Sakata la Lwakatare na sababu 2 za uthibitisho wa Mtonyaji Serikalini kuihujumu CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Lwakatare na sababu 2 za uthibitisho wa Mtonyaji Serikalini kuihujumu CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Mar 18, 2013.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huko nyuma ktk moja ya mada zangu JF nilieleza habari nilizoelezwa na mtonyaji wangu Serikalini kwamba kuna mipango mibaya ya kuihujumu CHADEMA ili kuithibiti kabla ya 2015
  Nilielezwa kwamba serikali ya JK imepewa kuchagua jambo moja kati ya options 3 kuhusu CHADEMA ambayo ni;
  1) awe tayari kuwapa nchi 2015
  2)aisambaratishe CHADEMA sasa kabla ya 2015 au
  3)waibatize CCM kiwe chama kipya kimya kimya ili iendeleze sera za ccm.


  Leo naomba kuthibitisha ukweli wa mtonyaji wangu kwa kutumia matukio mapya yaliyotokea baada ya mada yangu hapa JF. Ukweli huu ni wa kuthibitisha kwamba Serikali imeamua kutumia mkakati kuhakikisha kwamba demokrasia haitachukua mkondo wake 2015 na badala yake wameamua (no 2 na 3 kwa pamoja) na kuisambaratisha CHADEMA kwa mbinu zozote nzuri na mbaya na kuibaitiza CCM.

  A) Nitatoa mifano michache ya hujuma hiyo na Sakata jipya la Lwakatare halafu nitamalizia ubatizo mpya wa CCM.

  1. Sakata la Lwakatare linataka kugeuzwa kisiasa dhidi ya CHADEMA.
  sakata tata la Lwakatare ambalo linaonesha kwamba video yenyewe ina kila dalili kwamba ni ya kuchonga imeanza kutumika kimkakati dhidi ya CHADEMA kwa lengo la kuichafua. Ikumbukwe kuwa, jambo hili linatokea muda mfupi baada ya Mwigulu Nchemba kudai kwamba ametumiwa meseji ya kutiswa maisha na Mnyika jambo lililothibitika baadaye kwamba siyo kweli. Badala yake tukajuzwa kuwa kuna mtambo ulioingizwa kutoka nje ambao ulifanya kazi hiyo. Mwigulu hakushtakiwa kwa kudanganya ama kumchafua Mnyika? Swali ni je, kama meseji ya Mwigulu ilikuwa ni hujuma ya wazi ya CCM dhidi ya CHADEMA, ni kitu gani kitufanye tuamini video hii ya Lwakatare iliyoanza kurushwa hewani na Mwigulu Nchemba huyo huyo tangu Dec 2012? Na ni kpindi hicho hicho ambacho video hii ya Lwakatare inaonesha ilitengenezwa. kwanini hawakuileta public muda wote? Na je, juhudi na nguvu inayotumika kwa Lwakatare kwanini haitumiki kwa Mwigulu aliyedai kutumiwa meseji hiyo au kutafuta chombo hicho kilichotumiwa na Mwigulu? Kama siyo CHADEMA kupre empty ina maana Mnyika naye angelala Lupango kama Lwakatare. Hali hii mpaka lini?

  2
  Taarifa za kuwindwa kwa Dr Slaa, John Mnyika na Lema;
  Habari za kuwindwa kwa viongozi hao ni hujuma za wazi dhidi ya CHADEMA. Jana nimesoma magazetini kwamba Mbowe naye kaunganishwa ktk wanaowindwa. Pamoja hilo la viongozi wa CHADEMA kuwindwa, tishio la maisha ya waandishi wa habari nchini ambalo limesharipotiwa mpaka ktk magazeti ya ulaya ni wazi lengo lake ni kudhibiti habari. Na wazi pia kwamba kati ya habari inayothibitiwa ni habari za CHADEMA ambacho ni adui wao namba moja wa serikali ya CCM.

  3
  Wakati ule nilipotonywa sikujua kwamba, kutakuwa na mkakati wa kutoonesha Bunge live ulioibuliwa mwezi uliopita – bahati nzuri mkakati ukakwama. Japokuwa hoja dhaifu iliyotumika ni vurugu Bungeni lakini ni wazi kwamba walikuwa wanahujumu CHADEMA.

  4
  Hujuma za wazi dhidi ya Wabunge wa CHADEMA Bungeni kama vile kukwamishwa kwa hoja zao binafsi ,kuunganisha baadhi ya kamati za kuduma na kupindisha kanuni za Bunge wazi wazi, vinathibitisha kwamba kuna mkakati mkubwa wa kuihujumu CHADEMA.

  5
  Ununuzi wa viongozi wa CHADEMA kwa kutumia fedha na ahadi ya vyeo bila kusahau sakata la viongozi wa BAVICHA ni juhudi nyingine za kuithibiti CHADEMA.

  Hayo mambo 5 yanathibitisha kwamba kuna jitihada za kuisambaratisha CHADEMA.
  Je, kauli za Nape Nnauye, Mwigulu na Steven Wasira kwamba CHADEMA itakufa walikuwa wanategemea mkakati huu?

  B) Mbinu ya tatu ilikuwa ni kuibatiza CCM au kuibadilisha CCM kwa kuanzisha chama kipya.
  Wakati ule nilipoleta habari ya mtonyaji kwamba kuna mkakati wa ndani kabisa wa kuibadilisha CCM au kuibatiza CCM watu hawakunielewa hata kidogo. Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa ktk mitandao ya kijamii iliyomnukuu msajiliwa vyama akisema kwamba, ofisi yake inaandaa mswada wa sheria wa kuruhusu vyama kuungana. Baada ya tamko hilo nadhani sasa ninaeleweka zaidi kuliko wakati ule nilipokuwa naleta taarifa za mtonyaji.
  Ikumbukwe, huko nyuma serikali ya CCM ndo iliyokwamisha sheria ya vyama kuungana. Sasa, iweje sheria hiyo ikaletwa na serikali ile ile ya CCM? Huu ni uthibitisho wa taarifa za mtonyaji wangu ya kuibatiza CCM kwa jina jingine au kuanzisha muungano na chama kingine ili jina CCM lililochokwa libadilishwe.
  Huu ni mkakati unafanywa na viongozi wa CCM na idara kwa siri sana kwa muda mrefu.

  Swali ni Je, watafanikiwa kuizuia CHADEMA kuingia Ikulu 2015. Jibu langu ni Hapana – hawataweza. LET US WAIT AND SEE.
   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,939
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  We shouldn't WAIT AND SEE, tutaendeleza kazi yetu ya kukisurubu chama hiki cha magaidi.
  Tuendelee na kazi kubwa ya kuimarisha mtandao wetu nje na nchi ili 2015 and beyond that tuoneshe kuwa ccm were just Hoodlums
   
 3. M

  Magesi JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2013
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yetu Macho
   
 4. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #4
  Mar 18, 2013
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,374
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Mh! Nafikiri hii siyo Movie ya kawaida...
   
 5. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,579
  Trophy Points: 280
  Mikael P Aweda,kwa ninavyoiona serikali yangu,na viongozi wake wanaopenda kulipizana visasi,mh!Nadhani tuko pabaya zaidi watanzania kuliko tunavyodhani.Viongozi wetu wengine toka niko shule ya msingi wao ni viongozi tu hivi swali la kujiuliza ni kwa nini hawasemi basi?Wanaogopa nini kama kweli walifanya kazi kwa uzalendo?

  Hata hayo wanayoplan mwisho wa siku yatatoka nje tu,maana mgongano uliopo ndani yao ni mkubwa.Muda mfupi ujao wataanza kushambuliana baada ya mkakati wa kumtwisha msalaba Lwakatare kutumbukia nyongo.Bado ningependa kuwaambia viongozi wetu waache siasa chafu hazitujengi zinatuletea uhasama siku hadi siku.Tutafika mahali watanzania tutagawanyika kulingana na vyama vya siasa na ndipo patakuwa pabaya kuliko huko tulikotoka.
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2013
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,515
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wao wana dola CHADEMA ina Mungu tuone nani ananguvu zaidi!
   
 7. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2013
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nadhani ni mhimu sana kujua namna gani kila mtu kwa nafasi yake anashiriki kikamilifu kuleta mapinduzi ya kweli katika nchi hii, Chadema pekee yao hawawezi, tukiendekeza hali hizi za propaganda, uongo uzandiki, majungu, chuki ushirikina baadae nchi itapoteza kabisa muelekeo, na hatutakuwa na historia ya kweli ya nchi hii, maana historia inatakiwa iwe ya kweli bila kujali ni mbaya au nzuri.

  Mfano mambo machafu ya laana yanayo fanyika ssa nchini kama kuuwa waandishi askari wanasema ni kitu chenye ncha kali, kumchukua mtu unaenda kumtesa kama mnyama alafu kila mtu anasingizia.,,tuna hitahija sasa tusimame pamoja kuiokoa nchi yetu
   
 8. m

  majebere JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Tatizo lenu mnajipa imani kubwa kushika Dola 2015, CDM kweli imepata nguvu lakini bado haikubaliki kama mnavyo taka kuaminisha watanzania. Hizi mbinu tunazo ziona ni maigizo yenu wenyewe ili kuonyesha umma kuwa CCM inataka kuwamaliza kwa sababu CDM ndio chama mbadala. Kundi linalo washabikia ni vijana wafata mkumbo na wengi wao sio wapiga kura bali ni wapiga kelele tu.
  CCM itafika wakati itang'oka lakini sio leo wala kesho, na wala haitakuja kutolewa na CDM. Wapiga kura bado hawajaona chama mbadala na hawako tayari kuwakabidhi Nchi nyinyi wakati hata chama kinawashinda kukiendesha.
   
 9. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2013
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,470
  Likes Received: 3,364
  Trophy Points: 280
  CHADEMA imekuja kwa maombi ya watu kwa muumba na Mungu wa Israel,Isaka na Yakobo atatupa Nuru na CHADEMA itawakomboa watesi wake
   
 10. F

  FUSO JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 12,685
  Likes Received: 3,050
  Trophy Points: 280
  kuna muda longo longo huwa hazifanyi kazi -- gia zote zimeshatumika sasa wanajaribu na hizi za kubambikiana bila kujua risk kwa taifa wanaloliongoza.
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2013
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 3,014
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Una uhakika na maneno yako au u just guess, kukaa Dar muda wote bila kurudi kwenu kijijini kunakudanganya, vijijini mambo ni tofauti, jaribu kuwauliza ccm wenyewe taarifa wanazo kuwa no more ccm in villages ndiyo maana unaona sarakasi hizi.Ujue mjusi kabanwa.just wait na see
   
 12. Ronn M

  Ronn M JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2013
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 1,283
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CDM has to prove that its hundred times smarter than CCM! Otherwise it may end being a permanent opposition. To fight with someone in power you need to be more brilliant than him.
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Umeisema kama utani lakini mmoja ya hoja ya wahafidhina ndani ya ccm na kutaka misingi ya TANU iliyoachwa irudishwe. Tatizo ni kwamba hakuna mwenye maadili ya kuisimamia jambo hilo.
   
 14. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #14
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mr Ronn,
  What are the optional means that CHADEMA could explore in handling situtitions it is facing currently???
   
 15. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2013
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,697
  Likes Received: 1,426
  Trophy Points: 280
  Lkn mbona wanatumia mbinu za kijinga?
  mie nafikiri hizi mbinu zitawafurahisha wao tu lkn wafuasi wengi wa cdm hawaamini kabisa neno lolote la ccm dhidi ya CDM!
   
 16. m

  majebere JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu ya kijijini ndio acha kabisa, usione watu wamejazana ukafikiri ni wapenzi wa chama, hao wanakuja kushangalia helkopta. Ni rahisi sana kubadili mawazo ya watu wanao ishi mjini lakini wa kijijini sio rahisi. Bila shaka wewe huna ndugu kijijini ndio maana unasema haya. Watanzania bado wanachagua mtu kutokana wanavyo shauriwa na mwenyekiti wa kijiji. Usimshangae mbunge wa ccm anae wapigia magoti wapiga kura ndugu yangu, hayo ndio mambo yanayo takiwa kijijini.
   
 17. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii inafaa zaidi kanisani!
   
 18. b

  bensog26 Senior Member

  #18
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 161
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kweli mkuu wasome nyakati wavijijini sasa ndio wameikataa ccm na ccm imewatupa ipo dar inacheza mchezo mchafu
   
 19. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,492
  Likes Received: 2,976
  Trophy Points: 280
  Wanaiandaa nchi kwa ajili ya New World Order na ndio maana haya matukio yamezidi kukithiri.
  Nchi maana wameingia hata kwenye Taasisi za Kidini zenye mitazamo tofauti na wao.
  Ashukuriwe Muumba kwa kuwa hakuna siku ambayo Shetani ameshawahi kumshinda Mungu.
  ...............Wao wana Dola, lakini sisi tuna MUNGU.............
   
 20. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #20
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwamba umejua hii ni movie ya ukweli - it about life or death.
   
Loading...