Sakata la Kuulipua Ubalozi wa Marekani Wanafunzi 8 Wakamatwa, Ubalozi Watoa Taarifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Kuulipua Ubalozi wa Marekani Wanafunzi 8 Wakamatwa, Ubalozi Watoa Taarifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  WANAFUNZI wengine wapatao wanane wa shule ya Sekondari Biafra wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano maalum kuhusiana na jaribio la kulipua ubalozi wa Marekani. Wanafunzi hao walikamatwa jana majira ya alasiri wote wakiwa wanafunzi wa shule hiyo na wanahojiwa chini ya maofisa wa usalama wa taifa wakishirikiana na polisi.

  Awali Jumapili majira ya saa 3 usiku, mwanafunzi wa kidato cha pili, Nassib Zukheri [16] wa shule hiyo alikamatwa katika ubalozi huo akiwa katika jaribio la kuuteketeza ubalozi huo kwa mabomu ya mafuta ya taa.

  Taarifa za awali zilisema kuwa mwanafunzi aliyekamatwa alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi ya Mtambani lakini taarifa za polisi zimethibitisha kuwa mwanafunzi huyo ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Biafra.

  Pia taarifa za awali zilisema kuwa mwanafunzi huyo aliingia ubalozini wakati walinzi wakiwa wamelala lakini ubalozi wa Marekani umekanusha mwanafunzi huyo kufanikiwa kuingia ndani ya ubalozi na leo umetoa taarifa ifuatayo kwa vyombo vya habari.

  TAARIFA YA UBALOZI WA MAREKANI DAR

  -----------------

  Siku ya Jumapili, tarehe 16 Mei, mnamo saa 2.30 usiku, mvulana mwenye umri wa miaka 15 alikimbia na kumpita mlinzi aliyekuwa mbele ya Ubalozi wa Marekani, akawasha moto kwenye chupa iliyokuwa na mafuta ya taa na kisha kuirusha chini ya moja ya malori mawili ya kubebea maji yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ukuta wa Ubalozi.

  Chupa hiyo ilivunjika lakini haikuweza kulipua moto. Walinzi wa Kampuni ya KK wanaolinda ubalozini hapo walimkamata mara moja kijana huyo kabla hajaweza kurusha chupa ya pili.

  Hakukuwa na mtu yeyote aliyejeruhiwa wala mali yoyote iliyoharibiwa katika tukio hilo. Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania aliwasili sehemu ya tukio sekunde chache baadaye na kumkamata mtuhumiwa. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.

  Baadhi ya maelezo yanayotolewa kuhusu tukio hili si sahihi, yamekuzwa na kutiwa chumvi mno na yasiyo ya kweli, yakidai kuwa mvulana huyo aliingia ndani ya ubalozi. Hii si kweli. Hakukuwa na mtu yeyote aliyeweza kuingia ndani ya Ubalozi wa Marekani.

  Taratibu zetu za kiusalama za kuzuia wahalifu kuingia ubalozini zilidhihirisha ufanisi wake hapo Mei 16.

  Walinzi wa kampuni ya KK na Polisi wa Tanzania walishughulikia suala hili kwa weledi mkubwa. Tunawashukuru sana.


  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Upumbavu mwingine bwana! Nani kawatuma wakalipue hayo mabomu ubalozi wa Marekani? Badala ya kusoma wanaanza mambo ambayo yatavuruga future yao yote na kuwaweka kwenye mistari inayoogopwa kama ukoma bila sababu
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Hivi alikuwa na mabomu au ni maneno tu!
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Si unasikia story kwamba alikuwa na chupa zenye mafuta? nadhani alikuwa na mabomu ya petrol yale! Kama walivyosema wao ni kwamba baada ya mafunzo alikuwa kwenye mazoezi.
  Hivi kweli hawa hawana tutor mtu mzima?
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  May 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wametumwa na mungu wao anaitwa allah!
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  May 21, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
 7. B

  Bull JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wavivu wa kufikiri utawaona, wataanza ku jump bila kujiuliza maswali, ripoti ilivyo jieleza kwa mtu mwenyefikra ataona na kuelewa tokeo zima ukianza tu msitari wa kwanza wa maelezo.

  Ngoja tuwaone wa upande wa kushoto walivyo kuwa wavivu wa kufikiri!!!!
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Wamarekani wanaogopa kuonekana taifa kubwa lakini ulinzi hafifu; nionavyo mimi hakuna chumvi kwenye yaliyosemwa. Sasa angalia maelezo yao kuwa mtoto alimpita mlinzi na baada ya kumpita mlinzi aliwasha hiyo chupa ya mafuta moto. Maswali: huyu mlinzi aliyefuzu mafunzo yake anapitwa vipi na mtoto wa miaka 15 kiulaini? Huyu mtoto mpaka anafanikiwa kuwasha moto na kutupia kwenye magari, huyu mlinzi alikuwa anamwangalia tu? Hivi ubalozi wa marekani huwa wanaegesha magari yao nje ya ukuta jamani?
   
 9. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Huyo dogo ni member wa al-qaeda?
   
 10. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna tatizo mahali haiwezekani mtu kupita mpaka akawasha moto! ila usalama wa taifa wa tz sikuhizi ni kama haupo maana mambo haya wangeyajua mapema kabisa,sijui tunakoelekea maana hata wahisani wameshaona kuna kutokuwajibika kwa hali yajuu watu hawafanyi kazi ipasavyo, basi bw wa tz tulifanya makosa sana na hili litatugharimu kwa 5yrs nyingine tena,
   
 11. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  labda kweli alikua anafanya majaribio! Lakini kwann akachagua ubalozi wa marekani? kazi sana ila inaelekea mtoto jasiri huyo, annanza umafya mapema.
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wee Mike, usalama wa taifa wako busy na uchaguzi kutafuta mbinu za kuiba kura na kuweka mapandikizi kwenye vyama. Hata hivyo siku hizi tunao usalama wa sisi M si wa taifa. Haya yote yanatoke usishangae.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Habari ya awali katika Habari Leo iliiandikwa kwa ushabiki mkubwa hasa ile ya kusema kuwa mhusika alikiri kuwa ni wa mtandao wa AlQaeda na alipewa mafunzo nao. Walipata wapi hii?
   
 14. B

  Bull JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Nilishasema watu wa mkono wa kushoto wataanza kuvamia na ku conclude kuwalaumu alqaida na waislam bila kufikiria au kujiuliza. hii inatokana na uvivu wao wa kufikiri, uzembe, ujinga na kuhubiriwa chuki vilabuni mwao!
   
 15. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #15
  May 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mnafikiri tatizo ni mtoto anayesoma Biafra? La hasha, akitoka huyo atakuja mwingine kwenda Tora Bora kupigana Jihad! Tatizo ni maandishi yatokayo kulia kwenda kushoto! Huo ndio mzizi wa fitina! Hayo mengineyo ni dalili tu za ugonjwa!
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  we Bull. mbona unajihami sana? hakuna mwislamu aliyelaumiwa hapo, bali al-qaeda sasa shida yako nini?

  [​IMG] Originally Posted by Counterpunch [​IMG]
  Habari ya awali katika Habari Leo iliiandikwa kwa ushabiki mkubwa hasa ile ya kusema kuwa mhusika alikiri kuwa ni wa mtandao wa AlQaeda na alipewa mafunzo nao. Walipata wapi hii?   
 17. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ulijuaje kuwa Moses ni Mtume?
  Ni nini kinachokufanya wewe uamini kuwa Moses ni Mtume?
  Rabbi Yitzhak Ginsburg declared, "We have to recognize that Jewish blood and the blood of a goy are not the same thing." (NY Times, June 6, 1989, p.5).
   
 18. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  alishajistukia tayari, anataka kuanza kuwatetea alkaeda mtandao unaotimiza mapenzi ya alah wakibaru wao.
   
 19. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kwani unamwabudu Mungu au allah,
  au wewe ni mfuasi wa Biblia? kuna mtu anaitwa mhammad huku ina maana ni yule mtume wenu au ni jina tu? na mwingine anaitwa abd allah ina maana ni mtoto wa mungu wenu allah au ni jina?
  unaweza kuita usicho maanisha na ukamaanisha usichoita,

  hata hivyo siyo topiki ya leo, tuendelee na topiki iliyo jamvini
   
 20. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  heheee mzee wa Talmud aya sasa lete zile nukuu zako
   
Loading...