Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

anyway nadhani wewe sina haja ya kukujibu sana, lakini kimsingi ningependa kusema wazi hapa kuwa mimi simpendi nape kama nape napenda wapiga vita ufisadi(baba zako) maana wewe ni fisadi mtoto.. So kila anayeonyesha msimamo wa dhati kupinga ufisadi namuunga mkono kwa dhati...so nape katika hili

Unapaswa kukua kutambua faidas na hasara za ufisadi ndani ya nchi yetu.usikae na kufata tu mkumbo.

Ukiangalia kwa makini ufiasadi hauna tofauti na marshal plan ambapo serikali iliwezesha asasi za kiraia kiuchumi... Hakuna nchi duniani imepata kuendelea bila kuwepo na primitive accumulation of capital,ambapo miaka iliopita nchi kama UK,germany,japan walipata capital kutoka kwenye makoloni yao.

Waka invest kwao na kupata maendeleo. Kwa sasa hakuna nchi unayoweza kuitawala, hivyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa wananchi wake wenye vipaji vya biashara wanawezeshwa....ufisadi waliofanya ni sustainable,kwa kuwa wamechukua hela zilizokuwa zimekaa bila uwekezaji BOT, na pesa yenyewe ya epa haikuwa ya serilali bali ya wafanyabiashara wa nje wao wamewekeza katika biashara mbalimbali na wananchi wanapata kazi...angalia kampuni ya simu ya celtel imeajili wananchi wangapi?

Angalia Kiwira coal mine ilikuwa imeshakufa na sasa imeajili wafanyakazi zaidi ya mia tatu na inazalisha umeme,angalia bank M imeajili watanzania na inalipa mishahara mizuri kuliko bank nyingine yeyote huko Tanzania.... ufisadi tunaokataa ni kama ule wa kuwakopesha wananchi fedha za kikwete kihalali lakini hauleti manufaa yeyote kwao zaidi ya kwemda kuchezea ngoma...sasa wanarudisha hizo pesa ni jambo zuri ambalo walipaswa kuwa mfano wa kuiga.
 
Unapaswa kukua kutambua faidas na hasara za ufisadi ndani ya nchi yetu.usikae na kufata tu mkumbo.

Ukiangalia kwa makini ufiasadi hauna tofauti na marshal plan ambapo serikali iliwezesha asasi za kiraia kiuchumi... Hakuna nchi duniani imepata kuendelea bila kuwepo na primitive accumulation of capital,ambapo miaka iliopita nchi kama UK,germany,japan walipata capital kutoka kwenye makoloni yao.

Waka invest kwao na kupata maendeleo. Kwa sasa hakuna nchi unayoweza kuitawala, hivyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa wananchi wake wenye vipaji vya biashara wanawezeshwa....ufisadi waliofanya ni sustainable,kwa kuwa wamechukua hela zilizokuwa zimekaa bila uwekezaji BOT, na pesa yenyewe ya epa haikuwa ya serilali bali ya wafanyabiashara wa nje wao wamewekeza katika biashara mbalimbali na wananchi wanapata kazi...angalia kampuni ya simu ya celtel imeajili wananchi wangapi?

Angalia Kiwira coal mine ilikuwa imeshakufa na sasa imeajili wafanyakazi zaidi ya mia tatu na inazalisha umeme,angalia bank M imeajili watanzania na inalipa mishahara mizuri kuliko bank nyingine yeyote huko Tanzania.... ufisadi tunaokataa ni kama ule wa kuwakopesha wananchi fedha za kikwete kihalali lakini hauleti manufaa yeyote kwao zaidi ya kwemda kuchezea ngoma...sasa wanarudisha hizo pesa ni jambo zuri ambalo walipaswa kuwa mfano wa kuiga.

Ndiyo maana napenda Watanzania mtu anaweza kutetea uovu ili uwe ukweli na akatoa na sababu kama hii hapa juu. Tanzania kupigana kwa risasi ni ndoto kwani silaha yetu kubwa iko kinywani kwetu.

Mtu anaweza kukuibia pesa zako mfukoni na utakapo mkamata anakuambia mimi niliona wewe huzitumii nikazichukua ili nizitumie!!!!!!!!
 
Wanabodi,

Naomba kushauri vijana kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu wa 2010:

Nafasi za madiwani na wabunge wa kuchaguliwa kwenye majimbo.

Vijana wanahitaji dira yao pia, kwa mfano kuwa na at least 10% ya wabunge wote by 2015. (Nasema yao kwa kuwa kijana wa leo ni mzee wa kesho)

Napendekeza vijana mufanye maandalizi mapema ili kujua changamoto mbele yenu.

Kama yawezekana kuwe na mfuko unaoweza kuundwa na wanaharakati kwa ajili ya kuwasaidia vijana watakaogombea haswa pale wanapokuwa wametishwa na vyama vyao husika.

Kwenye hili hakuna kuangalia kwamba kijana huyo mgombea anatoka chama gani?

Wote ni mashahidi kwamba mchango wa wabunge vijana umekuwa wa msaada mkubwa sana kwa taifa.


Mungu Ibariki Tanzania
 
Mwana mimi mwenyewe nina mpango wa kugombea kama sio ubungo basi ni moshi vijijini lakini zaidi ni moshi kwa sababu hapa ubungo kuna maslahi ya kibiashara sasa sitaki mambo haya yaingiliane na nia yangu ya kulitwaa jimbo la ubungo
 
Sasa wewe Shy,Kumbe wakati ulipokua unamkandia dogo mnyika hapa kumbe ulikua kwenye kampeni?Nawasikitikia waliokua wanadandia hoja zako
 
Actualy siyo porojo wala nini mimi binafsi nimeshaanza kampeni za chini chini za kuwania Ubunge kwenye kijiji kimoja huko Moshi.Nimeshawajengea kisima na madarasa mawili na tayari nimeshakuwa endorsed na wazee wote wa kijiji!Ila naomba nisiulizwe ni kwa tiketi gani nitagombea uchaguzi!
 
Lakini wakuu tutambue tu kwamba kwa sasa Tanzania haihitaji tu Kijana ilimradi umri wako ni mdogo.Tanzania ya sasa inahitaji ukomavu wa kimawazo.That's to say hata kama wewe ni mzee na mawazo yako yakawa yanachemka kama ya akina Lucas Salellii then bado utaonekana kijana.

Sometimes Age is just a number.Sasa kwa mfano kila mtu akishajiona kijana na kwa kuwa tunawataka vijana tuta-end up kupata vilaza.So tunamtaka kijana mwenye mawazo yaliyokomaa na mwenye kutafuta suluhisho la umaskini wetu,mwenye kusoma alama za nyakati zijazo ktk national interst wakati wa ku-sign au kupitisha sherea mbalimbali kuhusu raslimali zetu.

Pia kijana mwenye kuamsha ari ya ushindani wa kimaendeleo kati ya jimbo na jimbo,mkoa na mkoa na most importantly kati ya Taifa letu Tukufu Tanzania na na Mataifa mengine kwa kutumia nguvu ya uzalendo uchomaao ndani ya moyo wake.Hivi ndivyo America na Russia walivyojijenga na kuwa uper powers leo hii
 
Mgombea asiyetakiwa Vijana CCM ashangiliwa kwa nderemo Bungeni

nape.jpg
Date::8/29/2008


Mgombea wa kiti cha Uenyekiti, Vijana (UVCCM), Nape Nauye, ambaye anaelekea kutokuwa chaguo la uongozi uliopo madarakani aliyeshangiliwa kwa nderemo katika ukumbi wa Bunge, Dodoma Ijumaa.
Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi

MGOMBEA wa kiti cha Uenyekiti katika Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Nape Nauye, jana alilitikisa Bunge pale alipotambulishwa na kushangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kushangiliwa huko kulimfanya Nape, anyanyuke mara tatu kuwashukuru wabunge waliokuwa wakimshangilia kwa kugonga meza zao kama ishara ya kumkubali huku yeye akiwapungia mikono wabunge hao.

Shangwe hizo ziliwafanya wabunge hao kushindwa kuendelea kumsikiliza Spika Samuel Sitta, aliyekuwa akitoa matangazo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

Hali hiyo ilimlazimisha Spika Sitta, kusubiri Wabunge hao wamalize kumshangilia Nape, ambaye katika siku za hivi karibuni ameingia katika mzozo mkubwa na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM mara tu baada ya kutangaza kuwania nafasi hiyo na kutoa tuhuma zito kwa baadhi ya viongozi wa umoja huo.

Baada ya kuona hali ya mambo imetulia Spika Sitta, alisema Nape, ni mmoja wa vijana machachari aliyeibuka siku za hivi karibuni katika UVCCM.

Sitta alisema anamtakia kila la heri mgombea huyo, katika mambo yake hasa katika kipindi hiki anachoelekea bila kufafanua ni kipindi gani lakini kwa hali ya mambo ilivyo alikuwa akimaanisha mchakato wa uchaguzi wa UVCCM.

"Huyu ni kijana machachari umoja wa vijana wa CCM na nimtakia kila la heri katika mambo yake yajao," alisema Spika na kushangiliwa na wabunge wengi.

Wiki iliyopita iliripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari akidaiwa kupewa alama ya E katika kikao cha kuchambua majina ya wagombea kilikuwa chini ya Mwenyekiti wa Umoja huo, Dk Emmanuel Nchimbi mjini hapa.

Mwananchi ilipomfuata Nauye, na kumuuliza kuhusu tukio hilo, alisema kushangiliwa kwake kunaonyesha jinsi anavyokubalika na wabunge na ni ishara nzuri ya kule anapoelekea.

"Kushangiliwa kwangu inaonyesha ni kwa kiwango gani baadhi ya watu wanavyoheshimu mchango na matarajio yao kwangu," alisema Nape.

Katika siku za hivi karibuni Nape, aliwashutumu baadhi ya vigogo wa CCM kuingia mkataba tata wa ujenzi wa jengo la umoja wa vijana lililopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam .

Mmoja wa kiongozi ambaye Nape, alimtuhumu kujihusisha na kuingia mkataba huo ni aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, ambaye baadaye taarifa za kuhusika kwake katika makubaliano na si mkataba wa ujenzi huo zitolewa na kukanushwa kuhusika Mchakato wa uchaguzi huo ulimfanya mwanasiasa Mkongwe, John Samwel Malecela, wiki iliyopita kuwataka wazee wenzake kutoingilia uchaguzi wa Umoja wa Vijana kwa kupanga watu wao.
 
Simply PR gimmicks...

Watu wengine bwana!! Yaani wewe huoni kitendo alichokifanya huyu kijana cha kusimama hadharani na kusema mkataba wa jengo la vijana umejaa ufisadi na hauna maslahi yoyote kwa UVCCM ni cha kishujaa na kinahitaji kupongezwa!! Kazi kweli kweli!!!
 
Watu wengine bwana!! Yaani wewe huoni kitendo alichokifanya huyu kijana cha kusimama hadharani na kusema mkataba wa jengo la vijana umejaa ufisadi na hauna maslahi yoyote kwa UVCCM ni cha kishujaa na kinahitaji kupongezwa!! Kazi kweli kweli!!!

Kayaona hayo wakati anataka U-enyekiti wa UVCCM cio? Watu wengine bwana...
 
Kayaona hayo wakati anataka U-enyekiti wa UVCCM cio? Watu wengine bwana...

Angalau yeye alisimama akasema kweli, wagombea wengine wote wamefuata mkondo wa mafisadi kwa kuufumbia macho ufisadi huo.
 
Ndo kwanza safari imeanza, na sasa hizo ni salamu kwa mafisadi wote, hii ni kudhihirisha kuwa mafisadi wanachukiwa kupita maelezo...nilikuwepo Bungeni aibu waliyoipata Nchimbi na Makamba vibaraka wa mafisadi ilikuwa ni ya mwaka, hakika aibu yao haifichiki maana walibaki wana duaa tu!!! Hawaamini kilichokuwa kinatokea
Hata kama wana nuna HABARI NDIO HIYO....
 
NAJARIBU KUNUKUU MANENO YA SPIKA SITTA.....namtakia kila lakheri katika safari yake ya mchakato....na akaitikiwa AMINA kwa makofi mazito na wabunge, ambao ndani yake kuna wajumbe karibia robo tatu ya wajumbe wa kamati kuu CC ya CCM na NEC ya CCM ambao ni vikao vya juu kabisa vya chama vitakavyorudisha majina....sasa salamu kwenu mafisadi dogo anajua kupiga hesabu kawazidi kete kwa mbali mnooooooooooooo
 
"Huyu ni kijana machachari umoja wa vijana wa CCM na nimtakia kila la heri katika mambo yake yajao," alisema Spika na kushangiliwa na wabunge wengi.

With all respect kwa wakuu wote, naomba kuigusa hii topic kidogo, maaan imenigusa sana:-

1. Wa-Tanzania tumefikia mahali ni lazima tukubali kuwa ufisadi ndio siasa ya sasa kwa taifa letu, kwamba pmaoja na matatizo yote tuliyonayo ukweli wa mbali ni kwamba tukiweza kulikabili tatizo la ufisadi, basi mengine yote yaani matatizo tuliyonayo, yatajinyoosha yenyewe, lakini the name of the game ni ufisadi.

2. Sasa kwenye hili la ufisadi, lets be honest with each other, yaani wananchi at large ni lazima tuamue sasa tunataka kuwa upande gani kwa sababu, hakuna neutrality, wala middle position na ufisadi, either you are for it au you are not, either uko with us tunaoupinga au uko na wanaoufanya na wanaoushangilia.

3. Kwenye hili ninaomba kusema wazi kuwa ninatoa heshima nzito na a strong support kwa kiongozi huyu kijana Nape, ninajua for a fact kwamba record yake ni safi haina mikwaruzo, na heshima yangu kwake ilianzia pale ambapo yeye kama mimi pia, tuliitwa na muungwana kwa wakati tofauti wakati wa uchaguzi wa urais uliopita, katika kutaka our support kwa kambi yake, yeye ninajua kuwa alimkatalia kata kata muungwana, kwa sababu nyingi sana lakini ya msingi ilikuwa ni marafiki wengi wa muungwana, hawakuwa safi kushirki nao kwenye coaliton ya kisiasa kwa maneno mengine ni corrupt, kama wote tunavyojua sasa kutokana na ushahidi mbali mbali uliokwisha jitokeza, wazi.

4. Inanisikitisha sana kwamba somehow tumewaachia viongozi wasiofaa kuushika Umoja Wa Vijana ambao one time ulikuwa umeshikiliwa na Mzee Joseph Nyerere ambaye hakuwa na mchezo kabisa katika kufuata haki, sasa huu umoja umekuwa almost wa mtu mmoja, ambaye kwa kuamini kuwa ana ukaribu na the powers wa sasa basi anaweza kufanya atakalo that is pathetic.

Hapa again ninamlaumu Rais wa sasa, kwa sababu haiwezekani kiongozi mmoja wa CCM apewe alama ya E kiuongozi na uongozi huu suspect wa Vijana halafu aende bungeni na kushangiliwa namna hii na viongozi wengine tena wa CCM, something is not right na uongozi wa sasa!

Kwa kumaliza ninasema kuwa kwa wale wapenda mabadiliko kwa taifa letu, huwezi ukasema serikali ya sasa haifai lakini ukampondea huyu kijana Nape, huwezi ukampenda Obama, anayesimamia change, halafu ukamponda Nape ambaye pia anasiamia hiyo hiyo change, ila kwa njia tofauti kuliko ya Obama, hasa kutokana na tofauti ya mazingara ya kisasa ya grounds wanazozisimamia.

Nape, aendelee ksuimama kidete akielewa kuwa mabadiliko ya kisiasa sio kitu rahisi kukubalika, Umoja Wa Vijana yes ni step kubwa sana katika kutafuta nafasi ya kiongozi kuonyesha uwezo wake wa kulilia na kuleta mabadiliko, kwa hiyo Nape apokee kwa heshima kubwa vietndo kama hivi vya kusimamiwa na wabunge karibu wote bungeni kutoa heshima zao kwa ushujaa wake wa kusimama kidete,

Hakuna tatizo la time kwenye kutafuta mabadiliko, kwa hiyo ni sawa kabisa kwa Nape ksuema maneno mazito now kwa sababu politically huu ndio hasa wakati wa kusema na usikike wakati wa kukaribia uchaguzi, kwa sababu huyu mama Pelin huko kwao Alsaka kula Moose ni sawa, lakini sio sasa wakati yeye na Makeni wakigombea urais, sasa ataulizwa kwamba kwa nini unakula yule mnyama, asingekwua mgombea isingekuwa tatizo, ndio siasa inavyochezwa, maswali serious kuhusu nonesense huulizwa wakati wa uchaguzi sio kabla, kwa hiyo Nape hakukosea kuuliza kuhusu majengo sasa, yaani wakati wa uchaguzi kukaribia.

Mkuu Nape, tunakutakia mafanikio katika hivi vita ambavyo wengine tumevulia nguo siku nyingi sana, na sasa tuko kwenye kuvioga, usimame imara bila kuogopa, you have our attention sasa wewe ni kungalia mbele tu, hata ukikosa huu Umoja wa vijana, bado kuna nafsi nyingi sana tena muhimu kuliko hiii, ninasema bravo Nape, na kuna mabao tuko nyuma yako. na heshima kwa wabunge wote waliotoa heshima kwako.

Mingu Aibariki Tanzania.
 
Hawa CCM kweli wanatisha .Nimeona wameamua kujenga jengo jina na wameanzia kitu kinaitwa Videco .CCM kweli ni mali ya wahindi maana hata pesa za usafiri kwa Vijana wa CCM kwenda Dodoma kwenye kuchambua majina ya wagombea pesa zimetolewa na wahindi na huku JK anasema CCM ni ya watanzania .Ama kweli baba ombaombana mtoto the same .Aibu kubwa hii .
 
Back
Top Bottom