Mkuu bypass ni standby mode, ambayo kwa maelezo ya hiyo barua hapo juu alikuwa sahihi ili kunusuru ucheleweshaji wa upakuaji wa mafuta. Na kilikuwa ni kitendo cha muda mfupi, ili kurekebisha matatizo waliyokuwa nayo kwa kipindi kile. Ili kuongeza disharge rate inatakiwa kuongeza number of outlet vessels, ambalo ndio suluhisho la kudumu. Swali la kujiuliza kwa nini waliendelea na bypass system tangu 2009.?? Na kuacha njia halisi ya continous system ambayo ingesaidia kwa TRA kukusanya mapato yake kwa uhakika.??
Yes...hoja ya bypass kwa sababu ya foleni haina mashiko sana...kama kweli walikuwa na nia ya dhati ya kuondoa foleni wangesema tumeamua kuwa vessels 3 zitapakua mzigo kwa flow meters na 3 zilizobaki kwa stick ili kupunguza foleni. Unaposema tunazima kabisa meters hizo napata ukakasi. On the other end ni sahihi kuomba temporary bypass ukiambatanisha na majina ya vessels kama walivyofanya but sasa ikawaje huu ndio ukawa utaratibu kwa miaka yote hii....hapa ndio unaona uwizi ulipoanzia
Sijui huyo Mgawe kama kweli ni mhandisi.?? Hatua ya kufanya bypass ni hasara na ilitakiwa iwe kwa muda mfupi. Kwa sababu unapokuja kufanya auditing kwenye operational plant unaangalia kiasi kilichoingia na kiasi kilichotoka kwenye reserved tank, na obvious bypass huwa ina many errors due to wet spillage. Kwa hiyo unashindwa kupata data kamili ya kile kinachotolewa, ndio maana wakaonganisha kimagendo kwa kampuni nyingine. Hapa TRA walipigwa chenga..
Kuna response moja ya upande wa WMA nido nimeona wameandika kuhusu "misbehaviour" ambayo ikanifanya niwe na shaka kama wanaelewa vifaa vyenyewe in the first place. Then kuna nyingine hapo naona Mgawe amemjibu vizuri sana Chuwa hasa baada ya kufungia kabisa hizi flow meter....inaonekana kuna pressure kubwa ilikuwa huu upande wa WMA kutoka kwa "stakeholders".....
Hawa ni waongo kwa sababu flowmeter inakusaidia kufahamu ujazo wa mafuta kutoka kwa suppliers na inasaidia kucontrol na kuregulate kiasi cha mafuta kwa ajili ya clients. Kama vifaa hivi vilikuwa vibovu, TPA walikuwa na kazi gani wakati wote huo. Yaani kwa large operation kama bandari unatumia sticky.?? They cant be serious, hawa watu wanyongwe tu..
Hapa ndio ajabu ya mwaka....wanabalance kwa mfanyabiashara tu kisa kalalamika...kama vilikuwa na faulty tutegemee kuwa kunawakati walikuwa wanalitia hasara taifa..je hao stakeholders walireport kuwa aisee naona kama mmetucharge kodi kidogo zaidi ya kiwango tulichopakua?
Only in Tanzania, malalamiko bila utafiti wowote. Kwa sababu wakala wa vipimo alikuwa ni kuhakikisha contents na volumes ziko sawa kama zinavyotakiwa. Yeye ndio alikuwa kiungo kikubwa kati ya TPA na Clients kuhakikisha hakuna upande unapata hasara. Kwa maelezo yake ame-rely kwa stakeholders tu akasahau kwamba serikali inapata hasara, ambae ndio muajiri wake.
Wanaotakiwa kuwajibika ni TPA na WMA, kwa sababu mazingira ya kazi yanafanana huwezi kuwatenganisha. Na hii ishu walifanya wote kwa pamoja.