Sakata la Makamu wa Rais Riadha Tanzania John Bayo kuhusu Vyeti, BMT wakosa majibu

Melubo Letema

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
308
282
Olympic Games ni mchezo unaotazamwa na kufuatiliwa na watu wengi zaidi duniani (zaidi ya bilioni 4), wenye mamlaka na madaraka ya kimichezo wanapokataa kutoa majibu marahisi wasitegemee medali za Tokyo Olympics.

Huu ni mwaka muhimu wa Olimpiki, BMT na Wizara ya Michezo wanapaswa kutatua kero ndogondogo za kikatiba ili tusipoteze muda wa maandalizi kuelekea Tokyo Games. Ofisi ya RT ni “Public Office” ambayo ni lazima ili tuamini kwamba katiba imefuatwa ipasavyo; profile (CV) za viongozi wake ziwekwe hadharani badala ya kukazana kuficha jina la chuo alichosoma Makamu wa RT.

Ili mchezo wa riadha uendelee na kuleta tija kwa kuleta medali ni sharti uwajibikaji na uzalendo utekelezwe kwa vitendo kwa kuhakikisha katiba inafuatwa 100%. Baada ya uchaguzi wa RT uliosimamiwa na BMT kwa matumizi ya katiba iliyorekebishwa kwa muongozo wa BMT kumekuja wasiwasi kwamba Makamu Rais mpya wa RT hakuwa na vigezo (diploma) kama kigezo cha kikatiba kwa mujibu wa takwa la Sera ya Maendeleo ya Michezo.

Binafsi nilifanya jitihada za kufuatilia ukweli huo nikajiridhisha kwamba kuna asilimia kubwa kuwa, kuna ukweli kwamba hajakidhi kigezo cha diploma kutokana na “reaction” zake kila mara anapoulizwa na “defense” kali anayopewa na wenye mamlaka na madaraka ya kimichezo. Ili kupata majibu sahihi na kwa masilahi ya mchezo wa riadha niliwasilisha ushauri wangu kwa wahusika ambao wanahusiana na marekebisho ya katiba na uchaguzi wa RT.

Niliwaandikia ujumbe Jonas Tiboroah (M/Kiti Kamati ya Uchaguzi), Filbert Bayi (Mhusika Mkuu katika Marekebisho ya Katiba, Neema Msitha (Mtendaji Mkuu BMT) na Dr. Yusuph Singo (Mkurugenzi wa Michezo). Pamoja na jumbe hizi zenye kutaka majibu sambamba na ushauri hakuna lililofanyika zaidi ya ukimya.

TIBOROAH - March 31/2021 (11:00am): Morning Sir, kikatiba nafasi ya VP wa RT imehakikiwa "Pasipo Shaka"? kama ilivyofanywa kwa wagombea wengine? Itakua aibu ikiwa katiba itavunjwa "Within Few Months Since Its Creation" Wapo wengi waliozuiwa kugombea kwa kukosa sifa kwa mujibu wa katiba na wanafahamu educational status za wenzao wote, ni lazima haki itendeke kwa kamati ku-certify docs zinazotiliwa shaka. MPAKA NAANDIKA UJUMBE HUU SIJAKURUPUKA. It is never too late to fix this cover-up!

FILBERT BAYI - April 20/2021 (6:02am): Morning Coach, nimejiridhisha kwamba VP hana vigezo kikatiba, (Tiboroah, Rwambo, Irene na BMT) wanafahamu walichokifanya siku ya Usaili. Truth can be unveiled any time, siyo wote serikalini wanapenda ku-risk ajira zao na ni wazalendo wame-share credible infos. RT ndiyo hiyo ninayoidai 13m lakini wananiteta 24/7, juzi walikuambia nipo Dar kumbe nipo kwetu Nangwa (kijijini alipooa VP wako)! Inamaana hata wewe hujui profile yake? You pushed educational standard ukiwa mwanakamati wa katiba; now what do we do?

NEEMA MSITHA - April 28/2021 (6:05am): Habari za kazi Naibu Katibu Mkuu BMT. Nashauri uagize Kamati nzima ya RT ilete Vyeti na CV zao upya "Resubmission" kwako mwenyewe ili ujiridhishe. Usihangaike kuomba watu walete ushahidi, kama mtu hana Diploma uletewe ushahidi upi? kwani ofisini kwako hakuna faili? je hata chuo alichosoma VP wa RT halina jina? Hivi kama mtu anacho cheti kwanini asikionyeshe ili asiaibike? Ulisimamia vyema marekebisho ya KATIBA; usijipake doa!

DR. SINGO - May 1/2021 (1:09pm): Happy May Day Mh. Mkurugenzi. USHAURI: Ingefaa uagize Kamati nzima ya RT ilete Vyeti na CV zao upya kwako - yaani "Resubmission" ili ujiridhishe. Mimi nimejiridhisha kuna ambao hawana vigezo kikatiba na wewe unafahamu ila umelinyamazia. Nimewaandikia Neema, Bayi na Tiboroa ujumbe kwa nyakati tofauti ili warekebishe hili kabla halijaleta aibu. Wewe na BMT mlisimamia vyema marekebisho ya KATIBA; sasa msijipake doa! KAZI KWAKO.

Hizi message zilipaswa kuwa “private” iwapo majibu yangetolewa au ushauri kupokelewa. Je, kama Makamu Rais wa RT hana hiyo diploma nini kimejificha nyuma ya pazia kiasi kwamba hata wataalamu waliosimamia katiba wanaona taabu kulitatua?

Kuna kila dalili kwamba wahusika wote wanafahamu ukweli wa jambo hilo, sisi wadau tunapaswa kuambiwa kwamba wao (wenye mamlaka na madaraka) wamejiridhisha kwamba jamaa kasomea diploma yake chuo hiki na kabla ya hapo alihitimu sekondari shule hii. Badala yake eti wanamtetea lakini wanaogogo kutaja hata JINA LA CHUO KILICHOMPATIA DIPLOMA?

BMT acheni kumlinda asiyenacho, na kama anacho wekeni wazi ili tuamini anacho tusonge mbele.

“UBABE WENU WA KUMLINDA MTU MOJA UTAAIBISHA RAIA MILIONI 60 WA TANZANIA MIONGONI MWAO MKUU WA NCHI”

Imetolewa na,
Wilhelm Gidabuday,
Mwanaharakati wa Michezo Tanzania
0783 144 464
 
Hapo ndio utajua waandishi wetu ni takataka hivi wanashindwa kufatilia hii ishu na.kuweka kila kitu hadharani
Unaambiwa mwandishi akiipata hii story anampigia Bayo anapewa bahasha na story inafia hapo. Kuna Bayi, Neema Msita, Tiboroha ambae mwanzo nilimsafisha kumbe anaufahamu huu mchezo tangu mwanzo kabisa.

Yaani huyu Bayo ni tatizo na sasa wadau wa riadha wameamua kua hizi dharau zifike mwisho. Mtu hata form four hajamaliza na ndio maana anafanya mambo ya ajabu, aliwahi kumpiga ngumi mjumbe mwakilishi wa kanda ya riadha ya arusha bwana Alfredo Shahanga kwenye mkutano.
 
Gidabday Mungu atakubariki. Umebaki wewe tu unaejitoa hadharani kuipigania katiba ya RT. Wengine wote wameufyata wanasemea pembeni.

Bayo tangu ametoka Mbeya kwenye Tulia Marathon ambako nako alipiga hela kwa wakimbiaji aliowaleta kutoka kenya, sasa hv yuko Dar anawaweka sawa mambo. Hataki mtu mwingine yeyote ateuliwe kwa zile nafasi za kikatiba katika safu ya uongoziwa RT ili kusiwe na kauzibe kwenye deal zake.

Sasa yeye ndio Sekretary, yeye ndio mkurugenzi wa ufundi, yeye ndio mwenyekiti wa Kamati ya masoko, yeye na mtoto wake ndio wanasheria wa club ndio wanatafsiri katiba ya chama nyumbani kwake na kulipana pesa za chama, yeye ndio msimamiz wa kila kitu kwenye kambi ya timu ya taifa, yaan ndio anaeenda sokoni kununua hata nyanya za kambi. Ni tatizo.

Habari za kutokua na sifa wizara nzima inazijua mpaka naibu waziri Gekuli ambae nae hatudhani kama atachukua hatua, tetesi za ukabila zinatawala kila mahali.
 
Back
Top Bottom