Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
- Thread starter
- #61
Cha msingi wananchi waamini na kujiandaa,maana vita dhidi ya ukiritimba dola ndo imejiri
I think so.
Cha msingi wananchi waamini na kujiandaa,maana vita dhidi ya ukiritimba dola ndo imejiri
Nashukuru kwamba umejua hii ni movie ya ukweli - it about life or death.
Mr Ronn,
What are the optional means that CDM could explore in handling situtitions it is faceing currently???
Tatizo lenu mnajipa imani kubwa kushika Dola 2015, CDM kweli imepata nguvu lakini bado haikubaliki kama mnavyo taka kuaminisha watanzania. Hizi mbinu tunazo ziona ni maigizo yenu wenyewe ili kuonyesha umma kuwa CCM inataka kuwamaliza kwa sababu CDM ndio chama mbadala. Kundi linalo washabikia ni vijana wafata mkumbo na wengi wao sio wapiga kura bali ni wapiga kelele tu.
CCM itafika wakati itang'oka lakini sio leo wala kesho, na wala haitakuja kutolewa na CDM. Wapiga kura bado hawajaona chama mbadala na hawako tayari kuwakabidhi Nchi nyinyi wakati hata chama kinawashinda kukiendesha.
thread hii imejaa upuuzi mtupu!!!!!!!!!!!!
Ndugu yangu ya kijijini ndio acha kabisa, usione watu wamejazana ukafikiri ni wapenzi wa chama, hao wanakuja kushangalia helkopta. Ni rahisi sana kubadili mawazo ya watu wanao ishi mjini lakini wa kijijini sio rahisi. Bila shaka wewe huna ndugu kijijini ndio maana unasema haya. Watanzania bado wanachagua mtu kutokana wanavyo shauriwa na mwenyekiti wa kijiji. Usimshangae mbunge wa ccm anae wapigia magoti wapiga kura ndugu yangu, hayo ndio mambo yanayo takiwa kijijini.
Tatizo lenu mnajipa imani kubwa kushika Dola 2015, CDM kweli imepata nguvu lakini bado haikubaliki kama mnavyo taka kuaminisha watanzania. Hizi mbinu tunazo ziona ni maigizo yenu wenyewe ili kuonyesha umma kuwa CCM inataka kuwamaliza kwa sababu CDM ndio chama mbadala. Kundi linalo washabikia ni vijana wafata mkumbo na wengi wao sio wapiga kura bali ni wapiga kelele tu.
CCM itafika wakati itang'oka lakini sio leo wala kesho, na wala haitakuja kutolewa na CDM. Wapiga kura bado hawajaona chama mbadala na hawako tayari kuwakabidhi Nchi nyinyi wakati hata chama kinawashinda kukiendesha.
Ndugu yangu ya kijijini ndio acha kabisa, usione watu wamejazana ukafikiri ni wapenzi wa chama, hao wanakuja kushangalia helkopta. Ni rahisi sana kubadili mawazo ya watu wanao ishi mjini lakini wa kijijini sio rahisi. Bila shaka wewe huna ndugu kijijini ndio maana unasema haya. Watanzania bado wanachagua mtu kutokana wanavyo shauriwa na mwenyekiti wa kijiji. Usimshangae mbunge wa ccm anae wapigia magoti wapiga kura ndugu yangu, hayo ndio mambo yanayo takiwa kijijini.
well,
There are number of facts.Kwanza ni lazima tukubali kwamba ili umshinde mtu yakupasa uwe one or more steps ahead of him. Mkiwa at per, au chini yake forget it. Sasa ni lazima CDM wajithibitishe kuwa wapo mbele ya CCM in terms of planning, strategies and implementations. Kwa mfano
1. CCM wanajua kwamba kiwango chao cha kukubalika kwa wananchi kimeshuka sana. Wanajua kuwa pia CDM inapanda chati. Hivyo whatever a move they are taking its final aim ni kuwafrustrate, kuwapotezea muda, kuwashushia kiwango cha kukubalika katika jamii na zaidi kuwachanganya wananchi hasa wasio na elimu na wale wa kijijini kwamba CDM ni chama hatari kushika madaraka. Mkumbuke pia kwamba watanzania wanapenda amani na kama wakiambiwa chama hiki ni cha vurugu na mauaji, believe me, ni wale wachache wenye elimu wenye uwezo wa kuchanganua mambo ndio watakao weza kuwasupport. CDM inapaswa kuwa na uwezo wa kuweza ku-counter attach these moves bila kupoteza mwelekeo wake wakujijenga kitaifa.
Nadhani huu ni ushauri mzuri sana. Tunajua hilo tunatakiwa kuongeza tahadhari kama ulivyosema.
2. Kufafanua zaidi ninalosema hapo juu, lolote linaloletwa na CCM, lisipoteze muda wa chama katika kujijenga. Ningeshauri muibue na kuongeza idadi ya figure za kitaifa zinazoweza kuaddress maswala ya kitaifa. Wasiwepo watu wachache wanaokuwa wanang'ara kila siku. Mnapokuwa na watu wengi, ni rahisi kuhakikisha kuwa majukumu yanaendelea katika kila kanda kwa ujenzi wa chama wakati huo huo figure nyingine ziwe zinadeal na attacks za CCM. Mf issue ya Lwakatare inatakiwa iwe addressed simultaneously with party building activities at the grass root level
Hili la wasemaji wengi wa chama limeshafanyiwa kazi. Viongozi wa Kanda sasa wataanza kuwa wasemaji wa kanda na ultimately baadhi yao watakuwa national figures soon. Pili shughuli za ujenzi wa Chama ktk kila kanda na kila jimbo zinaendelea as you advised.
3. On intelligence side, you need more trusted insiders than ever. Strategically mnaweza hata kuhakikisha mna moles wenu kule wanaocheza double agent roles. Since CCM wameamua kuresort kwenye intelligence na vyombo vya dola mnaweza kuwashinda tuu kwa kuempoly advanced intelligence techniques na sio siasa za majukwaani. Mfano kati ya Dec na March ambapo hili swala la Lwakatare limekuwa likipikwa (if at all) insiders wangeweza kuwapa updates. Hii ingewaumbua sana wapinzani wenu.
Kiukweli Chadema ina wanausalama wazuri hata hivyo, ushauri wako wa maboresho hopfully ni ushauri wa kufanyiwa kazi. Thnks. Ni Ukweli kwamba ccm inahangaika sana na kutupandikizia mamluki kwa staili hiyo. Ila tunakula nao sahani moja mpaka sasa. Kama siyo intenligence tusingekuwa hapa tulipo leo. Huko serikalini wala hatuhitaji kuajiri wako wengi sana waliotayari kujitolea kutoa siri za hujuma haramu dhidi ya Chadema na wanasaidia sana kama alivyokwisha kusema Dr Slaa mara kadhaa.
4. Kama nilivyosema awali, CCM wanataka kuwapotezea muda. Mtakuwa mmegundua kuwa mtu mmoja wa CDM akihamia CCM story inakuwa kubwa sana. Dont try to play the same game. You need thousands votes of villagers in Nangurukuru, Masasi, Mto wa Mbu, Nguruka, Biharamulo,Moshi, Pangani, Kondoa, Geita than few people moving from CCM who at the end of the day may not vote at all. Mnahitaji base kubwa sana ya wapiga kura.
We are doing something around that very strategically, hata hivyo, sitaleza in detail maana ntakuwa nawafaidisha hapa.
5.Najua mnao, lakini jitahidi kupata watu wengi zaidi kwenye media. Watu ambao si kwamba wataandika uongo juu yenu, lakini watotoa proper weight kwenye habari zenu hasa kunapokuwa na many hitting headlines.
Noted.
6.Msipoteze sauti yenu mlionza nayo kwenye mabadiliko ya katiba. Msikae kimya katika kusukuma swala zima la maboresho ya wapiga kura. Mnahitaji kuhakikisha kwamba vijana wengi wanajiandikisha na wanapiga kura. Hakikisheni pia siku ambayo watanzani wanatakiwa kufanya maamuzi yatakayo waathiri haiwi siku ya ibada kwa dini yoyote. This is technically important. Angalieni ni wapi mna wapiga kura wengi. Arusha, Moshi, Mbeya, Mwanza, Iringa nk nk. Ikiwa kura inapigwa jumapili, trust me wapo wengi hawatapiga kura. Wapo ambao Ibada zinaanza saa mbili mpaka saa nane, unadhani watapiga kura saa ngapi?
Nakubaliana na wewe hata hivyo, nadhani msisitizo uwe Tume huru ya uchaguzi zaidi kuliko kingine chochote kwa sababu kwenye fair election mpaka sasa ccm wanajua kwamba tutawapiga vizuri sana. Hata hivyo, hilo la kuwaongeza wapiga kura nalo ni muhimu sawia.
7. Hakikisheni mnaandaa wagombea ubunge influential na wenye kukubalika. Hawa waanze sasa kukijenga chama kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi ya chini. Najua kwa sasa wagombea wengi wapo Dar. Ni vyema wakaanza kujenga chama kuanzia kwenye mashina ya maeneo walipotoka.
Correct. Ndivyo ilivyo.
8. Uchaguzi wa mwakani ni muhimu sana kwenu kuliko hata huo wa 2015. Huu ndio utakaoeleza mmekubalikaje Tanzania nzima. Kama hamtafanya vyema, tutayasikia maneno ambayo nimeyasikia sana 'CDM wanafanya vizuri lakini hawajawa tayari kuongoza nchi'. Mpaka sasa mnapaswa muwe mme eyemark watu watakaosimamisha bendera yenu kwenye ngazi za mitaa. Narudia tena kama mkishindwa mwaka mmoja uliobakia utakuwa mgumu sana hasa ukizingatia propaganda za wapinzani wenu.
Nch hakuna uchaguzi usiokuwa na kanuni na unaochezewa rafu kama uchaguzi wa serikali za mitaa. Hata hivyo, next year kitaeleweka tu.
9. Hakikisheni mnakuwa na mawakala wakutosha watakaosimamia kura zenu kwa uaminifu katika uchaguzi wa 2014 na 2015
Nakubaliana na wewe, lakini siyo tu wa kutosha lakini pia wasiohongeka. Siku moja nilikaa kiti kimoja na abiria. Njiani tukazoeana sana halafu akaniambia jinsi alivyokuwa wakala wa NCCR mwaka 1995 na jinsi saa sita usiku alipewa Tsh 300,000?= hela ambayo hajawahi kushika tangu azaliwe. Akapokea na kwenda kulala huku anatetemeka. Saa kumi na mmoja akarudi kituoni kusaini matokeo.
10. Tunafahamu nchi hii inategemea wahisani wa maendeleo. Sijajua how close are you to them lakini kama wakipewa objective analysis ya yanayondelea nchi from opposition point of view wanaweza kuwa na sauti juu ya serikali yetu. At least inaweza kupunguza makali ya vita mnayopitia.
I do think kwamba wanafuatilia kila kitu ndo maana hata kwenye baadhi ya matukio makubwa ya kitaifa wamekuwa wakitoa sauti yao. Hata hivyo, ushauri wako ni murua pia.
Sasa nimeandika kwa haraka na najua kunawezakuwa na some errors and may be no coherence. Please see what you can gather from it. Muhimu ni hii, learn you enemy silently, play smarter than him, of course in all spheres!
Copy to Mwita Maranya, John Mnyika, Crashwise, Joshua Nassari, Halima Mdee, Ruttashobolwa etc
View attachment 87331
Husiwe na mtazamo kama huo ndugu hao unaowaona hapo ni baadhi ya Umati wa watu wa Igunga waliohudhuria mkutano ulioitishwa na Viongozi wa Wilaya na kuwakaribisha Kigaila na Waitara, hakuna miongoni mwao alioletwa na fuso wote walikuja kwa mapenzi yao, halafu nikupe taarifa tu Wilayani Igunga DC ameishaitisha mikutano zaidi ya Mitatu hakuna mwananchi aliyehudhuria lakini CDM wakiitisha hata iwe kwa muda wa nusu saa watu nyomi, usijidanganye hali ni mbaya sana kwa upande wa CCM inatakiwa mbadirike sio kuwa na imani kuwa mnapendwa wakati sio.
Hopefully CUF yes, but will it change the situation in 2015?Kwenye mkakati wa 3 tunataka kuwawini CUF ili tuone kama CDM mtaweza kushindana na ccm + CUF.