Polen watanzania mwiz hapo anajulikana ila wanamkwepesha
Unamaanisha Moses?kama unafuatilia mpira wa bongo utakuwa unamjua tu. Kuna yule mwingine ni katibu wa malori ya usafirishaji, ana uhusiano mkubwa na waziri mkuu mstaafu aliyegombea urais mwaka uliopita. Wote wanahusika na usafirishaji wa mafuta ya magendo. Yaani ni cheni ndefu inakula hadi kwa viongozi wa serikali iliyopita..
Kwa hiyo Spinning zote ni kumsitiri Mkwere sio ?Mkuu anafanya kazi baada ya kupata ushauri wa kitaalamu namna ya kuvuruga mirija ya wakubwa bila kutikisa nchi. Haya mambo si ya mchezo mchezo kesho unaamka unamkamata Mkwere alafu biashara inafia hapo. Tuache spinning za ajabu kama kweli tunaipenda Tanzania. Tuunge mkono hizi juhudi badala ya hii tabia ya kuombeana mtu ashindwe tu alafu unajifanya mzalendo.
Hapana ni ya Managing Director wa Chadema mr Ngoyai Lowassa.Mengi yana originate Msoga
USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...Kuna uzi niliuona asubuhi somebody #jeneral aliuleta kuelezea uibaji unavyofanyika naomba mnitag
Mkuu si umeona wakati WMA wanasema mita Zina matatizo na zinatumika ndivyo sivyo, TPA waliiambia serikali mita haina tatizo lolote na haijawahi kusimama kufanya kazi.Mkuu bypass ni standby mode, ambayo kwa maelezo ya hiyo barua hapo juu alikuwa sahihi ili kunusuru ucheleweshaji wa upakuaji wa mafuta. Na kilikuwa ni kitendo cha muda mfupi, ili kurekebisha matatizo waliyokuwa nayo kwa kipindi kile. Ili kuongeza disharge rate inatakiwa kuongeza number of outlet vessels, ambalo ndio suluhisho la kudumu. Swali la kujiuliza kwa nini waliendelea na bypass system tangu 2009.?? Na kuacha njia halisi ya continous system ambayo ingesaidia kwa TRA kukusanya mapato yake kwa uhakika.??
Sijui huyo Mgawe kama kweli ni mhandisi.?? Hatua ya kufanya bypass ni hasara na ilitakiwa iwe kwa muda mfupi. Kwa sababu unapokuja kufanya auditing kwenye operational plant unaangalia kiasi kilichoingia na kiasi kilichotoka kwenye reserved tank, na obvious bypass huwa ina many errors due to wet spillage. Sio njia rasmi, ndio maana huwa inatumika kwa dharula tu. Kwa hiyo unashindwa kupata data kamili ya kile kinachotolewa, kwa kutumia mwanya huu waka-create another channel ili kuhakikisha ile spillage amount inakwenda direction tofauti na iliyokusudiwa, TIPER. Hapa TRA walipigwa chenga..
Hawa ni waongo kwa sababu flowmeter inakusaidia kufahamu ujazo wa mafuta kutoka kwa suppliers na inasaidia kucontrol na kuregulate kiasi cha mafuta kwa ajili ya clients. Kama vifaa hivi vilikuwa vibovu, TPA walikuwa na kazi gani wakati wote huo.?? Yaani kwa large operation kama bandari unatumia sticky.?? They cant be serious, hawa watu wanyongwe tu..
Only in Tanzania, malalamiko bila utafiti wowote. Kwa sababu wakala wa vipimo alikuwa na kazi ya kuhakikisha contents na volumes za mafuta ziko sawa kama inavyotakiwa. Yeye ndio alikuwa kiungo kikubwa kati ya TPA na Clients kuhakikisha hakuna upande unaopata hasara. Kwa maelezo yake ame-rely kwa stakeholders tu ambao ni wateja akasahau kwamba serikali inapata hasara, ambae ndio muajiri wake.!!
Wanaotakiwa kuwajibika ni TPA na WMA, kwa sababu mazingira ya kazi yanafanana huwezi kuwatenganisha. Na hii ishu walifanya wote kwa pamoja.
Hiyo ngazi ya juu nayo itumbuliwe haraka. Le Profeseri wananchi tulimkataa, raisi wangu JPM akaamua kuokoteza makapi ya JK acha avune alichopandaHakufanya bila maelekezo kutoka ngazi za juu kwa erikali ya ccm ya wakati huo. Pori lilelile nyani walewale
Yawezekana prof. Naye yupo kwenye kamrija ka upigajiWaziri mkuu alimuuliza swali huyo meneja WMA kwamba ni kwanini mashine hizo zinafanya kazi leo baada ya kusimama kwa miaka mitano, yule mama akajibu kwamba alipata maagizo kutoka ngazi za juu; PM akamuuliza hizo ngazi za juu ni zipi, Menaja akamjibu akamwambia Ni Prof. Sospeter Muhongo, PM akauliza ni utaratibu upi uliotumika kutoa hayo maagizo sijui alimjibu SMS.
PROF MUHONGO anatakiwa atoe maelezo yasiyo na shaka kwanini alimtumia huyo mama SMS moja kwanza sio utaratibu wa utendaji serikalini pili kwanini atume SMS baada ya kujua Waziri Mkuu anatembelea WMA ??
VINGINEVYO MUHONGO NA HUYU MAMA WOTE NI WA KUWAJIBISHWA
Tatizo la jam maana take ziko under design. Hili ni swala rahisi sana kwa serikali kama wange waka wazi na kuomba serikali itoe ata ruzuku ya kuredesign system nzima. Hapa lazima TRA na TPA walichukulia hili swala kama ka mrija ka kupigia pesaMkuu vunja mifupa kiini cha tatizo nionavyo mimi sio vibali vya ku-bypass metre hiyo nadhani ilikuwa plan B ya ku-control taratibu za upokeaji wa mafuta maana bila hivyo issue ingekuwa hivi.Metre zinapitisha mafuta kwa saa kadhaa halafu zina-jam masaa 24 hakuna kinachoendelea baharini huko kuna msululu wa meli 15 zinasubiri kushusha hali ingekuwaje?,ikaja plan kuwa kama zina-jam basi mtoa kibali ni kamishna wa TRA tu.Hizo metre za hovyo sana ni out-dated kabisa ni zile za mwaka 47,na hapa lazima kuna jipu la aliyeagiza zinunuliwe.Ni kweli zinazidisha volume na ndio maana TRA waliwahi kuzilipa kwa maana ya kuzirudishia pesa kampuni za mafuta,kwa maana kuwa ukipima kilichotoka melini ,kilichopita kwenye metre na kilichopokelewa kwenye tank la kampuni ya mafuta inayopokea mafuta kwa wakati huo utaona tofauti kubwa tu.
Kiongozi wako akikuambia tembea uchu uta tembea???. Hapa kuna walakini. Na ndio maana huwa wanaajiri mtu ambaye ni fani yake na mtu mwenye uzoefu na uongozi. Kuwa kiongozi ni pamoja na kuwa mshauri wa wenzako. Ukiambiwa utii swala ambalo liko kinyuma na maadili ya kazi utakubadili???. Huyu mama ajiandae tu moto unakuja!!NOPE, MAMA ALIKUWA KATIKA UTII WA VIONGOZI WAKE WAANDAMIZI
#MAADAM IS INNOCENT BY 100%,
KAZI NI PAMOJA UTII KWA VIONGOZI WAKO!.
Sasa kama alimwambia kwa simu ai "quote" na amtumie majaliwa. Hapa tunatafuta suruhu. Lakini pamoja na hayo. Huyu mama anajua sheria ya kazi. Kwanini anakubali kupekwa chaka na yeye anaenda tu??Mkuu serikali ni nani kama si waziri wa nishati??na yule mama alisema aliyemwandikia MSG kuwa ni Waziri Muhongo nina hakika serikali toka awamu ya kwanza ya JK ilikuwa inaijua vizuri tatizo la hizo metre.
Mkuu mimi sijui uchumi. Ila kuna kitu kinaitwa investiment cost, payback period na return on investment. Kwanza pa kuanzia ni sh ngapi zimepotea kwa watu kukwepa kodi kwa kuingiza mafuta bila ya kupimwa. Pili tuje kuangalia je hicho kiasi kisingetosha kununua flow meter mpya??. Na je hiyo pesa ingeweza kurudi kwa muda gani. Najua yote haya yangekuwa wazi serikali ingetoa pesa ya kununua hizo flow meter mpya au hata kuredesign system ya kupakulia mafuta hapo. Ifike atua hawa viongozi waendeshe mashirika kama ma CO wa makumpuniSerikali haina budi kulivalia njuga suala hili la Flow Meters kwani serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi kiasi cha US$ 40millioni every month!! just imagine kiwango hicho ni kikubwa mno ambacho kingeweza kudhibitiwa na serikali tusingehangaikia misaada kutoka kwa wahisani wanaotuwekea masharti lukuki. Nina mpongeza sana sana Mh.Majaliwa Waziri Mkuu wetu mpya hakika ameonyesha ana nia njema kabisa na maendeleo ya Taifa letu pamoja na Raisi JPM wote wanastahili, ziara kama hizi zinaamsha uozo mwingi sana ambao viongozi wengi wao walikuwa wanatengeneza mihela mingi ya kufa mtu wamejijenga hatari wanamiliki majumba miradi mikubwa mikubwa yakutisha, magari ndo usiseme hata salama maofisini hakuna ilikuwa ni full madharau kwa watumishi wenye vyeo vya chini na hata wageni walikuwa hawasikilizwi kwa sababu ya kiburi cha pesa nashauri Mh.Waziri Mkuu chukua hatua stahili kabisa aidha kuwashusha vyeo nakuwapangia vikazi vya hovyo pia serikali kupitia mkono wake wa usalama wa taifa na jeshi la polisi wafanye uchunguzi wa kina juu ya rasilimali wanazomiliki wakubwa hawa mtakuja kushangaa....
Mkuu hapo wote wanahusika. Walio by- pass na walio nunua flow meter za zaman. Na iman kuwa wanaofanya kazi hapo ni watanzania wenzetu wenye ueredi mkubwa wa haya mambo. Siku zote unapofanya kazi lazima ufikilie madhara yake. Walio fanya by pass wanahusika kwa wao kufanya kazi bila ya kufikilia outcome ya swala husika pia Audit inahitajika hapo kwani yawezekana wamenunua outdated kwa bei ya modern one. Yawezekana watu walisha piga pesa yao kwenye manunuzi.Cha msingi hapa rais Magufuli anapaswa kuachana kudili na hawa waliokuwa wakipokea na kuyafanyia kazi maombi ya ku_bypass flowmeters, hawa sio majipu halisi.Anapaswa kuwafuatilia wale waliohusika na mchakato wa ununuzi wa hizi flowmeters, haya ndio majipu halisi ya kutumbuliwa.Mimi nahisi hizi flowmeters zisizokidhi viwango zilinunuliwa kwa makusudi kabisa ili wapigaji wapate sababu ya kufanya yao ili hata kama ishu ikibumbuluka ionekane kweli kulikuwa na tatizo na hayo mengine yalitokea tu.Magufuli washughulikie wote waliohusika kununua hizi flowmeters.