Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Miezi mitatu tu baada ya kufariki kwa Rais wa Awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya mama Samia, ilianza mazungumzo na wawekezaji kufufua mradi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na ule wa Mchuchuma na Liganga.

Juni 26, 2021 wakati akifungua mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara(TBNC) Ikulu Jijini Dar Es Salaam mama Samia alisema: "Bagamoyo tunakwenda kuanza mazungumzo na taasisi iliyokuja kwa ajili ya mradi huu ili tuifungue na tuende nao kwa faida yetu.

Itakumbukwa kuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli aliwahi kukaririwa akisema ujenzi wa bandari hiyo una masharti magumu ya mwekezaji ndio sababu ya kusuasua kutekelezwa.

Lakini sasa tangu lianze sakata la uwekezaji wa kampuni ya DP World katika Bandari nchini, sisikii tena ishu ya Bagamoyo. Ina maana ndio imekufa mazima?
 
Back
Top Bottom