Sakata la Lwakatare na sababu 2 za uthibitisho wa Mtonyaji Serikalini kuihujumu CHADEMA

Mkuu Mikael P. Awenda, Umenena vizuri sana. Pengine nami niseme kitu kimoja amacho ninakiona kiko kinaendelea, CCM inataka kutumia mfumo wa chama kimoja lakini kutokana na kutembeza bakuli kila siku inabidi ikubali kuwa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa ili bakuli likubaliwe na nchi za magharibi. Wakati huo huo, mfumo wa chama kimoja bado inautumia zaidi katika kutembeza bakuli kutoka nchi kama za china (refer. katibu mkuu anavyotoka jasho kutembelea chama rafiki), lakini inajaribu kutengeneza tabaka la watawala wa milele,yaani ile style ya bandika bandua. Akifa baba, basi mtoto lazima awemo kwenye mfumo nk.
Kutokana na hiyo style, tulioko kati kati na chini basi nijuhudi zetu kuungana na kuhakikisha tunatengeneza mfumo unaotoa fursa sawa kwa wote. Hii itawezekana kama tutashikamana na kusema, tunaweza na watakaobaki ndo watakaotukumbuka.
 
Majebele, kuweweseka kwa CCM na Serikali yake ndio kunatoa huo mwanya kwa CDM kuamini 2015 wanashika dola, hili pia na jitihada za CCM na Serikali yake zinavyofanya juhudi kuidhibiti na kuichafua CDM.
Fikiria haya yafuatayo;
1. Wanachama 120 wa CDM wahamia CCM, inashangaza jinsi vyombo vya habari kugeuza matukio madogo kama hili kuwa ni habari ya maana!
2. Vyombo vya habari vya Serikali kutotangaza habari kuhusu harakati za CDM wa CCM kuwewesekea CDM, kila kitu CDM, CDM, CDM! CDM ndio chama pekee cha upinzani Tanzania.

3. Dhuluma dhidi ya haki za Wananchi na kupindisha sheria za nchi wakidhani wanaikomoa CDM kumbe wananchi wanapoteza imani kwa CCM na serikali yake. Rejea kutofanyika uchaguzi wa Madiwani Arusha pamoja na sheria kuitaka serikali kuitisha uchaguzi mdogo wa Madiwani Arusha. Mfano mwingine ni sarakasi za uchaguzi wa Meya wa Ilemela, kuvunjwa Kamati za Bunge, kuzima hoja za binafsi za wabunge wa CDM Bungeni na Spika kukalia rufaa na malalamiko ya Wabunge wa CDM.

Hakika huu ni mwanya wa CDM kujiaminisha hivyo na nathubutu kusema iwapo CCM itashinda uchaguzi 2015 kwa kutumia sheria za hovyo za uchaguzi tulizinazo naTume hii ya Uchaguzi isiyowajibika kwa wananchi na badala yake inawajibika kwa Watawala kutakuwa na vurugu kubwa.
Mungu apishie mbali.

Ubize huu wa CCM na dola dhidi ya CDM ni kuzidi kuipaisha CDM
 
Tatizo lenu mnajipa imani kubwa kushika Dola 2015, CDM kweli imepata nguvu lakini bado haikubaliki kama mnavyo taka kuaminisha watanzania. Hizi mbinu tunazo ziona ni maigizo yenu wenyewe ili kuonyesha umma kuwa CCM inataka kuwamaliza kwa sababu CDM ndio chama mbadala. Kundi linalo washabikia ni vijana wafata mkumbo na wengi wao sio wapiga kura bali ni wapiga kelele tu.
CCM itafika wakati itang'oka lakini sio leo wala kesho, na wala haitakuja kutolewa na CDM. Wapiga kura bado hawajaona chama mbadala na hawako tayari kuwakabidhi Nchi nyinyi wakati hata chama kinawashinda kukiendesha.

Stupid,liwalo na liliwe hata nikila ban
 
Hapo umenena, na hili ndio jambo wanalo litazama wapiga kura, watu wanaona bora kuwa na serikali uharo kuliko kutokuwa na serikali kabisa. Mzee sitta hakukosea kusema CDM haina kiongozi, wao wenyewe wanalijua hilo. Tuchuke mfano Dr.Slaa, anasifa gani ya kuwa Rais wa hii nchi? watakuja watu humu na kusema kwani JK alikua na sifa gani? Na mimi nawajibu kuwa je tuko tayari kufanya test tena?
Mkuu Majebere nilikuamini kuwa wewe ni wa maana kumbe ndio wale wale, sasa unaona kuna mtu gani aliye bora kuliko Dr Slaa au Mbowe kwenye CHADEMA???? Tena naona mmekuja na single nyingine ya Six kuwa eti ndani ya CHADEMA hakuna viongozi, wewe unafikili hizo ratiba zoote za M4C na mipango yoote inafanywa nani??? Mkuu tulia kama uko kambi ya magamba unyolewe pole pole hadi tumalize kazi, viongozi wetu ni wale wale majibu yake utayaona 2014 -2015 wacha kuyumbisha watu huwezi umechelewa!!!!

 
Habari za kazi watanzania tunaoitakia mema nchi yetu kiujumla.
Napenda kusema yafuatayo kuhusiana na mjadala wa tukio hili la kipropaganda la kutekwa na kuteswa bwana kabanda.
Nimekuwa napenda kufuatilia kila kinachojili ili kuweza kubaini na kutambua nini kinaendelea.
Nimefanya uchunguzi binafsi na kubaini yafuatayo kitaalamu.
1.Mtu aliyeweka Video clip katika mtandao wa youtube anaonekana ni mtu wa karibu na mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu anajiita BUKOBA BOY. Hakuna asiyejua akina RWEYAMANU ni watu wa wapi.
2.Video clip hii si ya hivi karibuni ilipigwa Mnamo tarehe 28-12-2012 yaani mwaka jana.uchunguzi unanionyesha Bwana Lwakatare alikuwa anajua anarekodiwa, na alikua anajua nini kinataka kufanyika baadae kwa makubaliano waliyokubaliana ukiiangalia na kuichunguza ni yeye kweli na inapoanza tu anasema sogeza MIC kiutaalamu nasema hivi kwa sababu linasikika neno MIC maneno ya nyuma nyuma (SOGEZA) Yamekatwa.
VID-20121228-00005 - YouTube
Click ama copy link na upaste kwenye browser yako uangalie na ikibidi download
Kwa sababu za kiusalama na kulitakii mema taifa letu,mtu mwema ambaye si mnafiki, angelifikisha hiyo video Polisi kuanzia tarehe 28/12/2012 na mapema January 2013 angekuwa na uzalendo. Kujua tu mambo flani kidogo katika technlojia ya sasa ya audio, video na computer kusimfanye akadharau watanzania walio wengi akidhani wako nyuma kwa kuwalisha pumba na mikakati mibaya kuchafua CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
3.Mtu aliyekuwa anapewa maelekezo ya huo utekaji unaozungumzwa ndio huyohuyo aliyekuwa anarekodi hiyo video tena kwa kutumia simu ya Nokia. Hii ni hakika . Alivyokuwa hajui hata mambo ya kiusalama ameshidwa kui RENAME clip aka uplod hivyo hivyo VID-20121228-00005. Ni clip ya tano kati ya clip alizo record siku hiyo.
Nina uhakika na hili. (BUKOBA BOY) Ukiangalia katika mtandao wa youtube ametuma video clip tano tu na zote zinahusiana naishu hii tu. Zikionyesha video hii , na karatasi anayodai Rwakatale alikuwa akiitumia kama rafu bwana rwakatale wakati ana toa maelezo. Bukoba boy anasema hivi
‘Hii kataratasi ndiyo aliyoitumia Lwakatare kuchukua note/ dondoo wakati anatoa maelekezo kwa vijana kwenda kuandaa mipango ya utekaji. hiyo namba hapo juu kulia ni ya MSACKY wa kampuni ya mwananchi ambaye naye ni target ya kutekwa. Nimeona mijadala mbalimbali ikieleza kwamba video iliyomwonyesha LWAKATARE ni ya UONGO, hivyo nimeweka hapa mwandiko wa mkono wa Lwakatare ili kuthibitisha UKWELI wa taarifa hizi. Tutazidi kuweka bayana ushahidi mwingine. NIPO HAPA KUWAFANYA WATANZANIA WAUJUE UKWELI WA MATUKIO HAYA YA KUSIKITISHA YANAYOENDELEA HAPA NCHINI. KWELI ITAKUWEKA HURU DAIMA.’ Mwisho wa kumnukuu. Na ndani ya hiyo karatasi inaonyesha namba ya mtu aliyekusudiwa hiyo namba ni 0764-331010
Ukiangalia hili unapata ukweli kujua kwamba baada ya kuweka video ya uongo, na watu kupinga amekuwa anaendela kulitetea hili na kuzidi kudhibitisha kwa kuonyesha hata karatasi aliyokuwa anaitumia mtuhumiwa kuandika andika . ndio maana nasema video haikupigwa bahati mbaya kila kitu kinachoendelea kinajulikana na kimeandaliwa.
Na kudhibitisha hili kama nilivyosema video hii si ya juzi wala jana ni ya tarehe 28-12-2012 siku tatu baada ya KRISMASI ndio utasikia ndani ya video kuna mtu anaingi ana kuwauliza za sikukuu. Jamani mbona vichekesho hivi,
Hivi ishu kama hii watu wanapanga mkakati kama huu, anaweza kuingia mtu ndani ghafla na mlango upo wazi mpaka anaingia na kuwasemesha mpaka anatosheka na kuondoka.?
4.(Bukoba boy)Pia kitaalamu kwa mtu kama mimi. Namuona bado ni mchanga kwenye masuala ya teknohama. Amejaribu kudanya wasioju teknohama. Amefungua akaunti kwa ajili ya kufanyia uongo huu mnamo tarehe 11 march 2013.
Nafanya trace na tracking kujua alituma hivi vitu akiwa wapi na kujua yeye ni nani hakika hili wala si jambo kubwa kwangu.
5. uzoefu unaonyesha CCM na serikali imekuwa ikifanya matukio na kuya propaganda hili linaushahidi wa kutosha,
i.Ukianzia kifo cha mkurugenzi wa usalama wa taifa kipindi hicho. Marehemu Kombe nani hajui alikufaje?
ii.Kutekwa kwa Dr Ulimboka ,walipofeli kumuua na kubahatika kupona walihaha kuanzia kuzuia gari wa kati anapelekwa hospital, Ghafla waka propaganda aliyemeteka ni mkenya kajisalimisha kanisani kutubu anashikiliwa najeshi ya polisi.kesi upepelezi haujakamilika. Dr ulimboka kwenda kumtambua hawataki.
Tuache hili hayatuhusu Tuangalie hili tunafanyaje:
Mimi napenda kushauri CHAMA CHA CHADEMA kumuachia Bwana Rwakatale BLACKMAILED YAKE kama alivyo pokea ujira wake.
Na hapo chama wala katikakuwa hivyo wanavyo taka wao, wala wanavyokusudia, kwa nini nasema hivi
Nani hakumbuki habari zilivyotawala vyombo vya habari mnammo tarehe 27 december 2011
DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Bi.Tusekile Mwakyoma (28), amechomwa kisu chini ya ziwa la kushoto na mchumba wake Mkurugenzi wa Mafunzo na Uenezi wa chama hicho, Bw.Songa Mgweno, mkazi wa Kijiji cha Kilimanjaro, ambaye alitoweka baada ya tukio hilo.
Akizungumza na Majira akiwa wodini katika Hospitali ya Misheni Bwagala, Bi.Mwakyoma alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo Bw.Mgweno, alikimbia na fedha zake sh.200,000.

“Huyu Bw.Mgweno ambaye ni mchumba wangu, alinipigia simu saa mbili usiku niende nyumbani kwake Kijiji cha Kilimanjaro ili nikachukue fedha zangu, niliamua kulala huko na ilipofika alfajiri, aliniamsha na kuniuliza nimefanya juhudi gani kuhakikisha wazazi wangu wanakubali anioe lakini nilimwambia sina jibu.
“Tuliendelea kulala lakini baada ya muda, alianza kunipapasa nikasikia maumivu makali chini ya ziwa la kushoto, baada ya kujichunguza, nikaona kisu kikining'inia,” alisema
Nini kikafuata?
Mtuhumiwa ghafla ikafanywa anaugonjwa wa akili , ikasemekana amepelekwa milembe hospital ya vichaa. Ahahaaaa inafurahisha mtuhumiwa hana historia ya uchizi hata kidogo ninavyo andika waraka huu mtuhumiwa yupo huru anakula bata mnajua.?
Kaka yake ni afisa usalama hapo ikulu dare s salaaa. Nani hamjui
Nao ni mpango ulishasukwa mapema.

Mwisho napenda kusema wanachama na watanzania tusizubaishwe na hili, kwa ni hili limekuwa ni mazoea kukiwa na jambo ya gesi kufunikwa na hili, kukiwa na migomo ya waalimu kufunikwa na jambo jengine ndio imekua fasheni.
Rwakatale sio chadema ,Rwakatale ni mwanachama ashikatikwe kwa mujibu wa Blackmailed yake wala chama Hakina sababu ya kumtetea kwa anajua alilolifanya na Mungu ni shahidi yake.

Natanguliza shukrani
MTANZANIA MWENYE UCHUNGU NA TANZANIA
 
Yote yanawezekana though mi nabaki kuwa 50/50 cuz najua kuwa maAgent wa pande zote 2 wapo kazini na wote kwa lugha za maandishi hapa jamvini wamekuwa wanakuwa na appearance yenye ushawishi mkubwa sana kiasi cha kuwaaminisha baadhi ya wa2 kuona kuwa huo ndio ukweli wenyewe wa mambo
 
cdm imekuja kwa maombi ya watu kwa muumba na mungu wa israel,isaka na yakobo atatupa nuru na cdm itawakomboa watesi wake
mpaka mtakapotubu midhambi yenu ndo mungu atawasamehe.hizo ni adhabu za hapa duniani za ahera bado zinawasubiri
 
1. Sakata la Lwakatare linataka kugeuzwa kisiasa dhidi ya Chadema.
sakata tata la Lwakatare ambalo linaonesha kwamba video yenyewe ina kila dalili kwamba ni ya kuchonga imeanza kutumika kimkakati dhidi ya Chadema kwa lengo la kuichafua. Ikumbukwe kuwa, jambo hili linatokea muda mfupi baada ya Mwigulu Nchemba kudai kwamba ametumiwa meseji ya kutiswa maisha na Mnyika jambo lililothibitika baadaye kwamba siyo kweli. Badala yake tukajuzwa kuwa kuna mtambo ulioingizwa kutoka nje ambao ulifanya kazi hiyo. Mwigulu hakushtakiwa kwa kudanganya ama kumchafua Mnyika? Swali ni je, kama meseji ya Mwigulu ilikuwa ni hujuma ya wazi ya ccm dhidi ya Chadema, ni kitu gani kitufanye tuamini video hii ya Lwakatare iliyoanza kurushwa hewani na Mwigulu Nchemba huyo huyo tangu dec 2012? Na ni kpindi hicho hicho ambacho video hii ya Lwakatare inaonesha ilitengenezwa. kwanini hawakuileta public muda wote? Na je, juhudi na nguvu inayotumika kwa Lwakatare kwanini haitumiki kwa Mwigulu aliyedai kutumiwa meseji hiyo au kutafuta chombo hicho kilichotumiwa na Mwigulu? Kama siyo Chadema kupre empty ina maana Mnyika naye angekulala Lupango kama Lwakatare. Hali hii mpaka lini?

lakini video never lie. You need to dilate on why you think the video is a product of photoshopping?
 

5
Ununuzi wa viongozi wa Chadema kwa kutumia fedha na ahadi ya vyeo bila kusahau sakata la viongozi wa Bavicha ni juhudi nyingine za kuithibiti Chadema.

sasa hii ni hujuma au ni unoko wa viongozi wa cdm ambao wanaabudu chapaa?
 
B) Mbinu ya tatu ilikuwa ni kuibatiza ccm au kuibadilisha ccm kwa kuanzisha chama kipya.
Wakati ule nilipoleta habari ya mtonyaji kwamba kuna mkakati wa ndani kabisa wa kuibadilisha ccm au kuibatiza ccm watu hawakunielewa hata kidogo. Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa ktk mitandao ya kijamii iliyomnukuu msajiliwa vyama akisema kwamba, ofisi yake inaandaa mswada wa sheria wa kuruhusu vyama kuungana. Baada ya tamko hilo nadhani sasa ninaeleweka zaidi kuliko wakati ule nilipokuwa naleta taarifa za mtonyaji.
Ikumbukwe, huko nyuma serikali ya ccm ndo iliyokwamisha sheria ya vyama kuungana. Sasa, iweje sheria hiyo ikaletwa na serikali ile ile ya ccm? Huu ni uthibitisho wa taarifa za mtonyaji wangu ya kuibatiza ccm kwa jina jingine au kuanzisha muungano na chama kingine ili jina ccm lililochokwa libadilishwe.
Huu ni mkakati unafanywa na viongozi wa ccm na idara kwa siri sana kwa muda mrefu.

Hivi kweli ccm itaungana na nani na hivi vyama vya musimu? labda jipange upya au hakikisha umenunua tembo mastercard ya ccm, lol!
 
MBona njama zote zimeabbort kwa msaada wa watu wa Tanzania,leo utafanya njama gani ambazo wananchi wataacha kuzipiga teke na kufanya CCM waendelee kujinyenyea tu
La msingi Chadema waendelee na ratiba za kazi zao walizojipangia kwa mwaka na CCM waendelee kudondosha machozi ya damu manake lichama la watu liko mioyoni mwa watu linajiuza lenyewe bila hata nguvu za mapesa CCM inatumia ,baada ya kutwanga chini na li CCM litakuwa marehemu kwa sababu limejitafutia maadui wengi mpaka kuku na mbuzi adui wa CCM
 
Hizi ni dalili za chama na serikali Dhaifu kushindwa kuongoza nchi! wananchi wanataka mabadiliko! CCM wanatumia Umafia ili waendelee kuongoza nchi.
 
Kama polisi wanafuatilia huu uzi wanapaswa kumchukua mleta mada ili awasaidie uchunguzi... jambo hili liko polisi lakini nashangaa kwanini watu wasiwe watulivu na kuelekeza nguvu zao kuhakikisha wanathibitisha njama hizi kuwa ni za uongo!
 
Tatizo lenu mnajipa imani kubwa kushika Dola 2015, CDM kweli imepata nguvu lakini bado haikubaliki kama mnavyo taka kuaminisha watanzania. Hizi mbinu tunazo ziona ni maigizo yenu wenyewe ili kuonyesha umma kuwa CCM inataka kuwamaliza kwa sababu CDM ndio chama mbadala. Kundi linalo washabikia ni vijana wafata mkumbo na wengi wao sio wapiga kura bali ni wapiga kelele tu.
CCM itafika wakati itang'oka lakini sio leo wala kesho, na wala haitakuja kutolewa na CDM. Wapiga kura bado hawajaona chama mbadala na hawako tayari kuwakabidhi Nchi nyinyi wakati hata chama kinawashinda kukiendesha.
Mwenye macho haambiwi tazama
 
Fedha zetu zilizofichwa Uswiss, SA,CayMans Island, majumba ya kifahari London to mantion just a few mtarudisha lini, usidhani hizo ndio kero peke yake!!! Nimesikia wameanza kulipana fedha za DOWANS na RICHMOND hapo napo unasema je?????
 
Gwargwet!CCm kwa sasa wamepoteza mashiko,ni raia wachache wenye maslahi binafsi na uwepo wa ccm ndo wanapigia chapuo.Hao nobility mwisho wao 2015.Hawaammini lakini ngoja mda ufike.Huu uhafidhina unaoendela sasa hivi ni dalili tosha kwamba mbinu za kawaida zimeshindikana.
Chamsingi mahakama za kimataifa zipo zenye HQ hapa nchini tutafanya kuwasogezea.
Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom