti mjini Dodoma.

Kikao cha Baraza Kuu ni cha tatu kuchuja majina ya wagombea hao baada ya Sekretarieti ya UVCCM iliyoketi jijini Dar es Salaam na Kamati yake ya Utekelezaji iliyokaa Agosti 16 na 17 mjini Dodoma.

Tofauti na vikao vya Sekretarieti na Kamati ya Utekelezaji, Baraza Kuu la Vijana, linatarajiwa kuwagawa wajumbe wakati wa kujadili jina la Mjumbe wa Baraza hilo na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Nape Nnauye kutokana na msimamo wake wa wazi kupinga ufisadi ndani ya jumuiya hiyo.

Tayari Nape amekwishawekewa alama mbaya ya F za kutompendekeza kuwania nafasi hiyo na baadhi ya wajumbe wanaamini kuwa kitendo hicho kimetokana na msimamo wake kupinga ufisadi aliodai unafanywa na watendaji wakuu wa UVCCM kuhusiana na Mkataba wa Jengo la Umoja wa Vijana.

Kikao cha kwanza kumwengua Nape ni Kamati ya Utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, anayemaliza muda wake Dk Emmanuel Nchimbi ambacho kilimwekea alama F inayomaanisha kuwa hafai kugombea nafasi hiyo kwa kigezo cha umri.

Kikao hicho kilimpa Nape alama F na kuwapendekeza wagombea wengine watano kuwania nafasi hiyo baada ya kupitia vyeti vya wagombea hao na kubaini kuwa Nape alizaliwa Novemba 26 mwaka 1977.

Majina yaliyopendekezwa ni Zainab Kawawa, Said Mtanda, Benno Malisa, Hussein Bashe na Suleiman Suleiman.

Hata hivyo, uamuzi wa kumwengua Nape uliwagawa wajumbe wa kikao hicho baada ya kundi moja kuridhia na lingine kukataa kutokana na kuamini kuwa uamuzi huo umetokana na msimamo wa Nape kupinga ufisadi.

Sababu zilizotolewa na upande uliounga mkono kuondolewa kwa Nape ni kutetea maamuzi ya vikao vyake vilivyopitisha kanuni ya kikomo cha umri katika uwania nafasi hiyo.

Msimamo huo wa Nape ndio uliofanya nyota yake izidi kung'ara na hivi karibuni alipotambulishwa bungeni alishangiliwa na wabunge na kutakiwa mafanikio na Spika, Samuel Sitta, hatua ambayo inaonyesha dhahiri kuwa anaungwa mkono katika mapambano yake dhidi ya ufisadi.

Zengwe la umri ni kanuni iliyoingizwa kwenye taratibu za Uchaguzi wa UVCCM mwaka 2003 wakati Mwenyekiti wa sasa, Dk Emmanuel Nchimbi anawania nafasi hiyo kwa mara ya pili, ikilenga kumuengua, lakini busara ya Kamati Kuu ya CCM iliiweka pembeni kwa muda.

Kulingana na kanuni hiyo, umri wa mwisho wa kugombea ni miaka 30 ili kiongozi husika asizidi miaka 35 akiwa madarakani umri ambao ni wa mwisho wa uanachama wa UVCCM.

Hata hivyo, ingawa Mkurugenzi wa uchaguzi huo, Francis Isack hakutaka kueleza mamlaka ya kikao cha Baraza Kuu la UVCCM, katika kuamua hatima ya wagombea, kikanuni, maamuzi ya kikao hicho yanafuta maamuzi ya vikao vyote vya awali vya jumuiya hiyo dhidi ya wagombea hao.

Nape aliliambia Mwananchi Jumapili jana kuwa, ana hakika Baraza Kuu litatenda haki dhidi yake kwani anaamini si wajumbe wote wa baraza hilo wanaotaka ufisadi uendelee kuitafuna jumuiya hiyo.

Alisema kikao hicho kinampa matumaini mapya ya safari yake kuusaka uenyekiti wa jumuiya hiyo na ndicho kitakachotoa dira na mtazamo wa wajumbe kuhusu ufisadi.

"Mimi naamini kwamba wajumbe wa kikao hicho wana busara kubwa na ninaamini ukweli wa mambo utajulikana hapo. Baraza lina busara nyingi na naamini wajumbe watatumia busara kusafisha jina langu," alisema Nape.

Akizungumzia mchakato huo kwa ujumla, Nape alisema anasikitika kuona baadhi ya wanasiasa wameacha kando hoja na kuanza kuingiza unafiki kwa masilahi binafsi.

"Mimi ushauri wangu kwa wanasiasa waache unafiki, tushindane kwa hoja za leo. Kwa wanahabari naomba wafuate maadili badala ya kukubali kutumiwa kwa masilahi ya wanasiasa wachache," alisema.

Mkurugenzi wa Uchaguzi huo, Francis Isack alithibitisha jana kuwepo wa kikao hicho leo na kusema kimsingi kikao hicho ni kikubwa kuliko vikao vingine vyote katika mchakato huo.

"Siwezi kukutajia agenda, lakini ni kweli Baraza linakaa kesho (leo) kuchuja majina ya wagombea," alisema Isack ambaye awali aligoma kuzungumzia suala hilo kabisa.

Kikao cha Baraza Kuu kitafuatiwa na Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu wake, Yusuf Makamba, kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM, Kamati Kuu (CC) na Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) vyote chini ya Mwenyekiti Jakaya Kikwete.

Nape aliwasha moto ndani ya UVCCM muda mfupi baada ya kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo na kuwatuhumu watendaji wakuu wa jumuiya akiwamo Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, Edward Lowassa kwamba wanahusika na mkataba tata wa Jengo la Makao Makuu ya Jumuiya hiyo.

Watendaji wengine aliowatuhumu kuhusika na mkataba huo ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo anayemaliza muda wake, Dk Emmanuel Nchimbi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amos Makala.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wameeleza kuwa, hawashangai kuona Nape anapata wakati mgumu katika hatua za awali za mchakato huo kwenye jumuiya ya vijana kwa kuwa viongozi wa vikao hivyo ni baadhi watendaji aliowatuhumu kwa ufisadi.
 
Mwalimu alimtaka Salim, akakataliwa na wajumbe wengi wa Zanzibar, Mwalimu hakumkataa Muungwana, alichosema ni kwamba hakuwa tayari ila asubiri mpaka Mkapa atakapomaliza amuachie that is exactly what he said na Mkapa did exactly what he was told,

Mwalimu aliwakataa kabisa Lowassa na Malecela, alisema Lowassa ni mla rushwa na Malecela hawezi kuaminiwa madaraka ya urais kwa sababu ya marafiki zake watamyumbisha, na akamuapisha Mkapa never to let that happen kwa Malecela kushika urais, ashike anything lakini not urais!

Lakini Mnyonge mnyongeni, Jk alipewa baraka na Mwalimu za kuwa rais baada ya Mkapa, JK amelelewa na kukulia mikononi mwa Mwalimu, hata alipokuwa Mlimani alikuwa siku zote akipelekewa hela za matumizi kutoka Ikulu.
 
Wazee CCM wamkaanga Nape Nnauye,wajumbe wataka afutwe uanachama
Na Habel Chidawali, Dodoma

WAZEE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametoa kauli ambazo zinaonyesha wazi kumshughulikia kijana machachari ndani ya chama hicho Nape Nnauye, katika mbio zake za kuwani Uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UV-CCM).


Sambamba na hilo Baraza la Umoja wa Vijana limemfuta Nnauye uanachama wa jumuia hiyo kwa kumnyang'anya kadi na kumzuia kuhudhuria vikao vyote ya UVCCM kuanzia sasa.



Wakizungumza katika mkutano wa Baraza hilo lililofanyika mjini Dodoma jana, wazee hao Katibu wa CCM, Yusufu Makamba, Kaimu Kamanda wa Vijana, Kingunge Ngombale Mwiru na Mshauri wa Vijana Mzee Rashid Kawawa waliwaonya wagombea wote na wapambe wao kuacha kukikosoa chama hicho badala yake wawe wapole.

Source;Mwananchi


CCM ina Wenyewe..!!
 
Wakati huo huo mapendekezo waliyopeleka CC ni kwa sababu ya Ujumbe wake wa NEC Taifa. Ni CC pekee yenye madaraka ya kumvua Ujumbe wa NEC. Huko kwenye CC Lowassa, Kawawa, Nchimbi, na Makamba wote ni miongoni mwa wajumbe.

Sawa sawa, hiyo ni hoja ya muhimu sana kwamba NEC itasema nini? Hii sagga bado haijaisha ingawa matumaini kwa Nape ni madogo sana, lakini ninaamini kuwa hii ishu italeta mtafaurku mkubwa sana ndani ya CCM.
 
Mmmhhh!! leo kumbe kuna makubwa hivyo?

Kufukuza/kusimamisha kiongozi naona ni njia mbovu kabisa. Kama Nape hafai, basi mkutano mkuu wa UVCCM ndio ungemwona hafai kwa kumnyima kura.

Kama hana sifa za kugombea inaeleweka, lakini asiye na sifa hafukuzwi uanachama.

Kawawa ana mtoto wake kwenye hili, hivi hapo kweli sio conflict of interest?

Nchimbi naona alivyolishughulikia hili suala kachemsha kweli kweli. Wacha tusubiri NEC ya CCM kama kuna watu wataamua kumfunga paka kengele. Hii ya CC naona tusahau maana huko wamejaa akina Kawawa, Kingunge na mashabiki zao.

Kuna siku CCM itaanguka vibaya sana.
 
Mkuu mbona habari hii ni confirmed soma Mwananchi la kesho ambayo tayari inapatikana hapa JF.

CCM wamkaanga Nape Nnauye,wajumbe wataka afutwe uanachama

Na Habel Chidawali, Dodoma
Source: Mwananchi

Sambamba na hilo Baraza la Umoja wa Vijana limemfuta Nnauye uanachama wa jumuia hiyo kwa kumnyang'anya kadi na kumzuia kuhudhuria vikao vyote ya UVCCM kuanzia sasa.

Habari kutoka ndani ya mkutano huo zinasema kuwa, wakati Dk Nchimbi akiendelea kuhutubia, mjumbe mmoja alisimama na kusema kwa nini mtu huyo asinyang'anywe kadi ya umoja wa vijana na kuadhibiwa? Mwenyekiti akajibu, ''imepitishwa".

Mbali na hiyo hilo, baraza liliazimia kuwa kuanzisa sasa asihudhurie vikao vyote vya umoja huo pamoja na kupeleka mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ili aweze kushughulikiwa zaidi ikiwa ni pamoja na kunyang'anywa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.

Yeboyebo,

Hii habari kutoka Mwananchi mimi naona kama imeandikwa na mtu aliyedata.

Kichwa cha habari kinasema "wataka afutwe," halafu ndani anasema "wamemfuta"! Halafu hasemi kwa nini wamemfuta.

Kumbe kumfuta kwenyewe kunaonekana ni Mjumbe mmoja kapayuka "afutwe" halafu Mwenyekiti akaitikia "imepitishwa"! Ndio Umoja wa Vijana wanavyofuta mtu uanachama kibangi bangi hivyo? Sidhani.

Na ni lini agenda ya huu Mkutano iligeuka kutoka uchaguzi kwenda kwenye uanachama wa mgombea?

Huu unaweza kuwa ni udaku.
 
NGUVU YA UMMA TUINDAE 2010. KAMA Chechescu NA WSOSHALIST WALITOKA SEMBUSE CCM? KAMA APARTHEID ILIANGUKA TUSHINDWE KUKATA NA KUANGUSHA CHAMA CHA MAFISADI? KIJANA MWENZANGU JIULIZE, VOTING BLOCK YA VIJANA INAWEZA KUIONDOA CCM 2010. OBAMA KAWEZA KUITENGENEZA HII UNDERUTILISED VOTERS BLOCK. SHIME VIJANA WENZANGU.TUPAMBANE KUAKIKISHA CHAMA HIKI HAKIPATI JAPO WINGI WA WABUNGE HAPO TUTAKUWA TUMEWAPIGA BAO.THEN TUTAANZA SAFISHA SAFISHA TUKIANZIA NA KATIBA. THIS TUNATAKA KATIBA KUJENGWA NA UMMA NA SI CCM. SHIME VIJANA KWA NINI TUSIANZISHE PRESSURE GROUP YA KUHAKIKISHA VIJANA WANAJIANDIKISHA KWA WINGI. WIKI JANA, NIMEPATA KUTEMBELEO OFFICE ZA CAMP YA OBAMA, KUNA MIKAKATI MIZURI NIMEPATA . BADALA YA KUPIGA KELELE AMBAZO HAZIMZUII NG'OMBE KUNYWA MAJI, TUPANGE MIKAKATI YA 2010 KISHA TUWEKE LENGO LA JUU NA LA CHINI.
NAOMBA KUWAKILISHA. ( sorry for the caps)
 
NGUVU YA UMMA TUINDAE 2010. KAMA Chechescu NA WSOSHALIST WALITOKA SEMBUSE CCM? KAMA APARTHEID ILIANGUKA TUSHINDWE KUKATA NA KUANGUSHA CHAMA CHA MAFISADI? KIJANA MWENZANGU JIULIZE, VOTING BLOCK YA VIJANA INAWEZA KUIONDOA CCM 2010. OBAMA KAWEZA KUITENGENEZA HII UNDERUTILISED VOTERS BLOCK. SHIME VIJANA WENZANGU.TUPAMBANE KUAKIKISHA CHAMA HIKI HAKIPATI JAPO WINGI WA WABUNGE HAPO TUTAKUWA TUMEWAPIGA BAO.THEN TUTAANZA SAFISHA SAFISHA TUKIANZIA NA KATIBA. THIS TUNATAKA KATIBA KUJENGWA NA UMMA NA SI CCM. SHIME VIJANA KWA NINI TUSIANZISHE PRESSURE GROUP YA KUHAKIKISHA VIJANA WANAJIANDIKISHA KWA WINGI. WIKI JANA, NIMEPATA KUTEMBELEO OFFICE ZA CAMP YA OBAMA, KUNA MIKAKATI MIZURI NIMEPATA . BADALA YA KUPIGA KELELE AMBAZO HAZIMZUII NG'OMBE KUNYWA MAJI, TUPANGE MIKAKATI YA 2010 KISHA TUWEKE LENGO LA JUU NA LA CHINI.
NAOMBA KUWAKILISHA. ( sorry for the caps)

Hakuna kinachoshindikana duniani penye nia pana njia na Mwalimu alisema it can be done, just play your part, lakini kwanza tuache udanganyika wetu eti Kikwete kaelemewa na Mafisadi!!!! Rais wa nchi hawezi kuelemewa na kikundi cha watu (mafisadi) wasiofika hata elfu au chochote kile ndani ya nchi yake kama ataweka maslahi ya wananchi wake mbele badala ya mtu mwingine yeyote yule.
 
Wanajamii lingine linaloudhi kwa upande wa CCM, mara nyingi kwenye mambo kama haya wanatoka nje badala ya kujadili issue inakuwa wanajadili watu zaidi, nadhani wangeweza kujadili yote mawili ingekuwa bora zaidi.

Mfano kwenye suala hili kuna ukiukaji wa taratibu walizojiwekea wenyewe kichama kuhusu kuingia mikataka etc ....sidhani kama waliofanya makosa hayo(Lowasa et al) watachukuliwa hatua zozote zaidi ya yule aliysema(Nape) na umma kujua....
 
Unaweza kuwa vetoed na mwenyekiti peke yake, sasa kama Lowassa, Mkamba, Kingunge na Nchimbi wako upande mmoja, the political wisdom inakataa kuwa hawezi,

The history ni only Mkapa could do that! Hata Mwalimu mwenyewe kwenye hili asingeweza.

Really? Are you kidding me? Yaani hata Mwalimu mwenyewe asingeweza ku-veto maamuzi ya akina Lowassa, Makamba, Kingunge na Nchimbi? Are you serious!?!

[1]:Marshall, sasa naona unazeeka vibaya! Kumbuka G-55? Ni nani kama sio Mwalimu aliyekuwa mstaari wa mbele kuwapiga akina Malecela, Kassaka na Mateo Qares?

[2]: Kumbuka uchaguzi wa kupendekeza mgombe wa CCM 1995? Bila Mwalimu, nani angemstopisha Lowassa?

[3]: Je, umesahau jinsi Mwalimu alivyomshutumu Prez. Mwinyi pale kilimanjaro Hotel kwa ujingaujinga wake?

[4]: The same Mwalimu ambaye aliyewahi kutamka kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Kawawa kwamba: "Kawawa alikuwa kibaka huyu...!"

[5]: I mean, I can go on and on and on...

Please, give me a break [here]!
 
Back
Top Bottom