Naibu Waziri wa Michezo, Hamis Mwana FA, tunaomba Ufuatilie Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) ni chombo kinachodidimiza Riadha Tanzania

Melubo Letema

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
310
288
RAIS NA KATIBU MKUU WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA WAMEONGOZA TOC TANGU 1/1/2002, HIYO NI ZAIDI YA MIAKA 21.

Katibu Mkuu huyo na familia yake wanamiliki Shule iliyopo Mkuza Kibaha iliyopewa jina la FILBERT BAYI INTERNATIONAL SCHOOLS, anapanga shughuli zote za TOC zinazofadhiliwa na International Olympic Committee (IOC) na zote zinafanyika katika Shule yake Mkuza Kibaha Mkoani Pwani.

Hii ina maana, malazi kwa washiriki katika shughuli zote kama vile chakula, usafiri, stationary na upishi wote ni mkataba na shule yake, (Milo inayotolewa na huduma za upishi ni kampuni inayomilikiwa na marehemu mke wake), hivyo viwango vyote vya kulipwa vinapangwa na mwenyewe kwa pesa alizonazo yeye mwenyewe zinazotoka IOC, hivyo kupitia vyombo vinavyomilikiwa na familia yake ananufaika moja kwa moja na wadhifa alionao kama Katibu Mkuu wa TOC.

Fikiria mpangilio huu;

1. Filbert Bayi anaamua ni shughuli gani itafanyika chini ya ufadhili wa IOC
2. Filbert Bayi huandaa hafla hiyo katika Shule yake iliyopo Mkuza Kibaha
3. Filbert Bayi na familia yake hutoa huduma zote zinazohitajika kwa shughuli hiyo (Milo, Ukumbi wa Mikutano na vifaa vingine, usafiri na malazi inapobidi)

4. Wote kwa pamoja; filbert Bayi mwenyewe, Rais wa TOC Gulam Rashid na Makamu Rais wa TOC Henry Tandau ndio wawezeshaji wa shughuli zote; mfano(Semina, kozi fupi, warsha n.k) na inasemekana wanajilipa mara kadhaa ya kiasi kinacholipwa kwa wanachama wengine ikiwa ni pamoja na Wajumbe wa Tume ya Wanariadha (Athletes Commission).

Malipo haya mara nyingi ni nyongeza ya kile wanachojilipa kwa mahitaji ya kila siku wakiwa viongozi wa TOC.

Pia kuna swala hili la Olympic Solidarity na Athletes Support Funds, sisi Wanariadha wa Tanzania hatuna ufahamu wa kutosha jinsi hii inavyofanyika, lakini tunaelewa kuwa kuna fedha zinazotolewa na IOC kusaidia Olympians (wanariadha waliokimbia mashindano ya Olimpiki) katika maandalizi ya Michezo yajayo ya Olimpiki , hiyo inapelekea maandalizi hafifu ya wanariadha Tanzania, pia kuna msaada unakwenda pamoja na WANACHUO kwa maana ya ufadhili wa kimasomo yaani (Schorlaships).

Taarifa za kuaminika ni kwamba IOC inafadhili Shule ya Filbert Bayi kama Kituo cha OLYMPAFRICA kwa maana inapaswa iwe mali ya serikali wala siyo taasisi ya mtu binafsi, mpango huo ni wa kuwafadhili Wanamichezo wa Kitanzania lakini Filbert Bayi inasemekana kaifanya mali yake. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya IOC pia maadili ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria na pia naweza kusema ni Uhujumu Uchumi.

Shule ya Filbert Bayi inatoza wanafunzi ada kubwa, wakati huko IOC wanapeleka ripoti kwamba wanafunzi wanapatiwa ufadhili, lakini cha kushangaza ni kwamba IOC ilishaweka kituo cha Olympafrica DOLE Zanzibar (japo usajili wake unadaiwa kuwa kwa jina la (GULAM RASHID) ambaye ni Rais wa TOC. Filbert Bayi inasemekana akafanya ujanja wa kusajili Shule yake kwenye program ya Olympafrica na hivyo kile cha Zanzibar kikibakia kuwa GOFU lisilotumika sababu program zote zinaelekezwa Kibaha.

Usajili wa Olympafrica shuleni kwa Bayi ulifanyika kwa taswira ya rushwa baada ya Msenegali , Alassane Thierno Diack (Mkurugenzi wa OlympAfrica) kuja Tanzania kisirisiri Tarehe 24 - 28 Aprili 2019 na kukamilisha usajili na kuondoka.

Baadae viongozi wakuu wa TOC ambao ni wanufaika wakuu wa ujanja ujanja uliodumu tangu January Mosi 2002 tangu Bayi, Gulam na wenzao walipochaguliwa.

Katika utangazaji inasemekana Wazazi wanaombwa kupeleka watoto wao huko kwa ahadi ya matarajio ya kuchaguliwa kufaidika na ufadhili wa masomo wa IOC, inasemekana IOC wanapokuja kwa ukaguzi kuna (MABANGO MAALUM) yanawekwa kwa muda ili IOC waamini kwamba shule inatekeleza masharti yao, ila wakaguzi wakiondoka mabango hayo yanaondolewa. Kwa kifupi kuna mambo mengi hayaendi vizuri pale Tanzania Olympic Committee. Inasemekana watu hawa ni wazuri sana wa kutoa taarifa nzuri, lakini kikubwa tunaamini ni uzushi, tunaambiwa kuna baadhi ya viongozi wa juu wa IOC wanaaminika kuwa ni washirika wa makampuni ya Filbert Bayi na ndiyo maana haogopi hata serikali.

Mambo ya kutisha ni pamoja na yafuatayo;

1. 2001 - 2004 - Athens Olympics Games, ($282,594).

2. 2005 - 2008 Beijing Olympics, ($293,893).

3. 2009 -2012, London Olympics , ($680,192).

4. 2013 -2016, Rio de Janeiro ($ 523,993)

5. 2017 - 2020, Tokyo Olympics ($586,132)

Jumla ($2,366,774) sawa na TSH. 5,443,580,200 Kwa rate ya (1$ =2300) zaidi ya (Tsh 5.4B) kwa miaka 19 ambapo Olympics TANO zimefanyika bila mafanikio ambayo ni - (Athens2004, Beijing 2008, London2012, Rio2016 na Tokyo2020), pesa zote hizo hazikutumiwa ipasavyo ndio maana Tanzania tunafeli

Programu ya Olympafrica inapokea pesa nyingi nje ya hizo za 2001 hadi 2020, kiasi ambacho bado tunafanyia utafiti.

Kuna ruzuku ya Wanariadha ijulikanayo kama (Athlete's Support Funds) hazijawahi kutolewa kwa Wanariadha na TOC wananufaika na uelewa mdogo wa Wanariadha.

Kuna ruzuku ya Covid-19 iliyotakiwa kupewa wanariadha kutokana na kuahirishwa kwa Tokyo Olympics pia hazijawahi kutolewa.

Kuna fursa za kimasomo (Scholarships) ambazo inasemekana zinatolewa kindugu ama kirafiki ama kwa njia ya rushwa.

Kuna taarifa kwamba milioni 27 za Olympafrica zilitumika kwa mradi wa kuku DOLE Zanzibar, mradi huo una utata.

Makamu Rais wa TOC (Henry Tandau) anadaiwa kutengeneza risiti za kuchonga za milioni 25 kufuatia semina ambazo washiriki walikuwa wanajilipia kila sessions na thesis book zao wenyewe.

January 20/2022 magazeti kadhaa (tunahifadhi majina) yaliripoti habari za miaka minne iliyopita kwamba Filbert Bayi, Henry Tandau na Irene Mwasanga wameteuliwa ANOCA; wakati hayo yalifanyika January 2018; pongezi hizo feki zilizotolewa na Rais wa TOC Gulam Rashid zililenga kupumbaza umma wa Watanzania.

Kuna Mashindano yanayodhaminiwa na OLYMPIC SOLIDARITY ambayo yalipaswa kuzunguka nchi nzima kama Michezo ya Olympics inavyozunguka katika miji na nchi tofauti; lakini haya ya Karatu yamefanyika kwa miaka 13 Karatu pekee ambapo ndiyo nyumbani alikozaliwa ndg FILBERT BAYI.

Swali la kujiuliza je Mtwara, Mwanza, Singida, Rukwa, Kagera, Kigoma, Dodoma na Dar es Salaam na Mikoa mingine haipaswi kutafuta vipaji kwa udhamini wa Olympic Solidarity?
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
 
Filbert Bayi hana tofauti na CCM! Huyu jamaa tangu enzi na enzi, yeye ndiye Katibu wa TOC!! Kila uchaguzi unapofanyika, lazima atagombea na kushinda kwa kishindo!!

Yaani utafikiri hakuna watu wengine wenye sifa kwenye hicho cheo chake!!! Halafu hiyo double standard ni ya muda mrefu, na hakuna anayejali!!!

Bora mtoa mada umeamua kutema nyongo.
 
Filbert Bayi hana tofauti na CCM! Huyu jamaa tangu enzi na enzi, yeye ndiye Katibu wa TOC!! Kila uchaguzi unapofanyika, lazima atagombea na kushinda kwa kishindo!!

Yaani utafikiri hakuna watu wengine wenye sifa kwenye hicho cheo chake!!! Halafu hiyo double standard ni ya muda mrefu, na hakuna anayejali!!!

Bora mtoa mada umeamua kutema nyongo.
Sio hilo tu, hata akisikia kuna mwanariadha anayesifiwa kuliko yeye …lazima amfanyie figisu asiendelee…! Ataanza kwa kocha hadi kwa meneja wa mchezaji. Filbert Bayi ni sumu kwenye riadha tanzania
 
Back
Top Bottom