Kiongozi wa jopo la wanasheria watano (5) wanaomtetea Lwakatare, Wakili Tundu Lissu mezungumzia mawasiliano ya mtu anayeitwa Michuzi, kuwasiliana na watumishi wenzake wa OBR, akiwapongeza na kutoa kudos kwa TISS kwa kazi nzuri, akiwataka wenzake wapige sana kelele kwani hiyo ni kete muhimu kwa CCM. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, hawaruhusiwi kufanya surveillance dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM, kwa sababu upinzani wa kisiasa ni suala lililoruhusiwa kisheria nchi hii.
Aidha, Lissue ameongeza kusema wamepata mawasiliano ya simu yakionesha kuwa siku hiyo hiyo ambayo video imerekodiwa, majira ya saa 5.59, mtu aitwaye Ludovick alimpigia simu mtu aitwaye Mwigulu Nchemba. Kwa mujibu wa Wakili Lissu, yamepatikana pia mawasiliano ya mtu aitwaye Dennis Msacky akimpigia simu Lwakatare, ambapo wamemuuliza Lwakatare iwapo ni kweli aliwasiliana na mtu mwenye jina hilo (ambaye kwenye charge sheet ya pili, polisi wameonesha ndiye aliyekuwa akipangiwa kutekwa/kufanyiwa vitendo vya ugaidi), naye amekubali kuwa ni kweli alimpigia simu siku moja kabla ya tukio la kurekodiwa, akimuuliza kama amerudi Dar es Salaam, naye akamwambia alikuwa njiani kutoka Bukoba.
Amemaliza kwa kusema kuwa kesi hii ni kama kesi nyingine za kupikwa, ambazo polisi wamekuwa wakifungua dhidi ya CHADEMA na viongozi wa chama hicho, kwa nia ya kuiokoa CCM, kwasababu chama hicho kimekaliwa vibaya na hakiwezi tena kufanya siasa za ushindani dhidi ya wapinzani wao wakuu, CHADEMA.
"Ni mambo yale yale, walianza chama hiki cha familia ya Mtei na Mbowe, ikashindikana, chama hiki cha kikabila, cha Wachaga
ikashindikana, wakasema chama hiki cha kaskazini, imeshindikana, wamesema chama hiki cha wakatoliki, ikashindikana, wamesema chama hiki cha wakristo bado Watanzania wamekataa, iemshindikana pia
Sasa unafanyaje? Tengeneza hii kitu, sasa kiwe chama cha magaidi
ITASHINDIKANA pia," alisema Wakili Lissu.