Mkuu,
mada ya leo ni
Je, ni sawa kuwinda maisha ya viongozi wa upinzani?
Je, ni sawa kubinya demokrasia bungeni?
Je, ccm kujibatiza itawasaidia 2015?
Hayo mawazo yako ya idadi ya viongozi wa chadema tuanzishie thread yake.
Kama haya ndiyo maswwali yako Aweda, huna mada ya kuwasilisha hapa.
Majibu ya maswali uliyouliza yote yana majibu yasiyokinzana labda kwa mwendawazimu tu ndiye anayeweza kuja na majibu tofauti.
1) Si sawa kumuwinda mtu yeyote yule awe mpinzani au wa chama tawala
2) Democracy haistahili kubinywa
3) Ni ngumu kujua kama itawasaidia. Hiyo inategemea na aina ya transformation watakayoifanya.
Kwa mfano, wakiamua kuwaweka mbele wale amabo hata CHADEMA inawakubali kama akina Magufuli, Sitta, Salim na wangine ambao wana clean record wanaweza kuwasumbua wapinzani wote. Issue ni je CCM wanaweza kufanya hivyo.
Lakini yote kwa yote, ukweli haupigiwi kura. Hapa ilibidi pia tujadili kama CCM imeshindwa CHADEMA itaweza kuwa ni mbadala wake.
In my opinion, CDM wanaweza kuweza but not now until you put your house in order.
Other wise hii nchi itayumba from bad to worse! Sishauri kufanya hayo majaribio.