Kitu muhimu ambacho mwandishi wa habari alitakiwa kukiweka wazi ama kuwauliza hao wana kamati ya utekelezaji ni swala la vigezo walivyotumia kutoa alama E kwa kijana Nape.
Usilolijua litakusumbua kwa utaratibu wa chama kutoa taarifa za kikao chochote cha chama kabla ya uteuzi wa mwisho ni makosa uteuzi wa mwisho hufanywa na kikao cha halimashauri kuu ya ccm taifa na wala siyo baraza kwa maana hiyo basi hata kama watakuwa wamempa alama E bado hawana madaraka ya mwisho kwa mujibu wa katiba ya ccmkama mnataka kumsaidia Nape Mwandosya mmechelewa kwa kuwa Nape hajakatwa na Mtu bali amekatwa na kanuni ambayo imemfikisha kikomo cha umri na umri ni ukuta,sasa kujaribu kudai ni Nchimbi ndio kamkata ni kusingizia kusiko na kikomo kwa kuwa kikao kilicho mkata sicho kilichopitisha hio kanuni,
mpita njia,
hilo swa na mimi niko upande wa said mtanda na nape coz ni vijana pekee ambao hawana makundi na nadhani wana nafasi kubwa ya kuchukua ushindi,tuwape nafasi waoneshe wanaweza.
Tatizo lipo kwa watu wa ina ya nchimbi,watu wanaoaminika walichangia ushindi wa mkulu,hapa kuna tatizo sababu moja kubwa kama mkuu akiwaaca watamziria nchi na ndiyo maana mkuu wa nchi yuko makini sana.kuna madhara kama nchimbi akipuuzwa ila atakchofanya ni kutumia wazee kuamua hili ili asionekane yeye anampendekeza nani.
Kimsingi mie nalijua chaguo la mkulu linaweza kuangukia kwa nani.
Watu juu mnauliza said ni nani kwa sababu gani,yaani kugombea lazima uwe flani?lazima uwe mtu kutoka sehemu atakayo mtu flani?au maarufu kiasi gani??hili ni tatizo na wakati mwingine nyani ngabu you are right..ndivyo tulivyo...tunapenda wenye majina na wale ambao tuwapendao kutoka nyumbani
gembe unamfahamu said mtanda?
Ndiye rafiki wa karibu sana wa ridhiwan jakaya mrisho kikwete, wengi wenu mnadhani ridhiwan anamtaka benno malisa, mmeingizwa mjini hapo, chaguo la ridhiwan ni said, said ni mtoto wa mheshimiwa hakimu mfawidhi mstaafu wa wilaya ya ulanga mzee mtanda, rafiki mkubwa wa marhemu hakimu ezekile ligema, said ndie aliyeongoza kampeni ya ridhiwan 2007 kuomba ujumbe wa mkutano mkuu wa ccm taifa na yeye pia kujitwalia nafasi huko bagamoyo, kiasili ni chinga toka lindi ila kwa sasa rasmi said ni raia wa bagamoyo maana sheikh mtanda ameamua kuishi bagamoyo kama mstaafu wa mahakama.
Ni kijana safi, muungwana ambaye ametoka ktk familia yenye maadili mema. Naamini kama si nape basi said ndiye anayefaa kwa nafasi kitaifa ktk kuiweka ccm vizuri.
Sometimes majina makubwa nayo yana gharama.
Nawashangaa sana nyie watu msiojua hata culture ya umoja wa vijana wa ccm...Ridhi hana ubavu wa kumweka mtu yeyote katika umoja wa vijana wa ccm...wakati wa uchaguzi wa uvccm wa ubunge huyo Ridh alikuja na mgombea wake Flora Jovin,lakini alichapwa kama amesimama....Uvccm huwa hawaangalii sura ya mtu wala cheo wala jina lako...uchaguzi wa Nchimbi uliopita mkapa,malechela,sumaye wote walimuunga mkono Nape na walikuwa na madaraka lakini haikuwasaidia kitu.walichapwa kama wamesimama.
Angalia alama za nyakati. Mambo yamebadilika sana na kesho msikilize JK utajua zama za UJIMA zimekwisha na yeye (JK) akichemsha naye anaingia matatani. Kwa hali ya sasa Nape ndiye atawasaidia UVCCM na kwa mantiki hiyo ataisaidia CCM. CCM kwa sasa ni sawa na jahazi linalotaka kuzama na abiria na nahodha wao JK wanatakiwa kujiokoa kwa kutumia maboya. Maboya hayo ni kina Nape, Mwakyembe, Kilango, Mpendazoe, Selelii na kadhalika. Hao kwa kweli mashua ikizama hawazami wao ni maboya tosha. Sasa kama CCM itayaachia maboya na kubebe mizigo kama vile kina Makamba na wenzake, wajue watazama
Angalia alama za nyakati. Mambo yamebadilika sana na kesho msikilize JK utajua zama za UJIMA zimekwisha na yeye (JK) akichemsha naye anaingia matatani. Kwa hali ya sasa Nape ndiye atawasaidia UVCCM na kwa mantiki hiyo ataisaidia CCM. CCM kwa sasa ni sawa na jahazi linalotaka kuzama na abiria na nahodha wao JK wanatakiwa kujiokoa kwa kutumia maboya. Maboya hayo ni kina Nape, Mwakyembe, Kilango, Mpendazoe, Selelii na kadhalika. Hao kwa kweli mashua ikizama hawazami wao ni maboya tosha. Sasa kama CCM itayaachia maboya na kubebe mizigo kama vile kina Makamba na wenzake, wajue watazama
Sasa una maana kuwa Nchimbi amukuwa ni serikali ya Bush mpaka ananipa visa ya kuniwezesha kukaa huku????Wewe ulidhani Nchimbi hana washabiki kwenye siasa?hangekuwa hana washabiki hasingeshinda chaguzi zake.Kaka nianze kwa kukuunga mkono kwa hoja zako, kwakweli kama CCM wanataka kupona wakishikilia maboya haya wamepona wakiyaachia wamekwenda!!!!!!!
Fisadi mtoto bahati mbaya twakujua kuliko unavyodhani, wewe ni kibaraka mkubwa wa Nchimbi na kwahakika hatan ukaaji wako US ni hisani zake nisingependa utupotezee heshima ya forum hii kama huna hoja kaa pembeni................
Wewei spinner kimsingi tangu lini Ridh akawa na uwezo wa kuwapanga wagombea na kuwachuja atakavyo ndani ya umoja wa vijana wa ccm.Atagawaje kura wakati hata majina ya wagombea wa mwisho bado hayajatoka maana ata mtanda kutoka ni hadithi...na kama issue ni kusini basi pia sio kweli kuwa Nape ana nguvu kusini kwa kuwa hawezi kuwa na nguvu Ruvuma.Pia kama ni kugawa nguvu za kusini kwa nini amtumie Mtanda wakati tayari alikuwepo Zainab Kawawa ambaye pia anatokea hukohuko kusini?acheni kutunga hapaswala la said mtanda na uvccm niliweke wazi hili, said kwa Beno malisa ni kijana wake mno hawezi kufurukuta kwa malisa, hata kidogo hivyo kaingizwa na kina Ridhiwani kwa lengo la kugawa kura za kanda ya kusini kwani naye kama Nape ni Chinga....huu ni mchezo wa Ridhiwani kujaribu kuzipanga kete kumpitisha Beno na sio Said kama wakuu wanavyo dai hapo juu
Mhhh hii ndo CCM alikosea kukomea hadharani angefanya kama Levy Mwanawasa kimya kimya kisha ukiukwaa unageuka kama kinyonga mbona mafisadi wangebanwa mbavu.
Ila Jk akitaka kushinda vita ya mafisadi amwongeze huyu dogo katika mapambano hayo....
sasa una maana kuwa nchimbi amukuwa ni serikali ya bush mpaka ananipa visa ya kuniwezesha kukaa huku????wewe ulidhani nchimbi hana washabiki kwenye siasa?hangekuwa hana washabiki hasingeshinda chaguzi zake.mbona wewe ni mshabiki wa nape nami sijakuzuia,mbona fieldmarshal ni mshabiki wa jsm nami naona ni kheri kwa upofu wake wa mtazamo hasi
Kikwete akitaka kuandaa njia yake kwa namna moja ahakikishe Nape anpew uenyekiti wa UVCCM watu wanataka cheche! Cheche za Fikra mpya!
Sasa una maana kuwa Nchimbi amukuwa ni serikali ya Bush mpaka ananipa visa ya kuniwezesha kukaa huku????Wewe ulidhani Nchimbi hana washabiki kwenye siasa?hangekuwa hana washabiki hasingeshinda chaguzi zake.mbona wewe ni mshabiki wa Nape nami sijakuzuia,mbona fieldmarshal ni mshabiki wa JSM nami naona ni kheri kwa upofu wake wa mtazamo hasi