Sakata la Bandari: Baraza la Mitume na Manabii Tanzania lakanusha kutoa Tamko

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
Baraza Kuu la Mitume na Manabii Tanzania limekanusha kuhusika na barua ambayo imesambaa mtandaoni ikieleza kinachodaiwa kuwa ni tamko la baraza hilo kuhusu sakata linaloendelea la Mkataba wa Bandari.

Akieleza katika video aliyoiposti kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ulinzi na Itifaki wa baraza hilo, Dkt. Peter Rashid Abubakar amesema kuwa barua hiyo haijatoka katika ofisi yake na pia haina vielelezo vyovyote vinavyothibitisha kuwa ni nyaraka rasmi ya taasisi hiyo.

Dkt. Abubakari pia ameeleza kuwa hajui ni nani aliyeiandika na kuisambaza.

 
Ngoja nishangae kwanza! Eeh! Mi naishi nchi gani, kumbe kuna baraza la mitume na manabii, lilianzishwa lini? Anyway, ni wananchi kama wengine, ila itoshe kwa waraka wa TEC umemaliza kila kitu. Waraka mwingine hautakuwa na maana labda uwe kinyume na wa TEC
 
Hatuwadharau, ila hawana ushawishi wale afadhali KKKT. Waraka wa wakatoliki ni kiboko mpaka serikali yenyewe inahaha na joto lake
 
Back
Top Bottom