Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA

Ha ha ha ha ha aaaaaaaaaaaaaaaa. mzazi anapotaka kucontrol maisha ya mkewe. huyo mama hafai kuwa kwenye uongozi. anaishi kwa hisia tu
 
Nina mashaka sana na habari hii, ila kama ni kweli basi nina kila sababu za kumuona Kibanda kuwa aliona mbali zaidi yetu.
 

Mkuu FP nilikuwa naichukia sana signature ya Masatu lakini naona taratiiiibu inaanza kupata nafasi katima Mtima wangu! Si watoto bali wanaamini katika Strategies za TUMPE WAKATI MGUMU ASHINDWE KUONGOZA, NI UPUUZI MTUPU
 
Kama habari hii ina chembe za Ukweli then Kibanda ni Jiwe walilolikataa Waashi
 

Kwa kweli hata mimi niliposoma habari ya gazeti la wiki hii la Rai ambayo limeeleza mambo haya nimebaki mdomo wazi.

serayamajimbo
 
Hivi Tanzania Mpaka lini???
CCM Tumewachoka jamani.
CHADEMA mlishaanza kuonesha mwanga kidogo. nilikua nategemea 2010, Wabunge waupinzani wangeongezeka Bungeni. Nimeanza kupata wasiwasi na mwenendo wa hiki chama tangu Zitto alipotangaza azma yake ya kugombea uenyekiti.
Jamani Tuombe Mungu hawa ''wapiganaji'' ndani ya sisiem waanzishe walau chama chao cha siasa. May be they might take us to another level.
 

Mkuu FP naungana nawe katika hili; at this point of time Mh. Zitto lazima awe makini sana, hii triangle inayomzunguka -- Marafiki, Siasa, Familia -- yaweza mpoteza mwelekeo, narudia tena he has to be extremely carefully coz any of the three components making that triangle yaweza kuwa na agenda ya siri aidha kwa kudhamiria au kwa kutokujua.

Ninaingiwa wasiwasi na uwezo wa kiupeo wa familia ya Zitto (samahani katika hili), hao ndugu wa familia zake wako-well exposed kweli?? wamesoma?? vinginevyo wanahitaji kuwa na busara ya hali ya juu katika kumshauri mtoto wao vinginevyo watampoteza ... na ninaanza kuhisi pia ndio maana mara nyingi Zitto amekuwa haeleweki na pia akiwachanganya wapenzi na wananchama wake kwa misimamo ya ajabu kabisa ... kosa laweza kuwa ni kuchanganywa na hiyo mihimili mitatu isiyo rasmi.

Ushauri mbaya wa Familia plus Marafiki na kudhorota kwa mahusiano na viongozi wenzake wa kamati kuu kwaweza kumuweka huyu kijana katika nafasi ngumu sana kwa ustawi wake kisiasa. Siamini kama Zitto anajua kila kitu katika siasa na fani mbalimbali hapa duniani; na kama ni hivyo, inakuwa mbaya zaidi kama washauri na wapambe wake anaowasikiliza wakiwa hawajasoma na upeo wao ukiwa mdogo sana.

Zitto ndugu yangu, you ought be very smart and careful on your next moves, coz waswahili walishasema "kikulacho kinguoni mwako!!"

Kuwa mvumilivu, na busara itawale mbele yako!
 
Bado nini?
Huu ni uzembe na uoga wako katika siasa.
Siku zote unadhani siasa ni lele mama kwa sababu mlizoea siasa za kibabe za ki sisi m.
 
Akufukuzaye hakwambii toka utajionea mambo yanvyokwenda! Hawa weshajua chama ni cha kina nani na kina malengo gani! Na wameshajua kwamba kitawafaa ama hakitawafaa! Embu tusubiri tuone kile cha wakulima
 
ee kama ni hivo kwa heri
Dr Slaa kaumiza wengi hivyo ana "maadui" wengi pia. Katika ile orodha yake ya MwembeYanga hakuna hata mmoja aliyejinasua na hawa wana ndugu, jamaa, rafiki, wapenzi, mashabiki, nyumbandogo,.....
 
Viongozi wa CHADEMA,
Wawekeni kando WAZAZI, WAKWE zenu. Hawa watakapoanza kuchambuliwa humu na kwenye majukwaa mengine chama chenu na ninyi wenyewe hamtabaki salama na amani itatoweka.
 
Unadhani vijana wetu wa chadema wanagombana au kutofautiana?
HAaaaaa! wanapiga miayo ya uchovu wa viako tu!!

Chadema Imara na ikulu yetu 2010.
 

Personally nitatafuta email ya Zitto nimshauri mambo kadhaa, sitaki kumshambulia hapa mpaka nimsikilize kwasababu naamini ni mwanasiasa mzuri akijirekebisha. Kuna namna ya kuelezea hisia zako bila ku attack mtu wala viongozi wenzako. Timu yake sio nzuri ...
 
Viongozi wa CHADEMA,
Wawekeni kando WAZAZI, WAKWE zenu. Hawa watakapoanza kuchambuliwa humu na kwenye majukwaa mengine chama chenu na ninyi wenyewe hamtabaki salama na amani itatoweka.

Point zako huaga nazikubali, lakini hapa umeteleza kidogo. Katiba ya Nchi inaeleza kila mtu ana haki ya kugombea, kutoa mawazo n.k. ukiwa tiyari umefikisha 18yrs. Hawa wazazi wako sawa tu kufanya maamuzi yao isipokuwa tu haya maamuzi wanayatolea wapi na kushirikisha nani! Ebu fikiria Mh. Zitto kwenye CHADEMA ni Dhahabu kwa hiyo wanaotafuta kumtumia hawapo mbali!!! na usikute wakapitia kwa wazazi wake!!! kumbuka familia ya Wangwe ulivyotumiwa kwenye Msiba wa Wangwe.

Pia unaweza kutumia uzoefu wako bado, siasa nikama inaambukiza kizazi na kizazi, chukulia familia ya Bush, Clinton, huyu Odinga, Karume, Mwinyi n.k. Mimi sioni cha hajabu kwanini kuishutumu familia ya Zitto kuingia kwenye siasa, isipokuwa tu pale inapoanza kuhujumu Chama.
 
wakati mwingine ni mambo ya kawaida sana sisi tunakuza sana kama nini
 
Jamani hayo ni mambo madogo sana kujadili kwa muda mrefu. Wansiasa wote ni wadogo hata zito si mwanasiasa wa kuitwa mkubwa ndio maana visifa vidodovidogo wanavyopewa na vyombo vya habari vina wachanganya wote.
 
Haya ya Katiba na uhuru wake nayafahamu. Siasa za Nchi hii ni kuchafua na kuchafuana na hasa wanasiasa wetu wanapoishiwa HOJA. Angalia ya Malecela na Mke wake mama Kilango!
 
Haya ya Katiba na uhuru wake nayafahamu. Siasa za Nchi hii ni kuchafua na kuchafuana na hasa wanasiasa wetu wanapoishiwa HOJA. Angalia ya Malecela na Mke wake mama Kilango!

Ukisha amua kuingia kwenye siasa hautakiwi kuogopa, yote hayo watakupaka hiyo ndo siri ya Siasa. Kwa huyo Malecela amezoea kupaka madongo wenzio hivyo, unadhani anashtuka huyo.

Cha kufahamu CHADEMA wanawindwa kila kona wasichanue.
 

Na kisha mafisadi waende wamkolimbe Dada Halima buree kwa madai yasiyo na msingi kama haya. Zitto, Omar, Msafiri, Ndanda, Kafulila na wengineo wote kambi ya Zitto.

Mchawi wenu sio Halima Mdee, Mchawi wenu ni matendo yenu wenyewe na maneno yenu mnayoyatoa bila kuyapima. Eleweni kuwa Tanzania (na chadema in this case), ni kubwa zaidi kuliko Zitto Kabwe (bila kujali umaarufu ambao nyie mnadhani kuwa Zitto anao).

Kinachowatokea leo hakikuanza leo, kilianza mara tu Zitto alipokubali kuingia kwenye tume/kamati ya madini ya Kikwete na hivyo kuondoa nafasi ya kuundwa kwa tume huru ya bunge kuchunguza barick na buzwagi.

Msimsingizie Halima kwa kile asichoweza na mkaja kumtia matatani bure. Muulizeni Max atawaambia ni nani anayejiita mwafrika hapa JF (kama akipenda) maana mimi nayeye tunafahamiana vyema. Vinginevyo - mnakoelekea, haitakuwa rahisi kwenu kurudi na kujenga chadema mnayodai kuwa mnaipenda kwa moyo wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…